Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daraja la Selander ni daraja kwenye Barabara ya Ali Hassan Mwinyi (Bagamoyo Road) ambalo linavuka mto Msimbazi jijini Dar es Salaam, Tanzania.Naomba kujua kuhusu daraja la Salender ambalo liko jijini Dar es Salaam
1. Lilijengwa mwaka gani.
2. Mkandarasi / engineer aliyelijenga daraja hilo.
3. Na ni nani aliyesimama ujenzi kipindi hicho.
4. Na kwa nini eneo hilo la barabara na daraja hilo linaonekana liko imara sana.
5. Na je hatuwezi kuwapata walioshiriki kujenga daraja hilo wakatusaidia mawazo nini kilipelekea kujenga daraja imara kiasi hicho.
6. Pia naomba kujua kiasi cha fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.
7. Na ni kwa nini maji ya mito yote hayajazi eneo hilo la daraja.
Natanguliza shukrani kwa yoyote atakusaidia kwa namna moja au nyingine...
"My take: kwangu mimi DARAJA HILI LINGEWEKWA KWENYE MAAJABU YA DUNIA, kwa kuweza kupitisha maji ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam bila wasiwasi!
Hata ukipita kwa gari unaliona la pili. Ukiwa unatoka Mjini kuja Traffic Light za pale Stanbic lenyewe liko kushoto (Upande wa Mikoko, sio Upande wa Bahari).Huwa napita nikiwa kwenye gari sikujua kama kuna madaraja mawili pale.
Hilo daraja bado linaendelea kujizolea mahistoriaHata ukipita kwa gari unaliona la pili. Ukiwa unatoka Mjini kuja Traffic Light za pale Stanbic lenyewe liko kushoto (Upande wa Mikoko, sio Upande wa Bahari).
Kaka unavuta nini wakati unapoendesha gari??? Daraja jipya liko upande wa bahari!!! Haidhuru unapoelekea.Hata ukipita kwa gari unaliona la pili. Ukiwa unatoka Mjini kuja Traffic Light za pale Stanbic lenyewe liko kushoto (Upande wa Mikoko, sio Upande wa Bahari).
Wewe huelewi kinachojadiliwa hapa, yaani umekurupuka kujadili bila kujua chochote.Kaka unavuta nini wakati unapoendesha gari??? Daraja jipya liko upande wa bahari!!! Haidhuru unapoelekea.
Unasema kweli (labda) kumbe lile daraja la baisikeli na waenda kwa miguu ni lile la Selander mwenyewe? Sawasawa, nitaiangalia sasa kwa macho mapya!Wewe huelewi kinachojadiliwa hapa, yaani umekurupuka kujadili bila kujua chochote.
Ukiacha lile Daraja linalojengwa sasa kule baharini kutolea Coco mpaka Agha Khan, pale Selander tunapopita kuna madaraja mawili, moja jembamba lililojengwa na mkoloni lililoko upande wa mikoko, na jingine upande wa bahari ndo linalopitisha magari lililojengwa na Kajima miaka ya 1980s.
Sasa wapi Mimi nimesema daraja jipya ndio liko upande wa mikoko?
Hapo Sasa tuko pamoja MkuuUnasema kweli (labda) kumbe lile daraja la baisikeli na waenda kwa miguu ni lile la Selander mwenyewe? Sawasawa, nitaiangalia sasa kwa macho mapya!
Asante!
JE WAJUA? JE UNAJUA Kituo cha Polisi cha Selander Bridge zamani ilikuwa ni hoteli moja maarufu sana?
Jengo hili zamani ilikuwa ni hoteli maarufu iliyokuwa inaitwa “Sun and Sands Hotel”
iliyokuwa inamilikiwa na familia ya Punja waliokuwa mabepari wakubwa wa kihindi miaka ya 1920- 50. Hotel ilijengwa mwaka 1949.
Hii hoteli ilikuja kutaifishwa na kuchukuliwa na serikali baada ya makomando wa kikaburu kulipua daraja la Selander, Nyumba ya Balozi wa Uingereza pale Toure Drive na Oil Depot Kurasini mwaka 1972. Makomando hawa (South African Special Forces Brigade-RECCE) waliitumia fukwe mbele ya hili jengo kujitayarisha na mission yao. Baada ya huu mkasa ndo serikali ikaamua kuongeza ulinzi na ikajenga Kituo cha Polisi cha Selander Bridge na hili jengo likataifishwa.
Na Zuwena wa Mr Paul piaOngezea pia kuwa nisehem ambayo jojina dem wa marijani alipata ajali
kinazungumzia tukio la 1980 hapo selander bridge?
FROM SUN & SAND HOTEL TO SELANDER BRIDGE POLICE STATION.Urejee mkuu, nna hamu ya kujua kuhusu hilo.
Ndio, ni mkusanyo wa operation zao zote ikiwemo Tanzani na Angola, Namibia, Zambia, Lesotho, Mozambique and Botswana.kinazungumzia tukio la 1980 hapo selander bridge?