Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani kufukuzwa shule kunaathiri chochote kwenye historia yake.Kwa nn Magufuli alifukuzwa seminari ya wakatoliki wenzake alikokuwa akisoma?
SANA TU huwa yanajirudiaKwani kufukuzwa shule kunaathiri chochote kwenye historia yake.
Au mimi sijaelewa
Kwani kufukuzwa shule ndio kupita milembe? Kwanza sisi tunaamini huo ndio umwambaSANA TU huwa yanajirudia
kwani hata Mkiti wa CCM Mkoa wa Mwanza antony Diallo alisema tusirudie kuwachagua watu waliopitia Mirembe
Kunaathiri maana yake huyu alionekana mbele ya viongozi wa kanisa lake kuwa hafaiKwani kufukuzwa shule kunaathiri chochote kwenye historia yake.
Au mimi sijaelewa
Kwani kufukuzwa shule ndio kupita milembe? Kwanza sisi tunaamini huo ndio umwamba
Lake Secondary sio ya Serikali!Kumbe hujui hata historia uliyoiandika mwenyewe! Mwaka 1975 alijiunga seminary ya Katoke huko Mkoa wa Kagera, ilikuwaje akahamia Lake Secondary ambayo ni ya serikali mkoa wa Mwanza akiwa form 4? So sad hujui halaf bado unabisha...Kama hujui uliza!!!
Huenda walitaka afanye wanayo taka wao kwa mfano swala la wito, huku wanaweza kukufanyisha kazi ngumu eti kisa ni wito.Kunaathiri maana yake huyu alionekana mbele ya viongozi wa kanisa lake kuwa hafai
Wanao sema hivyo labda walikuwa nae huko.View attachment 1928086 mm nilidhani namuelimisha mtu kumbe mtoto MFU
hao viongozi wa chama kilichokosea mpaka leo wanajuta wakati walijua ni Mirembe wewe unasema milembe kweli hujui kitu hapa, upo km msukule, ukikua utaelewa vizuri
Muulize marehemu aliwezaje?unaweza kutoka shule ya private ukahamia serikali?? yani utoke mbezibeach sec uende azania kwa kuhamia
Teteeh ngoja mzimu wake ujeMuulize marehemu aliwezaje?
AsanteLake Secondary sio ya Serikali!
itakua wamemsingizia maana zamani private zilikua zinaitwa shule za kufeli ,government ndio waliofaulu sasa hata sasa huwezi kutoka private kwenda governmentMuulize marehemu aliwezaje?
Nipe link mkuuMajibu yake yako humu ndani kwenye michango ya wadau
Barabara za Dar, Magu kateleza na ganda la ndizi tu! Yeyote ambae angeingia madarakani angejenga kwa sababu by March 2015, World Bank walikuwa wamesha-approve mkopo!!Mleta uzi nimepita hapa shekilango road sinza ...kati ya vitu vinanifanya nimmiss ni hizi barabara
Yaan sinza kumekuwa kutamu balaa ni unaslide tu, sawa ni hela za kodi yetu but namshukuru Kwa utekelezaji
Sio HATERS, tatizo mkiambiwa ukweli, tunaosema ukweli mnatuita haters, na u-hater wetu unatokana na kuweka kumbukumbu sawa!! Mnatamani hata UDSM, mseme imejengwa na JPM!!Asante madam kwa kurejesha shuhuda hiyo.
Kiukweli mzee alifanya mambo japo haters wanapinga.
Barabara za Dar, Magu kateleza na ganda la ndizi tu! Yeyote ambae angeingia madarakani angejenga kwa sababu by March 2015, World Bank walikuwa wamesha-approve mkopo!!
Tena hivi umewahi kufika Kijichi?! Sinza ina-sound kwa sababu ni "main road" inayotumiwa na watu wengi, na majority wanafika Sinza!!
But last time nilivyoenda Mtoni Kijichi... jamaa naona ni kama wamependelewa, though ndo lengo lenyewe la DMDP! Karibu barabara zote za mitaani, full mkeka unlike Sinza ambako barabara za mitaani bado za hovyo (at least from the last time nilivyoenda huko)
Sio HATERS, tatizo mkiambiwa ukweli, tunaosema ukweli mnatuita haters, na u-hater wetu unatokana na kuweka kumbukumbu sawa!! Mnatamani hata UDSM, mseme imejengwa na JPM!!
Barabara za Dar zimejengwa chini ya the so-called Dar es salaam Metropolitan Development Project(DMDP), na mradi kuwa financed na mkopo World Bank.
JPM kaingia madarakani, kakuta mkataba umeshasainiwa, na mkopo umeshakuwa approved. So, yeyote ambae angeingia madarakani, barabara za Dar angejenga tu labda awe mwendawazimu!!
Au kama ingetokea emergence ya kumfanya Mzee wa Msoga aendelee kukaa madarakani kwa angalau mwaka mmoja zaidi, ambae angefuata angekuta barabara zimeshaanza kujengwa, na zingine kukamilika!
Project Details ni hizi hapa chini:-
View attachment 1958278
WASIFU:
Taaluma yake;
Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).
Kuzaliwa
Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Katoma tarafa ya Bugando wilayani Geita jimbo la Geita vijijini.
Kipindi hicho Geita ikiwa ni moja ya wilaya mkoa Mwanza.
Baadaye wakahamia Chato mkoani Geita, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
Elimu
Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.
Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.
Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.
Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati
Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza
Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mafunzo ya Kijeshi
Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.
Kazi
Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.
Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.
Siasa
Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.
Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.
Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.
Urais
Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.
Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.
Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.
Muhula wa Pili
Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ameacha watoto 7 ambao ni Suzan, Edina, Joseph, Jesca, Ruth, Jurgen na Jeremiah.
Lakini pia mwanae mmoja aitwaye Juliana yeye alifariki.
Pia amemuacha mjane Janeth Magufuli.
Magufuli majina yake kamili ni John joseph pombe Magufuli mtoto wa Suzan.
Jina pombe alipewa na bibi yake likiwa ni Jina la utani lenye maana ya jina walwa yaani pombe katika lugha ya kisukuma.
Kwa sababu kipindi Magufuli anazaliwa bibi yake alikuwa akitengeneza pombe.