Historia ya Elimu ya Chenge kwenye website ya bunge ina walakini

ujinga umekujaa kichwani uwe unasoma historian basi itakusaidia sana .unalinganisha nyakati hizi na hizo za kipindi kile
Wewe ndio mjinga na huelewi chochote hata ukiambiwa mfumo wa lazima kwa wahitimu wa kidato cha sita kwenda JKT ulianza 1963 na ulitumia mwaka mzima kwa (compulsory) na kujitolea (volunteer) miaka miwili utabisha kwa sababu ya kuwa na matope kichwani.
 
View attachment 2918909
Andrew Chenge ni mzee anayefahamika kwa wanaofuatilia siasa nchini. Video yake ya hivi karibuni ambayo alikuwa anamuuliza kijana mmoja kama amesoma imenifanya nimtafute huko bungeni ana elimu.

Elimu yake imeanza kwa kuweka elimu ya msingi (CPEE) ila ghafla imeenda kwenye elimu ya sekondary ya kati, yaani advance, huku ikiwa haina taarifa alisoma wapi sekondary ya upili (CSEE)
Hujaona hapo palipoandikwa o level cambrige certificate 1963-1966
Hapo kosa ni la aliyerekodi cv yake kwenye tovuti ya bunge ndo hakupangilia ila kila kitu kipo hapo mkuu cheki vzr,jibu lako lipo hapo hapo
Otherwise wewe elimu yako ndo inawalakini umeshindwa kung'amua vitu vidogo kama hvi
 
Oho, na wewe Pascal ulikuwa hujui? Ndivyo ilivyokuwa. Wahitimu wa shule za sekondari zetu walikuwa wanatunukiwa vyeti vya Cambridge University incorporating a general certificate of education. Fanya utafiti kidogo utajua.
Hapana,Paschal kamshangaa huyo kilaza ndo maana kamuuliza hukuiona palipoandikwa o level
 
Kijana, hilo Baraza la Mitihani Tanzania (National Examination Council of Tanzania aka NECTA) ambalo wewe ndilo lilikutahini, lilianzishwa mwaka 1971. Kabla ya hapo kulikuwa na baraza la mitihani nchi zote za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda) ie The East Africa Examination Council ambalo lililosimamiwa na Uingereza na mitihani yake ilitungwa na Cambridge University huko London.

The Ordinary Level Certificate ilikuwa ina incorporate a General Certificate of Education (GCE) ambayo ni ya nchi zote za Jumuiya za Madola ya Muingereza zilizokuwa makoloni ya Muingereza.

Hivyo hata hiyo ACSEE ya Chenge ya mwaka 1968 ni Cambridge University na siyo ya NECTA kama ya kwako. Baada ya nchi zote za EA kujitoa kwenye baraza hilo la mitihani la Cambridge University mwaka 1971, ndipo kila nchi nchi hizo ikaanzisha baraza lake la mitihani na kutunga curriculum zake kwa wanafunzi wake wa shule za sekondari. Curriculum hizi hapa kwetu zimekuwa zilibadilishwa kila kukicha kwa matakwa ya wanasiasa hadi kupelekea elimu ya vijana wetu kushuka sana ukilinganisha na viwango vya kimataifa.

Kushuka huku kwa elimu ya vijana wetu ni hadi kwenye vyuo vikuu vyetu. Utakuta sasa mhitimu wa shahada ya udaktari wa binadamu hawezi kufanya operesheni ya kutoa kidole tumbo kwa mgonjwa wa acute appendicitis. Utakuta wahitimu hawa hawawezi kutoa mtoto kwa njia ya operesheni (Ceaserian Section) kwa mama mjamzito mwenye pingamizi la uzazi (obstructed labour) ili hali huko nyuma wahitimu ya diploma in medicine (AMO) waliweza kufanya operesheni hizo kwa ufanisi mkubwa.

Hivyo ndivyo kwa wahitimu wetu wa sasa kwa profession zote hususani wanasheria na wapelelezi wa kesi za jinai, wahandisi, wahasibu na kadhalika. Wanachokijua na walichobobea kwa sasa ni kupiga dili tu.
Baada ya Jibu hili Nilitegemea Moderator wafunge Uzi kwa kuandika "No Further replies Needed"
 
Kwa kawaida kidato cha tano huanza mwezi wa tano na hukamilika mwaka mzima kwa mwaka unaofuata hivyo huyu alitakiwa kuwa amemaliza mwaka 1969 sio 1968
Kwa Curriculum ya Necta Ni sawa lakini kumbuka Necta imeanza mwaka 1971 na yeye kamaliza kabla ya Necta kasome Elimu ya Cambridge
 
Siyo porojo. Waulize wakubwa zako kujua elimu ya enzi hizo hadi za akina Kikwete na Mkapa. Enzi za Mwl Nyerere O level ya Cambridge ukiifaulu unakuwa admitted Makerere University College huko Uganda ambayo ilikuwa ni constituent college ya London University. Nakufundisha historia ya elimu yetu, tulikotoka.
Hata UD pia ilikuwa ni constituent ya University of London mkuu.
 
Wewe ndio mjinga na huelewi chochote hata ukiambiwa mfumo wa lazima kwa wahitimu wa kidato cha sita kwenda JKT ulianza 1963 na ulitumia mwaka mzima kwa (compulsory) na kujitolea (volunteer) miaka miwili utabisha kwa sababu ya kuwa na matope kichwani.
Mzee hiyo sheria unayosema imeanza mwaka 1967..
Japo ilitungwa mwaka 1963 na Bunge likaipitishwa mwka 1964
 
View attachment 2918909
Andrew Chenge ni mzee anayefahamika kwa wanaofuatilia siasa nchini. Video yake ya hivi karibuni ambayo alikuwa anamuuliza kijana mmoja kama amesoma imenifanya nimtafute huko bungeni ana elimu.

Elimu yake imeanza kwa kuweka elimu ya msingi (CPEE) ila ghafla imeenda kwenye elimu ya sekondary ya kati, yaani advance, huku ikiwa haina taarifa alisoma wapi sekondary ya upili (CSEE)
Typing error mkuu juu hapo o-level inaonekana mbona
 
View attachment 2918909
Andrew Chenge ni mzee anayefahamika kwa wanaofuatilia siasa nchini. Video yake ya hivi karibuni ambayo alikuwa anamuuliza kijana mmoja kama amesoma imenifanya nimtafute huko bungeni ana elimu.

Elimu yake imeanza kwa kuweka elimu ya msingi (CPEE) ila ghafla imeenda kwenye elimu ya sekondary ya kati, yaani advance, huku ikiwa haina taarifa alisoma wapi sekondary ya upili (CSEE)
Wote waliofanya mitihani mpaka mwaka 1969 ilitoka uingereza Cambridge siyo Kijitonyama.
Mtihani wa Cambridge ulikuwa wa nchi zote zilizokuwa kwenye himaya ya uingereza, inamaana na silabasi ilitoka huko huko. Pamoja na kutoka huko wapo watanzania waliopiga A masomo yote na kuwa wa kwanza duniani siyo taifa.
 
Kijana, hilo Baraza la Mitihani Tanzania (National Examination Council of Tanzania aka NECTA) ambalo wewe ndilo lilikutahini, lilianzishwa mwaka 1971. Kabla ya hapo kulikuwa na baraza la mitihani nchi zote za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda) ie The East Africa Examination Council ambalo lililosimamiwa na Uingereza na mitihani yake ilitungwa na Cambridge University huko London.

The Ordinary Level Certificate ilikuwa ina incorporate a General Certificate of Education (GCE) ambayo ni ya nchi zote za Jumuiya za Madola ya Muingereza zilizokuwa makoloni ya Muingereza.

Hivyo hata hiyo ACSEE ya Chenge ya mwaka 1968 ni Cambridge University na siyo ya NECTA kama ya kwako. Baada ya nchi zote za EA kujitoa kwenye baraza hilo la mitihani la Cambridge University mwaka 1971, ndipo kila nchi nchi hizo ikaanzisha baraza lake la mitihani na kutunga curriculum zake kwa wanafunzi wake wa shule za sekondari. Curriculum hizi hapa kwetu zimekuwa zilibadilishwa kila kukicha kwa matakwa ya wanasiasa hadi kupelekea elimu ya vijana wetu kushuka sana ukilinganisha na viwango vya kimataifa.

Kushuka huku kwa elimu ya vijana wetu ni hadi kwenye vyuo vikuu vyetu. Utakuta sasa mhitimu wa shahada ya udaktari wa binadamu hawezi kufanya operesheni ya kutoa kidole tumbo kwa mgonjwa wa acute appendicitis. Utakuta wahitimu hawa hawawezi kutoa mtoto kwa njia ya operesheni (Ceaserian Section) kwa mama mjamzito mwenye pingamizi la uzazi (obstructed labour) ili hali huko nyuma wahitimu ya diploma in medicine (AMO) waliweza kufanya operesheni hizo kwa ufanisi mkubwa.

Hivyo ndivyo kwa wahitimu wetu wa sasa kwa profession zote hususani wanasheria na wapelelezi wa kesi za jinai, wahandisi, wahasibu na kadhalika. Wanachokijua na walichobobea kwa sasa ni kupiga dili tu.
Point[emoji4][emoji106]
 
Back
Top Bottom