Historia ya Hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, Mti Mkavu (1940-2011)

Karata

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Posts
357
Reaction score
156

Hayati Luteni Jenerali Mayunga Mti Mkavu

Wakuu taarifa za uhakika nilizopata kutoka nchini India kuwa mpiganaji wetu shupavu na kiongozi mwadirifu, Meja Gerenali Silas Mayunga (Kushoto pichani akiwa na Gen. Musuguri) hatuko naye tena, amefariki leo katika hospitali ya Apollo New Delhi, India ambako alikuwa amelazwa tangu mwezi, Julai 2011.

Generali Mayunga atakumbukwa kwa mengi kwa jinsi alivyotumikia Taifa letu kwa utumishi uliotukuka, atakumbukwa daima kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin.

M/Mungu ailaze roho yake mahali pema.


KATIKA KUMBUKUMBU :MJUWE KAMANDA LUTENI JENERALI MAYUNGA


Musuguri (Kulia) akiwa na Silas Mayunga.Picha hii ilipigwa kipindi walipowasili nchini kutoka Vita vya Kagera

Itakumbukwa Novemba mosi, 1978, majeshi ya aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin yalivamia Mkoa wa Kagera. Uvamizi huo ulimsukuma Mwalimu Nyerere kuashiria ushindi kabla vita kuanza.

Nyerere aliashiria ushindi kabla vita kuanza akisema; "sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao." Hakika, kauli hii ilihitaji si tu risasi za kutosha, mizinga au makombora na silaha za kila aina kuisimamia, bali mashujaa wa mstari wa mbele vitani.

Miongoni mwa wapiganaji waliotwikwa dhima hiyo nzito ni pamoja na Luteni Jenerali Silas Mayunga, sambamba na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Watanzania kwa ujumla, waliotoa ng'ombe hata kuku kulisha wapiganaji uwanja wa mapambano.

Mstari wa mbele katika uwanja wa vita, Luteni Jenerali Silas Mayunga na wenzake, kazi ilikuwa moja tu-kufa au kupona ili kulinda si tu hadhi ya Tanzania, heshima ya wapenda haki duniani.

Ni vita hii ya Kagera ndiyo inayotajwa kumtambulisha zaidi Luteni Jenerali Mayunga ndani ya JWTZ na Jeshi la Uganda. Vita hiyo ilimpambanua ni mpiganaji wa aina gani akiwa mstari wa mbele.

MAYUNGA;Safari yake kijeshi imegusa nchi za Israel na Canada, akihitimu mafunzo ya kijeshi Julai 26, mwaka 1963 nchini Israeli na miaka 10 baadaye (1973), akafuzu kozi ya unadhimu na ukamanda wa jeshi nchini Canada. Kozi ya Ukamanda wa Juu wa Jeshi alihitimu mwaka 1974 nchini.

Juni 21, mwaka 1995, ni siku ambayo Mayunga alijiwekea rekodi binafsi ya kushika cheo cha juu jeshini, akipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na miezi sita baadaye (Desemba 31, 1995) alistaafu.
Mti mkavu akiwa jeshini

Mayunga ni kamanda kiongozi. Amekuwa Mkurugenzi wa Mafunzo makao makuu ya jeshi, Kamanda wa Brigedi ya 202 ya Tabora, na Kamanda wa Divisheni za 20 na 30 za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Huwezi kuzungumzia Operesheni Chakaza wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Idi Amin bila kumtaja kiongozi wa operesheni hiyo ambaye ni Luteni Jenerali Mayunga.

Katika Operesheni Chakaza, Mayunga ndiye aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya 206. Ndani ya Jeshi la Uganda Mayunga ana historia muhimu. Amekuwa Kamanda wa Kikosi Maalumu cha JWTZ nchini Uganda kati ya 1979 na 1980.

Lakini ukiondoa pilikapilika za kijeshi, Mayunga amekuwa Mkuu wa Mkoa Singida mwaka 1977 – 1978, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria mwaka 1989 hadi 1998 na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC) 1998 na 2002, alipostaafu.


Mwili wa Lt. Gen Silas Mayunga ukiwa kwenye Jeneza.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka Shada kwenye kaburi la Lt. Gen Mayunga

Luteni Jenerali Silas Mayunga, alifariki Agosti 5, 2011 nchini India,hakufa kwa risasi, mizinga wala milipuko yoyote pengine kama familia yake ilivyohofia kipindi yupo vitani bali alikufa akiwa kitandani wakati wa matibabu.

Ewe Kamanda Mayunga tunakulia ,tunasikitika kwa kifo, lakini tunafurahi umetimiza wajibu.

 
R.I.P Lt General Mayunga.

Steve Dii

 
RIP, naomba sababu za kifo chake.
 
dah !!! Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. tutakukumbuka daima mti mkavu!!!
 
Kifo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu wakati mwingine tukubali kuwa kifo ni kazi ya Muumba wala haiitaji sababu

Naikumbuka sana sanamu yake pale mjini Bukoba maarufu kama viwanja vya Mayunga,may God rest his soul in peace,Amen!!
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi
Poleni sana wafiwa.
 
RIP Major General Mayunga.Daima mchango wako utakumbukwa hasa vita vya Uganda.Naomba kuweka rekodi sawa nikotayari kusahihishwa Mayunga alikuwa na cheo cha Major General si Luten General.
 
RIP Major General Mayunga.Daima mchango wako utakumbukwa hasa vita vya Uganda.Naomba kuweka rekodi sawa nikotayari kusahihishwa Mayunga alikuwa na cheo cha Major General si Luten General.

Asante Mkuu kwa masahihisho
 
Mungu aiweke mahali pema peponi marehemu. Kwa kweli ni mfano wa kuigwa katika kullitetea taifa na uongozi bora uliotukuka
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa..... Dodosa basi na ile Trilioni 3 kama ni kweli au ilikuwa ni changamsha baraza maana jamaa aliyeiwasilisha mwanzoni katoka nduki hata hatujui ukweli wake
 
Nami nimemkumbuka jinsi viongozi wa majeshi yetu walivyokuwa na nidhamu na nidhamu hiyo kuisambaza hata kwa askari jambo lililopelekea kushinda vita. Pia pale mjini BKB kuna sanamu inayofanana na yeye ambayo wenyeji wanaita oluwanja lwa mayunga.
 
RIP Mti Mkavu (Hauchimbwi dawa).

Kama Mwanajeshi alikuwa juu sana ila alipoingia kwenye Siasa na kuwa Mkuuwa Mkoa, nafikiri ilimshinda (nisahihisheni kama nimekosea).
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa..... Dodosa basi na ile Trilioni 3 kama ni kweli au ilikuwa ni changamsha baraza maana jamaa aliyeiwasilisha mwanzoni katoka nduki hata hatujui ukweli wake

Mkuu mbona unachanganya habari tena! tuko kwenye masikitiko ya kuondokewa na mgpiganaji wetu shupavu, tafadhari husitibue hali ya hewa Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…