Historia ya Jackson Namfua

Historia ya Jackson Namfua

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alikuwa ni mchapa kazi sana na miongoni mwa Wakuu wa Mikoa waliokuwa kipenzi cha Baba wa Taifa miaka hiyo. Katika uongozi wake, alipandisha hadhi ya Wakulima wa zao la kahawa mkoani Kilimanjaro. Alipendwa na kukubalika sana na wana Kilimanjaro.

Mkuu huyu wa Mkoa alifariki kwenye ajali ya gari na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake Duniani.

Katika kumuenzi kwake, CCM iliamua kuupa uwanja wake wa Michezo uliopo Singida jina la kiongozi huyo. Uwanja huo unatambulika kama Uwanja wa Namfua.

Mwenye nyongeza anaweza akaendelea.
 
Alikua kiongozi kuanzia mwaka upi na alifariki mwaka gani? Tujuze kwa faida ya wengi!
 
Nikisikia alikuwa na mpango wa kuwanya ng'anya watawa wa Kilacha ardhi Tena kwa dharau alisema ardhi uwende kwa wanaozaa kuliko kuwaachia hawa matasa . Kiluchofuatia ni historia
Hebu fafanua zaidi inaonekan unamfahamu huyu mtu. Alikuwa mwenyeji wa wapi? Ilikuwaje hadi akawapa makavu namna hiyo watawa wa Kilacha?
 
Alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alikuwa ni mchapa kazi sana na miongoni mwa Wakuu wa Mikoa waliokuwa kipenzi cha Baba wa Taifa miaka hiyo. Katika uongozi wake, alipandisha hadhi ya Wakulima wa zao la kahawa mkoani Kilimanjaro. Alipendwa na kukubalika sana na wana Kilimanjaro.

Mkuu huyu wa Mkoa alifariki kwenye ajali ya gari na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake Duniani.

Katika kumuenzi kwake, CCM iliamua kuupa uwanja wake wa Michezo uliopo Singida jina la kiongozi huyo. Uwanja huo unatambulika kama Uwanja wa Namfua.

Mwenye nyongeza anaweza akaendelea.
aongoze kilimanjaro then uwanje uwepo Singida mbona tofauti, au lengo ilikuwa kuitangaza k.njaro mi siamini kama aliongoza mkoa mmoja tu
 
Mbona watu wazuri wote enzi za Nyerere walikuwa wanakufa kwa ajali na yeye haikumtokea? Rejea,Sokoine,Shekilango,Kreluu etc.
 
Back
Top Bottom