Historia ya Juma Nature

Historia ya Juma Nature

Inaendelea

JUMA NATURE NDANI YA WANAUME HALISI

Baada ya kuvunjika kwa kundi maarufu la Wanaume TMK, alitoa albamu akiwa peke yake aliyoipa jina la ‘Ubinadamu Kazi’, iliyosheheni nyimbo mbalimbali zikiwamo ‘Mtoto Idi’, ‘Dance With Me’, na ‘Salio Lovers’, aliipa albamu hiyo jina hilo kutokana na misukosuko aliyopitia hadi kufika hapo na kundi lililovunjika, ambapo licha ya kutamani liwepo aliumia kwa kutokuwapo Wanaume TMK.

“Ni kundi lililokuwa na nia njema, lilianza kama utani lakini mafanikio yalikuwa makubwa. Kuvunjika kwake kulinikera sana, hasa nikiamini kwa asilimia 100 kuwa ni binadamu wachache wasiokuwa na uelewa wala kujitambua wanatakiwa kufanya nini katika dunia, ndiyo waliochangia kulivunja. Nikaamua kuja na ‘Ubinadamu kazi’, ninasisitiza ni kazi kweli kweli, “anasema Nature.

Nature hakupenda kuwa peke yake katika muziki kwa kuwa aliamini wapo vijana wengi wanaopenda kazi hiyo na kwamba kuwa nao pamoja kimuziki ni kupigana na tatizo la ajira linaloongezeka nchini, hivyo akafikiria kuanzisha kundi lingine.

Wakati akiwaza hayo hakukaa na yeyote, bali aliwasiliana na baadhi ya vijana alikuwa nao katika kundi la mwanzo(TMK), ambao aliwaona wana uelewa na kuwaeleza azma yake hiyo, wazo hilo halikupingwa kutokana na uaminifu aliojijengea kwa vijana hao kipindi chote alichokuwa nao katika Kundi la Wanaume TMK, ndipo wakaanzisha kundi jipya na kuliita, Wanaume Halisi.

Wasanii alioanzisha nao kundi hilo kuwa ni pamoaj na Mzimu, Luteni Kalama, Dollo, BK ambaye kwa sasa ni marehemu, Kakaman, Bob Q , D. Chief, Abdu Malipo, Inspector Haroun na baadaye KR Mulla akajiunga nao kuongeza nguvu na kulifanya liwe na mwonekano tofauti na bora zaidi .

“Nakwenda nao pamoja kwa kuwa natambua mchango wa kila mmoja katika kundi. Nafahamu na kusisitiza hakuna aliye bora kuliko mwingine bali tunategemeana kwa namna moja au nyingine. Kwangu mimi, huo ndiyo uongozi,”anasema Nature maarufu pia kwa jina la msitu wa vina.

Kuanzishwa kwa kundi la Wanaume Halisi kulimpa wazo la kutoa albamu mpya aliyoipa jina la ‘History’ likieleza maisha yake tangu alipoanza muziki, katika albamu hiyo kulikuwa na nyimbo iliyojulikana kwa jina la ‘Mgambo’ ambayo ilibamba vilivyo kila kona ya Jiji la dar es Salaam na kujenga historia mpya kuwa kila anapotoka na kitu lazima aache gumzo.

Kila alichopata katika muziki, fedha na heshima kilimfanya awe karibu na jamii aliyoamini imemfikisha alipo akifafanua kuwa anawaheshimu ‘masela’, ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakifuatilia kazi zake hata kuwa ni sehemu ya maisha yao.

“Kuna vijana nawafahamu, wanatamani hata wabadili majina yao na kujiita Nature, wapo pia waliothubutu kufanya hivyo kwa kuthamini kazi yangu nawaheshimu sana, popote walipo napenda kuwaambia kwamba nafahamu kama wapo kwa ajili yangu na muziki wa nchi hii, “anasema Nature kwa hisia.

Tuzo alizowania na kushinda

Mwanzoni mwa mwaka 2006 alichaguliwa kuwania Tuzo za Msanii Bora wa Afrika zilizoandaliwa na M.T. V nchini Denmark, lakini alishindwa kuhudhuria kutokana na kutosa msaada wa Serikali.

“Uongozi wangu haukuwa makini kama nilivyosema awali, nilijitahidi kwenda wizarani mara kadhaa ili waniwezeshe kwenda safari hiyo, lakini ilishindikana. Hivyo, sikuhudhuria, niliumia sikuwa na jinsi zaidi ya kutokwenda,” anasema Nature anayejulikana pia kwa jina la Kibla.

Oktoba 11 mwaka 2007 alichaguliwa kuwania Tuzo Video Bora kutoka Afrika Mashariki kutokana na wimbo wake ‘Mgambo’
Kuchaguliwa kwake ilikuwa ni furaha na uthibitisho kuwa muziki wake unakua na kwamba alihakikisha hapotezi nafasi hiyo kwa kutokwenda kama ilivyokuwa kwa uteuzi wa awalinchini Denmark.
Tuzo hizo zilitolewa Johanesburg City Hall nchini Afrika Kusini ambapo aliibuka kidedea kutokana na video ya wimbo ‘Mgambo’.

Akiwa nchini humo baada ya kupata tuzo hiyo, vyombo vya habari vilikuwa vikimuuliza anazungumziaje ushindi huo, jibu lilikuwa moja tu ni kwa ajili ya Watanzania na kuitangaza nchi yake.
Studio iliyorekodi wimbo huo kuwa ni Bongo Records chini P- Funk, huku video ikitengenezwa na Visual Lab iliyokuwa chini ya uongozi wa Adam Juma.

INAENDELEA
 
Iliwachukua siku nyingi sana kwa Wanawume Halisi kutunga mashairi la wimbo mmoja na kwamba walifanya hivyo ili zidumu, hivyo shairi moja lilikuwa likimchukua hadi mwezi mzima kukamilisha kulitunga.

“Labda uwezo wetu ulikuwa mdogo, naona siku hizi mtu anatunga nyimbo 12 kwa siku. Mimi huwa nashangaa sana, au msanii mchanga anakwambia ana albamu nne ingawa inasikika kwa singo moja,”anasema Nature.

Ugumu wa kazi hiyo ulimfanya hata augue homa kila alipomaliza kutunga nyimbo za albamu, kutokana na uchovu uliotokana na kuishughulisha akili bila kutaka kubugudhiwa. Nature anaeleza kuwa ilifikia wakati alikwenda kushinda ufukweni mwa bahari ili kukimbia marafiki ambao wangemsumbua wakati anatunga mashairi.

“Hakuna albamu niliyotunga bila kupata homa, hasa ya ‘Ugali’ ndiyo niliumwa sana, ndiyo sababu nikiona mtu ametunga nyimbo zaidi ya 10 kwa siku, namshangaa na kuona ana uwezo sana, “anasema Nature.


“Hapa nawataka wasanii wenzangu kuwa makini na watu hawa wanaojifanya wanapenda kuendeleza muziki na wasanii

Kumwimbia Sinta

Kuhusu kumwimba msanii Sinta aliyekuwa mwenzi wake baada ya kuachana, Nature aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa hatua hiyo ilitokana na ujana lakini kwa sasa hawezi kufanya jambo kama hilo, akisema kushindana na mwanamke ni kupoteza muda.

“Alikuwa mpenzi wangu tulikwazana na maisha ya ujana kama unavyojua ‘nikamchana’. Sasa naangalia mbele, hilo siwezi tena na nimeshawavulia kofia kinadada,” anasema Nature.

Pia aliwahi kufafanua kuwa yaliyotokea yamepita na sasa wana uhusiano mzuri na kwamba wakati mwingine maishani wazo baya linaweza kuwa zuri.

MAFANIKIO YAKE

Tofauti na wanamuziki wengine Nature amepata mafanikio mengi katika muziki ikiwa ni pamoja na kumiliki nyumba nzuri ya kuishi, kumiliki gari zuri la kutembelea na kumiliki studio yake mwenyewe.

Baadhi ya wasanii waliofanya kazi katika studio yake inayosimamiwa na mtayarishaji Hunter G, ni pamoja na Kala Jeremiah, Squezer , Big Dog Poz na Spark Dog.

UVUTAJI WA BANGI

Kuhusu tuhuma za yeye na kundi la wanaume halisi kujihusisha na uvutaji bangi, Nature anasema: “Mambo mengi yalifanyika kipindi cha nyuma wakati hawajafahamu maisha ni nini ulikuwa ni ujana.

Katika kundi langu, huwezi kuona kijana ‘anakula ganja’ na akifanya hivyo watu wote wanamshangaa kwa kuwa sasa tumeshakuwa na tunaangalia nini kina faida na kisichokuwa na maslahi nasi tunakiacha,” anasema Nature huku anacheka.

Binafsi Nature anaamini kuwa mtayarishaji wa muziki P- Funk Majani kuwa kwake huyo ndiyo mtayarishaji mkali kati ya wengine, wakati alipofanya kazi na mtayarishaji huyo hakuwa akimtumia kujitangaza, bali alimshauri cha kufanya na yale ya kuacha.

“Achana na Majani, ukimwona kama siyo yeye, lakini ukiwa naye kwenye kazi ni makini sana. Kulikuwa na vitu ambavyo naliviamini, lakini nikifika kwake ananiambia hiki achana nacho na hiki fanya. Ilikuwa inakera, lakini faida nilikuwa naiona baadaye,” anasema Nature.
Nature amewahi kusimulia kuwa walikuwa wakiiona studio ya Majani kama wapo nyumbani kwani naye (Majani), alijivunia kuwa nao.

“Watayarishaji wa siku nyingi kama yeye walikuwa na heshima yao, hakuna uhuni zaidi ya kazi.
Kwa sasa sNature harekodi muziki kwake kwa sababu anamiliki studio yake.

Lakini bado ana hamu ya kufanya kazi na majani ya kushirikiana na anaamini kuwa atalitimiza hilo kama heshima kwake,”.

NDOTO ZA UBUNGE
Licha ya kuwa na mpango wa kugombe ubunge Temeke mwaka 2015 aliahirisha na nguvu zake amezitunza kwa ajili ya mwaka 2020.

“Ubunge Temeke, nitapita tu. Wenyewe wanajua kwamba mimi naweza kuwasaidia. Kwa sasa nimewaachia kina Profesa Jay na wengine wachukue nafasi hizo, ila miaka mitano ijayo usishangae ukanikuta pale mjengoni nimevaa suti nikiwakilisha wananchi. Kwa sasa sijaamua na malengo yangu ni mwaka 2020,” alisema Nature.

Ndoto zake ni kuwa akipata nafasi ya kuwa mbunge wa Temeke, jambo la kwanza kufanya kwa wananchi wake ni kushughulikia kero zilizopo hasa Barabara ya Mbagala.

“Barabara ndiyo kipaumbele, kwani mvua ikinyesha kidogo ni shida, ile hospitali ya Temeke ni ndogo, kumwona daktari ni kazi ngumu. Pia, soko siyo safi, inatakiwa vichimbwe visima na kujengwa vyoo kwani watu wanachafua sana mazingira. Temeke mitaro ni mibovu, mvua ikinyesha ni maafa kwa sababu watu wamejenga kiholela,”
 
Juma Nature a.k.a kiroboto msitu wa vina.

Huyu jamaa ana maneno Fulani basi burudani
 
Juma Nature a.k.a kiroboto msitu wa vina.

Huyu jamaa ana maneno Fulani basi burudani
Wimbo wa "mzee wa Busara" ulikuwa ni balaa na hatariiiii sana.

"...Basi mtaani mashaka hofu tele tele"....., kisa mzee wa Busara anapita.
 
Vantete Vakuntanzaniano Fomwamwentu Nontenaga Jibaba. Haya maneno sijajua huwa anamaanisha nini Juma Nature anayapenda sana. Yani burudani jinsi anavyoyatamka. Anayejua maana yake atufahamishe.
 
Umenifanya ni i google track ya 'history' ...thanks I got it..


Anyways...muda wake umeisha. Awe mshauri tu sasa. Ila tunammiss sana.
 
Wimbo wa "mzee wa Busara" ulikuwa ni balaa na hatariiiii sana.

"...Basi mtaani mashaka hofu tele tele"....., kisa mzee wa Busara anapita.
Ule wimbo sio mchezo. Ana wimbo unaitwa kidaruso amemshirikisha cannibal yule jamaa mkenya
 
Game jamaaa bado lipo sana,ndio maaana anamtaka D'Mond
 
Ningefurahi saaana kama ataitaja shule ya Sekondari aliyosoma. Mimi nilikuwa shabiki sana wa huyu bwana ila baada ya kuanza migogoro na wenzake huku kila wakati akiona anadhurumiwa ndipo taratiiibu nilipo mtafuta mkubwa Fella.
 
Vantete Vakuntanzaniano Fomwamwentu Nontenaga Jibaba. Haya maneno sijajua huwa anamaanisha nini Juma Nature anayapenda sana. Yani burudani jinsi anavyoyatamka. Anayejua maana yake atufahamishe.
mkuu bila kusikia haya maneno kwenye nyimbo ya sir nature ladha ya nyimbo itakuwa imepotea
 
Ugaliiii....washa video nimesema washa hukooooooooo dah! hili jimbo nikilisikiliza lazima nitoe kachozi kwa hisia
 
Back
Top Bottom