Saint Changas
Member
- Dec 19, 2015
- 24
- 32
Hii historia ya Nature ni batili. Yawezekana msimuliaji amepata taarifa alizozitumia katika andiko lake kutoka katika chanzo kimoja na ambacho si cha uhakika.
Nasema hivi kwa sababu, mambo mengi yaliyoelezwa na nyakati zake za kutokea vinakosa unasaba. Nianze na hili la Nature kujiunga na TMK mara baada ya kumaliza shule;
waliokua wakiufuatilia muziki tangu zamani wanajua kundi la TMK wanaume family liliundwa mwaka gani.
Na wanajua kuwa TMK ilianzishwa na wasanii kutoka makundi ya wachuja nafaka, Gangstarz with Matatizo(GWM) na Manduli Mob.
kimsingi sauti ya Nature kwenye redio ilianzia kwenye wimbo wa 'mtulize' wa Mabaga Fresh na baadaye katika wimbo wa 'jirani mtani' wa kundi ambalo kidogo nimelisahau jina kabla ya yeye (Nature) kutoka na wimbo wake binafsi uliokua ukiitwa jinsi kijana.
Mwandishi anaonekana anapenda kuandika na ni mwandishi mzuri kwa maana ya kutumia lugha kushawishi ila kasoro ya mwandishi ni kutokuandika ukweli. Jambo hili ni hatari hasa linapowafikia watu wasio na a,b,c ya jambo waliloandikiwa.