Historia ya Juma Nature

Hii historia ya Nature ni batili. Yawezekana msimuliaji amepata taarifa alizozitumia katika andiko lake kutoka katika chanzo kimoja na ambacho si cha uhakika.

Nasema hivi kwa sababu, mambo mengi yaliyoelezwa na nyakati zake za kutokea vinakosa unasaba. Nianze na hili la Nature kujiunga na TMK mara baada ya kumaliza shule;

waliokua wakiufuatilia muziki tangu zamani wanajua kundi la TMK wanaume family liliundwa mwaka gani.

Na wanajua kuwa TMK ilianzishwa na wasanii kutoka makundi ya wachuja nafaka, Gangstarz with Matatizo(GWM) na Manduli Mob.

kimsingi sauti ya Nature kwenye redio ilianzia kwenye wimbo wa 'mtulize' wa Mabaga Fresh na baadaye katika wimbo wa 'jirani mtani' wa kundi ambalo kidogo nimelisahau jina kabla ya yeye (Nature) kutoka na wimbo wake binafsi uliokua ukiitwa jinsi kijana.

Mwandishi anaonekana anapenda kuandika na ni mwandishi mzuri kwa maana ya kutumia lugha kushawishi ila kasoro ya mwandishi ni kutokuandika ukweli. Jambo hili ni hatari hasa linapowafikia watu wasio na a,b,c ya jambo waliloandikiwa.
 
Sasa mkuu si ndo uweke mambo sawa... huenda mtoa mada nae alichokoza tu.
 
Ni kweli kabisa hii taarifa unatakiwa uisome vizuri ila wimbo wa Jinsi Kijana Anavyobadili Tabia ulikuwa na vionjo vya 'Hiyo Mibangi Mnavuta ni Stimu za Burudani Kama Hii sio fani yako kwa kweeeli utaumbuka' ulikuwa na mashairi mazuri sana na ulionesha kwamba Juma Kassim Kirobotto ni mwimbaji mzuri lakini alivyoanza mambo mengine na ubishi usio na mashiko, ndipo alipojipeleka kuzimu.
 
Ningefurahi saaana kama ataitaja shule ya Sekondari aliyosoma. Mimi nilikuwa shabiki sana wa huyu bwana ila baada ya kuanza migogoro na wenzake huku kila wakati akiona anadhurumiwa ndipo taratiiibu nilipo mtafuta mkubwa Fella.

Kasoma Nur lyakeen pale Tandika kama Private Candidate.
"..Mtoto iddi kazua balaa..." sichoki kuisikiliza hii ngoma kwa kuwa kuna kichwa panzi wangu home ana character hizo kwa asilimia nyingi sana.
 
Kasoma Nur lyakeen pale Tandika kama Private Candidate.
"..Mtoto iddi kazua balaa..." sichoki kuisikiliza hii ngoma kwa kuwa kuna kichwa panzi wangu home ana character hizo kwa asilimia nyingi sana.
Ni kweli huyu bwana alikuwa mtunzi na mwimbaji mzuri.
Kama alikuwa Private Candidate, fuatilia maandishi ya huyo mleta uzi utagundua kuna sehemu ya historia inapindishwa sasa ni makusudi au bahati mbaya mimi na wewe hatujui ila kwa maneno yako mleta uzi hayuko sahihi
 

Namjua sana huyu Kijana Juma Nature enzi hizo akijiita Kibla ana mdogo wake kishawahi kumrusha kwny nyimbo anaitwa Rashed kwny nyimbo ya "Mzee wa busara" alikuwa anaishi kurasini "kijiji cha wavuvi" bhangi alikuwa anakuja kuvutia Uwanja wa Taifa kila jioni akiwa na ki baiskel chake cha watoto japo yeye ni jemba. Alivokula Uchi wa Sinta ndo Nuksi zikaanza.
 
Watu wengine wana mikosi!
 
Duh nakumbuka uzinduzi wa nature na solo thing
Kilimanjaro pool side....watu shazi tulijaaa ...baadaye wakaja wahuni wa feri wakakinukishaa show ikavurugikaaa...kila mtu alitoka duki mbaya
Hehehe
 
Kiroboto kama Kubenea kumbe.
Mbona hasemi shule aliyosoma!
Sio kama Kubenea... Nature kasoma Thaqafa sema ingawaje historia ni ya kwake mwenyewe lakini imekosewa kosewa utafikiri imesimuliwa na mtu mwingine na sio yeye mwenyewe! Kwa mfano anasema "ndo akajiunga kundi la Wanaume Family!" wakati baada ya yeye kufanya kazi bila ya management ya kueleweka ndipo akapata management ya Fella wakati huo akiwa yeye peke yake! Baadae, wakaingia GWM kundini kabla ya akina Chege na ndipo Wanaume Family ikazaliwa! Wakati huo tayari Nature alishakuwa na jina kubwa ambalo lilianza kuchomoza rasmi na ngoma ya Mtulize!
 
Kwenye INAUMA SANA kuna line Nature anasema..Sinta alipigwa denda hadi gari likagoma kwenda..Ili denda inaonekana lilikuwa amazing sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…