Historia ya kweli ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda

Historia ya kweli ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda

niw
Ndugu mtoa uzi na swali je imekuaje bizimungu kuendelea kuwa rais mpaka mwaka 2000 wakati kagame alikua tayari kaisha iweka nchi chini ya himaya yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Niwie radhi kujibu japo hujaniuliza mimi kumsaidia mtoa mada ni kwamba Kagame ni mtu mwenye akili nyingi sana hakutaka mara moja jumuiya ya kimataifa aonekane ana uroho wa madaraka zaidi ya yote alifanya makusudi sababu Bizimungu vile alikuwa Mhutu basi waliobaki kwa vyovyote wataona hakuwa anapigana kwa nia ya watusi watawale nia yake ni kukomesha mauaji na kuwafanya wahutu na watusi wote wawe kitu kimoja.Pia angekuwa mtu wa visasi angeamuru auwawe hii ni mbinu nzuri sana
Alivyo na akili nyingi alijua kuwa iko siku watampa uraisi tu na ikawa hivyo hata hivi karibuni kabla ya kuapishwa alisema uraisi aliupata kwa bahati tu hakutegemea.
 
Nimejifunza kuwa katika wakoloni wote Wabelgiji walikuwa watu wabaya sana.Wasingekuwa wabelgiji yote haya yasingetokea Rwanda,Burundi na Congo hadi leo.Wabelgiji ndio walimuua Lumumba hiyo laana bado inatembea.Wabelgiji wasingewatenga Watusi na kuwaita wao ni bora na kuwapima hadi urefu wa pua zao kusingekuwa na migogoro yote hii ya ndugu hawa wahutu,watusi na watwa.
Mtizamo niliokuwa nao kwa Kagame umebadilika kabisa namuona kama masiha aliyetumwa na Mungu kukomboa watu.Vita vya Kagera alisaidia,vita vya Frelimo alisaidia.
Kwa mtizamo wangu ni the best Tactical military intelligency leader Africa Mashariki nzima na maziwa makuu.Ningekuwa na contact naye ningempa salamu zangu za pongezi ila ataona hapa kupitia watu wake.
Kitu kingine nilichojifunza kuna mahali inafika ni faida mtu mmoja afe ajili ya kuokoa maelfu ya watu.
Rwanda sasa hivi kuongelea neno Mimi Mhutu au mimi Mtusi ni dhambi kubwa wote ni wanyarwanda poleni sana ndugu zetu yote haya wakoloni ndio walituletea shida yasingetokea ombeni mungu muishi pamoja.
 
Back
Top Bottom