Historia ya kweli ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda

Historia ya kweli ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda

Mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994 yakisaidiwa sana na kanisa katoliki ambalo TEC ni sehemu ya kabisa hilo.

Mapadre wake na maaskofu huko Rwanda walishiriki kukusanya watu wanaokimbia machafuko na kuwaweka ndani ya makanisa yao wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.Walipokwisha kumaliza kufanya hivyo wakawaita wauaji na kuruhusu waanze kuwabaka na kuwauwa wahanga ndani ya makanisa hayo ya wakatoliki.

Haya ni mambo ambayo TEC hawatataka myajue na hawataki kuyasema na sina kumbukumbu kama wamewahi kuyatolea tamko maana mwaka 1994 TEC ilikuwepo na ilikuwa bize na majukumu yake ya kutoa matamko.

Inachokifanya TEC kwenye tamko lake na maagizo yake kuwa makanisa yote yasome waraka ule leo kwenye misa zao huko makanisani maana yake ni kuwa wamejipanga kuleta uchochezi kwa staili ile ile ya Rwanda. Wanachochea watu kwenye mambo ambayo tayari mamlaka za kisheria zimeshayapitisha kwa kufuata utaratibu ili kutokee machafuko kama wakivyoyaratibu huko Rwanda miaka hiyo.

Najiuliza hivi BAKWATA nao wakitoka hadharani na wakatoa waraka kuwa mkataba ule ni sawa na wakaagiza usomwe kwenye misikiti yote nchini , je? Nini kitatokea? Au TEC wanadhani hatuna akili za kujua kuwa walichofanya kanisa katoliki Rwanda ndiyo wanachotaka kukifanya Tanzania?

Au wanaringia uzoefu wao kwenye mauaji ya Rwanda basi wanadhani kila kitu wanachotaka wao lazima kifanyike na kisipofanyika basi watafanya kama Rwanda ? Sawa mna uzoefu na shughuli hizo za nauaji ya hakaiki kama mlivyofahya Rwanda,lakini hamna haki ya kujifanya mnawawakilisha watanzania kwenye jambo lolote , nyie mnawakilisha wakatoliki wenzenu tu.m huko makanisani na hamtakiwi kujipa usemaji wa watanzania wote.

Lini TEC waliwahi kutoa tamko kulaani mapadre wenzao waliouwa maelfu ya watu kule Rwanda? Lini waliwahi kutubu kutumia makanisa yao na kuyageuza kuwa uwanja wa kuulia watu waliokuwa wanataka hifadhi na kunusubu maisha yao?

Au hawa siyo mapadre wenu wa katoliki? Au historia hii mmeisahau na hamtaki watu waijue? Sisi tunaikumbuka na tunawakumbusha kwa sababu hili ndilo lengo lenu na mnachotaka ni kuchukua mbinu zile zile za Rwanda kulitumbukiza taifa kwenye machafuko kwa kisingizio cha mkataba wa bandari.

Tuna taarifa zenu kijana wenu anayetaka kubadili dini kuwa mkatoliki bwana January Makamba yuko nyuma ya hizi vurugu ndiye mtoa fedha za mkakati huu na mmesikika mkisema lazima mvuruge
/m -frustrate mchakato wa kupata Rais 2025 ili January Makamba awe mgombea kutoka kabisa lenu la katoliki.

Kama mliweza kusababisha na kusaidia mauaji kufanyika Rwanda basi hilo hamtakaa muweze kulifanya Tanzania. Endeleeni na chokochoko zenu na hayo matamko halafu tuone mwisho wake.


Baraza la maaskofu lingeweza kujikita kwenye vifungu vinavyoonekana vina kasoro kuliko kubeba makando kando mengine yanayoharibu ujumbe na nia njema ndani yake.

#KigogoMediaUpdates
Ule waraka unaletaje vurugu! hata Bakwata watoe tu si watanzania!
 
pwani ni tanzania sio Rwanda mr mud
Pwani ni sehemu ya tz lkn pwani si tanganyika.

Asili ya watanganyika wa watz kutoka interior (mikoa ya bara).

Tanganyika ni jimbo ktk nchi congo.

Katika kuelekea kuunda serikali ya majimbo, majimbo yote yatakuwa na uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ndio maana tunasema #pwaniSiTanganyika
 
Pwani ni sehemu ya tz lkn pwani si tanganyika.

Asili ya watanganyika wa watz kutoka interior (mikoa ya bara).

Tanganyika ni jimbo ktk nchi congo.

Katika kuelekea kuunda serikali ya majimbo, majimbo yote yatakuwa na uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ndio maana tunasema #pwaniSiTanganyika
Acha uongo..
 
Pwani ni sehemu ya tz lkn pwani si tanganyika.

Asili ya watanganyika wa watz kutoka interior (mikoa ya bara).

Tanganyika ni jimbo ktk nchi congo.

Katika kuelekea kuunda serikali ya majimbo, majimbo yote yatakuwa na uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ndio maana tunasema #pwaniSiTanganyika

Hatuwezi kukulaumu kwa upuuzi huu unaouandika hapa. Tatizo huna elimu wala upana wa mambo. Elimu za kipuuzi huko madrassa ndio mnalishwa mimavi namna hii. Sehemu ya tanganyika haiwezi gawanywa na kuitwa pwani. Hayo ni matamko ya kuonesha ukanda flani kama vile kaskazini, kanda ya nziwa, nyanda za juu kusini. Namashaka na asili yako huenda wewe ni mwarabu wa kizazi chotara usie hata na ndugu arabuni
 
1994....Magerwaa Rwanda nipo na Abdalah Kitambi(nimepotezana nae kwa sasa).....tupo na scania 113...310.....tunarudi Tanzania.....maiti zimelazwa juu ya barabara....tuna amriwa tuzikanyage...daaah...akili ziliniruka kabisa...sikuwa kwenye hali ya kibinadamu ..........tukio hili lilinifanya nionje pombe na fegi....lakini Mungu alinijalia nikaweza kuacha..."binadamu ni kiumbe hatari sana".
 
Hatuwezi kukulaumu kwa upuuzi huu unaouandika hapa. Tatizo huna elimu wala upana wa mambo. Elimu za kipuuzi huko madrassa ndio mnalishwa mimavi namna hii. Sehemu ya tanganyika haiwezi gawanywa na kuitwa pwani. Hayo ni matamko ya kuonesha ukanda flani kama vile kaskazini, kanda ya nziwa, nyanda za juu kusini. Namashaka na asili yako huenda wewe ni mwarabu wa kizazi chotara usie hata na ndugu arabuni
Nilipaswa kukupuuza. Hata hivyo nafsi ikasema nikuelimishe.

1. Unaumwa ugonjwa wa Stockholm. Na matokeo yake unawapenda waliokudhulumu na kuwachukia wanadhulumiwa.

Pwani si Tanganyika ni vuguvugu la ukombozi kutoka ktk serikali ndani ya serikali ya ccm kupitia imani ya kijamaa. Ujamaa ni laana kwetu.

Lkn kwa kuwa uko contaminated na athari za Ujamaa. Leo uko tayari kuwatukana wanaotaka kujivua na kuiondoa imani hii ukanda wa pwani.

Tutauondoa kwa kutumia sera ile ile ya chadema.

Kutoa uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe ndani ya majimbo 10 ya chadema
 
Nilipaswa kukupuuza. Hata hivyo nafsi ikasema nikuelimishe.

1. Unaumwa ugonjwa wa Stockholm. Na matokeo yake unawapenda waliokudhulumu na kuwachukia wanadhulumiwa.

Pwani si Tanganyika ni vuguvugu la ukombozi kutoka ktk serikali ndani ya serikali ya ccm kupitia imani ya kijamaa. Ujamaa ni laana kwetu.

Lkn kwa kuwa uko contaminated na athari za Ujamaa. Leo uko tayari kuwatukana wanaotaka kujivua na kuiondoa imani hii ukanda wa pwani.

Tutauondoa kwa kutumia sera ile ile ya chadema.

Kutoa uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe ndani ya majimbo 10 ya chadema

Hata baba yako na babu yako waliikuta ardhi hii ni moja na kamwe haiwezi kugawanywa. Pwani ni sehemu ya Tanganyika wala sio sehemu ya dubai au oman. Ujamaa upi bwana kobazi? Una matatizo ya akili pia udumavu wa akilini na mwili.
 
Hata baba yako na babu yako waliikuta ardhi hii ni moja na kamwe haiwezi kugawanywa. Pwani ni sehemu ya Tanganyika wala sio sehemu ya dubai au oman. Ujamaa upi bwana kobazi? Una matatizo ya akili pia udumavu wa akilini na mwili.
Kupitia fikra mpya kwa maana ya falsafa mpya yawezekana.

Kabla ya Tanganyika kulikuwa na dola kubwa moja. Iliyoanzia Somalia, Kenya, tz, znz, mozambique, hadi Zimbabwe. Walikuwa na pesa yao. Dola hiyo ikijulikana kama kilwa. Leo kiko wapi.

Hata hivyo unahitaji kusoma sana vitabu vya falsafa, Kwani kusoma sana ni kuona sana.

Nikuulize, unaishi dar au wapi.
Nikuulize; kwa mara ya kwanza uliwaona watu wa pwani ulipokuja dar.
Je pindi ulipowaona uliona wanafanana na watu wa miji ya kwani kule interior huko ileje, tukuyu, ngarinalo nk.

Bila shaka jibu ni hapana.

Ndio maana nasema sisi ni watu wa pwani. Wakati wakoloni sisi hatukuwa sehemu ya watanganyika.

Kuhusu Ujamaa na itikadi yake ya Usekyula hii kwetu ni jinamizi. Limeturudisha nyuma sana. Namna pekee la kuliangamiza ni kuuondoa mfumo wa serikali kuu na kusaport mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe
 
1994....Magerwaa Rwanda nipo na Abdalah Kitambi(nimepotezana nae kwa sasa).....tupo na scania 113...310.....tunarudi Tanzania.....maiti zimelazwa juu ya barabara....tuna amriwa tuzikanyage...daaah...akili ziliniruka kabisa...sikuwa kwenye hali ya kibinadamu ..........tukio hili lilinifanya nionje pombe na fegi....lakini Mungu alinijalia nikaweza kuacha..."binadamu ni kiumbe hatari sana".
Duh!Kwa hiyo mlizikanyaga mkuu?.
 
Kupitia fikra mpya kwa maana ya falsafa mpya yawezekana.

Kabla ya Tanganyika kulikuwa na dola kubwa moja. Iliyoanzia Somalia, Kenya, tz, znz, mozambique, hadi Zimbabwe. Walikuwa na pesa yao. Dola hiyo ikijulikana kama kilwa. Leo kiko wapi.

Hata hivyo unahitaji kusoma sana vitabu vya falsafa, Kwani kusoma sana ni kuona sana.

Nikuulize, unaishi dar au wapi.
Nikuulize; kwa mara ya kwanza uliwaona watu wa pwani ulipokuja dar.
Je pindi ulipowaona uliona wanafanana na watu wa miji ya kwani kule interior huko ileje, tukuyu, ngarinalo nk.

Bila shaka jibu ni hapana.

Ndio maana nasema sisi ni watu wa pwani. Wakati wakoloni sisi hatukuwa sehemu ya watanganyika.

Kuhusu Ujamaa na itikadi yake ya Usekyula hii kwetu ni jinamizi. Limeturudisha nyuma sana. Namna pekee la kuliangamiza ni kuuondoa mfumo wa serikali kuu na kusaport mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi au kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe

Una matatizo ya akili pia haupo timamu kimaarifa. Unajumaa hata maana ya falsafa kweli?. Nina shaka na race yako toka awali huenda wewe ni chotara wa kiarabu, babu zako walibaka bibi zetu ndio mkatoka nyinyi ambao wengi wenu hamna hata ndugu huko arabuni.
Eti watu wa pwani ndio kina nani hao maana bara la africa kusini mwa jangwa la sahara ni waafrika halisia. Hao machotara vizazi vya wabakaji sio race ya Africa wewe pia ukiwemo. Viongozi wa kiserikali si unawaona? Je ni race ya pwani, Jibu ni Hapana. Dar es salaam yote imejengwa na kutawaliwa na watanzania weusi tii hata wavaa kobazi mamia kwa mamia wameuza majengo hao hapo kkoo kwa wachaga, wakinga, waha. Watu wa pwani ndio wapi hao, Hawa wazee wa dar es salaam weusi tiiiii au machotara feki?
 
Una matatizo ya akili pia haupo timamu kimaarifa. Unajumaa hata maana ya falsafa kweli?. Nina shaka na race yako toka awali huenda wewe ni chotara wa kiarabu, babu zako walibaka bibi zetu ndio mkatoka nyinyi ambao wengi wenu hamna hata ndugu huko arabuni.
Eti watu wa pwani ndio kina nani hao maana bara la africa kusini mwa jangwa la sahara ni waafrika halisia. Hao machotara vizazi vya wabakaji sio race ya Africa wewe pia ukiwemo. Viongozi wa kiserikali si unawaona? Je ni race ya pwani, Jibu ni Hapana. Dar es salaam yote imejengwa na kutawaliwa na watanzania weusi tii hata wavaa kobazi mamia kwa mamia wameuza majengo hao hapo kkoo kwa wachaga, wakinga, waha. Watu wa pwani ndio wapi hao, Hawa wazee wa dar es salaam weusi tiiiii au machotara feki?
Uliyoyasema yote yanakaribia ukweli kwa 90%.

Ajenda iliopo na si siri.... pwani si Tanganyika ni ajenda yenye lengo la kui conquer daru salaam urudi miongoni mwetu.

Tuilinde na tuwadhitibi ninyi mulioyoiteka, ninyi munayoitawala dar kwasasa.

Hili litawezekana kupitia kuundwa kwa chama kipya cha kisiasa ngome yake ukiwa ni mwambao wa tz.

Hili yawezekana kwa kuwatumia watu wa pwani kwa kuwa wana falsafa na itikadi inayofanana. Tofauti na yenu
 
Uliyoyasema yote yanakaribia ukweli kwa 90%.

Ajenda iliopo na si siri.... pwani si Tanganyika ni ajenda yenye lengo la kui conquer daru salaam urudi miongoni mwetu.

Tuilinde na tuwadhitibi ninyi mulioyoiteka, ninyi munayoitawala dar kwasasa.

Hili litawezekana kupitia kuundwa kwa chama kipya cha kisiasa ngome yake ukiwa ni mwambao wa tz.

Hili yawezekana kwa kuwatumia watu wa pwani kwa kuwa wana falsafa na itikadi inayofanana. Tofauti na yenu

Pwani ni Tanganyika ila wewe sio mtanganyika maana huna ndugu weusi wewe ni uzao feki hata babu zako historia yao huijui na hujui wako wapi binafsi yako na wenzako hata koo wala kabila nchi hii nyinyi vyote hamnavyo. Ajenda iliyopo toka zamani ni kupoka mamlaka toka kwenu na hilo limefanikiwa kwa 100% kwasasa hamna ushawishi, nguvu Hadi mamlaka. Babu zako feki walifanywa vibaya na karume, baba wa taifa genius kambarage aliwatupilia mbali mlipojaribu kuinua midomo hayati mkapa aliwaonesha rangi halisi ya wamiliki wa tanganyika.

Lakukwambia ni kuwa huna/hamna uwezo wala nyenzo za kuigawa pwani kwanza pakuanzia huna watu huna mitaani hadi serikalini au uraini. Chakukushauri fuga sana kuku kuliko kuwa na mawazo ya kijinga na kipuuzi namna hio.

Hujui maana ya itikadi, hujui maana ya falsafa pia hujui nini unataka kwa lugha ya kawaida tunasema unatapa tapa. Dar es salaam kwa 99% ni waafrika weusi tiiiiiiiii. Mbwa nyinyi 1% mtafanya nini, jaribu hata kujamba uone kipigo chake.
 
Pwani ni Tanganyika ila wewe sio mtanganyika maana huna ndugu weusi wewe ni uzao feki hata babu zako historia yao huijui na hujui wako wapi binafsi yako na wenzako hata koo wala kabila nchi hii nyinyi vyote hamnavyo. Ajenda iliyopo toka zamani ni kupoka mamlaka toka kwenu na hilo limefanikiwa kwa 100% kwasasa hamna ushawishi, nguvu Hadi mamlaka. Babu zako feki walifanywa vibaya na karume, baba wa taifa genius kambarage aliwatupilia mbali mlipojaribu kuinua midomo hayati mkapa aliwaonesha rangi halisi ya wamiliki wa tanganyika.

Lakukwambia ni kuwa huna/hamna uwezo wala nyenzo za kuigawa pwani kwanza pakuanzia huna watu huna mitaani hadi serikalini au uraini. Chakukushauri fuga sana kuku kuliko kuwa na mawazo ya kijinga na kipuuzi namna hio.

Hujui maana ya itikadi, hujui maana ya falsafa pia hujui nini unataka kwa lugha ya kawaida tunasema unatapa tapa. Dar es salaam kwa 99% ni waafrika weusi tiiiiiiiii. Mbwa nyinyi 1% mtafanya nini, jaribu hata kujamba uone kipigo chake.
Hahahahaha ndugu unafurahisha sana. Hujui mikakati, we subiri mafungu yaingie.
Si unasema hatuna ndugu,

Ndugu Pesa ina nguvu hata wewe utaimba nyimbo tunapotaka uimbe
 
HUU NI MFULULIZO WA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA

Sehemu ya kwanza

“..kama unasoma ujumbe huu, muda huu… uko mpweke! Pengine ushahidi pekee uliobakia ni kijipande hiki cha maandishi. Sijui kama kuna yeyote kati yetu aliyesalimika kufika kizazi chenu mwaka huu mtakaosoma andishi langu. Sijui hata kama tumeshinda au tumeshindwa vita tunayopigana sasa hivi. Sijui, lakini naamini mwaka huu mliopo nyinyi sasa mwaweza kuwa na jibu sahihi. Vyovyote vile lakini jambo lililo dhahiri ni kwamba hakuna yeyote wa kizazi chetu mliye naye sasa hivi kwenye miaka yenu muusomapo ujumbe huu. Kwa hiyo wacha niwaeleze sisi tulikuwa akina nani, na kwa namna gani tulipambana mpaka tone la mwisho la damu mwilini mwetu ili kutetea kizazi chetu kisifutwe juu ya uso wa dunia. Wacha niwaeleze namna ambavyo japo tulikamuliwa damu mpaka kutiririka kufanya mifereji lakini lakini tulisimama kutetea kizazi chenu na ninyi watoto wetu. Wacha niwaeleze kisa kilichotikisa ulimwengu. Wacha niwaeleze kuhusu mifereji ya damu kwenda Ethiopia.!”

March 21, 1994 maeneo ya Uganda ambayo yanapakana na Rwanda, katika ziwa viktoria serikali ilituma vikosi vya jeshi kudhibiti eneo hilo kwa hali ya dharura. Agizo hili la serikali kutuma jeshi halikuwa kwa ajili ya kidhibiti eneo hilo kutoka kwa adui bali agizo lilikuwa ni kudhibiti eneo hilo dhidi ya maiti, maiti za binadamu. Sio maiti mbili au tatu, si mamia bali maelfu ya maiti za binadamu ambazo zilikuwa zinaingia ziwani Victoria zikiletwa na maji ya mto Kagera.

Maiti hizi zilikuwa nyingi kwa maelfu kiasi kwamba mapaka zilikuwa zinafanya maji yatoe harufu. Serikali ya Uganda ilituma jeshi eneo hili ili kudhibiti eneo hili maji yake yasitumiwe na wananchi kwa matumizi ya nyumbani au shughuli za uvuvi. Lakini jeshi lilikuwa eneo hili ili kuhakikisha kuwa taharuki iliyozuka baada ya maelfu ya miili hii kuonekana haigeuki na kuvuruga amanai katika eneo hili. Lakini pia jeshi lilikuwa hapa ili kubaini miili hii ilikuwa inatoka wapi.

Kadiri ambavyo jeshi la Uganda lilivyokuwa linafuatilia kwa kurudi nyuma kufuata mto Kagera ndivyo ambavyo walizidi kubaini kwamba maiti hizo zinaletwa na maji kutoka tawi la mto Kagera lililopita kusini mwa Rwanda. Na kadiri ambavyo walizidi kufuata chanzo cha maiti hizo zinakotoka ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia Rwanda na maji ya mto rangi yake kuwa nyekundu zaidi.

Wanajeshi wa Uganda ambao walishiriki kwenye ukaguzi huu wa mto huu wanakiri kwamba licha ya baadhi yao kupigana mstari wa mbele kwenye vita mbali mbali lakini hakuna yeyote kati yao ambaye aliwahi kushuhudia ukatili mkubwa wa kiasi hiki.

Siku hii jeshi la Uganda linakisia kwamba waliokota si chini ya miili elfu kumi ya binadamu na yote ilionekana kuletwa na maji ya mto Kagera kutoka nchini Rwanda. Ajabu ni kwamba miili yote hii ilikiwa inamfanano fulani. Maiti zote zilikuwa za watu warefu, wembamba, wenye nyuso ndefu na pua za kuchongoka. Haikuhitaji kufikiria sana kufahamu kuwa maiti hizi zilikuwa za watu wa kabila la Tusi (Tutsi).

Miezi kadhaa baadae ndipo ambapo jeshi la Uganda na ulimwengu wote walikuja kuelewa kwa nini maiti zilikuwa zinatupwa mto Kagera. Ni ujumbe gani ambao ulikuwa unajaribu kutumwa.

Kwamba Watusi nchini Rwanda walikuwa waapenda kujisifu kuwa mababu zao wana asili ya nchi ya Ethiopia. Kitendo hiki cha watesi wao kuwatupa mtoni, walikuwa wanawaua na wakiwa wanatupa maiti zao mto wanawaambia kwamba “wanawasafirisha warudi kwao Ethiopia ambako wamekuwa wakijisifu ndio asili yao.”

Sio kwamba jeshi la Uganda hawakuwa na taarifa juu ya hali tete iliyopo Rwanda kwa muda wa karibia wiki nzima iliyopita bali hawakujua kama hali hiyo tete ilikuwa ni ya kinyama kiasi hicho.

Wanajeshi hawa wa Uganda walikuwa wameshikwa na bumbuwazi na vihoro vilivyo wapasua mioyo kwa kuona miili hii elfu kumi ya binadamu isiyo na uhai. Kitu ambacho walikuwa hawakijua na hakuna ambaye alidhahania ni kwamba ndani ya siku mia moja zijazo ulimwengu ulikuwa unaenda kushuhudia moja ya tukio la kikatili zaidi tangu kuubwa kwa ulimwengu. Karibia maiti za binadamu milioni moja zikiwa
zimetapakaa mitaani nchini Rwanda iking’ong’wa na nzi na kuliwa na mbwa.

GENESIS

Rwanda: Kabla ya Ukoloni


Asili rasmi kabisa ya watu wa kwanza kuishi katika eneo ambalo leo tubalitambua kama nchi ya Rwanda ni watu wa kabila la ‘Twa’ (Watwa). Kabila hili la wawindaji si la kibantu bali ni sehemu ya makabila yanayotambulika na wanahistoria kama ‘pygmy’ ambao sifa yao kuu ni ufupi. Mtu mzima anayetoka makabila ya namna hii anakadirwa kuwa na wastani wa urefu chini ya sentimita 150. Watwa waliishi Rwanda enzi za kale sana miaka ya 8000 BC na 3000 BC.

Kuanzia miaka ya 700 BC mpaka 1500 AD makabila ya Kibantu kutoka maeneo ya jirani yalianza kuhamia eneo hili.

Kuna nadharia mbali mbali kuhusu ni namna gani haswa makabila haya ya kibantu yalihamia hapa na baadae kupelekea kutokea Makabila ya sasa ya Wahutu na Watusi.

Nadharia ya kwanza inadai kwamba; Wahutu ndio walikuwa wa kwanza kuhamia eneo hili na kuanzisha shughuli za kilimo. Baadae watu wenye asili ya Ukushi (Watusi wa sasa) nao wakahamia kwenye eneo hili na kulitawala.

Nadharia ya Pili inadai kwamba; kuna uwezekano kwamba Watusi si wakushi bali ni wahamiaji tu kutoka maeneo ya jirani kipindi hicho cha kale ambao walihamia na kujichanganya na jamii waliyoikuta hapo (Wahutu) lakini wao walikuwa wafugaji. Chini ya nadharia hii inadai kwamba kuibuka kwa Wahutu na Watusi hakukutokana na kuwa na utofauti wa kinasaba au asili ya mababu bali ulitokana na utofauti wa kimadaraja/matabaka ya kijamii.
Tabaka la wale walio wa daraja la juu ambao walikuwa wafugaji walijitanabaisha kama Watusi wakati ambapo tabaka la chini ambao walikuwa wakulima walijitanabasha kama Wahutu.

Makabila haya yote matatu, Watwa, Wahutu na Watusi wanazungumza lugha moja na kwa wote kwa pamoja wanajulikana kama ‘Banyarwanda’.

Idadi ya watu ilipoongezeka katika eneo hili walianza kujitambua kupitia makundi madogo madogo yaliyoitwa ‘Ubwoko’ au ‘koo’ kwa kiswahili. Ilipofika katikati ya miaka ya 1700 koo nyingi ziliungana na kuunda ‘Falme’.
Moja ya Falme ambazo zilikuwa imara zaidi ulikuwa ni ‘Kingdom of Rwanda’ ambayo watawala wake wote walitokea katika koo ya Kitusi ya Nyiginya.

Ufalme huu ulifikia kileleni kipindi cha utawala wa Mfalme Kigeli Rwabugiri chini ya falsafa yake ya kujipanua na kuteka falme nyingine na kuzifanya sehemu ya Kingdom of Rwanda.

Chini ya Mfalme Rwabugiri alianzisha mfumi wa kiuchumi wa ‘ubuhake’ na baadae ‘uburetwa’.
Katika mifumo yote hii miwili, iliwanufaisha zaidi Watusi na kuwafanya Wahutu kama vijakazi wao kuwafanyia kazi za uzalishaji na kuwa askari vitani kwa ujira wa kupata fursa ya kumiliki mifugo na kutumia ardhi.

Watusi walipaa juu zaidi na kuwa raia daraja la kwanza ma Wahutu kubakia kuwa tabaka la chini kabisa ndani ya Kingdom of Rwanda.

Rwanda: Wakati wa Ukoloni

Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 ulilitoa eneo hili kuwa koloni la nchi ya Ujerumani. Wajerumani walitawala eneo hili kwa kushirikiana na Mfalme na hivyo kuwapa wepesi wa kutawala koloni bila kuwa na askari wengi wa kijerumani ndani ya ardhi ya Rwanda. Yuhi V Musinga ndiye walikuwa Mfalme wa Rwanda kwa kipindi hiki na anakumbukwa zaidi kwa kuwapokea Wajerumani kwa mikono miwili.

Ikulu ya Mfalme wa Rwanda maeneo ya Nyanza

Wajerumani ndio walikuwa watu wa kwanza kuanza kuwapandikizia Watusi kasumba ya kuwa wao si Wabantu. Wakoloni wa Ujerumani ndio ambao walieneza propaganda kwa kuwafundisha Watusi kwamba kutokana na tafiti zao za kina wamegundua kwamba wao (Watusi) mababu zao wa kale walihamia eneo hilo kutokea Ethiopia. Hivyo wakawashawishi kuamini kwamba Watusi wana vinasaba vya ‘uzungu’ (Caucasian) na hivyo ni wao pekee ndani ya Rwanda walistahili kupata nafasi za ajira kusaidizana kazi na wazungu chini ya utawala huo wa Wajerumani.

Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Ubelgiji iliziteka Rwanda na Burundi kutoka mikononi mwa Ujerumani na mwaka 1919 League Of Nations ilizifanya rasmi nchi hizo kuwa makoloni ya Ubelgiji.

Mwanzoni Wakoloni wa Ubelgiji walianza kuitawala Rwanda kwa mtindo ule ule wa kushirikiana na Ufalme lakini baadae wakajilimbikizia madaraka yote ya kutawala kama ambavyo walifanya kwenye koloni lao la Kongo.

Baadae wakaanza ‘kutaifisha’ mali za Wanyarwanda katika mfumo wa kufanana kabisa na mfumo wa asili wa uburetwa na walioathirika zaidi na kampeni hii ya utaifishaji walikuwa ni Wahutu.
Ardhi yao ilinyang’anywa… Mifugo ilitwaliwa na kuwafanya Wahutu kuwa si tu vijakazi wa Wakoloni bali pia vijakazi wa Watusi.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930s Ubelgiji walifanya upanuazi mkubwa wa sekta ya Elimu, afya na ajira za umma. Lakini wanufaika wakuu walikuwa ni Watusi.

Mwaka 1935 Ubelgiji walifanya kitu ch a ajabu sana ambacho kilipanua zaidi mpasuko wa kijamii na kitabaka uliopo ndani ya Rwanda. Walianzisha mfumo wa raia wote kuwa na vitambulisho. Vitambulisho hivi viliwatambua raia wote katika makundi manne kulingana na makabila yao. Watwa, Wahutu, Watusi na Raia wa kuomba (Naturalised).

Kutokana na Watusi kuwa ndio raia wa daraja la kwanza na tabaka la juu huku Wahutu wakiwa ni watu hafifu wa kudharaulika nchini humo, ilifikia hatua Wahutu wenye mali au ushawishi walikuwa wanahonga fedha ili kupatiwa vitambulisho vya Kuonyesha ni Watusi na watawala hawakuwapa Utusi kamili bali waliwapa ‘utusi wa heshima’ (Honorary Tutsi).

Hadhi ya Wahutu wote iliendelea kushuka kwa kasi wakionekana ni kabila na kizazi cha “Washenzi” huku Watusi wakionekana ndicho kizazi cha “wastaarabu” na kabila lenye darja.

Lakini kuna suala ambalo lilifanyika mwanzoni likionekana kuwa na manufaa makubwa lakini kadiri siku zilivyokwenda lilianza kuwa kama mkuki mgongoni. Kanisa Katoliki.

Kanisa Katoliki lilikuwa limeenea sana nchini Rwanda na raia wake wengi wakiwa ni waumini wa kanisa hilo. Tukumbuke kwamba tangu kipindi hicho Wahutu ndio walikuwa idadi kubwa zaidi ya raia wote ndani ya Rwanda. Hii ilimaanisha pia kwamba waumini wengi wa kanisa Katoliki walikuwa ni Wahutu.

Kwa kiasi fulani ndani ya kanisa Katoliki mapadri na watawa wengine walikuwa wanajisikia hatia kuacha waumini wao kuwekwa kwenye kundi la kizazi cha “washenzi” na kudharaulika ndani ya jamii. Kwa hiyo zikaanza juhudi za makusudi za kanisa katoliki kutoa elimu kwa vijana wenye asili ya Kihutu.

Baada ya miaka kadhaa kukaanza kuwepo walau kidogo uwiano wa wasomi wa Kihutu na Kitusi.

Mwaka 1957, mwezi March kikundi cha wasomi na watu wenye ushawishi wenye asili ya Kihutu walifanya jambo la “kimapinduzi” ambalo lilipanda mbegu mpya kwenye nafsi za watu wa kabila na kizazi cha cha Kihutu. Waliandaa waraka ulioitwa _'Manifeste des Bahutu' (Bahutu Manifesto).
Huu ndio ulikuwa waraka wa kwanza rasmi kubainisha kwamba Wahutu na Watusi ni mbari (race) mbili tofauti.

Katika waraka huu, wasomi hawa na watu hawa wenye ushawishi walijenga hoja kuu kwamba… Watusi wanapaswa kutoka kwenye jukumu lao walilojivesha la kuwa watawala wa Rwanda na badala yake nafasi hiyo ya kutawala Rwanda wapewe Wahutu. Hoja yao hii waliijenga kwenye nadharia ambayo wenyewe waliita “Statistical Law”, kwamba kitakwimu Wahutu ni wengi mno kushinda Watusi. Si sawa wakiendelea kutawaliwa na kufanywa vijakazi na Watusi.

Wanasema kwamba kabla kibanda cha nyasi kuungua kwanza utaanza kukiona kinafuka moshi. Kuna vugu vugu lilianza chini kwa chini ndani ya Rwanda.

Waraka huu… Bahutu Manifesto, ulitoka tarehe 4 March mwaka 1957. Japokuwa ilikuwa ni miaka takribani 37 kabla ya mwaka 1994, lakini ndio siku ambayo mbegu ya mauaji ya kimbari ilipandwa.

Usikose sehemu inayofuata.

Itaendelea...
Wafanganye hao hao mauaji mpange wenyewe na muandike wenyewe
Tunaijua hiyo
 
NI MFULULIZO WA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA

Sehemu ya tano.


Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Historia yetu ambayo watoto wetu wanafundishwa mashuleni na kuandikwa kwenye vitabu imechujwa mno kiasi kwamba inakuwa kama ni hadithi tu za kusadikika.
Kwa mfano kama umebahatika kuijui historia ya ukweli kuhusu Vita ya Kagera kisha ukasoma 'version' ambazo zimeandikwa kwenye vitabu na kuaminishwa kwa umma, machozi yanaweza kukutoka.

Ubaya ni kwamba hata wale ambao wamebahatika kujua ukweli halisi wa matukio na vilivyo nyuma ya pazia hawawezi kuthubutu kutia mkono na kuandika kile ambacho wanakijua.

Ndio maana naamini ni busara hata kwangu pia niandike kwa sehemu kile ambacho historia zetu hakivisemi lakini pia ni muhimu kuandika kwa "ustaarabu" kwa faida ya pande zote.

Kutengenezwa kwa Jasusi Paul Kagame

Katika sehemu iliyopita nilieleza kwamba, Paul Kagame mwaka 1977 alitembelea nchi ya Rwanda ambapo hakuwahi kuikanyaga tangu alipokuwa mtoto wa miaka miwili tu. Paul Kagame alifanya safari hii kutokana na kukosa amani ndani ya moyo wake. Alikuwa anatafuta 'kusudi' lake la maisha. Katika kipindi hiki alikuwa amempoteza baba yake mzazi na pia rafiki yake kipenzi Fred Rwigyema alikuwa amepotelea kusikojulikana.

Kwa hiyo Paul Kagame alienda Rwanda kwa ajili ya 'soul searching'. Alikuwa anataka kupata hamasa kwenye roho yake ili aweze kujua kusudi la maisha yake.

Kutokana na historia ya familia yake kuwa na ushawishi kwa kiasi fulani (nilieleza kwamba baba yake ana undugu wa kiukoo na Mfalme Kigeli na mama yake ana undugu wa damu na Malkia wa mwisho wa Rwanda) kwa hiyo hizi safari zake za Rwanda alizifanya kwa siri kubwa pia ukizingatia kwamba serikali ilikuwa makini sana na watusi ambao wako nje ya Rwanda kama wakimbizi kutokana na harakati zao na kiu yao ya kutaka kuipindua serikali mara kwa mara.
Safari hii ilikuwa ya maana sana kwa Kagame na alijenga 'connection' ambazo zilikuja kumsaidia sana miaka ya baadae kwenye harakati zake.

Mwaka 1978 alifanya safari nyingine kwenda Rwanda na safari hii hakupitia mpaka wa Uganda bali aliingia kupitia Zaire (Congo). Kwa wiki kadhaa ambazo alikaa Kigali kwa siri kubwa, alitumia muda huo kuimarisha 'connection' ambazo alikuwa nazo na pia kusoma hali ya kisiasa na uimara wa serikali.

Safari hizi mbili ziliamsha hari kubwa mno katika nafsi ya Paul Kagame. Aliona kwa uhalisia kabisa mateso na manyanyaso ambayo watusi walikuwa wanapitia nchini Rwanda. Akajihisi kabisa kwamba alikuwa ana jukumu la kufanya kitu kuyamaliza mateso hayo.

Aliporejea nchini Uganda Kagame akageuka kama mwanaharakati hivi katika kambi za wakimbizi akihamasisha vijana wenzake kujizatiti na kuweka mipango ya kuikombia Rwanda.

Wakati huo huo, rafiki yake Fred Rwigyema ambaye alipotea bila yeyote kujua ni wapi alikuwa ameelekea… alikuwa nchini Tanzania katika kambi ya FRONASA chini ya uongozi wa Yoweri Musseveni ambao walikuwa wanaweka mikakati ya kumuondoka madarakani Dikteta Idd Amin.

Habari kuhusu kijana mahiri, mwanaharakati Paul Kagame zilimfikia Yoweri Musseveni na alitamani awe sehemu ya 'timu' yake.
Ndipo hapa ambapo Fred Rwigyema ambapo ndio kwanza alikuwa amerejea Tanzania kutoka msumbuji ambako alipelekwa na Musseveni kwenye mafunzo ya pamoja na wapiganaji FRELIMO juu ya vita za msituni…alitumwa kwenda nchini Uganda kwa ajili ya masuala kadhaa lakini mojawapo ilikuwa kumshawishi Paul Kagame kujiunga na wapiganaji wa Yoweri Musseveni walioko nchini Tanzania.

Sasa basi…

Kuna mahala mkoani Morogoro, sitapaja kwa jina au exactly sehemu gani… lakini ni nje ya mji kidogo kuna 'Espionage Farm' ya siri ambayo mwaka 1978 Paul Kagame na maafisa kadhaa wa kikundi cha FRONASA walikuwa recruited na kupata mafunzo ya Ujasusi na masuala ya Intelijensia.

Niseme kwamba Paul Kagame ni moja ya maafisa bora na hodari kabisa kuwahi kuzalishwa na Idara yetu Usalama wa Taifa.

Kagame amewahi kutumia kwenye 'high profile missions' kadhaa lakini kubwa zaidi ni ile ambayo aliongoza kikosi cha Intelijensia ya wapiganaji wa UNLA (Ugandan National Liberation Front) katika vita ya Kagera.

Tofauti na historia ilivyoandikwa kuhusu vita ya Kagera, lakini ukweli na uhalisia ni kwamba wapiganaji wa UNLA ambao walikuwa ni zaidi ya 20,000 walikuwa ni kiungo muhimu sana katika ushindi wa vita ya Kagera. Suala hili tutalizungumzia siku moja kama tukipata wasaa wa kuichambua vita ya Kagera.

Kuna kikao cha siri sana kilifanyika pale Moshi ambacho kinajulikana kana "Moshi Conference" ambacho kiliudhuliwa na watu adhimu kabisa wapatao 28 na mmoja wao alikiwa Paul Kagame.
Katika kipindi hiki, Rais ambaye alikuwa amepinduliwa na Amin na kukimbilia Tanzania, Bw. Milton Obote alikuwa na kikundi chake cha wapiganajia ambacho alikiita kwa jina la Kiswahili "KIKOSI MAALUM" ambacho makamanda wake walikuwa ni Tito Okello na David Oyite Ojok. Hawa nao pamoja na Obote mwenyewe walikuwepo kwenye kikao cha mjini Moshi.
Pia Yoweri Musseveni alikuwepo kuiwakilisha FRONASA. Pia walikuwepi wanaharakati wengine mashuhuri kama vile Akena p'Ojok, William Omaria, Ateka Ejalu, Godfrey Binaisa, Andrew Kayiira, Olara Otunnu pamoja na baadhi ya 'wakubwa' kutoka kwenye vyombo vya ulinzi vya nchi yetu ambao kwa sababu ya 'staha' sitaandika majina. Jumla walikuwa watu ishirini na wanane.

Kikao hiki kilizaa mpango mkakati wa kijeshi ambao ndio ulitumika kwenye vita ya Kagera na kumshinda Amin. Paul Kagame ndiye ambaye alibebeshwa mzigo wa mikakati ya Intelijensia ya kijeshi.

Octoba 1978 tukaingia vitani dhidi ya majeshi ya Amin. Licha ya swahiba wake Kanali Muammar Gaddafi kutuma wapiganaji 2,500 pamoja na silaha nzito za mivita na za kisasa kwa kipindi hichi kama vifaru aina ya T-54, T-55, magari ya kivita ya kisovieti aina ya BTR APC na Grad MRL pamoja na ndege za kivita aina ya MiG 21 na ndege hatari za kivita (supersonic bombers) aina ya Tu-22 kumsaidia Amin… ajabu ni kwamba licha ya majeshi ya amini kuwa imara kiasi hiki kwa maana ya vifaa vya kivita lakini mwanzoni mwa mwezi April 1979 tulimpiga Amin mpaka "Ikulu" na kumlazimu kukimbilia Libya kwa swahiba wake Gaddafi na baadae kukimbilia Saudi Arabia.

Siku moja kabla ya kutangaza kuisha kwa vita ya Kagera, yaani April 10 Tanzania tukamsimika Yusufu Lule kuwa Rais mpya wa Uganda. Yusufu Lule ameishi sana hapa Tanzania hasa baada ya Idd Amin kuingia madarakani.
Pamoja na hilo lakini akina Musseveni nao waliunda chombo chao cha kijeshi ambacho kiliitwa National Consultative Commission (NCC). Hiki kwa kiasi fulani ndio walikifanya kama chombo chenye maamuzi ya mwisho kuhusu nchi.

SILAHA NZITO ZA KIJESHI AMBAZO UGANDA ILIPOKEA KUTOKA KWA KANALI GADDAFI


Gari za kivita aina ya BTR APC

Miezi miwili tu baada ya majeshi ya Tanzania kumsimika Yusufu Lule kuwa Rais, kukaanza kutokea mvutano mkali kati ya NCC ya kina Musseveni na Rais Yusuf Lule. Mvutano huu ulikuwa ni juu ya mamlaka ya Rais ambayo NCC walimuona Lule kama anavuka mipaka yake. Lule naye kwa upande wake alikuwa anaonekana hataki nchi kuingozwa na jeshi (NCC).
Hatimaye tarehe 10 June mwaka huo 1979 NCC kwa ushawishi mkubwa wa Musseveni wakamuondoa madarakani Godfrey Binaisa kuwa Rais mpya wa Uganda.

Kimsingi Binaisa alikuwa kama 'kikaragosi' tu lakini kiuhalisia NCC ndio walikuwa wanaongoza nchi.

Lakini taratibu naye utamu wa madaraka ukaanza kumkolea.

Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki chote Milton Obote bado alikuwa nchini Tanzania hajarejea Uganda.
Kulianza kuzuka taarifa kwamba mnadhimu mkuu wa jeshi Brigedia Jenerali David Oyite Ojok ambaye kipindi cha vita ya Kagera alikuwa kamanda wa jeshhi ka pamoja la Tanzania na UNLA, alikuwa anafanya maandalizi ya kuhakikisha Obote anarejea Uganda.

Jeneralari Ojok anatokea eneo la kaskazini mwa Uganda kama ilivyo kwa Obote. Licha ya Ojok kuanza mikakati ya kumrudisha Uganda Obote lakini pia kwenye jeshi nyadhifa za juu zote alikuwa anahakikisha zinashikiliwa na watu wanaotoka ukanda wa kaskazini mwa nchi.

Harakati zote hizi Binaisi aliziona kama juhudi za kumuondoa madarakani ili kusafisha njia kwa Obote kurejea madarakani.

Mwezi May 1980 Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Ojok kwenye cheo cha Mnadhimu mkuu wa jeshi.
Suala hili lilipingwa vikali na NCC na wakafikia hatua ya kumuondoa madarakani Rais Binaisa na kuunda tume maalumu ambayo waliita Presidential Commision ambayo ndiyo ilifanya kazi ya kuongoza nchi badala ya Rais.
Tume hii wanakamati wake walikuwa ni Museveni, Oyite Ojok, Okello na Muwanga.
Muwanga alipewa cheo cha uenyekiti wa tume japokuwa kiuhalisia wenye nguvu za ushawishi kwenye tume walikuwa ni Museveni na Ojok.

Baada ya hapa ndipo ambapo hasa umahiri wa Paul Kagame unaonekana. Ikumbukwe kwamba wakati yote haya yaliendelea Paul Kagame alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye jeshi la Uganda kutokana na umahiri wake wa masuala ya Intelijensia. Kwa hiyo yeye ndiye ambaye alikuwa anawashauri ni nani anafaa kuwa Rais na nani hafai.

Baada tu ya nchi kuanza kuongozwa na Tume maalumu niliyoitaja hapo juu, Ojok akaanza tena mipango ya kumrejesha Milton Obote ndani ya Uganda. Ilikuwa wazi kwamba Ojok alikuwa anataka Obote ashike madaraka. Lakini watu wengi wa kabila la Baganda/Waganda walikuwa wanampinga Obete kwa kuwa yeye ndiye ambaye alimpindua Mfalme wao wa Baganda miaka kadhaa nyuma na kushika Urais kabla ya yeye pia kupinduliwa na Ids Amin. Kwa hiyo kulikiwa na mvutano kati ya watu wa maeneo ya kaskazini na kusini mwa Uganda.

Ndipo hapa ambapo Paul Kagame akaona fursa. Kwamba 'vita ya panzi, furaha ya kunguru'.
Yoweri Museveni yeye hatokei Kusini wala Kaskazini mwa Uganda… yeye amezaliwa na kukulia eneo la magharibi mwa nchi linalopakana na Rwanda sehemu inaitwa Ntungamo. (Hii ni moja ya sababu ya baadhi ya watu kuamini ana asili ya Kitusi).
Kwa hiyo huu ugomvi wa watu wa kaskazini na wa kusini haukuwa na mslahi nao kabisa. Ndipo hapa kwa kushauriana na Paul Kagame wakaanza michakato ya siri pembeni ya kujitenga na NCC na UNLA japokuwa Museveni alikuwa na ushawishi kwenye vyombo vyote hivyo.

Hatimaye mwaka 1980 Milton Obote alirejea Uganda na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu mwaka huo na "kushinda". Matokeo ya uchaguzi yalipingwa vikali na watu wengi akiwemo Yoweri Museveni.

Ndipo hapa ambapo Yoweri Museveni, Pual Kagame na Fred Rwigyema pamoja na Waganda wengine thelathini na saba tu walianzisha kikundi chao cha kijeshi walichokiita National Resistance Army (NRA) lengo kuu likiwa ni kumuondoa madarakani Rais mpya Milton Obote.

Kikundi hiki kiliendesha mapigano ya msituni dhidi ya majesho ya serikali kwa karibia miaka sita.
Licha ya udogo wake kwa idadi ya watu (japo baadae waliongezeka kuzidi watu arobaini wa awali) lakini ufanisi wao kwenye kushambulia kwa uhodar na kulichosha jeshi la serikali ulikuwa wa hali ya juu. Miaka hii sita ya kupambana na majeshi ya serikali yalidhihirisha namna ambavyo Paul Kagame alikuwa ni nguli wa 'psychological warfare' ambayo pia ilikuja kudhihirika kipindi cha mauaji ya kimbari (tutaongelea zaidi tukifika hapo).

Katika kipindi hiki cha vita kwa masuala ya kijeshi Paul Kagame alikuwa mtu muhimu na mwenye kuheshimika zaidi na wapiganaji wa NRA kuzidi hata Museveni mwenyewe. Nyadhifa zao ndani ya NRA zilikuwa karibia kwenye usawa mmoja.

Kwa upande wa jeshi la serikali hali ilianza kuwa tete. Kukaanza kutokea mifarakano ya kikabila kati ya wenyewe kwa wenyewe. Kaskazini mwa Uganda kuna makabila makuu mawili, Walangi (kabila wanalotokea Obote na Ojok) na Waacholi (kabila la Tito Okello ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kamanda wa jeshi).
Askari wengi wa miguu walikuwa ni Waacholi na ndio ambao walikuwa wanakufa zaidi kwenye vita hiyo dhidi ya NRA. Walangi wengi walikuwa ni maafisa wa jeshi na 'Special Forces'. Kwa hiyo askari wa miguu wakaanza kushinikiza serikali ifanye mazungumzo na NRA na kumaliza vita.

Yoweri Museveni na wapiganaji wa NRA msituni

Serikali ikafanya shingo ngumu na kukataa.

Wanasema lakuvunda halina ubani, mwezi Desemba 1983 Oyite Ojok alifariki kwa ajali ya ndege ambayo kuna kila dalili ya mkono wa Kagame. Kwa kipindi hicho Ojok ndiye alikiwa mkuu wa jeshi la Uganda. Ilikuwa inategemewa Obote amteue Tito Okello au mwenzake mwingine aliyeitwa Bazilio Olara-Okello (hakuna undugu wa damu kati yao licha ya kufanana ubini japo wanatokea kabila moja la Waacholi) ambaye naye alishiriki vita ya kumuondoa Idd Amin. Lakini ajabu Obote alimteua afisa wa chini kabisa wa jeshi aliyeitwa Smith Apon-Achak ambaye anatoka kabila lake la Walangi kuchukua nafasi ya Oyite Ojok. Hii iliwafanya wanajeshi wenye asili ya kabila la Waacholi kumchukia Obote na serikali yake na hatimaye miaka miwili baadae kumpindua kutoka madarakani.

Baada ya Miltob Obote kupinduliwa na jeshi kutoka madarakani kukaanza mapigano baina ya vikundi vya msituni kila kimoja kikitaka kushika usukani wa kuongoza nchi. Ndipo hapa yalifanyika maongezi ya pamoja baina ya vikundi vyote vya msituni nchini Kenya chini ya Rais Daniel Arap Moi ili kuleta suluhu na kuweka muelekeo mpya wa nchi ya Uganda.

Tarehe 29 January mwaka 1986 Yoweri Kaguta Museveni akaapishwa kuwa Rais mpya wa Uganda.

Paul Kagame akateuliwa na Rais kuwa Chief of Millitary Intelligence.

Swahiba wake Fred Rwigyema akateuliwa kwenye wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.

Pia baraza la mawaziri lilikuwa limejaa watusi kibao.

Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa Paul Kagame alikuwa ameiweka Uganda kwenye kiganja chake cha mkono japo hakuwa Rais. Lakini mtandao wa ushawishi ambao alikuwa ameujenga ndani ya serikali ya Uganda, baraza la mawaziri na kwenye jeshi ulikuwa ni mkubwa na una nguvu zaidi hata ya Yoweri Museveni ambaye aliapishwa kuwa Rais. Uzuri ni kwamba Museveni anafahamu umahiri wa Paul Kagame na hakutaka kutengeneza mvutano wowote naye kwa kuwa alikiwa anajua lengo kuu la Kagame lilikuwa ni lipi. Kagame hakuwa na nia yoyote ile ya kuwa Rais wa Uganda au kuendelea kuliendesha jeshi la Uganda. Ndoto yake ilikuwa ni moja tu, ndoto ambayo aliipata mwaka 1978 alipotembelea kwa siri nchi yake ya Rwanda, kwamba siku moja anataka kuwaokoa ndugu zake watusi kutoka kwenye unyanyasaji, kuuwawa, kudhalilishwa na mateso ambayo walikuwa wanapitia katika nchi yao.

Na sasa alikuwa amekamilika kwa kila kitu. Alikuwa na uzoefu wa kutosha. Alikuwa na weledi wa kutosha, tunaweza kuthubutu kusema kwamba katika kipindi hiki hakuna ambaye alikuwa anaweza kufikia daraja la umahiri wa Kagame katika masuala ya Ujasusi Afika Mashariki yote.

Lakini pia alikiwa na ushawishi katika nchi za kimakakati ambazo zinapakana na Rwanda, kwa maana ya Congo (huku aliwapeleka wapiganaji wa NRA kupata mafunzo ya siri ya Special Forces kipindi cha mapigano ya miaka 6 msituni dhidi ya majeshi ya serikali ya Milton Obote). Lakini pia alikuwa na ushawishi nchini Tanzania (mtoto wetu tuliyemfunza wenyewe ujasusi na alitusaidia sana kwenye vita ya Kagera). Na hakuna haja hata ya kusema kiwango cha ushawishi ambacho alikuwa nacho nchini Uganda.

Mbele yake kulikuwa na jambo moja tu la mwisho ambalo alikuwa anatamani litimie kabla hajaondoka juu ya uso wa dunia. Kuiweka nchi ya Rwanda mkononi mwake.

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
Duhh mleta mada nimegundua usemi usemao no evidence no right to speak
na namanisha unaweza mlaumu Kagame kwa mambo kadhaa kumbe ana historia muhimu sana kwa nchi ya Tanzania,Uganda,Msumbiji na hata Congo ndio maana namuita brilliant solder anayeona mbali fikiria mtu uko nchi za watu kupigana ajili yao kumbe lengo ni kupata mafunzo hii ni akili
 
Mtoa mada ahsante sana wako wanaokukatisha tamaa kuwa umeiba mada ya bold lakini wanashindwa kujua ukweli kwamba mambo mengi tunayofanya ya kiuandishi ni copy and paste.
Hata wagunduzi wa sayansi wengi wamefanya makubwa yao kwa ku copyy kwa watangulizi wao ni jambo la kawaida suala ya la kumuomba bold kuwa ume m quote tunawachia wenyewe.
Ngoja nikapumzike nitaendelea kesho sehemu ya 12
Nikifika mwisho nitatoa mawazo yangu kwa ujumla
 
Back
Top Bottom