Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Post bank kumbe kutamu 3%,Akikimbia unampatia wapi?? Hiz banks mbona zinapigika haswa...kuna bnk moja nimechukua pesa bila dhamana alafu fresh kias kwamba nikiamua hata mahakaman hawatashinda...posta bank wametoa fedha kibao zaid ya bil 300 kwa wafanya biashara wadogo na wakati lakin watu bado hawajielewi...riba asilimia 3...bado watu wanalia umasikin...hovyo kabisaa
Mbona bado upo kwenye umasikini bro?Mkopo silipi. Serikali ililipa. Make nilikuwa napokea sms ya makato Kila mwezi.. Hadi 2017.. yoga wako ndo umaskn wako.
Hahaha! Nilikua najitafuta tu halafu yule maza alikua bado hajaiona dunia.....Yaani ukampeleka mama wa watu kwenye site za mapilau una dhambi we binti[emoji16][emoji16]
wanafunz 300@1,200,000 ada/yr lets say, turnover ya 360m/yr kibongobongo si haba mkuuMbona bado upo kwenye umasikini bro?
Kama ukiwa ni mtumishi na ukachukua mkopo kwa dhamana ya salary nadhani watakusubiria kwenye pensheni yako,labda iwe hujakaa muda mrefu..Akikimbia unampatia wapi?? Hiz banks mbona zinapigika haswa...kuna bnk moja nimechukua pesa bila dhamana alafu fresh kias kwamba nikiamua hata mahakaman hawatashinda...posta bank wametoa fedha kibao zaid ya bil 300 kwa wafanya biashara wadogo na wakati lakin watu bado hawajielewi...riba asilimia 3...bado watu wanalia umasikin...hovyo kabisaa
Lakini si atakuwa ameacha makato yake ya pensheni?Sasa mtu kaacha kazi,mkopo atalipa vipi wakati kazi hana?
Okay so makato ya pensheni yalikuwa yanaendelea kama kawa Huku salary jamaa wanaigonga hahahaaaaa...mimi nilivyotoka serikalini niliomba secondment kwa sababu iko kisheria. Pia niliwahi kuchukua mkopo na nikawa sijaumaliza kuuulipa. Huko nilikoenda baada ya mambo kuwa mazuri nikawa naendelea kuulipa mkopo wao ili huko usoni wasijenikata mafao yangu. Hoja yangu ni kwamba huko uzeeni haujui utaishiaje hivyo ikiwa mafao yako yatafyekwa while you need them most inaweza kuwa mtihani...Sikuwahi kuulipa. Ila Hadi 2016. Mshahara ulikuwa unaingia halimashauri wakawa wanaula . Magu ndo amekuja kuondoa Kwa operation hewa ya wafanyakazi kazi. Make nilikuwa napokea sms ya makato ya mkopo wa Bank
It is ur biography,ccm inaingia vp hapo.hacha ujingaMimi sio mwandishi mzuri. Lakini nitaeleweka Kwa hiki kisa changu Cha kweli.
Nilimaliza masomo yangu ya degree udsm mwaka 2011 nakuajiriwa mwaka 2012. Huko shinganya vijijini kama Mwalimu. Hii kazi niliifanya Kwa mda wa mwaka mmoja na nusu tu. Nikaacha na kurudi mitaan. Baada ya kuona ndoto zangu za kuishi maisha ninayoyataka hazitatimia.
Siku Moja nilikuwa naenda mjini Kwa kipewa lift. Jamaa aliyenibeba tulianza kupiga story za maisha.
Akanambia kwenye shughuli zake Kwa mwezi zinamwingizia faida ya zaidi ya ml 2.. na ana elimu ya darasan la 7. Nikatafakari Sana na jambo hili likaniumiza Sana. Mimi na degree yangu nalipwa laki 4. Hii ikanifanya kufikiria Sana. Kumbe nafanya kazi ya kitumwa. Nikajiuliza maswali mengi Sana.
Hivi watanzania tupo wangapi? na walioajiriwa Kwa hizi kazi za kitumwa ni wangapi? Si hata hatufiki mil Moja.? Nikiacha kazi maisha hayaendi?
Baada ya kujiuliza maswali. Niliamua kuacha kazi. Ila Sasa naachaje Ili hali Sina mtaji. Wazo nililolipata ni kuchukua mkopo bank. Kweli nikachukua mkopo wa ml 10 na ndo ukawa mtaji wangu wa kuanzia maisha mapya nje ya ajira.
Maisha mapya yanaanza Kwa kuanza kuzunguka Kampala Kwa week nzima nikisaka furusa za Biashara na nikafanikiwa. Kuanza Biashara ya kushona masweta na school uniform Kwa Ujumla. Kumbuka sikuwa na hii elimu Wala ujuzi. Biashara ilienda vizur Sana na ndani ya miaka 4 Toka 2013 mwezi wa 8 mpaka 2016. Niliweza kupata faida kubwa Sana make nilikuwa mwenyewe kwenye game kabla mafisi hawajaingialia na kuweka mitaji Yao mikubwa. Ndani ya mda huu wa miaka minne niliweza kujenga nyumba mbili. Ya kuishi na Moja ya kazi zangu. Na kuweza kununua usafiri wangu na gari ndogo ya kusambaza mzigo. Wateja wangu wakubwa walikuwa shule za private.
Changamoto zinaanza
Mwaka 2017 Biashara ikaanza kuyumba Kwa shule nyingi kuyumba kiuchumi kutkona na Heka Heka za anko Magu. Matajiri wakaweka wakavamia Biashara. Biashara ikayumba Sana. Na kufikia 2019 ikafa rasimi. Nikafilisika kabisa. Nikabaki na nyumba tu. 2019. Nikawa nakosa hata nauli ya kunitoa home kwenda kutafuta mishe. Ila wazo la kutafuta kazi ya kuajiriwa niliapa kulikataa kabisa. Jamaa angu mmoja akanitafutia kazi. Ambayo ilikuwa na salary ya laki 6 Kwa mwezi. Nikaikataa jamaa angu akanilaumu Sana. Nikamwambia hapa ni mjini nitapambana Hadi tone langu la mwisho lakni sio kuajiriwa.
Mwaka 2019 mwishon napata wazo la kuanzisha shule ya day care na chekechea kwenye jengo langu nililokuwa nafanyia kazi zangu. Kweli naanza watoto wanne tu. Nikiwa Mimi ndo Mwalimu wao. Kwa ada ya elfu 30 Kwa mwezi. Nikapamba kufanya marketing kubwa Kwa kufundisha vizur. Wazo jingine nilanikjia Kwa kutafuta Mwalimu wa kikenya kweli nafanikiwa kumpata. Watoto wakaanza kuongezeka. Kufikia January 2020 tunapofungua shule tulifanikiwa kuwa na watoto 50. Nikapambana Sana katikat ya changamoto. Nikafanikiwa kupata kiwanja na kuanza kujenga shule.badaa ya watoto kuwa wengi na eneo halitoshi la kujenga shule. Kufika 2023 nikapata usajiri. Na mwaka huo huo nikawa na watoto wa kumaliza darasa la Saba Kwa watoto 12 ambao niliwatoa shule zingine. Watoto walianza kuhamia kwangu hata kabla sjawa na usajili wa serikali. Wazazi waliniamini Kwa kile nilichokuwa nafundisha watoto wao. Nilifanya kazi ya kuajiri walimu wazuri. Tukisidiana Kila palipo hitajika.
Kufikia Hadi Sasa nimeisharudi barabarani Kwa kufungua shule yangu Hadi Sasa nikiwa na watoto zaidi ya 300 ambao naamini Kwa uwezo wa Mungu kufikia 2030. Nitakuwa nimesimama vizuri. Hela zote Kwa Sasa nazielekeza kwenye miundo mbinu Kwa kuandaa Mazingira kuwa Bora sana. Na nimeapa Kwa uwezo wa Mungu 2031 nafungua international school.
Mwisho katkat ya mapambano Kuna changamoto kubwa Sana ila inahitaji uvumilivu. Na ni achoshukuru ni kupata mke mzuri mwenye kujielewa na amekuwa msaada mkubwa Sana kwangu.
Mimi niliwatosa nmb ,crdb ma Barclay's.Dhamana si ajira na ww,kaweka wazi hapo aliajiriwa 2012 alikua muajiriwa kama mwalimu,alivochukua mkopo akaacha kazi mbona wengi wanakimbia mkuu
Ata mm nina cousin wangu alilala mbele na mkopo akatoka kijijini alikokuwa anafundisha😀
Matajiri na watu wa kipato cha kati waliopo nchini, chama chao tawala siyo CCM? Umasikini umasikini unaletwa na mtu mwenyewe.Adui wangu no moja ni CCM Kwa kweli. Kwa sababu umaskn wetu umeletwa na CCM