Historia ya Makamu wa Rais wa Tanzania: Kuanzia Karume hadi Ndejembi

Historia ya Makamu wa Rais wa Tanzania: Kuanzia Karume hadi Ndejembi

KAWETELE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2015
Posts
738
Reaction score
1,787
Historia ya nafasi ya Makamu wa Rais nchini Tanzania imebadilika sana tangu Muungano wa mwaka 1964. Tanzania ilianza ikiwa na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili, mfumo ambao ulihusisha kwa karibu nafasi ya Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Mwaka 1995 mfumo huo ukabadilika na Tanzania ikawa na Makamu mmoja wa Rais.

Katika historia hiyo, baadhi ya Makamu walifariki wakiwa madarakani, wengine wakahamia kwenye nafasi nyingine za juu, na Samia Suluhu Hassan akawa wa kwanza kupanda kutoka Makamu wa Rais hadi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Sasa mwaka 2026, historia hiyo inaendelea kuandikwa kwa sura mpya: Emmanuel Nchimbi ameondoka katika nafasi hiyo baada ya kipindi kifupi, CCM imemvua uanachama, na Deogratius John Ndejembi amependekezwa kuwa mrithi wake.

*****************************************

Katika miaka ya mwanzo baada ya Muungano, Tanzania ilikuwa na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais. Makamu wa Kwanza alikuwa pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, huku Makamu wa Pili akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Mfumo huo uliendelea hadi mabadiliko ya kikatiba ya miaka ya 1990, ambapo kuanzia mwaka 1995 Tanzania ikaanza kuwa na Makamu mmoja wa Rais.

Hii ndiyo historia ya viongozi waliowahi kushika nafasi hiyo chini ya kila Rais wa Jamhuri ya Muungano.

1. AWAMU YA 1 Enzi za Mwl. Julius Kambarage Nyerere : Rais wa Jamhuri ya Muungano: 1964–1985

i. Sheikh Abeid Amani Karume : Makamu wa Kwanza wa Rais: 1964–1972

Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa mmoja wa viongozi wakuu waliounda msingi wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na baada ya Muungano mwaka 1964 akawa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Karume hakumaliza kipindi chake cha uongozi. Aliuawa tarehe 7 Aprili 1972 Zanzibar.
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume alifariki mwaka 1972.

ii. Rashid Mfaume Kawawa : Makamu wa Pili wa Rais: 1964–1977

Rashid Mfaume Kawawa alikuwa mmoja wa viongozi wa karibu wa Mwalimu Nyerere na alikuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika na baadaye Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
Baada ya Muungano mwaka 1964 akawa Makamu wa Pili wa Rais. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi na kushiriki katika ujenzi wa taasisi muhimu za taifa.
Hayati Rashid Mfaume Kawawa alifariki mwaka 2009.

iii. Aboud Jumbe Mwinyi ;Makamu wa Kwanza wa Rais: 1972–1984
1787818791624.png

Baada ya kifo cha Karume mwaka 1972, Aboud Jumbe akawa Makamu wa Kwanza wa Rais na Rais wa Zanzibar.
Alikuwa mmoja wa viongozi muhimu katika kipindi cha kujenga na kuimarisha Muungano. Mwaka 1984 alijiuzulu katika mazingira ya mvutano wa kisiasa kuhusu masuala ya Muungano.
Hayati Aboud Jumbe alifariki tarehe 14 Agosti 2016 akiwa na miaka 96.

iv. Ali Hassan Mwinyi ;Makamu wa Kwanza wa Rais: 1984–1985

Ali Hassan Mwinyi alichukua nafasi ya Aboud Jumbe mwaka 1984. Wakati huo alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Mwaka 1985, Mwalimu Nyerere alipostaafu urais, Mwinyi akachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Kwa hiyo, Mwinyi ni miongoni mwa viongozi waliopitia moja kwa moja kutoka nafasi ya Makamu wa Rais hadi kuwa Rais wa Tanzania.
Hayati Ali Hassan Mwinyi alifariki tarehe 29 Februari 2024 akiwa na miaka 98.

2. AWAMU YA 2. ENZI ZA ALI HASSAN MWINYI
v. Joseph Sinde Warioba ; Makamu wa Kwanza wa Rais: 1985–1990
1787818895827.png

Jaji Joseph Sinde Warioba alikuwa mwanasheria, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Alijulikana kwa msimamo wake katika sheria, utawala bora na uadilifu.
Baadaye aliendelea kushika nafasi mbalimbali za kitaifa, ikiwemo kuongoza Tume ya Rais ya Kupambana na Rushwa, maarufu kama Tume ya Warioba.
Jaji Warioba bado ni mmoja wa viongozi wastaafu wanaoheshimika nchini.

vi. Sheikh Idris Abdulwakil : Makamu wa Pili wa Rais: 1985–1990
1787819023507.png

Sheikh Idris Abdulwakil alikuwa Makamu wa Pili wa Rais na wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alikuwa sehemu ya kizazi cha viongozi waliokuwa wakisimamia Muungano katika kipindi muhimu cha miaka ya 1980.
Hayati Sheikh Idris Abdulwakil alifariki mwaka 2009.

vii. John Samwel Malecela ; Makamu wa Kwanza wa Rais: 1990–1994

John Samwel Malecela alikuwa mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa katika diplomasia na Serikali. Aliwahi kuwa balozi na Waziri wa Mambo ya Nje kabla ya kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais.
Alihudumu katika nafasi hiyo kuanzia 1990 hadi 1994 na baadaye akaendelea kuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe wa Tanzania.

viii. Salmin Amour : Makamu wa Pili wa Rais: 1990–1995
1787819159464.png

Salmin Amour alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuanzia 1990. Katika mfumo wa wakati huo alikuwa pia Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Alikuwa mmoja wa viongozi wa mwisho kuhudumu katika mfumo wa Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais.

ix. Cleopa David Msuya ; Makamu wa Pili wa Rais: 1994–1995
1787819230204.png

Cleopa Msuya alikuwa mwanasiasa na mtumishi wa umma mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya uchumi na utawala.
Alikuwa Waziri Mkuu kwa vipindi viwili na mwaka 1994 akawa Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais hadi mwaka 1995, wakati mfumo wa Makamu mmoja wa Rais ulipoanza.
Hayati Cleopa David Msuya alifariki tarehe 7 Mei 2025 akiwa na miaka 94.

3. AWAMU YA 3 BENJAMINI W MKAPA: Rais wa Jamhuri ya Muungano: 1995–2005


Mwaka 1995 ulikuwa muhimu katika historia ya nafasi ya Makamu wa Rais. Mfumo wa Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili ulimalizika, na Tanzania ikaanza kuwa na Makamu mmoja wa Rais.

x. Omar Ali Juma :Makamu wa Rais: 1995–2001
1787819536018.png

Dkt. Omar Ali Juma alikuwa mwanasiasa kutoka Zanzibar mwenye taaluma ya udaktari wa mifugo. Mwaka 1995 akawa Makamu wa Rais wa kwanza katika mfumo mpya.
Alifanya kazi na Rais Benjamin Mkapa hadi alipofariki akiwa bado madarakani.
Hayati Dkt. Omar Ali Juma alifariki tarehe 4 Julai 2001 jijini Dar es Salaam.

xi.Ali Mohamed Shein ; Makamu wa Rais: 2001–2010

Dkt. Ali Mohamed Shein alichukua nafasi ya Omar Ali Juma mwaka 2001.
Alikuwa Makamu wa Rais katika kipindi cha mwisho cha Rais Mkapa na pia kipindi cha kwanza cha Rais Jakaya Kikwete.
Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, hivyo kuondoka katika nafasi ya Makamu wa Rais.
4. AWAMU YA 4; ENZI ZA JK KIKWETE
xii. Ali Mohamed Shein ;Makamu wa Rais: 2005–2010
Shein aliendelea kuwa Makamu wa Rais katika kipindi cha kwanza cha Rais Jakaya Kikwete.
Hivyo, Ali Mohamed Shein ni miongoni mwa watu wachache waliowahi kuwa Makamu wa Rais chini ya Marais wawili tofauti.Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.

xii. Mohamed Gharib Bilal ; Makamu wa Rais: 2010–2015
1787819711060.png

Dkt. Mohamed Gharib Bilal alikuwa mwanasayansi mwenye taaluma ya fizikia ya nyuklia na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kuingia katika uongozi wa kisiasa.
Alikuwa Makamu wa Rais kutoka mwaka 2010 hadi 2015.


​
5. AWAMU YA 5, ENZI ZA John Pombe Joseph Magufuli ; Rais wa Jamhuri ya Muungano: 2015–2021

Xiv Samia Suluhu Hassan ; Makamu wa Rais: 2015–2021


Samia Suluhu Hassan aliingia katika historia mwaka 2015 alipokuwa mwanamke wa kwanza kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alihudumu pamoja na Rais John Magufuli hadi alipofariki tarehe 17 Machi 2021.
Kwa mujibu wa Katiba, Samia alimrithi Magufuli na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Hivyo, Samia ndiye Makamu wa Rais wa Tanzania aliyepanda moja kwa moja kutoka nafasi hiyo hadi kuwa Rais.


​
6. AWAMU YA 6, ENZI ZA Samia Suluhu Hassan ; Rais wa Jamhuri ya Muungano: 2021–hadi sasa

xv. Philip Isdor Mpango ; Makamu wa Rais: 2021–2025

Dkt. Philip Mpango alikuwa mchumi na mwanasiasa aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha kabla ya kuwa Makamu wa Rais.Aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais mwaka 2021 baada ya Samia Suluhu Hassan kuwa Rais.
Alihudumu katika nafasi hiyo hadi mwaka 2025, ambapo alikabidhi ofisi kwa mrithi wake, Emmanuel Nchimbi.

xvi. Emmanuel John Nchimbi; Makamu wa Rais: 2025–2026
1787820036050.png

Emmanuel John Nchimbi aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais baada ya Samia Suluhu Hassan kushinda uchaguzi wa mwaka 2025 na kuanza kipindi chake cha pili. Nchimbi amehudumu kwa kipindi kifupi sana, chini ya mwaka mmoja.

Mnamo Agosti 2026, Nchimbi alitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na pia kustaafu siasa na utumishi wa umma, huku kujiuzulu kwake kukiwa na tarehe rasmi ya kuanza 4 Septemba 2026.
Lakini kabla ya tarehe hiyo kufika, CCM ilichukua hatua nyingine. Tarehe 26 Agosti 2026, Chama Cha Mapinduzi kilimvua Nchimbi uanachama wa chama, kikieleza kuwa amekiuka kanuni za nidhamu na maadili ya chama.

Hivyo, katika historia ya Tanzania, Nchimbi anaingia katika kundi la Makamu wa Rais waliomaliza muda wao kwa mazingira ya kipekee sana: alitangaza mwenyewe kujiuzulu, kisha akavuliwa uanachama wa CCM siku iliyofuata.

Deogratius John Ndejembi ; Mteule wa CCM wa nafasi ya Makamu wa Rais: 2026
1787819991637.png

Baada ya kuondoka kwa Nchimbi, CCM ilimpendekeza Deogratius John Ndejembi, ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chamwino, kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais. Uamuzi huo ulipitishwa na uongozi wa juu wa CCM tarehe 26 Agosti 2026.

Ndejembi ana historia ya kupanda hatua kwa hatua katika uongozi. Aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, baadaye akachaguliwa kuwa Mbunge wa Chamwino mwaka 2020. Baada ya hapo alishika nyadhifa mbalimbali za uwaziri, ikiwemo Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Baadaye akawa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu na hatimaye Waziri wa Nishati
 
Ni nafasi ambayo hutakiwi kuwa popular - Samia Suluhu Hassan akimueleza Nchimbi katika moja ya hotuba zake
 
Back
Top Bottom