Historia ya mapenzi ya Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Historia ya mapenzi ya Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
FB_IMG_1630211069780.jpg

Ulishawahi kusikia japo kwa uchache kuhusu Emanuel Macron Rais wa sasa wa ufaransa? Je ushawahi kusikia kuhusu mke wake?

Ni hivi Rais Emanuel Macron wa ufaransa ana miaka 43 ndio rais kijana kuliko maraisi wote waliowahi kuiongoza ufaransa

Emmanuel Macron alianza kumpenda mwalimu wake wa darasani aliyeitwa rigitte Trogneux, kipindi hicho Emanuel Macron akiwa na miaka 15 huku Mwalimu rigitte Trogneux akiwa na miaka 39

Lakini Walianzisha mahusiano yao rasmi baada ya Emanuel Macron kutimiza miaka 18....licha ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na wazazi wa Emanuel Macron ili waweze kuwatenganisha wasiwe kwenye mahusiano lakin hawakufanikiwa

Ukumbuke binti wa Mwalimu rigitte Trogneux alikuwa anasoma darasa moja na Emanuel macron.... Hebu vuta taswira yaan mtu unasoma darasa moja nae halafu ndio mpenz wa mama yako mzazi

Mwaka 2006 Mwalimu Rigitte Trogneux aliachana na mume wake na mwaka 2007 aliolewa na Emanuel Macron ....huku Rigitte Trogneux akiwa na watoto watatu kati ya hao wapo waliomzidi umri mumewe wakati Emanuel macron hana mtoto hata mmoja

Emanuel Macron amezidiwa miaka 24 na mke wake huyo

Emanuel Macron amezidiwa miaka 3 na mtoto wa Kwanzaa wa mke wake

Je, wewe unaweza kuwa na mahusiano na mtu aliyekuzidi zaidi ya miaka 20?
 
Mapenzi upofu na upofu huo uhusisha nafsi na sio viungo kama macho n.k ndipo mtu apendwe la hasha! Kumuoa mwenye umri huo si ajabu,naamini nguvu ya mapenzi ni kubwa mno kuliko hata sayansi yenyewe ya mapenzi
Na hapo ndio huja msemo wa mapenzi ni hisia.
 
Asante mtoa mada,
Niliwahi ona hii kitu, sikuwahi kufikiria inakuaje kuaje
 
Tukiwa form 4,
Kuna jamaa angu MAGNUS aliwahi mtongoza madam wa Field kwa njia ya barua,
Akafunguka kila kitu jins gani anavyomfeel

Kilichotokea Sasa[emoji2],
Madam kumkomesha alikwenda kuisoma barua ya jamaa mbele ya SCHOOL ASSEMBLY.

Jamaa alikula viboko Sana na akapewa suspension ya miez 2[emoji4]

WAAFRICA KWENYE SUALA LA MAPENZI, MAHUSIANO na MAHABA bado Sana.[emoji4]
 
Tukiwa form 4,
Kuna jamaa angu MAGNUS aliwahi mtongoza madam wa Field kwa njia ya barua,
Akafunguka kila kitu jins gani anavyomfeel

Kilichotokea Sasa[emoji2],
Madam kumkomesha alikwenda kuisoma barua ya jamaa mbele ya SCHOOL ASSEMBLY.

Jamaa alikula viboko Sana na akapewa suspension ya miez 2[emoji4]

WAAFRICA KWENYE SUALA LA MAPENZI, MAHUSIANO na MAHABA bado Sana.[emoji4]
Sisi waafrika kuna baadhi ya mambo hua tunafeli kwa mfano mwanafunzi akimfuata mwalimu na kumtongoza, mwanafunzi huyo atacheza hatari.
Ila wenzetu mwalimu atamukataa na kushukuru pia kwa swala hilo.
 
Back
Top Bottom