Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano usilolijua usiku wa kiza

Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano usilolijua usiku wa kiza

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
1784997087489.png
1784997127999.png
1784997263655.png

Baadhi ya vitabu vya historia ya Zanzibar vilivyopo Maktaba

Huwa nasoma nyuzi hapa JF mtu anaandika kuwa John Okello ni Baba wa Taifa la Zanzibar.
Anaishia hapo.

Ukimuuliiza kama anajua historia ya mapinduzi ni ubishi tu na mjadala kurefuka bila ya sababu.
Ukimuuliza kama anaijua kambi ya Kipumbwi haijui wala hajapata kusikia neno hilo.

Kambi ya Kipumbwi na Shamba la Mkonge la Sakura ni muhimu katika kufahamu historia ya mapinduzi.
Halikadhalika ukimuuliza kama anawajua Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa hajapata kuwasikia.

Lakini mtu huyu anakuja na jina moja katika mapinduzi jina la Okello na kumuita ati Baba wa Taifa la Zanzibar.
Hakika mdomo haumkatai bwana wake.

Usilojua usiku wa kiza.


View: https://youtu.be/OEEPe8qN92A
 
Mimi ninachokijua Okello ndio Baba wa Taifa la Zanzibar.
Ndie aliyeongoza Mapinduzi 12 January 1964.
Na ndio alitangazaa Radioni Mapinduzi ya Zanzibar.

Karume alikuwa amejificha Ikulu ya Tanganyika Magogoni akiwa na Mwalimu Jk Nyerere.

HAKUNA MTU WA KUNIBADILISHA HUU UKWELI.
 
kwa hiyo ugaidi wee mzee umeleta tanganyika.We mzee hesabu siku zako na kufahamu sana sio kwa ubaya ila kwa kushabikia dini yako ukisema haki.Weka dini pembeni hapa kila mtu ana dini tunataka utanganyika wetu.
 
View attachment 3636863View attachment 3636865View attachment 3636868
Baadhi ya vitabu vya historia ya Zanzibar vilivyopo Maktaba

Huwa nasoma nyuzi hapa JF mtu anaandika kuwa John Okello ni Baba wa Taifa la Zanzibar.
Anaishia hapo.

Ukimuuliiza kama anajua historia ya mapinduzi ni ubishi tu na mjadala kurefuka bila ya sababu.
Ukimuuliza kama anaijua kambi ya Kipumbwi haijui wala hajapata kusikia neno hilo.

Kambi ya Kipumbwi na Shamba la Mkonge la Sakura ni muhimu katika kufahamu historia ya mapinduzi.
Halikadhalika ukimuuliza kama anawajua Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa hajapata kuwasikia.

Lakini mtu huyu anakuja na jina moja katika mapinduzi jina la Okello na kumuita ati Baba wa Taifa la Zanzibar.
Hakika mdomo haumkatai bwana wake.

Usilojua usiku wa kiza.


View: https://youtu.be/OEEPe8qN92A

Kwa hakika Baba wa Taifa Zanzibar ni John Okello.
 
Mimi ninachokijua Okello ndio Baba wa Taifa la Zanzibar.
Ndie aliyeongoza Mapinduzi 12 January 1964.
Na ndio alitangazaa Radioni Mapinduzi ya Zanzibar.

Karume alikuwa amejificha Ikulu ya Tanganyika Magogoni akiwa na Mwalimu Jk Nyerere.

HAKUNA MTU WA KUNIBADILISHA HUU UKWELI.
Hii ndio historia ya kweli ya Zanzibar.
 
Mimi ninachokijua Okello ndio Baba wa Taifa la Zanzibar.
Ndie aliyeongoza Mapinduzi 12 January 1964.
Na ndio alitangazaa Radioni Mapinduzi ya Zanzibar.

Karume alikuwa amejificha Ikulu ya Tanganyika Magogoni akiwa na Mwalimu Jk Nyerere.

HAKUNA MTU WA KUNIBADILISHA HUU UKWELI.
Capo...
Hicho unachokijua wewe ndiyo hapa nakueleza kuwa sicho.

Soma historia ya Kambi ya Kipumbwi na vijana wa Kimakonde waliovushwa Zanzibar 1961 kwa kuipigia kura ASP kisha 1964 kushiriki katika mapinduzi.

Unamuona John Okello hapo?
Unajua uzito wa kuwa na Kambi kama hiyo Tanganyika kwa minajili ya kupindua serikali ya nchi jirani?

Karume hakukimbia kwa maana ya kukimbia.

Kuja kwake Dar es Salaam ilikuwa sehemu ya mipango ya mapinduzi endapo itatokea mapinduzi yameshindikana.

Wala Karume hakuwa Government House (Ikulu).
Karume alikuwa kwenye nyumba jirani ya hapo.

Hii mipango unamuona John Okello?
Nimeweka clip fupi nazungumza uhusiano wa ASP na TANU.

Sikiliza na jitahidi kuelewa nataka kufikisha ujumbe gani?
 
Moja ya sababu tunazoambiwa za mapinduzi ni ASP kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi. Sasa kama ASP ilisomba watu toka Tanganyika kwenda kupiga kura Zanzibar na bado wakashindwa, mapinduzi yale yalikuwa batili toka mwanzo.
 
Tunarudi kule kule kupindisha historia!
J.okello hawataki hilo jina
Jina litajwe kabisa ktk mapinduzi huko

Ova
 
Mrangi,
Jina la John Okello lazima liwepo katika historia ya Zanzibar halliwezi kufutika.

Ila Okello hana sifa ya kuwa yeye ndiye aliyepanga mapinduzi na kupewa sifa si zake ati Che Guevara, Baba wa Taifa la Zanzibar nk.
Tunarudi kule kule kupindisha historia!
J.okello hawataki hilo jina
Jina litajwe kabisa ktk mapinduzi huko

Ova
 
Huku anapigania wapigania uhuru kina Mzee Sykes watajwe, kule anapambani mpigania Uhuru Okello asitajwe.

Maisha bila unafiki hayaendi.
 
Huku anapigania wapigania uhuru kina Mzee Sykes watajwe, kule anapambani mpigania Uhuru Okello asitajwe.

Maisha bila unafiki hayaendi.
Magnificio,
Sijapata kusema John Okello asitajwe.

Nisemacho ni kuwa asipewe sifa asizostahili.
 
Back
Top Bottom