Historia ya Marehemu Bibi Titi Mohammed, Baba yake bibi titi alikataa mwanae asisome shule maana atakuwa kafiri. Nyerere alikosa waislamu wasomi wengi

Kakuambia nani kutengeneza basi kunahitaji vyeti zaidi.
Ulisomea ujinga
 
Kakuambia nani kutengeneza basi kunahitaji vyeti zaidi.
Ulisomea ujinga
tuambie ni basi gani bokoharam, au mwarabu yeyote aliwahi kutengeneza. taja moja tu. ila usitaje Ngamia, hilo sio basi ni mnyama na hatengenezwi.
 
umeshindwa kutaja. mwarabu alichotengeneza ni mkojo wa ngamia na tende tu. isingekuwa mafuta wangekuwa wanakula mchanga wa jangwani wale.
Mfalme...
Ndugu zanguni.

Mambo haya yanahitaji mtu kusoma vizuri ili ayajue.
Yako mengi lakini tunaweza kuanza na huu ubishi wa Waarabu

Tuutumieni huu ukumbi kujielinisha siyo mahali pa kuzozana na kufanya kejeli.

Ingieni Google: Arab Scientists and Their Inventions.
 

ADUI YA WAISLAMU WA TANZANIA NI UTAMADUNI WA KISHENZI WA MWARABU

Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni viwili: dini nzuri ya Kiislamu na utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo, sijateleza ulimi wala mkono, Waarabu walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu.

Watanzania wengi wanachanganya haya mawili kwa kutokuwa na upeo. Tuulizeni tuliosafiri duniani, kuna Wazungu na Wachina Waislamu na kuna Waarabu Wakristo kama Wakoptiki wa Misri. Uislamu siyo Uarabu na Uarabu siyo Uislamu na kwa hakika Uislamu ndio uliopunguza ushenzi wa Waarabu (ujahiliya) na kuwapa utu na ustaarabu.

Tukumbuke pia, Uislamu ndiyo ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya sita, saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya waislamu, na haya majoho ya mahafali za leo yalianzishwa na Waislamu, siyo wazungu.

Nirejee kwenye rekodi. Taasisi ya kwanza ya kielimu kwa Waarabu duniani ilikuwa Ez-Zitouna ya
Tunisia iliyoanzishwa mwaka 737, lakini kinachokubalika kama chuo kikuu cha kwanza duniani ni
Al-Karaouine cha Moroko cha mwaka 859. Chuo kikuu cha pili duniani kilikuwa Al-Azhar cha Misri
mwaka 970 na cha tatu kilikuwa Nizamiyya cha Iraki mwaka 1065. Wazungu pamoja na kelele zao zote, chuo kikuu chao kwa kwanza ni Bologna cha Italia mwaka 1088 na baadaye mwaka 1096 kile cha Paris. Hakuna, ubishi, Waislamu ndio waanzilishi wa vyuo vikuu duniani.

Saba, lakini si waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini nyingine pia. Ukienda kwenye
nchi za Maghrebu (Afrika Kaskazini) kama Moroko, Algeria, Tunisia, na Misri na zile za Mashariki
ya Kati kuanzia na Uturuki, Siria, Iraki, Lebanoni, na Yodani kidogo, hadi Irani, kuna waislamu
wengi wenye elimu kubwa.

Hapa Marekani Waislamu wa mataifa haya wanaheshimika, mathalani, wahandisi na wataalamu mahiri wa teknohama hutoka Uturuki, Pakistani na India wakati madaktari mahiri hutoka Irani. Mataifa ya Pakistani na Irani ndiyo pekee yaliyomudu kuwa na wataalamu wake wenyewe wa nyuklia bila kusaidiwa na mataifa ya Ulaya na Marekani na wote walikuwa Waislamu, akiwemo Abdul Qadeer Khan wa Pakistani.

Aidha, mwanasayansi aliyesimamia urushaji wa satelaiti ya India ya kwanza mwaka 1980, ni mwislamu Avul Abdul Kalam ambaye baadaye alikuwa Rais wa India mwaka 2002 hadi 2007. Ninachotaka kusema ni kwamba ukiondoa Waislamu walioko kwenye
Ghuba ya Uarabuni, wengine wote ni wasomi wa uhakika. Sababu ni moja tu: UTAMADUNI.

Nane, hali ni tofauti sana kule Ghuba kwenye nchi za Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani,
Katari, Imarata (Falme za Kiarabu) na Bahareni. Huko Ghuba watu hawataki shule. Tusiwasitiri sana na kuficha ukweli: Ghuba hawataki shule. Hawa watu wa Ghuba ndiyo waliotuletea utamaduni wao huu Afrika Mashariki kuanzia kule Somalia, shuka hadi Lamu, Malindi na Mombasa Kenya, njoo kwetu Tanzania anzia na Pangani hadi Kilwa na Mafia, teremka mpaka Pemba iliyoko kaskazini mwa Msumbiji - kote huku kuna watu wenye utamaduni wa Ghuba wa kukataa shule.

Tusifichane ukweli, maeneo haya watu hawataki shule. Hili liko wazi. Kwa kuwa Waarabu wa Ghuba ndiyo walioleta pia Uislamu, basi watu hujumuisha kwa pamoja tatizo la kukosa elimu na hii dini nzuri ya Uislamu. Narudia tena, utamaduni wa kukataa shule ni wa Waarabu wa Ghuba, siyo Waislamu hapa duniani. Tatizo letu Tanzania ni kwamba Waislamu wengi (siyo wote) wamechukua utamaduni wa kimwinyimwinyi wa Ghuba wa kuzikimbia shule kana kwamba ndio ujanja. Hiki ndiyo chanzo cha malalamiko yote haya; hakuna cha uonevu wala nini!

Saudia watu ni vilaza watupu kiasi kwamba kuna Wamisri milioni moja na zaidi wanaofanya kazi za kitaalamu. Kila taifa la Ghuba isipokuwa Yemeni na Omani, lina wageni wengi zaidi nchini mwake kuliko wenyeji kwa sababu wananchi wao ni vilaza; hawataki shule. Yemeni na Omani hawana mafuta wala gesi asilia, yaani ni maskini na ndio maana hakuna wageni wengi. Hata hivyo, ukienda Omani kuna Watanzania wengi sana (hasa wenyeji wa Zanzibar), laki sita na ushee na wao pia shule hamna kitu; wanaiga uvivu wa wenyeji wao.

Tisa, hivyo basi, Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia, Lamu, Malindi, Mombasa, Pemba, Unguja, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na Waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Usukumani, au kule Bukoba, na hata wale wa Uganda (kabila la Baganda), wao wanapenda shule.

Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo, halafu fuata ile barabara ya watumwa hadi Kondoa, nenda hadi Tabora, fika mpaka Ujiji, ingia mpaka Kongo Mashariki, kote huku shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI NI UTAMADUNI WA UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.

Kumi, tafiti tatu ninazozijua, moja ya Ilana Kessler wa Chuo Kikuu cha Georgetown cha Marekani
ya mwaka 2005, na ile ya Erasmus Kaijage wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya mwaka 1999,
zinaonesha kwamba wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa Waislamu ni kati ya asilimia 14 15 tu ya wanafunzi wote.

Aidha, Baraza la Udhamini la Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUMT), liliwahi kutoa taarifa yake kwamba kati ya mwaka 1986 hadi 1990, kwa wanafunzi walioingia chuoni hapo kusoma shahada ya kwanza Waislamu walikuwa asilimia 13 tu. Hiki ni kiasi kidogo mno, lakini ni kidogo cha kiasi gani cha Waislamu nchini? Lazima tujue hili nalo pia, hata kwa makadirio tu.

Kumi na Moja, sasa turudi kwenye jingine. Nyerere aliamua tuachane na sensa ya kupekua dini za watu kwa sababu nzuri kabisa - alitaka Watanzania tusitambuane kwa dini zetu (na makabila pia). Hivyo, ili kuweka usawa tukaanzisha msemo huu: Tanzania sisi nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Huu ni msemo tu na hauna usahihi. Aidha, hata kama sensa ya zamani ilionesha kwamba waislamu, ama wakristo, au wapagani ndiyo wengi, haina maana yoyote leo wakati taifa letu lina watu milioni 45 hivi. Tulipata uhuru tukiwa milioni 12 na baadaye Zanzibar ikaongeza laki tatu. Watanzania hatukuwa na kelele za asilimia ngapi ni dini hii na ile. Leo zimerudi. Inakera sana!

Kwa mujibu wa taarifa kadhaa za kitafiti (siyo mimi), Waislamu nchini Tanzania ni theluthi moja ya wananchi wote. Aidha, kwa bahati ama kwa mpangilio, rais wetu wa sasa, Mheshimiwa Kikwete, alipoteua mawaziri Novemba 2010 aliweka theluthi moja waislamu, na hivyo hivyo kwa manaibu. Wote tunajua. Hali kadhalika, alipoteua mawaziri na manaibu wao hii juzi, aliweka theluthi moja waislamu kwenye uwaaziri na pia kwenye unaibu.

Alipoteua Tume ya Kupitia Katiba, kwa wajumbe wa Bara aliweka pia theluthi moja yake waislamu. Iko wazi. Rais Kikwete, nijuavyo mimi, anajaribu kwa kila hali kuliangalia hili suala la kelele za udini ili asiiharibu nchi yetu. Hatopenda kukumbwa na malalamiko akishaondoka kwani na yeye ni binadamu kama sisi. Anakuwa mwangalifu sana hata kama kuna wakati anateleza kibinadamu. Je, hesabu zake zina maana gani? Nina hakika anajua anachokifanya na kamwe hawezi kuwaonea waislamu ambao ni Watanzania kama sisi wote. Hawezi kufanya uonevu.
 
Mkata...
Haya hapo chini yanaweza kusaidia kuelewa matatizo haya tunayojadili hapa:

Warsha kikundi cha vijana wasomi wa Kiislam waliweza kujipenyeza BAKWATA na uongozi wa BAKWATA uliwakubali na kuwaamini.

Hapo ndipo walipofanya utafiti huo hapo chini ambao baada ya kukamilika ulitolewa kama waraka kwa kila Muislam wa Tanzainia.

Table 1
Selection of Std.VII Pupils to Form I in Dar es Salaam Region 1978-1981
YearTotal SelectedMuslimsPercentage of
Muslims Selected
197895621623
197990319422
1980107124723
Source: Dar es Salaam City Council, Department of Education.
NB: In 1967 census Muslims in Dar es Salaam Region were 67%; therefore the number of Muslim students in Dar es Salaam Primary Schools is greater than that of Christians. This should have reflected in the selection.
Table 2
Religious Distribution University of Dar es Salaam 1971/72-1973/74
YearMuslim %Non-Muslim %Total
1969/701783100
*1970/71---
1971/721387100
1972/731486100
1973/741387100
*1974/75---
1975/761585100
*1976/77--1. -
*1977/78---
1978/791486100
**1979/801486100
**1980/811189100
**1981/821684100
* Official Statistics not available
** Students selected for Faculty of Agriculture, Forestry and Veterinary Science and medicine not included.
Source: 1969/70-1978/79 University of Dar es Salaam Students Directory.
1979/80-1981/82 Daily News June 1979/1981.

Table 3
Religious Distribution of University Admission 1971/72-1973/74
Year% Muslim% ChristiansOthers% TotTotal
1971/7213861100
1972/7314842100
1973/7413798100
Source: University of Dar es Salaam Student Directory

Table 4
Christian Seminary Secondary Schools 1980
No.SchoolLevelRegion


1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
11.
12.
13.
14.
15.
16.
17.
18.
19.
Mafinga
Ujiji
Kilema
Maua
Uru
Nanupa
Makoko
Kasita
Lutheran Junior
Saint Peter’s
Nyegezi
Kaengesa
Likonde
Mwadui
Dungunyi
Itaga
Soni
Katoke
Rubiya
“O”

“A”
“O”








“A”
“O”

“A”
“O”

Iringa
Kigoma
Kilimanjaro
Kilimanjaro
Kilimanjaro
Lindi
Mara
Morogoro
Morogoro
Morogoro
Mwanza
Rukwa
Ruvuma
Shinyanga
Singida
Tabora
Tanga
Kagera
Kagera
Source: Ministry of National Education, Dar es Salaam.

Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania February 14, 2014 0


Reinventing BAKWATA, 1981
Part One
 

Nyongeza:

ANASEMA MSEMAJI KUWA WAISLAM TANZANIA NI THELUTHI MOJA

Msomaji kamsoma huyu msemaji sasa kaniuliza anasema kuwa mimi nimeandika kitabu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (London 1998) je, hii struggle ya Waislam kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ya hawa Waislam theluthi moja?

Hili swali lake la kwanza.

Swali la pili anauliza hii theluthi mbili ilikuwa wapi haikushiriki katika kupigania uhuru kiasi kupigania uhuru wa Tanganyika kubebwe na Waislam wachache theluthi moja peke yao?

Jibu langu ni kuwa kama kweli Waislam wangekuwa theluthi moja na kama historia ya kupigania uhuru inavyoonyesha kuwa Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kupambana kwanza na Wajerumani kwa silaha katika Vita Vya Maji Maji (1905 - 1907) kisha Muingereza kwa siasa kitendo hiki kingeweka historia ya pekee ulimwenguni.

Hapa ieleweke kuwa hakuna nchi duniani ambayo jamii yake ya watu wachache ndiyo iliyojitokeza kuihami nchi yao kwa silaha dhidi ya wakoloni wakati walio wengi wamejitenga pembeni.

Uko ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukweli huu.

Ukichukua mfano huu jibu lisilo na shaka ni kuwa Waislam hawajapata kuwa theluthi moja Tanganyika.

Wangekuwa theluthi moja historia ya uhuru isingekuwa kama historia niliyoandika katika kitabu changu hicho nilichokitaja hapo juu.

Kwa ukweli huu basi yote ambayo mwandishi kaandika kuhusu Waislam si sawa kwa kukosa ushahidi unaosimama kwenye ukweli wa utafiti.
 
USHAHIDI WA PICHA KWA HAYO NILIYOANDIKA HAPO JUU


Hassan Omari Makunganya na wenzake walinyongwa na Wajerumani kwa kunyanyua silaha dhidi yao 1895


Nduna Abdulrauf Songea Mbano
alinyongwa baada ya Vita Vya Maji Maji 1905 - 1907


 


Mzee Mohammed, kwenye hoja ya waislamu wengi kushiriki kupigania uhuru , sababu kuu ni advantage ya location. yaani hayo ni makabila yaliyopokea uislam. na ardhi yao ipo kwenye miji iliyotumika kupiganiwa uhuru.

mfano Dar es salaam, harakati nyingi za kupigania uhuru zimefanyikia Dar es salaam, na Wote tunajua Dar es salaam ni mji wa wazaramo na wandengereko ambapo hayo makabila yameupokea uislam. wazaramo na wandengereko ni waislamu. imagine uhuru umepiganiwa kwao. lazima wengi washiriki kupigania uhuru. Binafsi sijawai kuona mzaramo mkristo na wala mndengereko mkristo.

sababu kuu ya waislam wengi kuwa kwenye harakati za kupigania uhuru ni kwamba harakati hizo zilifanyikia kwenye ardhi ya nyumbani kwao walipokuwa wanaishi.


kama harakati za uhuru zingefanyikia Mbeya maana yake wanyakyusa ambao wengi ni wakristo ndio wangejaa kwenye kupigania uhuru huo.

kama harakati za uhuru zingefanyikia Kilimanjaro Moshi maana yake wachaga ambao wengi ni wakristo ndio wangekuwa wengi
 
Fresh...
Unaijua historia ya TANU Moshi?
Waliokuwa mstari wa mbele walikuwa Mama bint Mwalimu, Bi. Halima Selengia, Amina Kinabo, Lucy Lameck na Yusuf Olotu.
 
Huyu Bibi hajapewa heshima anayostahili...ni miongoni mwa wapigania Uhuru muhimu sana nyakati zile.

Uhusiano wake na Kambona adui wa Nyerere ndio uliompa mama wa watu kifungo kile cha kikatili....siasa za visasi hizi

Rip Titi Mohammed, mwanamke shupavu, jasiri na mpigania uhuru
JokaKuu Mohamed Said Pascal Mayalla zitto junior
 
Nyerere alikuwa hatari sana jamaa ...Mungu ndio anajua.
 
msubiri yule mzee mwenye profile la soda mixa udini aje kujaza maelezo kwa nini baba yake kakosa kuwa serikalini
 
msubiri yule mzee mwenye profile la soda mixa udini aje kujaza maelezo kwa nini baba yake kakosa kuwa serikalini
Utasoma vip elimu mkoloni ili uwe kibaraka ,enzi hizo waliokuwa wanakataa elimu ni wale wanaotaka uhuru ...Waliokubali elimu ndio walitunga mashairi ya kupinga ukombozi..
 
Hahahahaha..nimependa hiyo , magomeni we want fire ...hahahahaha Bibi Titi alitisha ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…