Mfalme...
Ndugu zanguni.
Mambo haya yanahitaji mtu kusoma vizuri ili ayajue.
Yako mengi lakini tunaweza kuanza na huu ubishi wa Waarabu
Tuutumieni huu ukumbi kujielinisha siyo mahali pa kuzozana na kufanya kejeli.
Ingieni Google: Arab Scientists and Their Inventions.
ADUI YA WAISLAMU WA TANZANIA NI UTAMADUNI WA KISHENZI WA MWARABU
Waarabu walipokuja kwenye karne ya 13 walileta vitu kadhaa vikuu vikiwa ni viwili: dini nzuri ya Kiislamu na utamaduni wao wa kishenzi. Ndiyo, sijateleza ulimi wala mkono, Waarabu walileta utamaduni wa kishenzi. Utamaduni wa Kiarabu siyo dini ya Kiislamu na dini ya Kiislamu siyo utamaduni wa Kiarabu.
Watanzania wengi wanachanganya haya mawili kwa kutokuwa na upeo. Tuulizeni tuliosafiri duniani, kuna Wazungu na Wachina Waislamu na kuna Waarabu Wakristo kama Wakoptiki wa Misri. Uislamu siyo Uarabu na Uarabu siyo Uislamu na kwa hakika Uislamu ndio uliopunguza ushenzi wa Waarabu (ujahiliya) na kuwapa utu na ustaarabu.
Tukumbuke pia, Uislamu ndiyo ulioongoza elimu duniani kwenye karne ya sita, saba na nane na hata vyuo vikuu vya kwanza duniani vilikuwa vya waislamu, na haya majoho ya mahafali za leo yalianzishwa na Waislamu, siyo wazungu.
Nirejee kwenye rekodi. Taasisi ya kwanza ya kielimu kwa Waarabu duniani ilikuwa Ez-Zitouna ya
Tunisia iliyoanzishwa mwaka 737, lakini kinachokubalika kama chuo kikuu cha kwanza duniani ni
Al-Karaouine cha Moroko cha mwaka 859. Chuo kikuu cha pili duniani kilikuwa Al-Azhar cha Misri
mwaka 970 na cha tatu kilikuwa Nizamiyya cha Iraki mwaka 1065. Wazungu pamoja na kelele zao zote, chuo kikuu chao kwa kwanza ni Bologna cha Italia mwaka 1088 na baadaye mwaka 1096 kile cha Paris. Hakuna, ubishi, Waislamu ndio waanzilishi wa vyuo vikuu duniani.
Saba, lakini si waislamu wote hupenda elimu, kama ilivyo kwa dini nyingine pia. Ukienda kwenye
nchi za Maghrebu (Afrika Kaskazini) kama Moroko, Algeria, Tunisia, na Misri na zile za Mashariki
ya Kati kuanzia na Uturuki, Siria, Iraki, Lebanoni, na Yodani kidogo, hadi Irani, kuna waislamu
wengi wenye elimu kubwa.
Hapa Marekani Waislamu wa mataifa haya wanaheshimika, mathalani, wahandisi na wataalamu mahiri wa teknohama hutoka Uturuki, Pakistani na India wakati madaktari mahiri hutoka Irani. Mataifa ya Pakistani na Irani ndiyo pekee yaliyomudu kuwa na wataalamu wake wenyewe wa nyuklia bila kusaidiwa na mataifa ya Ulaya na Marekani na wote walikuwa Waislamu, akiwemo Abdul Qadeer Khan wa Pakistani.
Aidha, mwanasayansi aliyesimamia urushaji wa satelaiti ya India ya kwanza mwaka 1980, ni mwislamu Avul Abdul Kalam ambaye baadaye alikuwa Rais wa India mwaka 2002 hadi 2007. Ninachotaka kusema ni kwamba ukiondoa Waislamu walioko kwenye
Ghuba ya Uarabuni, wengine wote ni wasomi wa uhakika. Sababu ni moja tu: UTAMADUNI.
Nane, hali ni tofauti sana kule Ghuba kwenye nchi za Saudia Arabia, Yemeni, Kuwaiti, Omani,
Katari, Imarata (Falme za Kiarabu) na Bahareni. Huko Ghuba watu hawataki shule. Tusiwasitiri sana na kuficha ukweli: Ghuba hawataki shule. Hawa watu wa Ghuba ndiyo waliotuletea utamaduni wao huu Afrika Mashariki kuanzia kule Somalia, shuka hadi Lamu, Malindi na Mombasa Kenya, njoo kwetu Tanzania anzia na Pangani hadi Kilwa na Mafia, teremka mpaka Pemba iliyoko kaskazini mwa Msumbiji - kote huku kuna watu wenye utamaduni wa Ghuba wa kukataa shule.
Tusifichane ukweli, maeneo haya watu hawataki shule. Hili liko wazi. Kwa kuwa Waarabu wa Ghuba ndiyo walioleta pia Uislamu, basi watu hujumuisha kwa pamoja tatizo la kukosa elimu na hii dini nzuri ya Uislamu. Narudia tena, utamaduni wa kukataa shule ni wa Waarabu wa Ghuba, siyo Waislamu hapa duniani. Tatizo letu Tanzania ni kwamba Waislamu wengi (siyo wote) wamechukua utamaduni wa kimwinyimwinyi wa Ghuba wa kuzikimbia shule kana kwamba ndio ujanja. Hiki ndiyo chanzo cha malalamiko yote haya; hakuna cha uonevu wala nini!
Saudia watu ni vilaza watupu kiasi kwamba kuna Wamisri milioni moja na zaidi wanaofanya kazi za kitaalamu. Kila taifa la Ghuba isipokuwa Yemeni na Omani, lina wageni wengi zaidi nchini mwake kuliko wenyeji kwa sababu wananchi wao ni vilaza; hawataki shule. Yemeni na Omani hawana mafuta wala gesi asilia, yaani ni maskini na ndio maana hakuna wageni wengi. Hata hivyo, ukienda Omani kuna Watanzania wengi sana (hasa wenyeji wa Zanzibar), laki sita na ushee na wao pia shule hamna kitu; wanaiga uvivu wa wenyeji wao.
Tisa, hivyo basi, Waislamu wa pwani ya Tanzania, kama wenzao wote wa Somalia, Lamu, Malindi, Mombasa, Pemba, Unguja, Mafia, Kilwa, Lindi na Pemba ya Msumbiji, wana utamaduni wa Waarabu wa Ghuba wa kugomea shule. Tofauti na Waislamu wa Tanzania walioko Machame na Usangi mkoani Kilimanjaro, au Usukumani, au kule Bukoba, na hata wale wa Uganda (kabila la Baganda), wao wanapenda shule.
Maeneo yote waliyokaa Waarabu, kuanzia Bagamoyo, halafu fuata ile barabara ya watumwa hadi Kondoa, nenda hadi Tabora, fika mpaka Ujiji, ingia mpaka Kongo Mashariki, kote huku shule si mali kitu. TATIZO SI UISLAMU BALI NI UTAMADUNI WA UARABU WA GHUBA. Anayebisha hongera zake.
Kumi, tafiti tatu ninazozijua, moja ya Ilana Kessler wa Chuo Kikuu cha Georgetown cha Marekani
ya mwaka 2005, na ile ya Erasmus Kaijage wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya mwaka 1999,
zinaonesha kwamba wanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa Waislamu ni kati ya asilimia 14 15 tu ya wanafunzi wote.
Aidha, Baraza la Udhamini la Waislamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUMT), liliwahi kutoa taarifa yake kwamba kati ya mwaka 1986 hadi 1990, kwa wanafunzi walioingia chuoni hapo kusoma shahada ya kwanza Waislamu walikuwa asilimia 13 tu. Hiki ni kiasi kidogo mno, lakini ni kidogo cha kiasi gani cha Waislamu nchini? Lazima tujue hili nalo pia, hata kwa makadirio tu.
Kumi na Moja, sasa turudi kwenye jingine. Nyerere aliamua tuachane na sensa ya kupekua dini za watu kwa sababu nzuri kabisa - alitaka Watanzania tusitambuane kwa dini zetu (na makabila pia). Hivyo, ili kuweka usawa tukaanzisha msemo huu: Tanzania sisi nusu ni Waislamu na nusu ni Wakristo. Huu ni msemo tu na hauna usahihi. Aidha, hata kama sensa ya zamani ilionesha kwamba waislamu, ama wakristo, au wapagani ndiyo wengi, haina maana yoyote leo wakati taifa letu lina watu milioni 45 hivi. Tulipata uhuru tukiwa milioni 12 na baadaye Zanzibar ikaongeza laki tatu. Watanzania hatukuwa na kelele za asilimia ngapi ni dini hii na ile. Leo zimerudi. Inakera sana!
Kwa mujibu wa taarifa kadhaa za kitafiti (siyo mimi), Waislamu nchini Tanzania ni theluthi moja ya wananchi wote. Aidha, kwa bahati ama kwa mpangilio, rais wetu wa sasa, Mheshimiwa Kikwete, alipoteua mawaziri Novemba 2010 aliweka theluthi moja waislamu, na hivyo hivyo kwa manaibu. Wote tunajua. Hali kadhalika, alipoteua mawaziri na manaibu wao hii juzi, aliweka theluthi moja waislamu kwenye uwaaziri na pia kwenye unaibu.
Alipoteua Tume ya Kupitia Katiba, kwa wajumbe wa Bara aliweka pia theluthi moja yake waislamu. Iko wazi. Rais Kikwete, nijuavyo mimi, anajaribu kwa kila hali kuliangalia hili suala la kelele za udini ili asiiharibu nchi yetu. Hatopenda kukumbwa na malalamiko akishaondoka kwani na yeye ni binadamu kama sisi. Anakuwa mwangalifu sana hata kama kuna wakati anateleza kibinadamu. Je, hesabu zake zina maana gani? Nina hakika anajua anachokifanya na kamwe hawezi kuwaonea waislamu ambao ni Watanzania kama sisi wote. Hawezi kufanya uonevu.