Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Historia ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda: Kilio Cha Mifereji ya Damu iendayo Ethiopia

Lelommassy,
@zitto junior
Wakuu mahakama ya ICTR ilishathibitisha pasipo na shaka kuwa hakukuwa na mipango ya genocide na washitakiwa wote wakafutiwa mashitaka ya conspiracy to commit genocide. Kwa hiyo genocide dhidi ya watutsi haikupangwa and that is a FACT iliyothibitishwa na mahakama. labda kwa upande wa genocide against hutus kama na yenyewe ilipangwa au la bado hatujui kwa kuwa ICTR ilishinikizwa na marekani kutomshtaki kagame na wenzake ingawa prosecutor tayari alishaandaa mashtaka.
So mkuu jmali, mahakama ya ICTR ilituibitiswa genocide ilipangwa na pk wenyewe au vipi hapo
 
jMali na zitto junior
na huyu mshabiki wa PK,Jestkilla.
👉 JAMANI haya Mambo Ni simple kabisa Kama PK aliwaokoa watutsi wenzake na haku plan mauaji wa kimbali ya 1994 angeshapewa tuzo na nchi yoyote kubwa au international community yoyote, ila baadae tuzo wamepewa wengine walio wasaidia watutsi wasiuwawe
Kama ,👇

Selman_PeacePost_Rwanda_Paul_Rusesabagina_02.jpg
 
Unaweza ukanionyesha ni lini wahutu waliochinjwa congo wamewahi kujumuishwa kwenye kumbukizi ya genocide ya 1994??

Mkuu haya mambo ni vzuri uyafanyie utafiti kabla hujapotosha watu humu..... Wanaokumbukwa ni wale wa 1994 genocide ambao licha ya kuwa walikufa wahutu laki 7 ila yanaitwa TUTSI GENOCIDE!!!! As if hakuna wahutu waliolengwa na RPF hasa huko gitarama na cyangugu

Naopigia kelele mimi ni wale waliouawa kwenye makambi ya wakimbizi huko DRC wameshakufa mamilion tokea 1996 hadi 2003 na nlishasema humu nlipokuwa nyiragongo nlishuhudia makambi yao yamechomwa moto na wote wamechinjwa kma kuku alafu kagame anakanusha mpka leo ilihali ushahidi upo wa RPF kuhusika then mnasema huwa wanakumbukwa?? Are you serious??

Mkuu acha kuwa pro-kagame kubali kuwa kagame alichemka issue ya genocide ila kuendelea kumtetea humu haibadilishi ukweli kuwa 80% ya ukweli wa genocide mnafichwa na huyo kagame

Ni hayo tu
Mkuu zitto junior tumsamehe huyu ndugu jay-millions
👉Hajui kuwa ICTR ilithibitisha kuwa wahutu zaidi ya 500,000 waliuwawa na RPA during the genocide and after month of genocide, na hata hivyo upo ushaidi mwingi tuu kwamba zaidi ya 60% waliokufa during genocide Ni wahutu Tena waliuwawa na RPA.
👉 Kasahau kuwa PK alikuwa nikibaraka wa USA, na ndio wanaomlinda mkapa Leo kwenda kushitakiwa.
👉 Hata hivyo nafikili ndugu yetu huyu Hajui kuwa Kuna congo war 1 ambayo ilichukua maisha ya wahutu wengi Sana wanakadiliwa zaidi ya wahutu 300,000 waliuwawa wengi wao Ni watoto, wamama , wagonjwa na wazee, na zaidi ya 200,000 hawajulikani walipo mpaka leo.
👉 Kuna congo war 2 ambayo ilichukua maisha ya watu zaidi ya 6 million ambao Ni wacongo na baadhi Ni wahutu, na Ni Vita aliyo alianzisha PK , kwa masada ya marekani.
👉 Lakini Sasa PK munamuona Kama pan africanist,
Hivi pan Africanist gani ambaye kasababisha vifo vya zaidi ya waafrica million 1 rwanda na million 6 congo , na ambaye pia alikuwa kibalaka wa marekani, na Ni ambaye anafadhili makundi ya waasi mchi jirani.
Ndugu jay-millions fikilia vizuri sawa,
Hata Gaddafi alikuwa dikteta japo alijulikana Ni pan Africanist.
 
Zitto nitafsirie maana ya genocide unavyoielewa!! Yawezekana!! Unachanganya mambo!!
MLA PANYA SWANGA na zitto junior
-Mauaji ya kimbali Ni mauaji ya watu wengi kwa muda mfupi , ambapo jamii Moja au nchi moja hufanya mauaji kwa jamii nyingine au nchi nyingine, kwa lengo la kuwaangaliza kabisa
AU jamii mbili zinapigana kwa kupingana na kila jamii moja inafanya Mauaji kwa jamii nyingine ,mfano Rwanda genocide
-Rwandan genocide Ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe ( Civil war) ambapo interhamwe na Far waliwaua watutsi na wahutu msimamo wa Kati na pia RPA chini ya kagame ili waua wahutu na baadhi ya watusi Kama watutsi wa bisesero na bagogwe.
 
Nani hana huruma?? Nyie mnasema wazungu waliacha tutsi wakiuawa ilihali wakati wazungu 14 wanachinjwa na interhamwe RPF haikusaidia what did u expect wazungu wafanye?? Wenyewe walikua ordered waondoke

Mbona hushangai wanajeshi wa UN walishindwa kuzuia RPF kumimina risasi kwa wahutu huko kwenye makambi ya wakimbizi !!

Tuache unafki haya mambo ni ya pande mbili so kma tunataka haki tulaumu pande zote sio pale tu anapokufa mtutsi
Mkuu Hawa Ni wahuni tuu kumbuka pia may 12 1994 kagame alizuia UN to intervention kustop genocide , hivi fikilia wangesaidia watu wangapi wasiuawe , Afu hao watusi wanamchukuria Kama kawasave ,


👉 Pia Kuna ushuunda wa former bodyguard wa kagame ambaye alikuwa member wa high command battalion pale mulindi anaitwa james munyandinda alisema kuwa April 30 1994 kagame aliandika barua kuzuia UN to intervention to stop genocide.

mr qns , Jestkilla ,manzi james , MLA PANYA SWANGA
Lakini tunajua genocide iliendelea mpaka july na siku zake.
 
KILIO CHA MIFEREJI YA DAMU IENDAYO ETHIOPIA

View attachment 718281

FINALE

Chiefs kutokana na ushauri wa watu wengi kuhusu nilichotaka niandike juu ya kudunguliwa kwa ndege ya Rais Habyarimana na hatimaye kifo chake mimeona nifuate ushuri huo na nisiandike maoni hayo kwa sasa.
Naomba nifanye hitimisho la makala hii na kama tutapata wasaa huko mbeleni basi tuta revisit makala hii na kujadili zaidi.


Sitaingia deep sana kwenye sehemu hii ya mwisho, naomba nifanye hitimisho tu…




Baada ya Jenerali Dallaire kupata uhakika kwamba ndege iliyodunguliwa ilikuwa imembeba Rais Juvenal Habyarimana alituma wanajeshi kumi wenye asili ya Kibelgiji kwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu Agathe Uwilingiyimana ili kumpa ulinzi yeye na familia yake na pia kumpeleka mpaka kwenye kituo cha redio cha taifa cha Radio Rwanda ili apate kulihutubia taifa na kuwasihi raia wawe na utulivu.

Lakini kulikuwa na kikosi cha kijeshi cha weledi cha serikali ya Rwanda kinachoitwa 'Gendarmerie' (Presidential Guard) walikuwa tayari wameshaidhibiti Radio Rwanda na walianza kurusha matangazo na kuutangazia umma kwamba Rais Habyarimana ameuwawa na watusi (RPF) na hivyo wakati wa 'kuingia kazini' (kuuwa watusi) ulikuwa umewadia.

Askari wale wa Kibelgiji walidhibitiwa na makomando wa Presidential Guard na kunyang'anywa silaha. Kisha walimchukua Waziri Mkuu Uwilingiyimana mpaka nyumbani kwake ambako walimuua yeye pamoja na mumewe. Watoto wao walisalimika baada ya kujificha nyuma ya fenicha.
Kisha askari wale kumi wa Kibelgiji walipelekwa mpaka kwenye kambi ya jeshi la Rwanda ya Kigali ambako waliteswa na kisha kuuwawa kwa amri wa meja wa jeshi la Rwanda aliyeitwa Bernard Ntuyahanga.

Usiku wa siku hii ya tarehe 6 April mpaka siku ya tarehe 7 April 1994, wanajeshi wa Rwanda na wahutu wenye msimamo mkali walikuwa wanapita nyumba kwa nyumba mjini Kigali wakiwa na orodha mkononi wakiua wanasiasa wenye ushawishi pamoja na waandishi wa habari.

Ndani ya usiku huu wa kwanza mawaziri ambao wana msimamo wa kati waliuwawa na wale ambao walisalimika walienda kujificha.
Walifanya hivi ili kuondoa uwezekano wowote wa kuundwa serikali kwa dharura.

Katika kikao cha kamati ya dharura ambacho pia Dallaire aliitwa kushiriki, Kanali Bagorosa alimpendekeza Augustin Bizimungu kuwa Mnadhimu mpya wa jeshi (mnadhimu rasmi wa jeshi alikufa kwenye ndege pamoja na Rais Habyarimana) lakini Dallaire alifanikiwa kuweka msimamo wa kumkataa Bizimungu kutokana na msimamo wake mkali. Hivyo Marcel Gatsinzi ambaye ni muhutu mwenye msimamo wa kati akachaguliwa kuwa mnadhimu mpya wa jeshi.

Baada tu ya kuteuliwa, Gatsinzi alifanya juhudi kubwa kuzuia jeshi lisijihusishe na mauaji ya watusi. Kitendo hiki kiliwaudhi mno akina Bagorosa pamoja na viongozi wengine wa juu wa jeshi ambao walikuwa na msimamo mkali. Hii ilipelekea siku kumi baadae Gatsinzi kuuwawa na nafasi yake kuchukuliwa na Augustin Bizimungu ambaye alipendekezwa awali na Kanali Bagorosa.


Mauaji yalikuwa yanasambaa kwa kasi kubwa ya ajabu. Kingine ambacho kilisaidia zaidi ni tamaduni ya watu wa Rwanda kutii mamlaka.
Amri zilikuwa zinatolewa kutoka Kigali na kisha kufika kwa Magavana wa majimbo ambao nao walielekeza wananchi wao kutekeleza amri hizo kwamba wanapaswa kumuua kila mtusi wanayemuona mbele yao.


Vijana wa Interahamwe ambao niliwaeleza huko nyuma ambao walikuwa wameandaliwa siku nyingi kwa silaha za jadi (mapanga) pamoja na mafunzo walikuwa wanaongoza wananchi wengine kufanya mauaji kwa majirani zao na marafiki zao.
Kila mtusi aliuwawa na hata wahutu ambao walikiwa wanawaficha au kuwahirumia watusi nao waliuwawa.

Katika miji mengine mauaji yalikuwa yanafanyika kwa urahisi kabisa kutokana na majirani kujuana vyema makabila yao.
Ila kwenye sehemu kama Kigali ambako kuna mchanganyiko mkubwa wa watu mauaji yalikuwa yanafanyika kwa uangalifu. Ni hapa Kigali ambako kwenye barabara viliwekwa vizuizi lukuki vya wanajeshi na vijana wa Interahamwe.

View attachment 718282

View attachment 718283

View attachment 718286


Vizuizi hivi vilikiwa ni kwa ajili ya kukagua vitambulisho vya taifa. Vitambulisho hivyo vilikuwa vinaonyesha pia kabila la mtu. Wahutu walikuwa wanaachwa na watusi wakiuwawa mara moja.
Kama raia alikuwa hajabeba kitambulisho basi alihukumiwa kutokana na muonekano wake. Kwamba watusi ni wembamba, warefu, sura nyembamba na pua ndefu. Raia wenye muonekano huu walikuwa hawaulizwi mara mbili, shingo zao zilikuwa ni halali ya panga za vijana wa Interahamwe na jeshi la Rwanda.

Mauaji yalisambaa nchi nzima isipokuwa kwenye maeneo ambayo yalikuwa chini ya RPF kama vile majimbo ya Ruhengeri, Byumba, Kibungo na baadhi ya maeneo ya Kigali.

RPF walikiwa wanasonga mbele kwa ufanisi mkubwa wakiteka mji baada ya mji.

Wahutu kwenye miji ambayo RPF walikuwa wanaiweka kwenye himaya, walikuwa wanaikimbia miji hiyo kuhofia wanajeshi wa RPF kulipiza kisasi kwa kuwauwa. Ndipo hapa ambapo ndani ya siku chache sana za mwezi April karibia Wahutu 500,000 walivuka daraja maeneo ya Maporomoko ya Rusumo kuja Tanzania na kupokelewa kwenye kambi za wakimbizi za Umoja wa Mataifa.

Sehemu nyingine zote za nchi mauaji ya watusi yaliendelea na yalifanyika kimkakati kabisa.

Kanali Théoneste Bagorosa ambaye alijipachika uongozi wa kamati ya dharura, kupitia kamati hiyo wao ndio walikiwa kama wanaongoza nchi. Bagorosa ndiye ambaye alikuwa anatoa amri na kuhutubia kwenye radio kusisitiza mauaji ya 'mende' kwenye nyumba yao. Bagorosa pia alifanya vikao na viongozi wa juu wa vikundi cha Interahamwe na Impuzamugambi na kuwapa maelekezo ya namna ya kuongoza wananchi kufanya mauaji hayo.

Vinara wengine wa mauaji haya alikuwa ni waziri wa Ulinzi Augustin Bizimana, kamanda wa Paratroopers Aloys Ntabakuze, na kiongozi wa Presidential Guard Protais Mpiranya.
Lakini pia kulikuwa na mfanyabiashara maarufu mjini Kigali aliyeitwa Felician Kabuga ambaye alikuwa anawasaidia rasilimali fedha Interahamwe ili waendelee na morali ya mauaji.

Siku ya tarehe 8 April, mauaji yakiwa yanaendelea kwa kasi, kanali Bagorosa akaitisha tena kamati ya dharura na kupendekeza serikali ya mpito.
Theodore Sindikubwabo aliteuliwa kiwa Rais wa muda huku Jean Kambanda akiteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa muda.
Baraza la mawaziri lote liliundwa na wanachama wa 'power wings' wa vyma vya siasa vya MRND na CDR.
Serikali hii ya muda iliapishwa siku ya tarehe 9 April 1994 na mara moja makao makuu ya serikali yalihamishwa kutoka Kigali kwenda Gitamara ili kuepuka mapigano ambayo yalikuwa yanategemewa kati ya RPF na vikosi vya serikali.

Kamati ya dharura ilivunjwa… lakini Bagorosa ndiye alikuwa kwa uhalisia anaiendesha nchi. Yeye ndiye alikuwa na maamuzi ya mwisho ya katika kila jambo. Serikali iliyotangazwa ilikuwa ni kama geresha tu ili kuhalalisha kile ambacho kilikuwa kinaendelea.

Mauaji yaliendelea, amri ilitolewa kwamba asiachwe hata mtusi mmoja akiwa hai. Hata mtoto mchanga.

Kuna matukio mengi sana ya kusikitisha ambayo yalitokea lakini sitaingia ndani sana kwenye sehemu hii kama ambavyo nimesema awali.

Lakini hatuwezi kusahau tukio la mauaji kanisani eneo la Nyarubuye.
Siku ya April 12, watusi wapatao 1,500 walikuwa wamejificha ndani ya kanisa katoliki la eneo hili.
Kasisi wa kanisa hili, Padre Athanase Seromba aliwatonya Interahamwe juu ya uwepo watusi kanisano kwake. Interahamwe walitumia bulldozer kulisambaratisha kanisa lote na waliomo ndani. Wale ambao walikuwa wanajaribu kukimbia walikatwa mapanga mpaka kifo.

Tukio lingine ambalo hatuwezi kulisahau ni maelfu ya watusi ambao walikuwa wamejificha kwenye majengo ya shule ya ufundi ya Kigali (École Technique Officielle) mahala ambako wanajeshi wa Ubelgiji sehemu ya UNAMIR walikuwa wameweka kambi. Baadae Ubelgiji iliondoa wanajeshi wake wote nchini Rwanda baada ya wale kumi waliotumwa kumlinda waziri mkui Uwilingiyimana kuuwawa na Presodential Guard.
Baada ya wanajeshi wa Ubelgiji kuondoka eneo hili, vijana wa Interahamwe walivamia na kuua watusi elfu kadhaa ambao walikuwa wamejificha hapa.


View attachment 718287

View attachment 718288


Japokuwa mauaji haya katika historia inakumbuka zaidi watusi na wahutu wachache kwamba ndio waliuwawa. Lakini mara nyingi tunasahau zaidi ya watu wa kabila la Watwa 30,000 ambao nao pia waliuwawa. Watu wa kabila la Twa walikuwa nao wanahesabika kama wasaliti. Wahutu wenye msimamo mkali waliwashutumu kwamba walikuwa wanawasaidia RPF kuingia kwenye miji.


Sasa basi;

Nilieleza kwamba Kagame alikuwa amefanikiwa kuingiza makomando 1,000 ndani ya Kigali ambao walikuwa wanalinda wanadiplomasia wa RPF katika Bunge.
Mauaji ya kimbari yalipoanza tu, vikosi vya serikali vilishambulia jengo la Bunge kwa lengo la kuua makoamndo wa RPF ambao walikuwa pale. Lakini makomando hawa wa RPF walifanikiwa kwa ufasaha kabisa kudbibiti vikosi vya serikali na kuwarudisha nyuma nje kidogo ya Kigali.

Kagame aliongoza RPF kupambana kutokea Kaskazini mwa nchi wakiwa wamejigawanya kwenye makundi matatu na huku wakitafuta namna ya 'kulink' na makomando ambao walikuwa ndani ya Kigali.

Ndani ya siku chache RPF walipambana kuelekea kusini wakiiweka kwenye himaya mji wa Gabiro na sehemu kubwa inayozunguka kigali upande wa mashariki na Kaskazini.
Hawakutaka kuivamia Kigali mara moja au Byumba, bali walipigana katika mtindo ambao walikuwa wanauzunguka mji wote wa Kigali kwa nje.

Mwishoni mwa mwezi April, RPF walikuwa wameweka eneo lote la mpaka wa Rwanda na Tanzania kwenye himaya yao. Kutokea hapa walisonga mbele kuelekea magharibi ya mji wa Kibungo na hatimaye kusini mwa Kigali.

Mpaka kufikia May 16 walikuwa wamekata mawasiliano ya barabara kati ya mji wa Kigali na Gitamara ambao ndipo ilikuwepo serikali ya mpito.
Mpaka kufikia June 13, RPF walikuwa wameuweka mji wa Gitamara kwenye himaya yao na kuilazimu serikali ya mpito kukimbia na kwenda kuweka makazi kwenye mji wa Gisenyi.

Mpaka hatua hii RPF walikiwa wamefanikiwa kuizunguka Kigali kila pande na pia ndani ya mji kulikuwa na makomando wao.

Tusisahau kwamba vikosi vya serikali walikuwa na silaha nzito zaidi askari wengi zaidi.
Kilichokuwa kinawasaidia RPF ni mbinu adhimu za kivita za Kagame.
Ni hapa ambapo Jenerali Dallaiire alimuita Kagame "master of psychological warfare".

Kagame alikuwa anachukua advantage ya kwamba… kwanza vikosi vya serikali walikuwa wameelekeza nguvu zao zaidi na akili zao katika mauji ya kimbari badala ya kuweka kipaumbele cha kupambana na RPF. Lakini mafanikio ya RPF kuchukua mji baada ya mji pia yalikuwa yamefanya vikosi vya serikali kuishiwa morali na Kagame alifanya hivi makusudi ndio maana akaiweka Kigali kuwa ya mwisho kuiteka.

Kwa hiyo sasa alikuwa anafanya mashambulizi ya ufanisi ya kushtukiza kwa masaa kadhaa pale Kigali na kisha ana-retreat. Wanasubiri masaa mengine kadhaa wanashambulia tena kisha wana-retreat. Tena na tena na tena. Alichokuwa anafanya ni kama kuwachekecha vikosi vya serikali na kuwachosha. Hii ilifanikiwa, kwani tarehe 4 July, RPF walifanya shambulio kubwa na kufanikiwa kuwashinda kwa urahisi kabisa vikosi vya serikali na kuiweka Kigali kwenye himaya yao.
Ilipofika tarehe 18 July walichukua mji wa Gisenyi na eneo lote la kaskazini magharibi ya Rwanda na kuifanya ile serikali ya mpito kukimbilia Zaire.

Mpaka hapa maana yake ni kwamba Rwanda yote sasa ilikuwa chini ya himaya ya RPF isipokuwa eneo dogo la kusini magharibi ambalo lilikuwa chini ya jeshi la Ufaransa walioingia Rwanda chini ya Oparesheni maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa hiyo, mpaka hapa ni rasmi kwamba RPF walikuwa wamezima mauaji ya Kimbari. Tarehe rasmi ya mauaji ya kimbari kukoma ni tarehe 15 July 1994 japokuwa Rwanda wenyewe wanaadhimisha siku hii kila mwaka tarehe 4 July kama siku ya Ukombozi wa Taifa na ni siku ya mapumziko.

Umoja wa mataifa unatoa takwimu kwamba watu 800,000 waliuwawa kwenye mauji yale huku serikali ya Rwanda yenyewe ikisisitiza kuwa ni watu 1,071,000. Inakisiwa kwamba Wahutu walikuwa ni 10% ya watu hawa waliouwawa.

Mauaji haya ni moja ya mauaji mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya dunia yetu hii.
Ni mauaji ambayo yanapaswa kutufunza mambo mengi sana. Kwamba ubaguzi, unyonyaji, ukandamizaji na kujikweza huzaa chuki kwa wale wanaoteswa. Chuki hii inaweza kufurukuta rohoni mwa watu hawa kwa miongo kadhaa lakini siku itakapopata ufa wa kujipenyeza, moto wake unaweza usizimike pasipo kuitafuna dunia.

Kuna vitu vingi vingi sana sana najua sijavigusia kwenye hitimisho langu hili. Naomba kwa makala hii tuishie hapa… huko mbeleni tukipata wasaa tunaweza kuirejea na kugusia yale ambayo nimeyaacha katika mfululizo huu.

Dunia yetu itakuwa mahala salama na pazuri pa kuishi endapo wote kwa pamoja tutajifunza kwamba hakuna aliye mbora kuliko mwingine. Tukijifunza kuheshimu utu, kujiheshimu na kuheshimiana. Tukiwa mawakili wa haki na umoja. Na sote tukikumbuka kwamba sisi ni wana wa baba mmoja.

Kwa makala hii naomba niishie hapa ili kupisha makala nyingine kuanza.


View attachment 718290
Paul Kagame akiwana bunti yake

View attachment 718291
Kigali leo hii



Muhimu: Ushauri ambao mmekuwa mkinipa kwa muda mrefu hatimaye nimeufanyia kazi. Ndani ya wiki mbili zijazo nitatoa kitabu changu cha kwanza kabisa cha simulizi ya Vipepeo Weusi. Kama ambavyo mmekuwa mkiniunga mkono kwenye nyuzi hizi kwa miaka mitatu sasa naomba pia sapoti yenu katika hatua hii mpya ambayo naichukua. Kwa pamoja tupambane kurejesha utamaduni wa watu kujisomea na tuinue kizazi kipya chenye maarifa.

Naomba baraka zenu ili project hii iwe na mafanikio na hatimaye nitoe vitabu vingi zaidi na zaidi.

Asanteni sana.



Habibu B. Anga 'The bold' - 0718 096 811
-Pure fake documentary,
Makala hii Ni fake kabisa,
ICTR ilithibitisha zaidi wahutu 500,000 waliuwawa na kagama force during the genocide and after month of genocide mkuu.
-Ongelea pia dark side ya mahakama ya ICTR mkuu, umebezi kwenye upande mmoja tuu.
-vipi pia RPA commandoo in interahamwe millitia Kama Robert kajuga leader wa interahamwe alikuwa mtutsi.
 
Ni kweli kabisa mauaji ya watusi, kuchoma moto nyumba zao kubaka wake zao na kuwapora ng'ombe zao yameanza mwaka 1959 na kuendelea mpaka kufikia kilele 1994
Elezea vizuri mkuu kwa Nini waliuwawa mwaka 1959?? Usiongee juju tuuu sawa haiwezekani mtu kuchukua kitendo hicho tuu kunakuaga na sababu ambayo mzito ilipelekea , elezea , kuwa mtu Kama umeenda shule ???
manzi james
 
Watusi wapo Tanzania baadhi ya mikoa kama kagera, kigoma na tabora hatujawahi kusikia hayo mambo ya kujiona bora kuliko wabantu wengine, watusi wapo Uganda zaidi ya watu 4m na hakuna huo ubaguzi watusi pia wapo Kongo hakuna hayo machuki sasa inakuwaje wahutu ndo wawe na mtazamo huo tu kama sio kusumbuliwa na inferiority complex?? Na kama connection za makazini wanazo watusi inakuwaje na kwenye uwanja huru wa business watusi pia wawashinde? As the big population ni wahutu wangeweza kuwa na strong connection, kukopeshana kuaminiana kuinuana kwani wao ndo wenye big number ya market pia. Hii inaonesha wahutu ni hodari sana kwenye mambo yahusuyo chuki na kubomoa (negative side) ila upande wa kuinuana wao kwa wao na kujengana (positive side) ni total failure. Kama nguvu iliyotumika kuandaa genocide ingetumika kuwainua wahutu ki elimu, ki uchumi na kisiasa huenda watusi ndo wangekuwa watumwa wenu sasa ila all in all mnasumbuliwa na inferiority complex na hamko tayar ku deal nayo na kuishinda so mko defeated coz hamjui mnapambana na nini
Watutsi walioko Tanzania Ni wahamiaji tuu, uwezi kuja kwenye nchi ya watu ukaanza hayo Mambo, wapo huku wamejifunza kuwa ubaguzi sio mzuri so wameacha , kwa kuwa wamejifunza kutoka kwa wanyeji. Sawa mkuu
 
Umemaliza ubishi mkuu,,, awali sikua nayajua haya lakini tangu nisome uzi huu wa Bold nimegundua kumbe kweli wahutu ni binadamu wa ajabu sanaa na ni wajinga namba moja africa, imagine mko wengi na mna kila kitu na hamuwezi kuondolewa madarakani wala kuathiriwa chochote na kakundi ka dogo ka jamii ya kitutsi, then why muwaue? Si mngewaacha tu? Je mumuue mwenzako kisa ana akili na kupenda shule? Yaani hakukua na njia nyingine mbadala ya kumdhibiti? Una muua vp sasa mtu unaemzidi nguvu?

Toka wapate uhuru wao ndio watawala, sasa ya nini mshindwe kuijenga nchini yenu na mkawezeshana wenyewe kwa wenyewe? Lakin utaona wahutu jinsi walivyo wajinga toka miaka ya 50 hadi 90 walikua wanapanga mauaji tu hahahahahahaha yaani walikaa miaka 40 kupanga kuwaua ndugu zao? Asee Rwanda ni moja ya nchi ya kipumbavu kuwai kutokea duniani... Case Closed... Bold shusha vitu kaka.
Fuatilia historian ya rwanda walivyokuwa wanaishi before Uhuru.
 
View attachment 698540
Mkuu IBUKA wameweka final survivors hivyo ni kazi yetu kutohoa je walikuwa wahutu na watutsi wangapi Rwanda sasa twende polepole

Data za world bank na UN zinasema rwanda ilikuwa na watu million 6 (nmeattach screenshot hapo chini)

Then link ya UN inasema wahutu walikuwa 84% na tutsi 15% mwaka 1994
Source: Outreach Programme on the Rwanda Genocide and the United Nations

hivyo basi 15% ya million 6 ni 900,000 si ndio.... taasisi ya watutsi IBUKA nlioweka inasema survivors ni laki 4 si ndio??
Source:Statistics - Survivors Fund

Tutsi laki 9 - Tutsi survivors laki 4 = unapata 500,000 deaths si ndio maana yake

Haya official statistics za UN na IBUIA zinasema waliokufa kwenye genocide walikuwa watu 1,078,000 source:Statistics - Survivors Fund

hivyo basi

1,078,000 - 500,000 = 578,000 je hawa ni jamii gani maana hawakuwa watutsi kwa mahesabu tuliopiga si ndio?? Hivyo tunakubaliana ni wahutu

Mpaka hapa nafkiri umeshaona kuwa statistics zangu nlizoweka za IBUKA bado ni credible

NB: Kuhusu Wikipedia.... inasema takwimu zake zimetolewa CIA world factbook ambayo ni credible sana maana serikali ya rwanda haiwezi andika namba ya wahutu na watutsi kwa sababu zilizo wazi kabisa ila wao kma serikali kwa sababu za kiusalama huwa wanakuwa na hizo data mapema kabisa hivyo sioni kma CIA world factbook as citee na wikipedia haiwezi kuaminika

2. Mkuu ni vizuri tuwe tunafanya utafiti kabla ya kulaumu.... Hao watutsi mwaka 1990 waliandikiwa barua kuruhusiwa kurudi Rwanda kma raia wa kawaida ila sio tu kwamba waligoma kuja ila hata barua haikuwahi jibiwa hivyo kma walitaka kurudi kwanni walikataa wito wa mwaka 1990??? Huoni wao walitaka kurudi kwa mabomu na risasi ili wapate madaraka pekee!! Source: Omdirigeringsmeddelande

3. Mkuu unaposema hapakuwa na double genocide what's your reference?? Mimi nmekuwekea ripoti ya UN kwenye post uliyoreply inayosema RPF kwa ushahidi waliopata iliua wahutu wengi sana au unafkiri hao wahutu laki 6 walikufaje mkuu???

Unasema genocide ni lazima iwe prepared.... Na lipo wazi kabisa kuendana na ushahidi wa General katumba nyamwasa aliyekimbia Rwanda kisa kutoboa siri za RPF alisema ndege ilivyotunguliwa waliambiwa wajiandae kusonga mbele ikimaanisha walipanga ile vita in advance je haiwi genocide

Pia Kumbuka kabla ya RPF kuja hakukuwa na genocide ila RPF walivyoanza kuchinja wahutu kule ruhengeri ndio ikatia hasara wahutu wa pande zingine wakaanza kuua watutsi kwenye maeneo mengineyo je unafkiri hawakupanga??

Huu hapa ushahidi kwamba genocide ilianzia ruhengeri ambapo watutsi wa RPF walichinja wahutu ndio kusababisha wahutu nao kuanza kuua tena hii ilikuwa 1991https://www.google.com/amp/s/arnaudemmanuel.wordpress.com/2008/05/23/rwanda-rpf-crimes/amp/

Pia nmeweka hapo confession ingawa unasema hauiamini ila ilitumika kwenye kesi ntakupa reference..... Jamaa alikiri walitumwa kuua wahutu wote mbele yao je hiyo sio planned genocide too??

Kuhusu dallaire nimeshasema hawezi kuaminika maana alitangaza kuwa Rwanda imewekewa vikwazo wasipewe silaha ila ndio huyo huyo kwa siri alikuwa anawapa silaha RPF kuwamaliza wahutu je unaaminije kauli za huyu msaliti?? Alidai hakuona mtutsi akiua muhutu ila ripoti ya UN inasema watutsi walichinja wahutu je huyo dallare bado anaaminika??

Kuhusu uchafu wa dallare pia soma huu utafiti Omdirigeringsmeddelande

Hitimisho lako nakubaliana nalo ingawa unaposema ''ANGALAU '' sidhani ni sahihi sababu nmeshakupa ripoti nyingi na article zinazoonyesha RPF wanahusika na vifo vya wahutu kibao sasa kwanini bado huoni ina deserve kuitwa RWANDAN GENOCIDE...... remember Hutus died kuliko tutsis thats still enough to call it RWANDAN genocide if not HUTU genocide

Ahsante

Ushahidi huu hapa jinsi watutsi walivyochinja wahutu zaidi ya laki 5 Rwanda mara baada ya kupindua nchi

THE SLAUGHTER OF HUTU REFUGEES IN DRC - RWANDA DEMOCRACY WATCH

The Rwandan Patriotic Front (HRW Report - Leave None to Tell the Story: Genocide in Rwanda, March 1999)

Kibeho 1995: a massacre forgotten in Rwanda’s 20-year history - Jambonews EN

Kabila Army's Mass Murder of Rwandan Hutu Refugees


Lakini ndani ya 100 days kulikuwa na wakimbizi tunawaweka kundi gani hao .
 
Robert
KILIO CHA MIFEREJI YA DAMU IENDAYO ETHIOPIA



RAI: Inapendeza zaidi na ni busara zaidi, uzi huu ukawa ni chanzo cha kuchochea mijadala ya kufikirisha na hoja mujaribu zenye kutufanya kukuna mbongo zetu na kuelimika. Si vyema kutumia uwanja huu kuleta malumbano ya kikabila au kitaifa na kutukanana.
Tunaweza kutofautiana kiitikadi na bado tukala meza moja, tunaweza kutofautiana kikabila na bado tukawa marafiki na tunaweza kutofautiana kwa hoja na bado tukaheshimiana.

Tuchochee udadisi, kufikiri na kushindanisha hoja. Si matusi.


Habibu.


9c7748bda5c53f35a22becff756699a7.jpg



SEHEMU YA 11


Kwenye sehemu ya kumi tulijadili namna ambavyo serikali ya rais Habyarimana walifikia makubaliano na RPF ya kusitisha mapigano lakini baadae mauaji ya watusi yaliendelea na kumfanya Kagame kuanza tena mashambulizi na kulishinda jeshi la serikalinkwa urahisi kabisa.
Tuliona namna ambavyo Habyarimana safari hii aliomba mazungumzo na Kagame ili kusitisha makubaliano.


Tuendelee…


Mazungumzo ya Uganda yalichukua siku mbili na kisha kurejea tena Arusha.
Nchi za Ulaya zilikuwa zinamtaka Kagame arejeshe nyuma vikosi vyake kurudi kwenye eneo ambalo walikuwa wanalishikilia kabla ya February.

Baada ya mabishano makali ya siku kadhaa huku Kagame akitishia kwamba ataanza tena mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali.

Ndipo hapa ambapo pande zote mbili walifikia makuabaliano.

Kwamba;

Kagame atarudisha nyuma vikosi vyake mpaka kwenye maeneo ambayo walikuwa wanayashikilia kabla ya mwezi February, 1993. Lakini maeneo hayo mapya ambayo RPF walikuwa wameyaweka kwenye himaya yao baada ya Febrary, pindi tu RPF wakirejesha nyuma vikosi vyao kutokana na makubaliano hayo basi maeneo hayo yatatengwa kama 'De-militarised zone'. Kwamba serikali haitaruhusiwa kuingiza wanajeshi wake kamwe kwenye maeneo hayo.

Makubaliano haya yalikuwa ya maana sana kwa Kagame, kwani hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa rais Habyarimana kukubali rasmi kushindwa. Japokuwa bado kuna makamanda ndani ya RPF walikuwa wanahisi kama Kagame amemwachia Habyarimana upenyo mkubwa zaidi wa kupumua, lakini Kagame mwenyewe alisimamia msimamo wake thabiti kabisa kwamba anataka kulinda taswira chanya ya RPF kwenye jumuiya ya kimataifa na kuwaonyesha kuwa RPF wako tayari pia kushughulikia migogoro kidiplomasia.

Lakini kipindi mazungumzo haya yanaendelea na makubaliani yanafikiwa, nyuma ya pazia Rais Juvenile Hibyarimana akishirikiana na serikali ya Ufaransa walikuwa wanaunganisha nguvu ya waunga mkono wao chini kwa chini ili kuipinga RPF. Katika mpango wao huu walienda mbali hata kiwajumuisha viongozi wa CDR.

Kadiri muda ulivyokuwa unaenda kukaanza kuibuka mkanganyiko. Kuna kundi la watu ndani ya MRND na CDR walitoa tamko kwamba hawakubaliani na jinsi ambavyo Ufaransa inajiingiza kwenye uratibu wa mkakati huo wa chini kwa chini. Waliona kama vile wanatwanga maji kwenye kinu. Yaani wanapambana kumuondoka "mkoloni mweusi" (watusi) na wakati huo huo viongozi wao wanaacha mwanya wa mkoloni mweupe kurudi (Ufaransa). Ndipo hapa kwa hasira wakaanza kushinikiza kwamba mkataba ulio sainiwa Arusha uheshimiwe.

Lakini pia bado walibakia lile kundi lenye msimamo ambalo walikuwa tayari lolote lifanyike (hata kama ikibidi kushirikiana na Ufaransa) kuhakikisha kwamba watusi wanaondoshwa ndani ya Rwanda.

Ndipo hapa kwenye kipindi hiki kulipamba moto vuguvugu la 'Hutu Power'.

Vyama vyote vya siasa ndani yake viligawanyika katika makundi mawili. Kulikuwa na kundi ambalo walikuwa na msimamo wa kati (moderate) ambao waliunga mkono mazungumzo ya Arusha. Alafu kulikuwa na kundi la wale wenye msimamo mkali, ndio hawa waliitwa 'Power Wing' (Hutu Power). Hawa wao walikuwa tayari kufanya lolote na kwa gharama yoyote ile kuhakikisha kwamba watusi hawawi sehemu ya uongozi wa nchi na hawaishi Rwanda kama raia mwingine.

Hiki ndicho ambacho kilitokea kwenye vyama vyote vya siasa nchini Rwanda katika kipindi hiki. Kila chama kilikuwa na hizi 'two wings'. Lakini wing ambayo ilikuwa na nguvu na ushawishi kwenye kila chama ilikuwa ni 'Hutu Power'.



61cdcbc6276b6bb0e155365264282c61.jpg

Rais Juvenile Habyarimana na ujumbe wake kwenye mkutano Arusha


Hapa nchini kwetu Tanzania katika vyama vya siasa kwa miaka mingi tumekuwa na kasumba katika vyama vyetu vya siasa kwa kila chama kuwa na kikundi cha "ulinzi" cha chama. Pengine kuna walianzisha utaratibu huj walikuwa na sababu za msingi mpaka leo hii kuwa na 'Green Guard' ndani ya Chama Cha Mapinduzi na 'Red Brigade' ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Lakini kama tungekuwa tunaijua historia na kutumia mafunzo yake kujisahihisha si dhani kama tungelikumbatia kasumba hii ya vikundi vya ulinzi.




Kuibuka kwa Intarehamwe na Impuzamugambi

Intarahamwe na Impuzamugambi vilianza kama vikundi vya ulinzi katika vyama vya MRND na CDR kama ambavyo hapa kwetu Taznania tuna Green Guard na Red Brigade ndani ya CCM na Chadema.


Interahamwe
Maana halisi ya neno hilo ni "wanaopambana pamoja". Ni muunganiko wa maneno mawili ya kihutu, 'intera' ambayo ina maanisha 'kazi' na 'hamwe' ikimaanisha pamoja. Kwa nini sijasema "wanaofanyakazi pamoja" na badala yake nimesema "wanaopambana pamoja".
Hili neno 'kazi' (work) lilikuwa linatumika kama kauli mbiu katika radio za kibaguzi za kihutu wakimaanisha 'shughuli ya mauaji' kwa kutumia panga. Kwa hiyo lengo lao la kuchaganya neno hili halikiwa kwa ajili ya kumaanisha kazi ya uzalishaji bali ni kazi ya mauaji.

Kikundi hiki cha kihutu kilikuwa chini ya chama cha siasa cha MRND.
Ajabu ni kwamba kiongozi wa Kitaifa alikuwa ni muhutu aliyeitwa Robert Kajuga. Kajuga familia yake ilikuwa ni ya Kitusi lakini baba yake alifanikiwa kupata nyaraka za kiserikali ambazo ziliipa utambulisho familia yake yote kama wahutu. Kajuga mwenyewe alikuwa anafanya kazi kubwa sana kuficha ukweli wa mizizi ya familia yake ya Kitusi. Moja ya visa ambavyo vinasisimua sana ni namna ambavyo Kajuga alijitahidi kuificha familia yake Hôtel des Mille Collines ndani ya Kigaki kipindi mauaji yalipoanza. Tutakirejea kisa hiki hapo baadae.



Impuzamugambi
Kikundi hiki nacho pia cha kihutu kilikuwa chini ya chama cha CDR. Japokuwa hakikuwa kikubwa au maarufu kama Interahamwe lakini vyote viliwi vilikuwa na lengo moja linalofanana.

Makamanda wa kikundi hiki walikuwa ni viongozi wakuu wa chama cha CDR, yaani Hassan Ngeze na Jean Bosco Barayagwiza.

Kipindi mauaji ya kimbari yalipoanza kikundi hiki kilifanya kazi bega kwa bega na Iterahamwe kama ambavyo tutaona hapo mbele kidogo.



Vikundi vyote hivi viwili vilijizolea umaarufu mkubwa ndani ya Rwanda na vijana wengi wa Kihutu waliojitafsiri kama 'wazalendo' wa nchi yao walijiunga navyo.

Wahutu wenye msimamo mkali ndani ya vyombo vya usalama ambao walikuwa na nyadhifa za juu kama vile mkui wa jeshi la polisi na mnadhimu mkuu wa jeshi la Rwanda walianza kuweka utaratibu ambapo wanachama wa vikundi hivi walikuwa wanapatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi.
Kwa hiyo ndani ya muda mfupi sana vikundi hivi nguvu yake na ushawishi wake ukawa mkubwa kuzidi hata namna ambavyo watu walitegemea.

Japokuwa alikaa kimya na kufumbia macho lakini hii haikuwa dalili nzuri kwa uongozi wa Rais Habyarimana. Kwa sababu aliona fukuto ambalo lilikuwepo chini kwa chini. Kwamba kadiri ambavyo alikuwa anaviacha vikundi hivyo vikue na kuwa na nguvu zaidi, siku vikilipuka kwa ghasia kubwa nchi hiyo haitakuwa salama tena. Na si kama alijali zaidi usalama wa nchi bali aliogopa zaidi kupoteza madaraka kutokana na presha ambayo atapewa na jumuiya ya Kimataifa.


75d6e0719bd6a12cc9295f839286864c.jpg

7b98de27f56aee8b8751b4960c25afa5.jpg

7b4a1b9e2e0f3b952342c62aaa43a5a9.jpg

Wanachama wa Interahamwe na Impuzamugambi



Lakini pia nilieleza huko nyuma kwamba vuguvugu hili la Hutu Power lilikuwa linaratibiwa na 'inner cirlce' ya Akazu ambayo ilikuwa inafahamika kama 'le clan de madame'.
Hawa walikuwa ni maswahiba na ndugu wa karibu kabisa wa Agathe Hibyarimana, mkewe Rais.

Kwa upande mwingine pia kitendo cha Rais Hibyarimana kuendelea na mzungumzo ya Arusha kulikuwa kunazidi kuwachukiza wahutu wenye msimamo mkali na Habyarimana alihisi kabisa hasira hizi zinaweza kufikia kilele cha wahutu hao wakamuondoa madarakani kwa nguvu.

Hivyo basi Habyarimana tegemeo lake pekee katika kipindi hiki cha sintofahamu kubwa lilikuwa ni jumuiya ya kimataifa na RPF.

Habyarimana alikata shauri sasa kuingia kwa miguu yote miwili kwenye mazungumzo ta Arusha. Lengo lake lilikuwa ni kwanza kupata huruma na kuaminika na jamii ya kimataifa na pili aliamini kuwa kama RPF wangekuwa sehemu ya uongozi wa nchi basi ilikuwa ni njia nzuri ya kuwadhibiti wahutu wenye msimamo mkalai.

Safari hii kwenye mazungumzo alikubaliana karibia na kila sharti la RPF. Kwa mfano alikubali 40% ya jeshi jipya la nchi ambalo litaundwa liwe na wanajeshi wa RPF. Alikubali pia uongozi wa juu wa jeshi 50% wawe ni RPF na masuala mengine mengi zaidi ambayo yalikuwa ni ushindi mkubwa kwa Kagame na RPF.
Mkataba wa makubaliano haya ulisainiwa tarehe 4 August 1993.

Pia waliweka makubaliano kwamba katika kipindi hiki cha mpito lazima amani ya nchi isimamiwe na jeshi la kimataifa ili kuepuka upande wowote, wa serikali au RPF kutumia mwanya huo vibaya kujiongezea madaraka au ushaiwishi.
Ndipo hapa mwezi octoba jeshi maalumu la Umoja wa Mataifa vikosi vilivyopewa jina la UNAMIR (United Nations Assistance Mission for Rwanda) likiongozwa na Jenerali Roméo Dallaire raia wa Canada liliingia nchini Rwanda kwa ajili ya kulinda amani.

Kipengele kingine ambacho Kagame alikitaka kilikuwa ni kutaka uwakilishi wa RPF ndani ya Bunge la Rwanda katika kipindi hiki cha mpito.

Bunge la Rwanda muundo wake uko hivi; kuna 'Uper Chamber' (au Sena kwa kinyarwanda (senate kwa umombo ) na kuna 'Lower Chamber' (au Umutwe w'Abadepite (chamber of deputies kwa umombo).
Muundo na mfumo wa ufanyaji kazi wa Chamber hizi mbili ni kama vile Congress ya Marekani (House of Representatives na Senate).

Rais Hibyarimana alikubali kutoa nafasi za uwakilishi kwa RPF katika Chamber of Deputies.

Uhalisia ni kwamba Kagame hakuwa na haja sana na nafasi hizo za uwakilishi bali alikuwa ametumia akili ya mbali sana ambayo kwa kipindi hiki hawakumshitukia.
Kagame aliwaeleza kwamba, wanadiplomasia wake hao ambao wataiwakilisha RPF kwenye Bunge ni lazima wapewe ulinzi na wanajeshi wake wa RPF na si jeshi la serikali au UNAMIR ya umoja wa mataifa. Na alipendekeza kwamba itawapasa RPF kuingiza wanajeshi 1000 kwenye mji mkuu wa Kigali kwa ajili ya ulinzi wa wanadiplomasia wao.

Mwezi December 1993, kupitia mpango wa vikosi vya umoja wa Mataifa vya UNAMIR uliokuwa unaitwa 'operation Clean Corridor', wanajeshi 1000 wa weledi (special forces) kutoka RPF ya Kagame waliruhusiwa kuingia kwenye mji mkuu wa Kigali na kuweka makazi yao kwenye majengo ya Bunge.

Hii ndio moja ya akili adhimu ambayo Kagame amejaaliwa (psychological warfare)… alikuwa amefanikiwa kuingiza special forces wake elfu moja ndani ya Kigali tena kwa ruhusa ya serikali bila kumwaga hata tone la damu au kufyatua hata risasi moja.
Wanajeshi hawa 1000 aliowaingiza ndani ya Kigali walikuja kuwa nguzo ya ushindi wake dhidi ya wahutu na kuingia madarakani kama ambavyo tutaona hapo mbeleni.


Wahutu wenye msimamo mkali hili lilikuwa ni tishio kubwa sana kwao. Waliona kila dalili ya 'adui' yao kurejea kwenye kiti cha enzi.

Mbaya zaidi, nchini Burundi ambako nako kwa miongo mingi serikali ilikuwa inaendeshwa na Watusi mwezi october kwa mara ya kwanza wananchi walimchagua Melchior Ndadaye kuwa rais wa kwanza wa Burundi mwenye asili ya Kihutu.
Ndadaye alikuwa ni msomi na mwanazuoni, mtu wa fikra pevu. Huyu hakuwa mtu wa itikadi ya 'Hutu Power' bali alikuwa amelenga kumaliza utengano wa kikabila ndani ya Burundi.


Alitaka nchi hiyo iongozwe kwa pamoja. Akaanza kufanya mabadiliko kwenye jeshi ambalo lilitawaliwa na watusi pekee na kuanza kuwajumuisha wahutu.

Wanasema kwamba uking'atwa na nyoka hata ukikanyaga jani unashituka, ndicho ambacho watusi wa Burundi kilichiwashitua. Japokuwa Ndadaye alikuwa najaribu kuiunganisha nchi lakini watusi wa Burindi walimuona kama tishio na anataka kuwaletea maswahibu kama yale ambayo yanatokea Rwanda.

Kwa hiyo wanajeshi wa Kitusi wenye msimamo mkali walimtandika risasi Rais Melchoir Ndadaye mwishoni mwa mwezi octoba na kuzua vita kubwa ya kikabila nchini Burundi.


Wahutu wa nchini Rwanda walitumia kitendo cha muhutu mwenzao kupigwa risasi nchini Burundi kuhalalisha propaganda yao ya siku nyingi kwamba Watusi kamwe hawawezi kukubali kutawaliwa na Wahutu na watafanya chochote wawezacho ili kuitawala Rwanda na kuwafanya wahutu raia wa daraja la pili.

Propaganda hii safari hii ilikuwa na msisimko kwa wapokeaji huko mtaani hasa baada ya kushuhudia Kagame ameingiza wanadiplomasia wake ndani ya Bunge la Rwanda na wanajeshi elfu moja wa RPF ndani ya Kigali.

Kwenye jumuiya ya kimataifa Kagame na Habyarimana walikuwa wanapongezwa kwa hatua hiyo ya makubaliano. Lakini mtaani ilikuwa kana kwamba petroli imemwagwa ardhini na njiti ya kiberiti imeshikwa kiganjani tayari kufanya mlipuko.

Habyarimana alijua. Na Kagame alijua. Kwamba wakati ulikuwa uko karibu. Wakati ambao hakuna mtu aliombea ifikie. Wakati ambao utautikisa ulimwengu kwa mauaji ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwenye historia ya karibu. Wakati wa jino kwa jino, msumari kwa msumari… wakati wa panga na shingo za watu.

e882b6735139b877adae8bf71fd98953.jpg

Rais wa zamani wa Burundi marehemu Melchoir Ndadaye

Nikirejea tutajadili kuuwawa kwa Rais Habyarimana na Kuanza kwa mauaji yenyewe ya Kimbari.


Stay here.




Habibu B. Anga 'The Bold'- 0719 096 811
To Infinity and Beyond

Please Follow, subscribe and WhatsApp
Robert kajuga likuwa muhutu,
Mmmmmh rekebisha bro
 
Yani wewe unaona sawa kabisa mababu zetu kupigwa, kuuwawa, kukimbizwa na kufukuzwa kwenye taifa lao, lakini huon kama ni sawa pia wazazi wetu kurudi kwenye taifa lao


Kama unadhan wahutu hatuwawezi/tusingewaweza, ni nani alioko madarakani? aliingiaje???


walitutimua tukarud tukachukua kilichokua chetu, na ukumbuke tu, kabla hawajatutimua miaka ilee, sisi ndio tulikua watawala
Duuu aisee huko kwenu MUNGU awasaidie nyie watu, hizo fikila zenu hizo, one day zitawapeleka kubaya Sana, Sasa umethibitisha kuwa nyie mnaona kutawala Ni haki yenu , na hamko tayari kuwa kitu kimoja na wahutu, hip Ni shida tayari,
Nimewahi kumsikia kagame akiongea Baada ya kutoka" BBC untold story rwandan genocide", alisema kuwa" tulikuwa tunambana haki yetu tangu tuko wadogo baadhi yetu" , Sasa kutokana hio nimejua kuwa watutsi mnaona kuwa kutawala Ni haki yenu , duuu .
zitto junior , wanaitaji maombezi.
 
Tz nilifanya kazi now sipo Tz siwez kaa nchi dk 2 umeme umekatika wakat wanaita nchi ya viwanda sijui SGR sijui makinikia mnakamata mnabakiza Gold bars zinaenda Nje huo ni upumbav wa Rang nyeus ya mkaa
We Ni muongo Sana Mara nipo Kigali, Ethiopia , Mara Virginia Mara wapi acha uongo , inwezekana ukawa ata butare au rusumo😎😎😎😎😁
 
Back
Top Bottom