Papushikashi
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 10,963
- 13,287
safi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
View attachment 854807
Kitabu changu cha kwanza NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI & UJASUSI kiko tayari na kitakuwa mkononi mwako mwezi huu september... kaa tayari
So vizuri kufananisha Rwanda na Tanzania, nenda dodoma ukahesabu wadada watoahuduma poa kutoka Kigali kisha uhesabu na hapo Kigali Kuna wagogo wangapiKwenu Tz kwenye siasa nzuri na Vyama vingi Umeme tu umewashinda na mna mali kila mahala lakin shule hazina hata vyoo hospital watu wanalala chini Uvira hakuna wakimbiz wa Rwanda kajipange upya Rwanda yasonga Mbele Kagame is Our President forever Haya sema kingine piga kelele dunia ife ifufuke Kagame ndio President wacu...
Naunga maono hoja; Rip prof jwani mwaikusaHuwa nahisi Mtikila pia 'aliuwawa na hawa watu'
Kinapatikanaje?View attachment 854807
Kitabu changu cha kwanza NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI & UJASUSI kiko tayari na kitakuwa mkononi mwako mwezi huu september... kaa tayari
Ndg Bold inaonekana hata huku hupiti vipi kitabu tunakipataje huku mbeya.View attachment 854807
Kitabu changu cha kwanza NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI & UJASUSI kiko tayari na kitakuwa mkononi mwako mwezi huu september... kaa tayari
ina huzunisha sana! WATANZANIA TUJIFUNZE KWA HAWAHistoria ya Kweli ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
![]()
KILIO CHA MIFEREJI YA DAMU IENDAYO ETHIOPIA
SEHEMU YA KWANZA
“..kama unasoma ujumbe huu, muda huu… uko mpweke! Pengine ushahidi pekee uliobakia ni kijipande hiki cha maandishi. Sijui kama kuna yeyote kati yetu aliyesalimika kufika kizazi chenu mwaka huu mtakaosoma andishi langu. Sijui hata kama tumeshinda au tumeshindwa vita tunayopigana sasa hivi. Sijui, lakini naamini mwaka huu mliopo nyinyi sasa mwaweza kuwa na jibu sahihi. Vyovyote vile lakini jambo lililo dhahiri ni kwamba hakuna yeyote wa kizazi chetu mliye naye sasa hivi kwenye miaka yenu muusomapo ujumbe huu. Kwa hiyo wacha niwaeleze sisi tulikuwa akina nani, na kwa namna gani tulipambana mpaka tone la mwisho la damu mwilini mwetu ili kutetea kizazi chetu kisifutwe juu ya uso wa dunia. Wacha niwaeleze namna ambavyo japo tulikamuliwa damu mpaka kutiririka kufanya mifereji lakini lakini tulisimama kutetea kizazi chenu na ninyi watoto wetu. Wacha niwaeleze kisa kilichotikisa ulimwengu. Wacha niwaeleze kuhusu mifereji ya damu kwenda Ethiopia.!”
– Habib Anga alias The Bold
March 21, 1994 maeneo ya Uganda ambayo yanapakana na Rwanda, katika ziwa viktoria serikali ilituma vikosi vya jeshi kudhibiti eneo hilo kwa hali ya dharura. Agizo hili la serikali kutuma jeshi halikuwa kwa ajili ya kidhibiti eneo hilo kutoka kwa adui bali agizo lilikuwa ni kudhibiti eneo hilo dhidi ya maiti, maiti za binadamu. Sio maiti mbili au tatu, si mamia bali maelfu ya maiti za binadamu ambazo zilikuwa zinaingia ziwani Victoria zikiletwa na maji ya mto Kagera.
Maiti hizi zilikuwa nyingi kwa maelfu kiasi kwamba mapaka zilikuwa zinafanya maji yatoe harufu. Serikali ya Uganda ilituma jeshi eneo hili ili kudhibiti eneo hili maji yake yasitumiwe na wananchi kwa matumizi ya nyumbani au shughuli za uvuvi. Lakini jeshi lilikuwa eneo hili ili kuhakikisha kuwa taharuki iliyozuka baada ya maelfu ya miili hii kuonekana haigeuki na kuvuruga amanai katika eneo hili. Lakini pia jeshi lilikuwa hapa ili kubaini miili hii ilikuwa inatoka wapi.
Kadiri ambavyo jeshi la Uganda lilivyokuwa linafuatilia kwa kurudi nyuma kufuata mto Kagera ndivyo ambavyo walizidi kubaini kwamba maiti hizo zinaletwa na maji kutoka tawi la mto Kagera lililopita kusini mwa Rwanda. Na kadiri ambavyo walizidi kufuata chanzo cha maiti hizo zinakotoka ndivyo ambavyo walikuwa wanaikaribia Rwanda na maji ya mto rangi yake kuwa nyekundu zaidi.
Wanajeshi wa Uganda ambao walishiriki kwenye ukaguzi huu wa mto huu wanakiri kwamba licha ya baadhi yao kupigana mstari wa mbele kwenye vita mbali mbali lakini hakuna yeyote kati yao ambaye aliwahi kushuhudia ukatili mkubwa wa kiasi hiki.
Siku hii jeshi la Uganda linakisia kwamba waliokota si chini ya miili elfu kumi ya binadamu na yote ilionekana kuletwa na maji ya mto Kagera kutoka nchini Rwanda.
Ajabu ni kwamba miili yote hii ilikiwa inamfanano fulani. Maiti zote zilikuwa za watu warefu, wembamba, wenye nyuso ndefu na pua za kuchongoka. Haikuhitaji kufikiria sana kufahamu kuwa maiti hizi zilikuwa za watu wa kabila la Tusi (Tutsi).
Miezi kadhaa baadae ndipo ambapo jeshi la Uganda na ulimwengu wote walikuja kuelewa kwa nini maiti zilikuwa zinatupwa mto Kagera. Ni ujumbe gani ambao ulikuwa unajaribu kutumwa.
Kwamba Watusi nchini Rwanda walikuwa waapenda kujisifu kuwa mababu zao wana asili ya nchi ya Ethiopia. Kitendo hiki cha watesi wao kuwatupa mtoni, walikuwa wanawaua na wakiwa wanatupa maiti zao mto wanawaambia kwamba “wanawasafirisha warudi kwao Ethiopia ambako wamekuwa wakijisifu ndio asili yao.”
Sio kwamba jeshi la Uganda hawakuwa na taarifa juu ya hali tete iliyopo Rwanda kwa muda wa karibia wiki nzima iliyopita bali hawakujua kama hali hiyo tete ilikuwa ni ya kinyama kiasi hicho.
Wanajeshi hawa wa Uganda walikuwa wameshikwa na bumbuwazi na vihoro vilivyo wapasua mioyo kwa kuona miili hii elfu kumi ya binadamu isiyo na uhai. Kitu ambacho walikuwa hawakijua na hakuna ambaye alidhahania ni kwamba ndani ya siku mia moja zijazo ulimwengu ulikuwa unaenda kushuhudia moja ya tukio la kikatili zaidi tangu kuubwa kwa ulimwengu. Karibia maiti za binadamu milioni moja zikiwa zimetapakaa mitaani nchini Rwanda iking’ong’wa na nzi na kuliwa na mbwa.
![]()
GENESIS
Rwanda: Kabla ya Ukoloni
Asili rasmi kabisa ya watu wa kwanza kuishi katika eneo ambalo leo tubalitambua kama nchi ya Rwanda ni watu wa kabila la ‘Twa’ (Watwa). Kabila hili la wawindaji si la kibantu bali ni sehemu ya makabila yanayotambulika na wanahistoria kama ‘pygmy’ ambao sifa yao kuu ni ufupi. Mtu mzima anayetoka makabila ya namna hii anakadirwa kuwa na wastani wa urefu chini ya sentimita 150. Watwa waliishi Rwanda enzi za kale sana miaka ya 8000 BC na 3000 BC.
Kuanzia miaka ya 700 BC mpaka 1500 AD makabila ya Kibantu kutoka maeneo ya jirani yalianza kuhamia eneo hili.
Kuna nadharia mbali mbali kuhusu ni namna gani haswa makabila haya ya kibantu yalihamia hapa na baadae kupelekea kutokea Makabila ya sasa ya Wahutu na Watusi.
Nadharia ya kwanza inadai kwamba; Wahutu ndio walikuwa wa kwanza kuhamia eneo hili na kuanzisha shughuli za kilimo. Baadae watu wenye asili ya Ukushi (Watusi wa sasa) nao wakahamia kwenye eneo hili na kulitawala.
Nadharia ya Pili inadai kwamba; kuna uwezekano kwamba Watusi si wakushi bali ni wahamiaji tu kutoka maeneo ya jirani kipindi hicho cha kale ambao walihamia na kujichanganya na jamii waliyoikuta hapo (Wahutu) lakini wao walikuwa wafugaji. Chini ya nadharia hii inadai kwamba kuibuka kwa Wahutu na Watusi hakukutokana na kuwa na utofauti wa kinasaba au asili ya mababu bali ulitokana na utofauti wa kimadaraja/matabaka ya kijamii.
Tabaka la wale walio wa daraja la juu ambao walikuwa wafugaji walijitanabaisha kama Watusi wakati ambapo tabaka la chini ambao walikuwa wakulima walijitanabasha kama Wahutu.
Makabila haya yote matatu, Watwa, Wahutu na Watusi wanazungumza lugha moja na kwa wote kwa pamoja wanajulikana kama ‘Banyarwanda’.
Idadi ya watu ilipoongezeka katika eneo hili walianza kujitambua kupitia makundi madogo madogo yaliyoitwa ‘Ubwoko’ au ‘koo’ kwa kiswahili. Ilipofika katikati ya miaka ya 1700 koo nyingi ziliungana na kuunda ‘Falme’.
Moja ya Falme ambazo zilikuwa imara zaidi ulikuwa ni ‘Kingdom of Rwanda’ ambayo watawala wake wote walitokea katika koo ya Kitusi ya Nyiginya.
Ufalme huu ulifikia kileleni kipindi cha utawala wa Mfalme Kigeli Rwabugiri chini ya falsafa yake ya kujipanua na kuteka falme nyingine na kuzifanya sehemu ya Kingdom of Rwanda.
Chini ya Mfalme Rwabugiri alianzisha mfumi wa kiuchumi wa ‘ubuhake’ na baadae ‘uburetwa’.
Katika mifumo yote hii miwili, iliwanufaisha zaidi Watusi na kuwafanya Wahutu kama vijakazi wao kuwafanyia kazi za uzalishaji na kuwa askari vitani kwa ujira wa kupata fursa ya kumiliki mifugo na kutumia ardhi.
Watusi walipaa juu zaidi na kuwa raia daraja la kwanza ma Wahutu kubakia kuwa tabaka la chini kabisa ndani ya Kingdom of Rwanda.
Rwanda: Wakati wa Ukoloni
Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 ulilitoa eneo hili kuwa koloni la nchi ya Ujerumani. Wajerumani walitawala eneo hili kwa kushirikiana na Mfalme na hivyo kuwapa wepesi wa kutawala koloni bila kuwa na askari wengi wa kijerumani ndani ya ardhi ya Rwanda. Yuhi V Musinga ndiye walikuwa Mfalme wa Rwanda kwa kipindi hiki na anakumbukwa zaidi kwa kuwapokea Wajerumani kwa mikono miwili.
![]()
Ikulu ya Mfalme wa Rwanda maeneo ya Nyanza
Wajerumani ndio walikuwa watu wa kwanza kuanza kuwapandikizia Watusi kasumba ya kuwa wao si Wabantu. Wakoloni wa Ujerumani ndio ambao walieneza propaganda kwa kuwafundisha Watusi kwamba kutokana na tafiti zao za kina wamegundua kwamba wao (Watusi) mababu zao wa kale walihamia eneo hilo kutokea Ethiopia. Hivyo wakawashawishi kuamini kwamba Watusi wana vinasaba vya ‘uzungu’ (Caucasian) na hivyo ni wao pekee ndani ya Rwanda walistahili kupata nafasi za ajira kusaidizana kazi na wazungu chini ya utawala huo wa Wajerumani.
Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Ubelgiji iliziteka Rwanda na Burundi kutoka mikononi mwa Ujerumani na mwaka 1919 League Of Nations ilizifanya rasmi nchi hizo kuwa makoloni ya Ubelgiji.
Mwanzoni Wakoloni wa Ubelgiji walianza kuitawala Rwanda kwa mtindo ule ule wa kushirikiana na Ufalme lakini baadae wakajilimbikizia madaraka yote ya kutawala kama ambavyo walifanya kwenye koloni lao la Kongo.
Baadae wakaanza ‘kutaifisha’ mali za Wanyarwanda katika mfumo wa kufanana kabisa na mfumo wa asili wa uburetwa na walioathirika zaidi na kampeni hii ya utaifishaji walikuwa ni Wahutu.
Ardhi yao ilinyang’anywa… Mifugo ilitwaliwa na kuwafanya Wahutu kuwa si tu vijakazi wa Wakoloni bali pia vijakazi wa Watusi.
Mwanzoni mwa miaka ya 1930s Ubelgiji walifanya upanuazi mkubwa wa sekta ya Elimu, afya na ajira za umma. Lakini wanufaika wakuu walikuwa ni Watusi.
Mwaka 1935 Ubelgiji walifanya kitu ch a ajabu sana ambacho kilipanua zaidi mpasuko wa kijamii na kitabaka uliopo ndani ya Rwanda. Walianzisha mfumo wa raia wote kuwa na vitambulisho. Vitambulisho hivi viliwatambua raia wote katika makundi manne kulingana na makabila yao. Watwa, Wahutu, Watusi na Raia wa kuomba (Naturalised).
Kutokana na Watusi kuwa ndio raia wa daraja la kwanza na tabaka la juu huku Wahutu wakiwa ni watu hafifu wa kudharaulika nchini humo, ilifikia hatua Wahutu wenye mali au ushawishi walikuwa wanahonga fedha ili kupatiwa vitambulisho vya Kuonyesha ni Watusi na watawala hawakuwapa Utusi kamili bali waliwapa ‘utusi wa heshima’ (Honorary Tutsi).
Hadhi ya Wahutu wote iliendelea kushuka kwa kasi wakionekana ni kabila na kizazi cha “Washenzi” huku Watusi wakionekana ndicho kizazi cha “wastaarabu” na kabila lenye darja.
Lakini kuna suala ambalo lilifanyika mwanzoni likionekana kuwa na manufaa makubwa lakini kadiri siku zilivyokwenda lilianza kuwa kama mkuki mgongoni. Kanisa Katoliki.
Kanisa Katoliki lilikuwa limeenea sana nchini Rwanda na raia wake wengi wakiwa ni waumini wa kanisa hilo. Tukumbuke kwamba tangu kipindi hicho Wahutu ndio walikuwa idadi kubwa zaidi ya raia wote ndani ya Rwanda. Hii ilimaanisha pia kwamba waumini wengi wa kanisa Katoliki walikuwa ni Wahutu.
Kwa kiasi fulani ndani ya kanisa Katoliki mapadri na watawa wengine walikuwa wanajisikia hatia kuacha waumini wao kuwekwa kwenye kundi la kizazi cha “washenzi” na kudharaulika ndani ya jamii. Kwa hiyo zikaanza juhudi za makusudi za kanisa katoliki kutoa elimu kwa vijana wenye asili ya Kihutu.
Baada ya miaka kadhaa kukaanza kuwepo walau kidogo uwiano wa wasomi wa Kihutu na Kitusi.
Mwaka 1957, mwezi March kikundi cha wasomi na watu wenye ushawishi wenye asili ya Kihutu walifanya jambo la “kimapinduzi” ambalo lilipanda mbegu mpya kwenye nafsi za watu wa kabila na kizazi cha cha Kihutu. Waliandaa waraka ulioitwa _'Manifeste des Bahutu' (Bahutu Manifesto).
Huu ndio ulikuwa waraka wa kwanza rasmi kubainisha kwamba Wahutu na Watusi ni mbari (race) mbili tofauti.
Katika waraka huu, wasomi hawa na watu hawa wenye ushawishi walijenga hoja kuu kwamba… Watusi wanapaswa kutoka kwenye jukumu lao walilojivesha la kuwa watawala wa Rwanda na badala yake nafasi hiyo ya kutawala Rwanda wapewe Wahutu. Hoja yao hii waliijenga kwenye nadharia ambayo wenyewe waliita “Statistical Law”, kwamba kitakwimu Wahutu ni wengi mno kushinda Watusi. Si sawa wakiendelea kutawaliwa na kufanywa vijakazi na Watusi.
Wanasema kwamba kabla kibanda cha nyasi kuungua kwanza utaanza kukiona kinafuka moshi. Kuna vugu vugu lilianza chini kwa chini ndani ya Rwanda.
Waraka huu… Bahutu Manifesto, ulitoka tarehe 4 March mwaka 1957. Japokuwa ilikuwa ni miaka takribani 37 kabla ya mwaka 1994, lakini ndio siku ambayo mbegu ya mauaji ya kimbari ilipandwa.
Usikose sehemu inayofuata….
Itaendelea…
The Bold
To Infinity and Beyond.
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA PILI
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TATU
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA NNE
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TANO
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA SITA
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA SABA
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA NANE
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TISA
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA MOJA
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA MBILI
BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA KUMI NA TATU
---------------
Chiefs,
Naona malalamiko kwamba link hazifunguki au hazikupeleki kwenye sehemu lengwa.
Sijajua tatizo ni nini, lakini kwa upande wangu naona link ziko sawa kabisa maana nimeharibu link zote kwenye simu tatu tofauti na zinafunguka na kunipeleka sehemu lengwa.
Nilichokigundua ni kwamba kwa baadhi ya simu kama unatumia app na kisha kubofya link inakutoa kwenye app na kukupeleka kwenye browser na juu kabisa utaona Sehemu ya kwanza lakini kwenye page hiyo hiyo ukiscroll down utakutana na sehemu lengwa.
Tuelewe kwamba kwenye browser kila page juu kabisa inakuwa na original post (post # 1) kwa hiyo unatakiwa kuscroll down utakutana na sehemu lengwa iliyotajwa kwenye hiyo link.
I hope this is helpful.
Shukrani.
Umeuliza swali zuri Sana kwann waliamua kumuua waziri mkuu hpa napata ukakasi inawezekana wahutu wenyewe ndio walimuua habyalimanaNimeipenda historia nzuri nimejifunzamengi
naomba kujua
1.nani alitoa amri ya kuuawa kwa Waziri mkuuhizi
2. James kabarebe alishiriki sehemu ipi katika harakati hizi.
3.nini mapokeo ya kifo cha rais wa Burundi katika shambulio hilo
tuzidi kuelimishana wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mujibu ya maelezo ya wachangiaji na tafiti mbalimbali nimefikia hitimisho kwamba inaonekana wahutu walitaka wawatokomeze watusi kwa vile watusi walilishwa sumu ya superiority dhidi ya wahutu na makabila mengine na kua vibalaka wa wazunguSwali lako ni gumu sana, kuna baadhi ya watutsi niliwahi kuwahoji hilo swali mitaa fulani pale Kanombe karibu na airport .
Walikili wazi kwamba ukweli unapindishwa, waliokufa wengi ni wahutu na siyo wao.
Facta walizonipa ni
1. Mapinduzi yaliandaliwa na Jeshi la RPF chini ya wanajeshi wa kinyarwanda waliokuwa jeshi la Uganda wakiongozwa na Kagame, Fred na Musitu, pila kupepesa macho walikiri kwamba waliovamili bila kujiandaa (hutu )waliuwawa zaidi
2. Idadi ya watutsi waliokuwepo Rwanda wakati huo haikuwa inafika million moja, walidai miaka ya 1952 watutsi walitimuka Rwanda wakatimukia Uganda na nchi za jirani wakati wa cold war kati yao na watutsi.
Kagame na RPF yake waliingia kwa gia mbaya sana kutafuna madaraka kitendo kilichotafsiriwa na wahutu ndivyo sivyo na kuanza kuwafyeka watusi wasiokua na hatia na hivvyo RPF wakawa wanaendesha mauaji ya wahutu kwa maelezo kwamba wanawalinda jamii yao na navyoona wakati wanavamia na kutungua ndege waliunderestimate matokeo Sasa walilazimika kuretaliate kwa misingi ya damu ni nzito kuliko maji na kwa kweli lawama zote abebe pk ndo maana anahangaika kuficha ukweli alipata madaraka kwa damu nyingi ikizingatiwa chuki ya kikabila iliyokuwepo toka mwanzo wakoloni walipopanda mbegu1. Kuhusu statistics nimetoa link ya taasisi ya IBUKA ambayo ni ya watutsi na imesema watutsi walikuwa laki 7 na ikaenda mbali kusema waliopona ni laki 3 hivyo kwa mahesabu hayo hayo ndio nmetumia hapa kuhalalisha kuwa watutsi walikufa wachache kuliko inavyosemwa
Na hoja ya kusema inakuaje population iwe hiyo hiyo kuanzia 1990-1994 labda ningekuuliza pia kwamba imekuaje Rwanda wakati wa vita ya kimbari inaanza statistic zilisema wahutu 85% alafu watutsi 14% na leo mwaka 2017 statistics zinasema vilevile wahutu 85% na watutsi 14% je kama asilimia ni zile zile kwa miaka 20 kwanini huamini kuwa miaka 4 zinaweza kuwa zilezile au ongezeko dogo sana
Source:
: 2017 Demographics of Rwanda - Wikipedia
:1994
Outreach Programme on the Rwanda Genocide and the United Nations
2. Unaposema watutsi hawakuwa wachache ndio maana walikuwa na ubavu wa kupambana!! Naweza kubali kuwa watutsi hawakuanzisha vita ila RPF ndio walileta genocide.... Kma wasingevamia Rwanda na kuanza kuchinja wahutu basi watutsi wasingechinjwa na interehamwe.... Hivyo watutsi kma watutsi naweza kukiri hawakua na sababu ya kuchinja wahutu ila RPF kma jeshi lilitekeleza mauaji ya kimbari kma ambavyo wahutu wakawaida hawakuwa na sababu ila interehamwe walitekeleza majority ya vifo...... Na kuhusu namba yao source yangu ni taasisi ya watutsi IBUKA ambayo inadai watutsi walikuwa laki 7 sasa sitegemei watutsi wasushe namba yao!!
3. Naelewa maana ya genocide ndio maana nmekufa mfano kuna mass graves zilikutwa huko butare na rubavu wahutu wamekatwa katwa mapanga wametupwa kwenye mashimo ambayo yalifanywa na RPF na ripoti nyingi tu ikiwemo ya UN 1998 na human rights watch ya mwaka 2004 inadai RPF ilichinja watoto na wanawake wa kihutu wasio na hatia waliokuwa wanakimbilia mpakani kuingia mashariki ya congo
Source:Leaked UN report accuses Rwanda of possible genocide in Congo
Hitimisho langu ni kwamba wote wahutu na watutsi walitaka kufutana kutoka uso wa dunia hivyo iitwe RWANDAN GENOCIDE sio TUTSI GENOCIDE irrespective ya nani alikufa kuliko mwenzake
Ahsante
Sababu Kama hizo kwenye jamii ni mbaya sana yaani unawaona wenzako nguruwe afu wewe ndo mtu unafaa kuwatawala? Mbaya sana hii superiority complex lazima izalishe chuki ndio maana Nyerere aliwadhibiti wachaga kwa upuuzi Kama huo Hadi kesho wanajionaga wako na akili kuliko wengine unfortunately wamebanwa mbavu wanaishia kwenye mitandao hukuNimekuelewa kabisaa, waliokufa wengi ni wahutu na ni clear Rwanda Genocide, ila mimi bado nasikitishwa na alieanzisha vita hivi, je ni muhutu au mtusi? Yoyote alieanzisha vita hivi ilikua halali yeye kufa,,, labda kama kuna yalio nyuma ya pazia, lakin kama sababu ni hizo tulizoziskia za wivu dhidi ya watusi kua na akili, kupenda shule na kua civilized mapema basi wahutu pengine ndio binadamu wasio faa kabisaa kuwepo africa na ningesikia raha kama wote walioanzisha izo propaganda kuawawa.
Ila kweli icon ya nchi wanaonekana wao wahutu uwezi wajua ina maana wenyewe hawatembei?Najiuliza tu, kama watutsi ni wachache hivi huko Rwanda, inakuwaje kila nikiona mtu kutoka Rwanda ana asili ya watutsi? Wahutu wako wapi? Hamuoni kuwa bado kuna propaganda ile ile inaendelea?
Sent using Jamii Forums mobile app