Ndugu yangu mbona kama mjadala huu haukufai au si wewe ninaekujua.Hapa ungewaacha wenyewe japo hili si jukwaa la mijadara ya Wahutu na Watusi.Hata mleta uzi angepima kwanza mjadara utakuwaje,watu unawakumbusha machungu makubwa tena kwa kutengeneza Title yenye kuuzunisha si sawa kiukweli.Nakusihi usijifunue hata kama kuna ndugu zako walikumbwa na kadhia hiyo.Mwenyez Mungu amekupa kipaji ambacho kila wakati unatakiwa utafakari unakitumiaje kuleta amani,upendo na furaha kwa waja wake na si kuingia kwenye mtego wa Shetani wa kujadili kumbukumbu hizi tena kwa kuonyesha unaegemea wapi,bora ukaegemea kwenye chama lakini si kabira.Wahutu na Watusi wote wameinywesha ardhi yao damu na kuitililisha mto naili na bado inamlilia Mwenyezi Mungu kutoka ardhini na kwenye Mto,Kilia cha damu hii hakimwombi Mwenyezi Mungu alipize Kisasi bali ashushe roho ya upendo kwa watu waliobaki.Sasa Mwenyezi Mungu anajibu kwa mkakati maalumu,yeye ndie kamweka Kagame pale na yeye ndie atamtoa.Kwa nini uwe sehemu ya project ya Shetani kutaka kurudisha simanzi na kushindana na Mwenyezi Mungu.Ebu chukua dakika chache tafakari kabla ya kuchangia katika mada hii na uone kama si chuki ya kikabila inapambana uandike.We ni Mtanzania ambae tumeona vipawa vya Mwenyezi Mungu alivyokupatia bure,haya unayochangia ndio unamrudishia shukrani.Samahani kama ntakuwa nimekukwaza ila wewe ni Mtumishi wa Mungu kumbuka hilo na ndio maana unapendwa na watu si kwa sababu una uwezo wa kiuchumi bali Bwana anataka atumike nawe.ACHANA NA HIZI MADA NA KAMA UNAWEZA KUOMBA IFUTWE UTAKUWA KATIKA KUTEKELEZA WITO WAKO.