Hakuna historia ya kweli duniani. Zote zipo biased na huwa inategemea nani katoa ufadhili wa historia.
Nilikuwa Rwanda hivi karibuni. Kule kuna hali ya tension sana. Ni kwamba pengine watu wanalazishwa kuimba nyimbo wasiyoipenda. Ukitaka uishi salama kule sema genocide against Tutsi, usiseme genocide against Rwandans au Hutus. Na for sure wana vidonda sana wale watu... Tuliongea na mdada mmoja alipotupeleka kwenye makumbusho ya mauwaji ya kimbari kuwa kizazi hiki ni ngumu sana kusameheana kwa dhati maana walioua na kuuliwa familia zao wako pamoja mtaani...
Ila nikajiuliza swali moja, kama kweli wanataka kusamehe na kuanza upya, kwa nini kwenye makumbusho wanaongelea habari za genocide against Tutsi, kwa nini isiwe genocide against Rwandans? Haiwezi kuwa trick ya watusi kutawala Rwanda kwa minajili ya kutibu hatred?
Those guys, wanaongea lugha moja, kwa nini hatred ipo hivi? Na kwa style ya utawala wa kule unajenga amani ya mioyoni au kuna hofu ya kifo?
Mungu ibariki Rwanda