Historia ya mkoa wa Tanga

Watoto wa kisambaa ni weupe jamani hatare
 
Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
Utalii umeanza kupanuka kidogo hasa katika eneo la Pangani,Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho URITHI Tanga.
 
Josef Mambo (katikati), aliyezaliwa mwaka 1885 Tanga, Afrika Mashariki, na kununuliwa hadi Ujerumani akiwa mtoto mwaka wa 1897, na aliwahi kuwa mpiga ngoma kwenye 3rd Prussian Horse Grenadiers. Wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia, alipandishwa cheo hadi sajini na alijeruhiwa mara mbili, mara moja nchini Urusi, na mara moja huko Verdun.
 
Code:
 
Nadhan amezungumzia wilaya ya Handeni ndo haina hizo shule.
 
Burudani

Hakuna shaka Tanga ndio kitovu cha burudani Tanzania​


Ukiongelea filamu, Tanga ndiyo mkoa wa Tanzania wanaotoka magwiji wa filamu za kizazi kipya waliothubutu kuandaa filamu miaka ya tisini japo mazingira yalikuwa magumu. Japo wengi wanadhani filamu ya ‘Girlfriend (2003)’ ndiyo ilifungua ukurasa wa Bongo Movies, ni filamu ya 'Shamba Kubwa (1995)’ ya Mwl Kassim El-Siagi wa Tanga ndiyo iliyofungua milango ya filamu za kibiashara Tanzania.
Kipindi kile teknolojia ilikuwa bado ndogo na vituo vya televisheni ndo kwanza vilikuwa vimeanza, kwani wakati huo kulikuwa na vituo vya CTN, DTV na ITV tu, ambavyo hata hivyo vilirusha matangazo yake jijini Dar es Salaam.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ShbPgahWxmA Mwl. Kassim El Siagi akihojiwa na mwandishi

Filamu ya ‘Shamba Kubwa’ ndiyo iliyowaibua wasanii ambao wamekuja kutamba katika ulimwengu wa filamu; kama Hassan Master, Jimmy Master, Kaini na Amina Mwinyi, na iliteka wengi.

Baadaye zilifuatia sinema za ‘Love Story Tanganyika na Unguja (1998)' ya Amri Bawji, ‘Kifo Haramu’ ya Jimmy Master, ‘Dunia Hadaa (2000)' ya Mwl. Kassim El-Siagi, na ‘Augua (2002)' ya Amri Bawji. Zote hizi zilitengenezwa na magwiji kutoka Tanga.

View: https://m.youtube.com/watch?v=5SVOUYJ8cqw Video- picha: Amri Bawji katika tukio la kuzindua kitabu

Filamu hizi zilitengenezwa katika mfumo wa VHS (analogia), na hata uhariri wake ulitumia akili zaidi kutokana na teknolojia ya wakati huo kuwa ya kiwango kidogo, lakini ziliweza kuvutia sana kutokana na maudhui na msuko mzuri wa hadithi zake.

Filamu zingine zilizotengenezwa Tanga ni ‘Shahidi’ ya Amri Bawji, ‘Fimbo ya Baba’ na ‘Chukua Pipi’ ambazo zimetayarishwa na Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) la Pangani Tanga. Zipo pia ‘Ua la Matumaini’ na ‘Habari Kubwa’ za Mwl. Kassim El-Siagi.

Ukiuacha mji wa Dar es Salaam, ni mji wa Tanga ndio ulikuwa na majumba mengi ya kutazama sinema. Katika mji wa Tanga kulikuwa na majumba ya sinema ya Majestic, Novelty, Regal na Tanga Cinema.

Hapa sijagusia kuhusu mkoa wa Tanga kujaaliwa warembo wenye kujua kumliwaza mwanaume akaliwazika, ndio maana inasemwa ‘Tanga ndiko mapenzi yalikozaliwa!’ Sijui kama nitakosea nikisema Tanga ni ‘Los Angeles’ ya Tanzania. Yupo atakayebisha?
Source : Hakuna shaka Tanga ndio kitovu cha burudani Tanzania
 
24 December 2023

USHUJAA WA KIBANGA KUTOKA MKOA WA TANGA

Wakaazi wakifagilia na kuliweka sawa kaburi la shujaa Kibanga

View: https://m.youtube.com/watch?v=7QlPGiQT2YMMoja ya hadithi iliyovuma miaka ya nyuma kwenye mitaala ya lugha ya Kiswahili shule za msingi nchini ni ile ya Kibanga Ampiga Mkoloni, tukio ambalo historia inasema lilitokea mwaka 1944 katika kijiji cha Kwachaga wilayani Handeni mkoani Tanga.

KIBANGA KUMPIGA MKOLONI

Kwa mujibu wa mazungumzo yangu na Mzee Frank Mbelwa mkazi wa Kijiji na Kata ya Kwachaga alisema alizaliwa mnamo mwaka 1935 katika Kijiji hicho na mwaka 1942 wakati mzee Kibanga anampiga mkoloni yeye alishuhudia tukio hilo akiwa bado Kijana mdogo.“Wakati huo Kibanga nilimuona akiwa Mzee wetu hapa Kijijini na Huyo Mkoloni nilimuona alikuwa akijulikana kwa jina la Pina yeye alikuwa bwana shamba alikuwa anakagua mashamba ya mihogo hapa Kijijini akiona shamba halijastawi anakasirika na kucharaza bakora”

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ji4RbYp_YWIMzee Frank Mbelwa mkazi wa Kijiji na Kata ya Kwachaga Handeni, Tanga
 
2021 22 December

Mzee Wema Ally atupia historia


View: https://m.youtube.com/watch?v=jy3I2E84qS8
Baba wa mwandishi Shaaban Robert ambaye ni Robert alikuwa mkabila * na mama ni mdigo.

Licha ya umuhimu aliokuwa nao Shaaban Robert aliyezaliwa mwaka 1909 Vibambani Machui mjini Tanga na kuibuka kuwa nguli katika lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Nchi ya Tanzania amesahaulika kabisa.

Maandiko yake ya kwanza mwandishi nguli Shaaban Roberts yaliandikwa ktk gazeti la Mamboleo mwaka 1932, barua hiyo kwa mhariri wa gazeti ilienda ikiwa na kichwa cha habari Hirizi ya Shilingi Mia ikielezea kupinga ushirikina na aliweza kuandika jumla ya vitabu 24 huku akipokea tuzo kibao ikiwemo MBE - Member of British Empire. Aliandika kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwahusisha wanawake katika maamuzi katika ngazi zote za jamii.

Tazama makala hii kumfahamu na kujua maisha na mchango wake katika lugha ya Kiswahili
 
Wasegeju ni tawi la kabila la wadigo yaan n kama ilivyo wamachame au wakibosho kwenye kabila la wachagga. Wapo Tanga mjini kuanzia Pande mpaka Horohoro
Wasegeju ni wadigo wa pwani...wao mainly wanapakana na bahari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…