Historia ya mkoa wa Tanga

Historia ya mkoa wa Tanga

Mkoa wa Tanga una eneo la 27,348 km² na uko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji. Mkoa wa Tanga unaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.

Kuna wilaya 10 ambazo ni Handeni Vijijini, Handeni Mjini, Kilindi, Korogwe Vijijini, Korogwe Mjini, Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani na Tanga Mjini. Eneo linalofaa kwa kilimo ni 17,000 km². Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake.

Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka; Bonde lenye rutuba; Barabara upande wa mto na Shamba juu ya mlima, neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni wenyeji wa mkoa huo linamaana ya shamba, wao hulitamka N'tanga.

Tanga inasamekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 BK. Mji wa Tanga haikupata umuhimu kama mji wa jirani ya Mombasa. Tarihi ya Pate inasema ya kwamba kabla ya kuja kwa Wareno Pate iliwahi kutawala Lindi kwa muda fulani. Katika karne ya 19 BK Tanga ilikuwa chini ya utawala wa Omani na Zanzibar. Misafara ya biashara imeanzishwa hapa kwenda bara.

Kutokana na bandari yake nzuri ya kiasili Tanga ilikua sana wakati wa ukoloni wa Wajerumani waliojenga bandari wa kisasa pamoja reli kwanda Moshi. Reli iliwezesha kilimo kwa ajili ya soko la dunia Tanga ikawa bandari kuu kwa jili ya katani na kahawa. Baada ya Uingereza kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Tanga iliona mapigano makali tar. 3 - 5 Novemba 1914. Jaribio la Uingereza kuvamia Tanga kwa kikosi cha maaskari 8000 Waingereza na Wahindi kutoka meli kwenye Bahari Hindi ilishindwa vibaya na Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck.

Mwaka 1922 "Tanganyika Territory African Civil Services Association" (TAA) iliundwa Tanga ambayo ilikuwa shirika ya kwanza ya Kiafrika yenye shabaha za kisiasa.

Hali ya hewa
Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto ikiwa pakavu zaidi. Milima ya Usambara hapana joto sana. Miezi ya Desemba - Machi halijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.

Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi takriban milimita 1,100 hadi 1,400 mm ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka.

Makabila na wakazi
Makabila makubwa mkoani Tanga ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo. Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milimani ya Usambara, Muheza, Korogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.

Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga penyewe na sehemu za Muheza.

Msongamano wa wakazi ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto penye ardhi yenye rutuba nzuri. Wiyala ya handeni kuna machimbo ya madini.ila kuhusu elimu ipo nyuma sana.kwani mpaka sasa hakuna shule ya sekondari inayotoa huduma ya kidato cha tano na sita.kama haitoshi shule za watu binafsi hakuna ata moja

Elimu
Katika mkoa huu elimu inahitajika zaidi kuboreshwa hasa naeneo ya vijijini maana watu wengi wa mkoa huu hufanya shughuli zao za kimila hali hiyo huwafanya kushindwa kuendelea elimu pamoja na shughuli za kimaendeleo katika ujenzi wa taifa la tanzania

Uchumi
Wakazi wengi hutegemea kilimo cha riziki pamoja na ufugaji na uvuvi. Mazao ya chakula hasa ni mahindi, muhogo, ndizi, maharagwe na mpunga. Mazao ya biashara ni katani, pamba, kahawa, chai, nazi, tumbaku na korosho. Mifugo ni ngombe, mbuzi na kondoo pamoja na kuku.

Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba haya yalikuwa ya walowezi, yalitaifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani inategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ilirudi nyuma tangu miaka ya 1960.

Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
Utalii umeanza kupanuka kidogo hasa katika eneo la Pangani,Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho URITHI Tanga.

View attachment 1329161
Mkoa wa Tanga unapopatikana katika ramani Tanzania

View attachment 1329163
Ramani ya mkoa wa Tanga

View attachment 1329162
Picha ikionesha hali ya hewa mkoa wa Tanga

View attachment 1329165
Mapango ya Amboni ni moja ya vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani Tanga
Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
Utalii umeanza kupanuka kidogo hasa katika eneo la Pangani,Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho URITHI Tanga.
 
Josef Mambo (katikati), aliyezaliwa mwaka 1885 Tanga, Afrika Mashariki, na kununuliwa hadi Ujerumani akiwa mtoto mwaka wa 1897, na aliwahi kuwa mpiga ngoma kwenye 3rd Prussian Horse Grenadiers. Wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia, alipandishwa cheo hadi sajini na alijeruhiwa mara mbili, mara moja nchini Urusi, na mara moja huko Verdun.
JamiiForums-1389312019.jpg
 
Josef Mambo (katikati), aliyezaliwa mwaka 1885 Tanga, Afrika Mashariki, na kununuliwa hadi Ujerumani akiwa mtoto mwaka wa 1897, na aliwahi kuwa mpiga ngoma kwenye 3rd Prussian Horse Grenadiers. Wakati wa Vita vya Kwanza vya Kidunia, alipandishwa cheo hadi sajini na alijeruhiwa mara mbili, mara moja nchini Urusi, na mara moja huko Verdun.View attachment 2506594
Code:
 
Unaposema Tanga hakuna shule za kidato cha tano na sita, sijui unaelezea Tanga ipi.Lakini kama Tanga,Tanzania,ina shule zifuatazo za serekali na watu binafsi zenye vidato vya tano na sita,kwa Tanga mjini,Wacha huko wilayani:
Tanga Tech
Galanos
Usagara
Masechu
Popatlal
Coastal
Arafa
Istiqama
Al kheir
Hizo ni za Tanga mjini,bado za nje ya mji wa Tanga na wilaya zake.
Na kuhusu shule za binafsi ni nyingi,kuanzia msingi mpaka secondary,na vyuo pia vipo vingi.
Nadhan amezungumzia wilaya ya Handeni ndo haina hizo shule.
 
Burudani

Hakuna shaka Tanga ndio kitovu cha burudani Tanzania​


Ukiongelea filamu, Tanga ndiyo mkoa wa Tanzania wanaotoka magwiji wa filamu za kizazi kipya waliothubutu kuandaa filamu miaka ya tisini japo mazingira yalikuwa magumu. Japo wengi wanadhani filamu ya ‘Girlfriend (2003)’ ndiyo ilifungua ukurasa wa Bongo Movies, ni filamu ya 'Shamba Kubwa (1995)’ ya Mwl Kassim El-Siagi wa Tanga ndiyo iliyofungua milango ya filamu za kibiashara Tanzania.
Kipindi kile teknolojia ilikuwa bado ndogo na vituo vya televisheni ndo kwanza vilikuwa vimeanza, kwani wakati huo kulikuwa na vituo vya CTN, DTV na ITV tu, ambavyo hata hivyo vilirusha matangazo yake jijini Dar es Salaam.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ShbPgahWxmA Mwl. Kassim El Siagi akihojiwa na mwandishi

Filamu ya ‘Shamba Kubwa’ ndiyo iliyowaibua wasanii ambao wamekuja kutamba katika ulimwengu wa filamu; kama Hassan Master, Jimmy Master, Kaini na Amina Mwinyi, na iliteka wengi.

Baadaye zilifuatia sinema za ‘Love Story Tanganyika na Unguja (1998)' ya Amri Bawji, ‘Kifo Haramu’ ya Jimmy Master, ‘Dunia Hadaa (2000)' ya Mwl. Kassim El-Siagi, na ‘Augua (2002)' ya Amri Bawji. Zote hizi zilitengenezwa na magwiji kutoka Tanga.

View: https://m.youtube.com/watch?v=5SVOUYJ8cqw
Video- picha: Amri Bawji katika tukio la kuzindua kitabu

Filamu hizi zilitengenezwa katika mfumo wa VHS (analogia), na hata uhariri wake ulitumia akili zaidi kutokana na teknolojia ya wakati huo kuwa ya kiwango kidogo, lakini ziliweza kuvutia sana kutokana na maudhui na msuko mzuri wa hadithi zake.

Filamu zingine zilizotengenezwa Tanga ni ‘Shahidi’ ya Amri Bawji, ‘Fimbo ya Baba’ na ‘Chukua Pipi’ ambazo zimetayarishwa na Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) la Pangani Tanga. Zipo pia ‘Ua la Matumaini’ na ‘Habari Kubwa’ za Mwl. Kassim El-Siagi.

Ukiuacha mji wa Dar es Salaam, ni mji wa Tanga ndio ulikuwa na majumba mengi ya kutazama sinema. Katika mji wa Tanga kulikuwa na majumba ya sinema ya Majestic, Novelty, Regal na Tanga Cinema.

Hapa sijagusia kuhusu mkoa wa Tanga kujaaliwa warembo wenye kujua kumliwaza mwanaume akaliwazika, ndio maana inasemwa ‘Tanga ndiko mapenzi yalikozaliwa!’ Sijui kama nitakosea nikisema Tanga ni ‘Los Angeles’ ya Tanzania. Yupo atakayebisha?
Source : Hakuna shaka Tanga ndio kitovu cha burudani Tanzania
 
24 December 2023

USHUJAA WA KIBANGA KUTOKA MKOA WA TANGA

Wakaazi wakifagilia na kuliweka sawa kaburi la shujaa Kibanga

View: https://m.youtube.com/watch?v=7QlPGiQT2YM
Moja ya hadithi iliyovuma miaka ya nyuma kwenye mitaala ya lugha ya Kiswahili shule za msingi nchini ni ile ya Kibanga Ampiga Mkoloni, tukio ambalo historia inasema lilitokea mwaka 1944 katika kijiji cha Kwachaga wilayani Handeni mkoani Tanga.

KIBANGA KUMPIGA MKOLONI
1703521396365.png

Kwa mujibu wa mazungumzo yangu na Mzee Frank Mbelwa mkazi wa Kijiji na Kata ya Kwachaga alisema alizaliwa mnamo mwaka 1935 katika Kijiji hicho na mwaka 1942 wakati mzee Kibanga anampiga mkoloni yeye alishuhudia tukio hilo akiwa bado Kijana mdogo.“Wakati huo Kibanga nilimuona akiwa Mzee wetu hapa Kijijini na Huyo Mkoloni nilimuona alikuwa akijulikana kwa jina la Pina yeye alikuwa bwana shamba alikuwa anakagua mashamba ya mihogo hapa Kijijini akiona shamba halijastawi anakasirika na kucharaza bakora”

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ji4RbYp_YWI
Mzee Frank Mbelwa mkazi wa Kijiji na Kata ya Kwachaga Handeni, Tanga
 
2021 22 December

Mzee Wema Ally atupia historia


View: https://m.youtube.com/watch?v=jy3I2E84qS8

Baba wa mwandishi Shaaban Robert ambaye ni Robert alikuwa mkabila * na mama ni mdigo.

Licha ya umuhimu aliokuwa nao Shaaban Robert aliyezaliwa mwaka 1909 Vibambani Machui mjini Tanga na kuibuka kuwa nguli katika lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Nchi ya Tanzania amesahaulika kabisa.

Maandiko yake ya kwanza mwandishi nguli Shaaban Roberts yaliandikwa ktk gazeti la Mamboleo mwaka 1932, barua hiyo kwa mhariri wa gazeti ilienda ikiwa na kichwa cha habari Hirizi ya Shilingi Mia ikielezea kupinga ushirikina na aliweza kuandika jumla ya vitabu 24 huku akipokea tuzo kibao ikiwemo MBE - Member of British Empire. Aliandika kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwahusisha wanawake katika maamuzi katika ngazi zote za jamii.

Tazama makala hii kumfahamu na kujua maisha na mchango wake katika lugha ya Kiswahili
 
Wasegeju ni tawi la kabila la wadigo yaan n kama ilivyo wamachame au wakibosho kwenye kabila la wachagga. Wapo Tanga mjini kuanzia Pande mpaka Horohoro
Wasegeju ni wadigo wa pwani...wao mainly wanapakana na bahari.
 
Back
Top Bottom