Historia ya Qur'an

alimjuaje huyo allah kabla ya kuelezewa na korani

alikuwa anaswali wapi

Mkuu kwanini hutaki kukiri kuwa kabla ya Mohamad na korani yake hakujawahi kuwa na uislam
tupe pia historia ya uislam
036.Je, Uislamu ulikuwepo kabla Mtume Muhammad s.a.w?

Naam, ulikuwepo kabla,Uislamu ndiyo Msingi ambao kila mteule wa Mungu Mwenyezi alikuwa akiwahubiria watu wake,kila Zama ilikuwa Ni juu ya watu kutakiwa wasilimu,
Ukisoma hapa utaona Quran.com/4/163 quran.com/42/13

Sasa Soma hapa

127. Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.



128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.



129. Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.



130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.



131. Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote.



132. Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.



133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.



134. Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao.



135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.



136. Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.



137. Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.



138. Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu.



139. Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.



140. Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo myafanyayo.



141. Hao ni watu walio kwisha pita. Wao watapata waliyo yachuma, na nyinyi mt apata mliyo yachuma, wala hamtaulizwa nyinyi yale waliyo kuwa wakifanya wao.



Qur'an 2
 
Uislamu kabla ya Muhammad ulikuwa unaswaliwa Kwa Jina la Nan? Hakuna dini bila mwongozo(kitabu) kama uislamu ulikwepo kabla ya Quran basi walikuwa wanaabudu sanamu sabab hawakuwa na kinachowaongoza. Leta historia ya uislamu before muhammad
 
Nimeipenda hii
 
Allah hakuwa na watoto,na wala hatawahi kuja kuwa nao.hajazaa wala hajazaliwa na wala hakuna anaefanana nae.

Chanzo (Quran Surah Tul al Ikhlas)

Kabla ya Quran Allah alikuwa na Watoto.
Hiyo Quran imekuta Hapo Makka Allah anaabudiwa Kwa karne na karne. Huyo Allahu mwenye watoto.
Labda useme Quran ilikuja na Allah mwingine.
 

Kuna mdau kauliza swali hapo.

Kabla Jibril hajamtokea Muhamad, je Muhamad alikuwa Dini gani?

Pili, Hapo Makka uislamu ulikuwepo kabla ya Quran kushushwa?
 
Huu ni mfano wa yale niliyo zungumza,,,mumpuuze huyu

Usijadili kilokole.
Jadili kwa Hoja.
Historia inaonyesha Hapo Makka Allah alikuwa anaabudiwa kama Mungu mkuu Chief God kabla hata ya huyo Muhamad kuwako. Na simulizi zinaonyesha waumini waliamini alikuwa na watoto watatu.

Kabla ya mtume kuwa mtume alikuwa anaabudu dini gani?
 
Nakuheshimu lkn nasikitika sitoweza kujibu hoja dhaifu

Asante
 
Nakuheshimu lkn nasikitika sitoweza kujibu hoja dhaifu

Asante

Vizuri.

Kwenye dini la jambo huna taarifa zake ni bora uwe muwazi kuwa sina au sijui. Lakini tatizo la wenye dini kila kitu mnataka kujifanya mnakijua na kama hamna maelezo yake mnakumbuka.

Sio dhambi wala kosa kusema ni kweli kabla ya MUHAMMAD kina Allah lilikuwepo kihistoria ingawaje uislamu haukuwepo. Sio kosa
 
Allah hakuwa na watoto,na wala hatawahi kuja kuwa nao.hajazaa wala hajazaliwa na wala hakuna anaefanana nae.

Chanzo (Quran Surah Tul al Ikhlas)

Quran uliyoinukuu imeletwa na Mtume. Allah anatajwa hata kabla ya MUHAMMAD na simulizi zinaeleza alikuwa anawatoto watatu.

Muhamad mtoto wa juzi yeye anajuta hizo stori anakuja kukanusha katika kitabu chake kiitwacho Quran.

Sasa ndio nani mkweli kati ya jamii iliyomzaa Muhamad ambayo Muhamad kaikuta na huyo Allah kamkuta, au Mkweli Muhamad?
 
Hakuna namna yoyote Ile Kwa mtu yoyote yule anaweza kusema na kuthibitisha kuwa Qurani iliandikwa kabla ya BIBLIA TAKATIFU.
Qurani Kwa kifupi ni fabricated stories tu muhamad alipewa na majini basi.
Period.
 
Na simulizi zinaonyesha waumini waliamini alikuwa na watoto watatu.
Neno "Allah" ni kifupi cha neno la kiarabu La-ilah, ambalo maana yake ni "mungu". wapagani walitumia neno Ilah kwa maana ya mungu. Kabla ya Muhammad, kaaba jengo lililotunza sanamu 360 liliitwa Beit-Allah, au "Nyumba ya Allah".


Baba yake Muhammad ambaye alifariki kabla ya Muhammad kuzaliwa, aliitwa Abdullah maana yake, mtumwa wa Mungu. Miongoni mwa sanamu/miungu iliyoabudiwa Maka uliitwa "Allah."

Huyu alikuwa mungu maalum wa kabila la Wakureshi naye alikuwa na mabinti watatu maalum. Ukilinganisha na nguzo 4 kati ya 5 za Uislam, watu wa Maka kabla ya Muhammad walifunga kwa pamoja siku moja, walitoa sadaka kwa maskini wao, walisali wakielekeza nyuso zao Maka, na walifanya hija ('Umrah) Maka. Kulikuwa na tofauti nyingi pia, lakini inashangaza kuona muendelezo wa matendo yasiyobadilika yaliyokuwa yakifanyika kwenye ibada za kipagani za kikureshi.

Allah alikuwa na mabinti watatu walioitwa Lat, 'Uzza na Manat. Siku moja "Nabii wa Allah" aliafiki na kusema katika Quran (Sura 53:19) kuwa maombezi yao yanapaswa kutumainiwa. Kwa maneno mengine alisema tunapaswa kutumaini msaada wa miungu hawa watatu.
 
Uislamu Ulikuwepo ila quran kashushiwa muhammad
We unavyoona inamake sense

Kama uislamu ulikuwepo hakukua na haja ya muhammad kushushiwa quran na kupewa maelekezo ya kusali
 
Kuna wengine tumesoma lakini hatuwezi kufundisha(sio kila aliesoma anaweza kuwa mwalimu)

Lakini mkuu neno Allah ni neno la kiarabu, kwa kiswahili ni Mungu na kwa kimombo ni God kwaiyo usitatizike na ilo neno kuwa kila mwarabu akisema Allah ni yule Mungu wa kweli kwani hata wachina masanamu wanayaita Miungu aka God

Hivyo hata Muhhamad aliwakuta watu wa makkah(wakiwepo ndugu zake) wanaabudu masanamu na kuyaita Allah(Mungu) hivyo baada ya kupewa ujumbe na Mungu wa kweli ndio akaanza kuwahabarisha watu(ummah) kuwa Mungu wa kweli ni nani na sio hayo masanamu yao.

Hii hata kwa manabii waliopita kama Issa na Nuhu na wengine walikuta jamii zao katika upotofu na kuanza kuwahubiria Mungu wa kweli ni nani

Kwa kifupi tu jitahidi uelewe
 
Swadakta
 
Allah ni yale masanamu zaidi ya 300
Taratibu zote za uislamu walikuwa wazitumia babu zake muhammad kuabudu

Mfano kuzunguka alkaaba, kufunga, n.k yote hayo waliyafanya jamii za arabia hata muhammad kuzaliwa
Kituko ni muhammad kashushiwa kitu ambacho watu walikua wanakifanya
 
Uislamu Ulikuwepo ila quran kashushiwa muhammad
We unavyoona inamake sense

Kama uislamu ulikuwepo hakukua na haja ya muhammad kushushiwa quran na kupewa maelekezo ya kusali
Kuna msemo unasema kila zama na kitabu chake ikiwa na maana manabii/mitume waliopita walikuwa na vitabu vyao mfano wa torati, injili, zaburi na quran.

Kwa mujibu wa uislaam kila nabii alipewa kitabu chake kulingana na zama alizonazo lakini maudhui yakiwa ni kumtangaza Mungu mmoja.

Nmejibu kile nnachofaham mkuu mtoa maada atakujibu zaid kwa anachofaham na yeye
 
Hizi ni propaganda kama za marekani jikite kwenye maada mkuu soma historia ya quran upate mbili tatu za mtoa maada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…