Mtume alikuwa Muislam kwa miaka 23 (kuanzia miaka 40 hadi 53)..Mimi naomba kujibiwa maswali yafuatayo:
1. Tangu kuzaliwa kwake Mtume hadi alipofika umri wa miaka 40 alikuwa anaabudu wapi?
2. Mungu wake alikuwa nani?
3. Kibla chake kilikuwa wapi?
4. Msikiti wake ulikuwa wapi?
5. Utaratibu wake wa kuswali ulikuaje?
6. Alikuwa akifunga Ramadhan? (Ilikuwa na maana gani kwake?
7. Alikuwa akienda kuzunguruka Kabah? Je Kabah Ilikuwa na midoli au haikuwa nayo?
mgen
Che mittoga
HISTORIA FUPI YA MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam)
JINA LAKE NA NASABA YAKE.
Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul Mutwalib bin Hashim bin Abdul Manaf bin Quswai bin Kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim (Aleyhi Salam)
MAMA YAKE.
Mama yake ni Amina binti Wahab bin Abdul Manafi bin Zuhra bin Kilaab.
JINA LAKE MASHUHURI.
1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa ndani ya Qur’ ani tukufu kama:
2- Khaatamun nabiyyiin.
3- Al ummiyyi.
4- Al muzammil.
5- Al mudathir.
6- Al mubiin.
7-Al kariim.
8- An nuur.
9- An niima.
10- Ar rahmaan.
11- Ash shaahid.
12- Al mubashir.
13- An nadhiir.
14- Abdur rauuf.
15- Ar rahiim.
16- Ad daai na mengine mengi.
TAREHE YA KUZALIWA KWAKE.
Alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 571 A.D.kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa wanahistoria.
SEHEMU ALIPO ZALIWA.
Alizaliwa katika mji wa Makkatul Mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.
KUPEWA KWAKE UTUME.
Ali pewa rasmi utume tarehe 27 mwezi wa Rajab katika mji wa Makka baada ya kutimiza miaka 40 ya umri wake mtukufu.
MAFUNDISHO YAKE.
Mtume (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe wote, na alikuwa akilingania undugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye Dini ya ki islaam. kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu alizo zipokea kutoka kwa Allah Subhana Wa Ta'ala alie takasika, kisha waislaam wakazipokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
MIUJIZA YAKE.
Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’ ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi
sana kwani hai hesabiki.
WITO WAKE.
Mtume (Swalla Allahu Aleyhi wa Salam) ali walingania watu kwenye upweke wa Allah katika mji wa Makka na kwa njia ya siri kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia ya wazi kwa muda wa miaka kumi.
KUHAMA KWAKE.
Alihama kutoka katika mji wa Makkah kwenda Madina mwanzoni mwa mwezi wa rabiul awwal baada ya kupita miaka 13 tangu kupewa utume, na kuhama huko kulitokana na maudhi mengi ya makuraishi, mushrikina na makafiri kumuelekea yeye na maswahaba wake.
VITA VYAKE.
Allah Subhana Wa Ta'ala Alie takasika Alimpa idhini ya kuwapiga vita mushrikina na makafiri na wanafiki, na baada ya idhini hiyo aliweza kuingia kwenye mapambano na watu hao kwenye vita vingi sana, na kati ya hivyo vilivyo kuwa mashuhuri ni Badri, Uhudi, Khandaq (Al ahzaab) Khaibar, na Hunain.
WAKEZE MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Mtume alikuwa na wake Kama ifuatavyo : Wakwanza ni :
1 Khadijah bint Khuwailid.
2 Sauda bint Zam'ah. 3 'Aishah bint Abi-Bakr. 4 Zainab bint Khuzaymah.
5 Umm Salamah. 6 Hafsah bint 'Umar. 7 Zainub bint Jahsh. 8 Juwayriyah bint al-Haarith.
9 Umm Habibah bint Abi Sufyaan.
10 Safiyya bint Huyayy. 11 Maymuna bint al-Haarith.
12 Mariya Bint Sham'un - Mqibti (Mamake Ibrahim)
WATOTO WAKE MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Watoto wake ni kama wafuatao:
1- Abdallah.
2- Qaasim.
3- Ibrahiim
4- Fatima
5- Zainab
6- Ruqayya
7- ummu kulthum
BABA ZAKE WADOGO.
Mtume (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam) ana baba wadogo tisa (9), nao ni watoto wa Abdul Mutwalib kama wafuatao:
1- Al haarith.
2- Zubair.
3- Abu Twalib.
4- Hamza.
5- Al ghidaaq
6- Dharaar Al Muqawwim,
7- Abu Lahab.
8- Al Abbas.
SHANGAZI ZAKE MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Mtume (s.a.w) alikuwa na shangazi sita kutokana na akina mama tofauti nao ni kama wafuatao:
1- Umaimah.
2- Ummu hakiimah.
3- Burrah.
4- Aatikah.
5- Swafiyyah.
6- Arwy.
MLINZI WAKE.
Mlinzi wake alikuwa ni Anas.
WAADHINI WA MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
1- Bilal Al –habashi
2- Ibnu Ummu Makhtuum.
3- Saad Al-qurt.
NEMBO YA PETE YA MTUME (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Nembo ya pete yake ilikuwa ni (( Mohmmad rasuulu llah)).
UMRI WAKE (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Aliishi kwa muda wa miaka 63.
MUDA WA UTUME WAKE (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Utume wake ulidumu kwa muda wa miaka 23.
TAREHE YA KUFARIKI KWAKE (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Alifariki dunia tarehe 28 mwezi wa safar mwaka wa 11 hijiria.
SEHEMU ALIYO FIA (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Mtume alifia katika mji wa Madinatul Munawwarah.
SEHEMU ALIYO ZIKIWA (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Alizikiwa katika mji wa Madina ndani ya Chumba cha mkewe Bi Aisha bint Abubakar.
SEHEMU ALIOZALIWA MTUME MUHAMMAD (Swalla Allahu Aleyhi Wa Salam).
Hii nisehemu ya makumbusho kwa vizazi vyetu kwa sasa ambayo alizaliwa kiumbe bora kuliko viumbe vyote hapa Duniani. Na sehemu hii ni moja ya sehemu yenye kuheshimiwa Sana ktk mji wa makka.
Watu wa serikali ya kifalme ya mji wa makkah walipata taabu sana kuienzi sehemu kwa kuweka nini ili sehemu hii iweze kutambulika vyema.
Wapo waliosema ujengwe mnara mkubwa Sana ili ulitambulishe eneo hili, wapo waliosema eneo hili lisawazishwe tu kisha lizungushiwe wigo na liandikwe kuwa ndio sehemu Alipozaliwa Mtume Mohammad.
Baada ya mbishano mkubwa ikabidi serikali ya Saudia iwasikilize wataalam wa dini na wasomi wa dini wanahukumu vipi kuhusu eneo hili ndipo wasomi wadini hii tukufu wakatoa wazo kuwa sehemu hii tukufu alipozaliwa mtume wa Allah na kiumbe bora.
Pajengwe Maktaba ya kiislamu Na pawekwe vitabu vyoote vya kidini ili waislam wapate faida kupitia maktaba hiyo, ndipo lilipojengwa jengo hili la maktaba hapo na watu huingia bure kabisa kujisomea vitabu mbalimbali vya dini yetu tukufu ya kiislam hapa.