Historia ya Rais Magufuli na fikra za kujilisha bila kuombaomba!

Sema anakupotezea direction na siyo wote wanaopotezewa direction ndiyo maana hapingwi na wote
Hapa nazungumza na kundi la waelewa, wanaojitambua na kujua hali ya Nchi yetu hii kwa sasa. Huwezi kuwa na utimamu, uelewa, well informed bado ukakubaliana na yale yanayotendwa na utawala wa Magufuli Tanzania kwa sasa.
 
Huyu mtu siku aking'olewa nchi itafanya sherehe ambayo haijawahi kufanyika mahali popote duniani
 
hakuna mtu anaemchukia mwingine bila sababu unachotakiwa kurlewa kwanini inachukiwa na unaapendwa moja ya jambo linalomfanya mtu kuchukia ni kutokusikilizwa au kunyimwa kuzungumzia chambo linalomuhusu
 
Mkuu kwa pale tulipofikia hakuna cha zaidi angefanya zaidi ya kuwa mtemi. Kuna baadhi watachukuliwa kama wanakondoo kwa mstakabali mzuri. Hata katika vita vya kudai uhuru kuna watu walipoteza maisha kwaajili ya wengine waishi vizuri. Katika demokrasia Uingereza walichinja Mfalme wao. Fikiria na huu ukatili mnaosema anao na bado watu wanapiga kiaina je angekua mpole ingekuwaje?
 
Watanzania wanafiki sana, wacha atoke madarakani utakubaliana na hali hiii unayo iona JF kuhusu kutomkubali huyo jamaa.
Binafsi kutoka moyoni, anatupotezea uelekeo kama Taifa. Hatoshi kuwa rais si tu wa Nchi hii, taifa lolote Duniani.
Hakuna kitu kama hicho na nadhani huko nyuma ulikuwa mfaidika sasa umebanwa fanya kazi kijana dunia haipo hivyo hakuna madili siku hizi.
 
Hakuna kitu kama hicho na nadhani huko nyuma ulikuwa mfaidika sasa umebanwa fanya kazi kijana dunia haipo hivyo hakuna madili siku hizi.
Me si mwanasiasa Bro, naongea uhalisia. Hizo kazi unasema nifanye sijaanza leo/awamu hii.
 
Kwa maana hiyo anayo yafanya ni fahari? Yanasifa gani nzuri kwa nchi yetu?? Utekaji, uuwaji, ukiukwaji wa sheria na haki za bianadamu umetukwamuaje?

Lipi jipya la maana analofanya zaidi ya kufanya Taifa hili kuwa kisiwa na mambo mengine mengi ya kutia aibu??
Tusifungwe ufahamu kwa vitu vidogo visivyo na mashiko, utu ni bora zaidi.

Jifunze hata kwa majirani zetu Kenya basi!
 
Mamlaka zote hutoka kwa Mungu.

Tanzania is a blessed Country. We are blessed to have such a president like him.

We are blessed to have such a president like him.......Hakika hiki ni kiswahili cha kanda pendwa kabisa.
 
Huyu mtu siku aking'olewa nchi itafanya sherehe ambayo haijawahi kufanyika mahali popote duniani
Inakubidi uvumilie ama uhame nchi maana hakuna wa kumng'oa na upinzani kumejaa matutusa yanayosubiri makapi kutoka CCM. Na nina uhakika atakayefuata baada ya Magufuli labda atakua zaidi ya magufuli. Usitegemee Membe na genge lake kurudi madarakani labda kuingia kujiunga na genge la upinzani
 
Povu halitaokoa kitu , Shetani hajawahi kumshinda Mungu
 

Siri ya kudhibiti upigaji ni kuwa na taasisi imara sio kuwa na kiongozi mwenye jazba.. utashangaa eti anasifiwa kurejesha nidhamu kwenye taasisi za umma, huku yeye mwenyewe akiiziingilia mahakama, akiliingilia bunge, kwenye box la kura ndio kabisa analichezea waziwazi. Ukweli jamaa ni mzuri tu katika miundombinu, na sio zaidi ya hapo. Kwa maneno maraisi hastahili kuwa rais bali waziri wa miundombinu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…