Ni mwongo huyu mzee,hao walinyongwa kwa kupinga utawala wa kijerumani full stop.
Songea Mbano ana jina lake la mwanzo la kikabila,
Yeye kasema alitwa abdulratif songea Mbano.
Mkomanile kamuita Khadija.
Huyo nae na wengine wote 60 wana majina ya kikabila.
Ye kapindisha na kaweka uislamu.
Wajerumani waliwanyonga kwa kupinga maslahi yao.
Huy mzee na bias zake za udini kae da huko kufanya utafiti wake misikitini.
Kaingizwa chaka anatuletea utopolo hapa.
Babu...
Bahati mbaya umeghadhibika na unaandika ustaarbu umekutoka kwa hamaki.
Haya mambo yanasimama katika kusoma na kutafiti ndipo utayajua.
Soma barua hii kutoka nyaraka za Wajermani wenyewe:
Soma barua ya Chifu Songea bin Ruuf kwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
''Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe.
Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini.
Tupo katika kupigananao hapa.
Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano.
Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea.
Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu.
Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa.
Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe.
Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismail anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.''
(C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’,
Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p. 58).