..Waingereza wangekuwa wakatili kama Ccm / watawala tulionao uhuru wa Tanganyika usingepatikana muda mfupi baada ya kuundwa kwa Tanu.
..Mwalimu Nyerere na wenzake ktk Tanu hawakupitia misukosuko wanayopitia viongozi na wafuasi wa upinzani kwa mfano wakina Maalim Seif, Babu Juma Juni, na wengine.
..Hakuna mwana-Tanu aliyeuwawa kwa mateso, kutobolewa macho, na mwili kumwagiwa tindikali, kama Mzee Ally Kibao, wa Chadema.
..Nawaheshimu wazee waliodai Uhuru, lakini ni lazima tuwe wa kweli kwamba waliyopitia yana nafuu kubwa ukilinganisha na kinachoendelea sasa hivi.