MohamedPS: Kuna mtu kanipigia simu anasema, "Mohamed kila unapoulizwa swali na ukatoa jibu unazidi kunichanganya fikra zangu lakini linalonistaajabisha ni kuwa unaowajibu hawahisi kuwa unawapa kitu kipya hakijapata kujilikana kwa wengi. Inanisikitisha kuwa hawa ndugu zangu vichwa vyao haviwezi kupokea kitu kipya." MS
Huyu anayekuuliza alikuwa amelala? hujawahi kutoa jibu Mohamed. Unachofanya ni kuweka vipande vyako vya propaganda visivyohusiana na jibu, ukikamatwa mahali unakimbilia kusema andikeni vitabu. Unachoweza kujibu ni nyumba za wazee wako na mitaaa, lakini huwezi kujibu kamati kuu ya TANU ilikuwa na akina nani.
Unaposema mabucha yalivunjwa kwa umasikini wa Tabora,Kilwa, Kigoma na Mtwara kwa hakika ni kitu kipya!!! kwasababu kile cha zamani hakipo hivyo. Vinafanana kwa majina. Huyo aliyekupigia simu inaweza kuwa ni mwanachama wa gogovivu na angesema tofauti ningemshangaa.
Mwambie hivi: AMNUT walivurugana kama walivyovurugana shura ya maimamu wakati wa engineer Mbukuzi. Kama Zinavyovurugana taasisi za shura ya wazee, kamati ya mali, kamati ya haki. Unachowaambia watu sio kile kinachotokea. Mchawi hayupo ukumbini yupo chumbani, mwambie aingie uvunguni atamuona
Mwambie, Tewa S Tewa aliyekuachia makabrasha ni mmoja wa wanafiki waliokuwa informers na akathubutu kuitelekeza EAMWS ili achumie tumbo. Hicho ndicho kipya si wewe kubeba mafaili ya Tewa.
Mwambie hivi, kama asilimia 83 ya madaraka ni wakristo na 17% ni waislam, mapagani na wenye dini nyingine tunawaweka wapi? Mwambie umeshindwa kuthibitisha ukweli wa namba hizo achilia mbali kujibu. Au labda anamaana unapotuambia tukaandike vitabu ni kitu kipya!
Mueleze kuwa kwa mara ya kwanza baada ya ziara za ulaya, marekani, visiwa vya fiji, Tonga na Vanuata umerejea na kitu kipya nacho ni kukiri kuwa Rupia ni mzee wako kama Sykes, Kiyate, Makaranga na Munanka. Hiki ndicho kipya.
Mdokezee kuwa umeelewa kuwa historia ya Tanganyika ni zaidi ya Narung'ombe,Kipata na mchikichini
Mfikishie salamu za Kigarama kutoka Kalenga kama ulivyozipokea kwa unyenyekevu na taadhima.
Mwisho mpe nauli aende magogoni ofisi za wizara ya elimu akaulizie namba za mitihani zimeanza kutumika lini? kwa sababu umejibu mengi kama alivyosema lakini hilo hujapata jibu.
Waama hata sisi tunajifunza mengi, nani alijua kitoweo cha Nyerere na soksi ndeefu.