julaibibi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2020
- 3,081
- 4,224
mimi nimesoma sana historia hii.nashangaa wanakuja watu wanasema historia hii uongo oooh wazee wake!! sasa historia hii kama kweli unaiona sio ya kweli leta zenu na facts tusome tuone nan kasema sio sahihi!! naona kinachouma watu hapa kinajulikana hutuwez kujidanganya nafsi zinajua shida ipo wap hapa wote tunajua."yaliyo nyoyon ni mabaya kushinda wadhihirishayo"Vito...
Umesema kweli nimeandika historia ya wazee wangu hili nitalikataaje wakati mimi mwenyewe katika kitabu rejea yangu kuu ya vuguvugu ya kuasisiwa kwa African Association ni mswada wa kitabu wa Kleist Sykes?
Sikuishia hapo na nikaweka pia rejea mbili DA Sykes Buruku (1968) na John Iliffe (1973) kama ushahidi na rejea zote nikaeleza zinapatikana Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.
Hivi karibuni ikaongezeka rejea nyingine Dictionary of African Biography (DAB) hii unaweza ukaipata Library of Congress, Washington DC.
Rejea hizi zote utasoma historia ya Kleist Sykes na watoto zake Abdulwahid, Ally na Abbas kama watu muhimu katika historia ya TAA, TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hawa wote waliishi Mtaa wa Kipata, Gerezani Dar es Salaam.
Lakini sijalazimisha kuwa hii iwe historia ya taifa.
Historia ya taifa ipo na inaanza na Julius Nyerere 1954.
Historia niliyoandika mimi inaanza nyuma sana mwanzo kabisa wa karne ya 20.
Ni wazi kuwa hizi ni historia mbili tofauti kwa maudhui na nyakati.
Nahitimisha kwa kusema kuwa babu yangu Salum Abdallah alikuwapo toka African Association inaundwa na akashiriki katika kupigania haki za Waafrika akiwa TAA, TANU na akiwa ndani ya Tanganyika Railways African Union (TRAU) chama cha wafanyakazi wa reli.
Historia yake naijua na nimeiandika hapa JF sehemu nyingi.
Ikiwa mtu ataona historia ya wazee wangu haina uhusiano na ukombozi wa Tanganyika hii ni bahati mbaya kwangu.
kama historia na facts za Mohamed said unayepinga unaona sio leta facts zako .hivi ni vitu vya kielimu.ukipinga sema wewe sasa ipi ya kweli sio kukaa tu analeta historia ya wazee wake ooh nin ukiulizwa leten bas zenu tuone mnagwaya gwaya.