Mr. Mohamed Said kwanza tunashangazwa sana na maneno unayotumia mara kwa mara kwamba:
• Hatufurahiswi
• Tunaumia
• Nyoyo zinatuuma
• Hatupendi kusikia historia ya uislam n.k
Nikuambie tu baadhi ya wachangiaji wanaotoa maoni tofauti na unayoandika hawaamini katika imani hizi kubwa mbili hilo ulielewe vizuri, mtu akipinga mawazo yako haina maana kuwa anapinga imani yako na wala imani yako haimshughulishi kabisa what they need is clarity.
Pia unasema umekuja na historia ambayo tulikuwa hatuijui kabla, ni sawa lakini hilo nalo halituzuii hata kidogo kupima na kuangalia ukweli na uhalisia wa historia yenyewe. Kwa sababu hatukuijua kabla haitupi ithibati kuamini kuwa historia hiyo ina ukweli na uhalisia kwa 100%.
Shida nyingine ya wengi ni wewe kutaka kuuaminisha umma kuwa 'wazee wako' wametoa mchango mkubwa katika kudai uhuru wa nchi hii kisa tu walimpokea Mwalimu Julius Nyerere hivyo ni kama hawapewi coverage ya kutosha kwenye vitabu vya historia.
Lakini kuna mchangiaji mmoja alisema hata hao 'wazee wako' wasingempokea Mwalimu Nyerere au kumpa ushirikiano, uhuru wa nchi hii ungeapatika pasi na shida sababu Nyerere angepata back up kubwa zaidi sehemu nyingine zaidi ya ile ya 'wazee wa gerezani' naamini hili unalitambua la kama hukubaliani nalo unapaswa kufunga huu mjadala.
Pia Mohamed Said unasema na ni mara nyingi unasema watu kama Ally Sykes na Abdul Sykes kuwa wamefutwa kwenye historia hili nalo linatupa shida sana why unataka 'watu wako' wapate special privilege kuliko watu wa sehemu nyingine?
Siku zote historia ina tabia ya kujiimba yenyewe pasipo kuimbiwa. Leo hii katika nchi yetu kuna watu wengi na machifu wengi ambao kwa mchango wao mkubwa sana kwenye hili taifa hadi leo historia inawaimba pasipo kutumika nguvu kubwa kama unayotumia kuwaimba 'wazee wako'
Nakushauri acha kauli ya 'Siwezi kumlazimisha mtu kuamini ninachoandika'
Siku zote tumefunzwa kizuri kinajiuza..
Jones...
Mwaka wa 1968 Abdul Sykes alipofariki magazeti ya TANU Uhuru na The Nationalist walitoa taarifa ya kifo cha Abdul Sykes kama taarifa tu ya Julius Nyerere kuhudhuria maziko yake.
Hapakuwa na jingine.
Si taaza wala kueleza Abdul Sykes ni nani katika historia ya kupigania uhuru wa Tangayika.
Mhariri wa magazeti haya alikuwa Benjamin William Mkapa.
Mwaka wa 1981 wakati CCM imeunda jopo chini ya Dr. Mayanja Kiwanka kuandika historia ya TANU kupitia Chuo Cha CCM Kivukoni, mwanajopo moja jina lake Hassan Upeka (TANU Intelligence toka 1956) aliwasilisha ''notes,'' za Abdul Sykes alizoandika kuhusu hstoria ya TANU baada ya kufanya mahojiano na Abdul Sykes kabla hajafariki.
Jibu alilopewa na kiongozi wa jopo ni kuwa historia ya TANU haa uhusiano wowote na Abdul Sykes.
Haya hadi hapa yanatosha kueleza kuhusu kutofurahishwa na hayo mengine ya nyoyo kuuma.
Kitabu kilipotoka jina la Abdul Sykes na wengi walokuwa mstari wa mbele katika kuunda TANU hayakuwamo: Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache wa pale TANU HQ, Dar es Salaam.
Mwaka wa 1988 Africa Events ilichapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' ndani yake ilikuwapo historia ya Abdul Sykes na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Toleo lote lilikusanywa na kutolewa kwenye mzunguko lisisomwe.
Mimi sibabaishi kauli zangu nasema kweli hata kama itamuudhi mtu.
Hakuna Muislam aliyekichukia kitabu cha Abdul Sykes kilipotoka kwa mara ya kwanza mwaka wa 1998 khasa wale waliokuwa wanajua kuwa historia ya TANU ya Kivukoni haiko sawa.
Kizazi hiki cha sasa cha Waislam wa leo hiki ni kitabu chao na ndiyo waliosababisha kitabu leo kufikia toleo la nne.
Hawa wachangiaji wa mada hii wanaotaabishwa na historia hii wengi ni watu wa aina yako.
Hili nalo jibu ndlo hilo.
Ukweli gani utakaokuwanao wewe kwenye maisha ya wazee wangu unishinde mimi ninaotokana na wao wengine kwa nasaba na wengine kwa ujamaa?
Utayajuaje wewe yale yaliyofanywa na wazee wangu?
Au unahusika nini na yale ninayoeleza katika maisha ya wazee wangu kiasi uingie ndani ya maelezo yangu kunisahihisha?
Unaijua historia ya babu yangu Salum Abdallah au Mzee bin Sudi na Ali Jumbe Kiro katika African Association, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyka hadi TANU?
Nimekuwekea majina haya matatu kwa kuwa hawa waliishi toka vuguvugu la African Association linaanza hadi wakaunda TANU na wakauona uhuru wa Tanganyika 1961.
Hawa kwangu mimi ni babu zangu na baadhi yao nimewaona na nazijua historia zao.
Sijamlazimisha mtu yeyote kuamini historia ya wazee wangu katika kuunda vyama hivyo vyote na kuvitumia katika kupambana na ukoloni.
Tatizo liko wapi?
Kuhusu mchango mkubwa wa wazee wangu.
Wewe amini kuwa hata hawakufanya lolote wala hiyo AA na TANU hawakuasisi wao
Tatizo liko wapi?
Historia hii ilifutwa.
Nani kameguka kashtakiwa kwa kuwa kuwa historia ya babu zake Mohamed Said imefutwa?
Ngoja nikuambie.
Hata kama Nyerere asingefika Dar es Salaam uhuru ungepatikana.
Hata pia kama wazee wangu wasingeunda AA na TANU tusingetawaliwa na Waingereza daima.
Nadhani hapa tumeelewana.
Abdul na Ally Sykes.
Unadhani unaweza kuandika historia ya TANU bila ya kuwataja hawa?
Wala sijasema popote kuwa wao ni wazalendo makhsusi ila huwataja pale inapobidi kusahihisha historia ya uhuru.
Nakuuliza tu unaweza kuandika hstoria ya Mwalimu Nyerere na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika ukamtaja Nyerere peke yake?
Chuo Cha Kivukon wamelifanya hili katika kitabu chao, ''Historia ya TANU,'' na si unaona balaa lake?
Leo mnakuja kwangu kusoma historia mpya ya TANU na historia mpya ya Julius Nyerere.
Hii ndiyo sababu leo wewe uko hapa unajadili na mimi kuhusu historia hii.
Kwa nini hujadili na CCM?
Unasema kuna machifu walipigania uhuru wa Tanganyka.
Hawa machfu walipigania uhuru wa Tanganyika wakiwa wanachama wa chama kipi TANU?
Mimi namjua mmoja Mwami Theresa Ntare tena alinihadithia mwenyewe vipi aliingiza TANU Buha.
Ukipenda kumsoma nifahamishe nikuwekee historia yake hapa.
Hakuna nguvu kubwa yoyote ninayotumia katika kuisomesha historia hii.
Waliotumia nguvu kubwa kuifuta histora ya wazee wangu wapo na ipo historia yao.
Ikiwa unapenda kuisoma nifahamishe nitakuweka hapa.
Nakufahamisha kwa mara nyingine kuwa sikulazimishi kuamini historia ya wazee wangu.
Uko huru kuamini upendacho iwe historia ya TANU ya Temu na Kimambo (1969) au ya Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).
Hii ni nchi huru.