Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Asante sana Mkandara kwa observation makini.
Naamini wewe ni muilamu safi na mwenye muelekeo wa kimaendeleo zaidi.
Na kama itikadi yetu watanzania ilivyo tumachangia sana misikiti, makanisa shule na zahanati zenye kuleta maendeleo bila kujali dini.
Ndo watanzania tulivyo.
Kama kuna tatizo la mizani ya kimaendeleo mtu makini anajiandaa , tena kimya kimya, kusoma na kujichangia ili afike kileleni.
Type ya Mohammed Said na wapambe wake sijawahi kusikia wamechangishana kumsomesha hata mtoto mmoja hadi kufikia kiwango cha Phd.
Hao anaowasifia kina Sykes hadi leo wapo, hawana hata shule za kusingiziwa.
Lazima watambue kuwa maendeleo yoyote ni juhudi na si maneno maneno.
Na mods mnajaza upupu bure wa watu wa siasa kali , ambao wala hauna uhusiano wowote na uhuru wa Tanganyika humu jamvini.
 

Bwana "muisilam asiye njaa" Mkandara,

Umesema mengi sana mkuu na yanaweza kuakweli kwa ufahamu wa wa "uisilam"
Mimi nilikua natafuta waisilam Kumi tu wa namna yako wasio njaa ili tusaidiane. Katika ujenzi wa shule ya kiisilam ya msingi na sekondari lengo nikatika kuitikia wito wa Mushemiwa raisi kwamba,muslims should build new school"mimi nafamilia yangu tumebaba hili jukumu na infact tumeshaanza sasa tafadhali ni PM uje uone sight na maendelee ya ujenzi utusaidie waisilam njaa katika hili
 
Now you guys are talking , na wala msijibague.Mkiwa na mabo ya maendeleo hata mimi nitaweka shilingi yangu hapo najua itasaidia kuondoa umasikini na ujinga!
 
Now you guys are talking , na wala msijibague.Mkiwa na mabo ya maendeleo hata mimi nitaweka shilingi yangu hapo najua itasaidia kuondoa umasikini na ujinga!

Acha ushamba wewe

Mambo ya maendeleo yanayofanywa na waislam huyaoni au unajibaragua tu hapa...

Ukitaka kuchangia moja njia nzuri ni "Kuondoa dhulma" ...

Waislam wanafanya mambo ya maendeleo enzi na enzi..shule, misikiti, hospitals etc..zinajengwa pamoja na kwamba hatupewi pesa za umma kama wakristo through MoU..ok

Tuondoe dhulma na tuweke haki kwanza mengine ni mteremko ..
 

Mkuu T,

Hilo wao hawalioni
 
Mkuu nisome vizuri hapo juu utaelewa nilichoandika.
1. Huwezi kudai mfumo Kristu kuondoka wakati huna cha ku-replace, itakuwa ujinga mkubwa maana wanaondolewa Madikteta kwa sababu wananchi wanataka mfumo wa Demokrasia. Na hayo maswala mengine yote ulozungumzia hapo chini ni matokeo ya kuwepo mfumo usioukubali na unataka uondolewe. Je, wewe una mfumo gani unatakiwa kuchukua nafasi hiyo? Kama huna mfumo wowote in hand, utaweza vipi kurekebisha ya chini uloyaandika ambayo ni matunda na mfumo uliopo madarakani..sasa ili yasitokee tena ama yaondoke unataka tuwe na mfumo gani...kwa sababu hatari niyoisoma hapa JF ni kwamba Waislaam wanachotaka ni Kutesa kwa zamu..

- Uislaam hauko hatarini Tanzania hata kidogo na haujawa. kinachofanyika ni kwamba Uislaam unapigwa vita na watu wanaojiita Waislaam hali Islaam dini imesha waonyesha njia za maisha. Kama vile watu wanapigania demokrasia for the wrong reason huitwa magaidi. Ni wao ndio wenye matatizo na sii demokrasia.

Kinachofanyika nchini ni kwamba pamoja na kuchukua demokrasia kama mfumo wa utawala wetu, ukweli bado ni kwamba hatuna demokrasia hiyo. Ni sawa na mtu anayejiita Muislaam wakati ibada zote zinapiga chenga. Kusimamisha tu nguzo za Uislaam ni adhabu kubwa kwake, sasa unategemea nini atayafanya mtu huyu kwa binadamu wengine hali akidai yeye ni Muislaam?. Ama yawezekana pia wapo waislaam wanaokwenda kusali na kufunga hata Ramadhan kwa kufuata mkumbo maadam nduigu na marafiki zake ni Waislaam na wanasali basi naye anajiunga ktk mkumbo huo...

Hiii ndio hali halisi ya Tanzania, tunadai kuwa na demokrasia lakini hatufuati nguzo za demokrasia aidha tunakwenda kwa kufuata mkumbo au kutumia jina la demokasia kwa manufaa yao. Demokrasia haiwezi kufanya kazi ama sisi wenyewe tunaitumia kwa malengo kinyume cha demokrasia, kama vile mtu anaweza kuwa Muislaam na akatumia Uislaam wake kufanya mambo kinyume cha Uislaam..Kosa sio dini bali kosa lipo within ourselves maana Kuran imesha define IUislaam ni kitu gani..

Hivyo basi, kama hatuna demokrasia, utawala uliopo haufuati mfumo wa demokrasia na ndio maana tunapata matokeo kama hayo hakuna mtu ana own democracy, we all fight for democracy ili kuondoa tabaka za utawala dhalimu usiofuata demokrasia na kuwapa wananchi wote haki sawa. Kwa hiyo maadam CCM ndiye mtawala na hafuati demokrasia ipaswavyo, ni swala la kupinga utawala huu ufuate demokrasia ya kweli na sii kupendelea au kutafuta mtu au watu watakao geuza kibao na kupendelea upande mwingine.

Yes, mimi ni Muislaam..si own Uislaam wala dini hainihitaji mimi bali mimi ndiye naihitaji dini ktk kuhakikisha haki na UTU wangu unaheshimika lakini sii kwa gharama ya mkristu hata kama. Natambua nina viongozi wabovu toka utawala wa serikali hadi Bakwata kwa hiyo nachoweza kupigania mimi ni kuhakikisha watu kama wewe unatumia vizuri dini pale haki yako inapokosekana..Nachofanya mimi ni kuutangaza Uislaam na mzuri yake tofauti na wengi wanavyofikiria kama vile hao wana siasa wanavyotangaza demokrasia dhidi ya Udikteta. Lakini kama Uislaam utakuwa hatarini Tanzania, basi nitakuwa na sababu ari na uwezo wa kupigania kama mnavyopigania demokrasia mkitumia jina la dini.
 

T,

Muislam ni yule ambae Muislam mwenzake amsesalimika na shari ya mkono wake na mdomo wake. Hapana haja ya kushambuliana kati ya "Waislam wenye shibe na wale wenye njaa."

Naona pameingia fedhuli na hamaki hii si bishara njema.

Sisi tujikite katika kuuelimisha umma. Hapo ndipo penye tija.

Mohamed
 

Yap unataka demokrasia na utawala bora kama ambavyo mim na kila mtu anataka...

Yap utawala bora ni pamoja na kukataa mali umma kutumika kwa faida ya kanisa tu (MoU) ..mgawanyo wa kibaguzi wa rasilimali zetu..

Yap demokrasia na utawala imepotezwa na mfumo kristo (mfumo wa ubaguzi ulioasisiwa na Nyerere) lazima tupambane nao..

Yap Uislam hauko hatarini wala hakuna atakayewezi kuuhatarisha kwasababu kwanza Allah ataulinda, pili sisi waislamu hatutakubali dhulma hata kama tutabaki wawili

Yap wewe endelea kuwalamba miguu wakristo wanaotetea upendeleo na ubaguzi unaofanywa..

Yap watu kama nyinyi walikuwepo, watakuwepo hadi mwisho wa dunia..period
 

Shukran sheikh

InshAllah ntajitahidi
 
Ni kweli kuwa tofauti kati ya mjinga na mpumbavu huwa dhahiri katika jinsi mtu anavyo interact na mazingara yake.
Kwa bahati mbaya sana wewe ndugu yangu unaingia kundi hili la pili.
Kama imani yako inakutuma kuwa huwezi kijiendeleza hadi wengine wakupigie magoti wakati mtu kama wewe binafsi ni hohehahe wa kutupwa, basi haingii akilini kwa nini kushirikiana na mtu ambaye hawezi kufikiri zaidi ya kujifikiria yuko chini na ni duni.
Unayenifikiria kuwa mshamba nina uhakika nina maisha mazuri zaidi kuliko wewe ambaye hujastaarabika na elimu ambayo ingekuondoa si ujinga tu,bali na kaupumbavu dhahiri uliko nako.
 

Shakespeare anasema, "Gold begets more gold." Sasa haya matusi yataleta matusi zaidi. Kweli hili ndilo tulitakalo?
Tutulie tuupe heshima ukumbi.

Mohamed
 

Pole mkuu..

Hayo maisha mazuri nini? (very subjective term)

Nasisitiza waislam hawafundishwi na mtu kama wewe wala hawasubiri michango yako ili waendelee..far from that..

Kinachoitakiwa na kuondolewa Dhulma wanayofanyiwa waislam Tanzania

Na kuondoa upendeleo unaofanywa na serikali (kutumia pesa za umma) ku-finance shughuli za kanisa..

Hayo ya maisha mazuri ni misifa isiyo na tija kwenye mjadala huu..kwani hunifahamu sikufahamu
 
@Topical
Umewshambulia wachaga

Nimekuuliza je wachga walio waislam unawambiaje?

Kutokana na mtazamo wako na aoni yako uliouchambua makabila alafu ukauganisha na dini . Tuambie ni makabila gani ya Tanzania yanfaa kuwa waislam.

Maana unachofikiria wewe ni moja ya sumu iliyomo wenye tasisis za kiislam .Wale wa waislam wa pwani ndio wanajiona wasilam "safi" na "original " zaidi .Hawawapi nafasi baadi ya waisam wasomi wa dini na elimu dunia kutoka bara kuongoza taasisi zenu .Thats another ugly truth. swallow it.
 
@Topical
Umewshambulia wachaga

Nimekuuliza je wachga walio waislam unawambiaje?

Kutokana na mtazamo wako na aoni yako uliouchambua makabila alafu ukauganisha na dini . Tuambie ni makabila gani ya Tanzania yanfaa kuwa waislam.

Mkuu nimekujibu..

Narudia sijashambuli kabila..lolote

Nimesema jifunze lugha za mfano..
 
Wanaukumbi,

Mimi nakulaumuni kitu kimoja.
Kuna watu watakuja na maswali ambayo wenyewe wanaona magumu sana nami nitamwaga data.
Kimyaaaaaaa!

Mwanaukumbi hata mmoja hanipi mji wala nafasi ya kutoa salam.

Kuna mtu juzi au jana kanambia mie ninasema haya ninayosema baada ya Baba wa Taifa kuwa hayupo.
Nikamwaga historia yangu hapa nzima.
Kimyaaaaa!

Basi si angalau hawa jamaa wanaonifanya mimi "punching bag" wakarudi na kusema, "Mkuu nimekusoma."

Vibaya hivyo ndugu zangu.

Mohamed
 
Bw. Mohammed Said je unafikiri vitendo vya ufisadi au mfumo wa utawala wa kifisadi nchini vina mchango gani katika kudunisha maisha ya Waislamu au kuendeleza dhulma mbalimbali ambazo umezitaja?
 
Nashukuru sana umekuja na maelezo ya kina na nafaka ktk bongo zetu..
Sasa labda nikukumbushe nini maana ya MFUMO KRISTU! haswa na madhara yake.


Tanzania ilikuwa imetawaliwa na Muingereza, na toka Mjarumani hakuwepo na haki sawa kwa Watanzania kiasi kwamba huduma kama za Afya elimu, usafiri na hata access ya nafasi za kazi ziliytolewa kwa matabaka. Wakoloni walitumia njia za kututenganisha ili tupate kugawanyika na wapate kututawala.. Huu ndio mfumo kristu..

Nyerere alioingia madarakani, alivunja mfumo huu kwa kuundwa Azimio la Arusha. Azimio hili likiwa na lengo la kuondoa kabisa mfumo kristu lakini kwa matakwa ya viongozi wa kiislaam walio wengi ilikuwa zamu yetu kutesa wakati hawana mfumo wa ku replace isipokuwa walitaka tu mageuzi ya kuwapa wao kipaumbele. wakati waislaam wakichukuliwa shule zao sijui zilikuwa 20, wakristu walichukuliwa shule zao zaidi ya 200, hospital zao zilichukuliwa nyingi kuliko sisi kwa mara 200, na hata makazini waislaam walipewa nafasi za juu ktk uongozi..Mimi binafsi nimesema sana hapa kwamba nilikuwa mmoja kati ya waislaam walionufaika na Azimio la Arusha kwa sababu niliweza kusoma shule za wakristu wakati ktk kijiji changu ama niseme mkoa mzima hatukuwa na shule ya kiislaam isipokuwa madrasa..Leo waislaam mnamwita Nyerere alikuwa ndiye mchawi wenu akifanya Uislaam unavyotakiwa.

Kwa hiyo sii kweli Nyerere ndiye alokuja na mfumo Kristu isipokuwa yeye aliuondoa na nyie na Mwinyi wenu mkaurudisha. Madai yako yote hapo juu yameletwa na Mwinyi under his watch..Na haya tunayoyaona leo ni matunda ya mfumo kristu yaani kutugawa wananchi ktk makundi ya dini kabila Ubara na Uzanzibar hii ndio maana ya mfumo kristu tumerudi kama ilivyokuwa wakati wa mkoloni...

Sasa nambie nani hapa mwenye advantage? obvious atakuwa Mkristu kwa sababu tayari walikuwa na mashule, hospital na huduma nyinginezo nyingi kuliko waislaam na Wapagan..Wakristu wako organised kupitia vyombo vyao kuliko sisi sote na mfumo wao wa kiutawala ambao ni wakijamii zaidi ya kiimani..Kwa hiyo, haya yote unayoyaona na uloyaandika yametokana na kurudi kwa mfumo kristu ambao katiba yetu imeubeba..Na yamekuwa yakiombwa sana na wananchi wenyewe bila kuelewa athari zake.

Leo hii waislaam wamerudi ktk hali ile ile waliyokuwa nayo wakati wa Ukoloni, na kwa bahati mbaya wananshindwa kuelewa kwamba matatizo haya yametokana na CCM na hasa Mwinyi kukubali kuvunja Azimio la Arusha, kurudisha mali na mashule kwa wale waliofaidika wakati wa ukoloni kwa dhana ya kwamba Azimio la Arusha lilikuwa dhulma kwa wananchi.

Kwa upande wa waislaam wanapiga makelele na kupinga Azimio la Arusha walikuwa watu walioathirika directly, walikuwa matajiri na watu wenye asili ya kirabu zaidi.. samahani mkuu this is a fact..Na wengine ni wale viongozi ambao walifikiria kwamba Uhuru wetu uliwaletea zamu yao kujichanua..Hii kitu Muslim inatumiwa tu kisiasa hakuna mwenye kuutetea Uislaam ama waislaam kwa sababu waislaam hawana shida isipokuwa kwa kutokana na mfumo unaowagawa wananchi ktk makundi ya dini.

- Dawa yake ni demokrasia ya kweli, vyama ndivyo vitumike kudai haki ya wananchi. Katiba mpya uindwe na kama ikiwezekana maswala ya shule, Afya na huduma zote za kitaifa iwe ni jukumu la serikali na private School au Hospital ziwe mikononi mwa private people hivyo watalipa kodi na hakuna misamaha kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere shule kama Mzizima, Shaaban Robert, Lake ya Mwanza na kadhalika. Na zile za Jumuiya sijihusishe ktk maswala ya dini tu..Panga pangua mkuu wangu ktk mfumo huu na katiba hii, Waislaam hamuwezi kufaidika kwa lolote zaidi ya kuwatumikia baadhi ya matajiri wachache wanaotaka kutumia dini kama sababu ya kujinufaisha wao.

Kwa hiyo, ili kukamilisha yote hayo, Katiba mpya inatakiwa na ndio hoja kubwa ya Chadema, ni hoja ya wasomi na hata maprofesa wetu ktk matatizo yote yanayojenga matabaka toka umaskini, ukabila na hata udini. Azimio la Arusha ni msingi mzuri ulojengwa na Nyerere ktk utawala bora na mahusiano ya wananchi na umependekezwa na watu kama Profesa Shivji.. Yapo mazuri mengi ya Azimio la Arusha, tukiacha siasa za kiuchumi (Socialist) kwani hiii ni dhamana ya vyama vya kisiasa. Tukiweza kurekebisha haya, tukaijenga katiba yetu dhidi ya mabaya yote ya utawala wa mkoloni dhidi ya wananchi wetu mchezo umekwisha.. Kama maneno haya ni kuwalamba miguu wakristu, basi na iwe hivyo kwa sababu madai yako hayakuandikwa ktk kuran wala hadithi za mtume. Ni mawazo yako binafsi yaliyojaa Ubinafsi kwa sababu tu unataka upewe zamu yako kujichana.

Ohhh! na nyongeza tu kaa Nyerere akifufuka leo hii, atafurahi sana na kusema Alhamdulilaaah niliwambia hawa watu hawakunisikiliza..Ama atacheka sana, ataanguka mbavu kwa sababu alituasa hatukumsikiliza leo yakowapi?.Tulimwona kilaza sasa leo yametukuta yale yale alotuasa na yanakuja tena kwa kasi kubwa sana..
 


Hongera sana kwa kufaidika na mfumo Nyerere.
 

Hakuna Hata swali moja la maana ulilojibu, unarukaruka tu,

Uzuri ulianza kwa kujificha lakini mwisho wa siku umekuwa dhahiri (rangi yako imeonekana), na baada ya kueleweka watu walikuwa kimya wakifatilia huu mjadala kwa muda mrefu (Mkandara), akaamua kuja kukuelewesha wewe na wenzio wenye dhamira moja

lakini tatizo Halitaishia kwenye Dini tu, bali litakuja swala la Mwislamu wa kweli ni Mmanyema tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…