Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Mwanakijiji,

Kama ni hilo basi mimi sina haja ya kwenda kwa Mama Maria...nayajua mengi.
Wala sitathubutu kufanya hivyo huyu Bi Mkubwa na sawa na mama yangu.

Kuna vitu kwa ajili ya adabu huelezi watu wala huandiki watu wasome kwa kuwa
si mambo yatakayosaidia kuijua historia ya nchi yetu.

Baada ya uhuru palipitika upasi...tosheka na hilo ndugu yangu na turudi kwenye
yake yatakayotoa mwanga wa kuichambua historia yetu.

Mwanakijiji mimi ni mzao watu hawa...ndio walionileta duniani na kunilea hapa
hapa Dar es Salaam.

Kuna wakati mimi nikitembea Dar es Salaam Gerezani kule nina miaka kama sita
hivi akina mama wakiniita kwa jina la marehemu mama yangu "We mtoto wa Baya."
Nikenda wananishika kichwa na kunifariji kwani wakimkumbuka mama yangu, shoga
yao. Hapo kimoyomoyo wakiniombea dua Allah anikuze.

Hadi leo akina mama hawa wapo na kila n ikiwatembelea kwanza ni chozi kisha
mazungumzo.

Nenda kazungumze na Biti Hassan Machakomo. Bi wa Kizulu huyu jamaa zake akina
Sykes...

Huyu kaiona historia yote toka siku ya kwanza...


Mohamed
 

Kuwepo lakini mrudishe anapotakiwa awepo, apate darsa, mwenyewe kakiri kuwa anajifunza mengi aliokuwa hayajui, hii mimi inanionesha kuwa ile "shock" imeanza kumtoka na anatanabahi kuwa haya ni kweli lakini anajaribu kujitutumuwa, si unajuwa mila za "kikwetu". Kwa hiyo tumsaidie kumrudisha kwenye mada apate zaidi.
 

Mdondoaji,

Sheikh Mohamed ninamsoma vizuri sana. Nilichosema na ningependa kukirudia na ambacho ningependa nawewe unifahamu ni kwamba, Sheikh Mohamed kaahidi kutueleza namna kitabu chake kilivyomfikia Nyerere na majibu yake, hilo ndilo la msingi kwa sasa. Labda kama kuna sehemu imenipita.
Suala la kuongea na mama Maria hajasema kwamba ameshindwa, kwahiyo tumuachie sheikh Mohamed kwanza. Kama akitafuta mtu wa kumuunganisha nae hatakosa, ingawa kuna mahali amekiri kwamba ameshafika mwitongo, nadhani bila shaka alishaonana nae, kilichozungumzwa ndio hajatueleza.
 

Huyo wa kuchekeshwa ataishia kusahihisha spelling kwenye paragraphs zako alafu atadai kajibu hoja.
 

Sheikh Mohamed,

Hapa kuna jambo linanitatiza kidogo.

Umesema hauko tayari kwenda kuzungumza na mama Maria Nyerere, kwakuwa pamoja na mambo mengine, huyo bi. mkubwa ni sawa na mama yako.

Lakini hapo hapo unamshauri Mzee Mwanakijiji aende kuzungumza na Biti Hassan Machakomo, aliyeiona historia tangu siku ya kwanza. Bila shaka naye ni mtu mzima kama mama Maria ama kumzidi umri. Sasa sheikh wangu hapa unataka kufikisha ujumbe gani??
 
Hayo yote semeni nyinyi sisi tukiuliza swali mjibu basi na swali, kama hujaelewa rudia posts.

Maana ya Orthodox ni kukatana mikono?
 
Hayo yote semeni nyinyi sisi tukiuliza swali mjibu basi na swali, kama hujaelewa rudia posts.

Maana ya Orthodox ni kukatana mikono?

wakati mwingine huwa unasababisha watu watoke nje ya mnakasha bila sababu za msingi.

Orthodox inafahamika, lakini ni wazi kwamba kunaweza kuwepo na watu wasioifahamu. Sasa ulipoulizwa kuhusu orthodox, badala ya kulijibu kiungwana ili mnakasha uendelee vizuri, wewe ukaingiza kejeli, hapo ndipo uliharibu.
 

Kejeli ipi hiyo?
 
Hivi, utamuulizaje Mohammed juu ya data zilizonyofolewa kama hajatoa ushahidi kuwa kuna data zimenyofolewa? Mohammed hajawahi kufanya kazi katika kitengo cha kutunza nyaraka kiasi kwamba ana uhakika kuna data zimenyofolewa. Huenda hizi ni facts zilizopikwa tu kuongezea masimulizi yake ambayo mostly yako based on hearsay.
 

Mohamed Said atakuja kuijibu yeye mwenyewe kuhusu hili, au unaniuliza mimi? mimi sina shaka na ayasemayo.

Based on hearsay kutoka kwa nani?

Halafu hapo nilipokuwekea nyekundu una uhakika ulichokiandika ni sawa> au utapenda kuparekebisha?
 
Code:
[FONT=century gothic]
MM,

Kuna ninayoyajua mie wewe huyajui mathalan ndugu hawa waliokuwa wameshibana kiasi kile vipi udugu ukakatika. 

Sasa mie kama nitakwenda kwa Mama Maria itabidi mathalan nimuulize siku zao yeye na mumewe na wazee wangu. 

Miaka na miaka imepita si wa salamu wala barua kati yao.

 Abdulwahid hata katika historia kafutwa sasa kweli hapo unakwenda kuuliza maswali kama hayo si kutaka kumfedhehesha?

Lakini kwa Biti Hassani Mwanakijiji atamuuliza hebu nipe habari za kaka yako Bwana Abdu Sykes. Hapo huyu bibi utamsikia nini atasema kuhusu harakati zile nani akiwaona wakija pale, vipi thumni thumni ya kumpeleka mweshimiwa UNO.

 Vipi Mtemvu alivyowaudhi, vipi Tatu biti Mzee na Titi wakihamasisha wanawake kupiga kura na kutoa michango kwa TANU nk. nk.

Nadhani mantiki umeipata vyema.

Huendi nyumbani kwa mtu kumtia unyonge kwa maswali ambayo tayari unayo majibu yake.

Unajua hadi leo wazee wangu wote niliowataja humu ukumbini hawatambuliki kama mashujaa wa uhuru na kama huamini  subira kilele cha 9 Desemba utashuhudia mwenyewe.

Hakuna hata mmoja atakaeadhimishwa.

Sasa kweli umuulize Mama Maria vitu kama hivi si utakuwa unamuonea na  kumjaza simanzi bila sababu?

Mohamed[/FONT]
 
Mnapomzungumzia Mama Maria Nyerere mnajua amesoma mpaka darasa la ngapi?
Je mnaujua uwezo wake?
Je Nyerere mwenyewe alimuhusisha katika vitu vyake hususan vya kitaaluma na uongozi?
au alikuwa ni mama wa nyumbani wa pika pakua tu?

Kila la kheir.
Mama Maria alikuwa mwalimu wa shule ya wanafunzi wa kike kabla ya kuolewa na Nyerere. Kwa kisomi cha wakati huo ni mtu aliyesoma sana tu.
Usianze kutuletea hapa kama ulivyofanya kuhusu makabila ya Kenya na Uganda. Do your research before you speak.
 

Asante sana sheikh mohamed,

Ndio sababu nilimuuliza Maranya je mtu mzima akiwa hajataka kuonana na wewe hufahamu tu jibu lake? Huu msumari ni hatari Mohamed unalo la kujitetea Maranya?
 
Mama Maria alikuwa mwalimu wa shule ya wanafunzi wa kike kabla ya kuolewa na Nyerere. Kwa kisomi cha wakati huo ni mtu aliyesoma sana tu.
Usianze kutuletea hapa kama ulivyofanya kuhusu makabila ya Kenya na Uganda. Do your research before you speak.

Tawire mkuu au kwa jina lengine ni No research no right to speak mkuu au vp? Ila sio mbaya ukatupatia elimu yake ameishia darasa la ngapi au degree ya ngapi. Fahamu kuwa enzi zile ukijua kuongea kiingereza tu unakuwa mwalimu. Ukiwa mstaarabu unajua kuvaa vizuri basi unakuwa tarishi. Hebu tupatie elimu yake mkuu tutashukuru sana!!!
 
Mohamed Said atakuja kuijibu yeye mwenyewe kuhusu hili, au unaniuliza mimi? mimi sina shaka na ayasemayo.

Based on hearsay kutoka kwa nani?

Halafu hapo nilipokuwekea nyekundu una uhakika ulichokiandika ni sawa> au utapenda kuparekebisha?

Jasusi,

Nizue uongo ili iweje?

Mangapi ya ukweli hata nione hayatoshi nijazie kwa uzushi?
Kama kuaminika wengi wameniamini sina sababu ya kusema uongo.

Isitoshe hilo la nyaraka zilizopotea si mimi peke yangu ninalolijua ukipenda
fika Maktaba ya CCM Dodoma, TNA Dar es Salaam na wewe ufanye utafiti.

Mswada wa historia ya TANU aloandika Abdu na Dr Kleruu si umeibiwa hapo
hapo?

We ukiyajua haya? Au na hili nasema uongo?

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…