Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hivi unafahamu msemo unaosema birds of same feathers fly together??? Unajua kuwa rafiki yako wa karibu anakujua zaidi kuliko hata mkeo. Especially yule mlieshibana naye? Kama umeoa mkuu utafahamu kwamba kuna mambo mengine huwezi kumwambia mke mathalani mfano ukipatwa na matatizo fulani ambayo unayamudu ni aghlabu sana kwa wanaume kuwaambia wake zao mpaka pale akiwa hana jinsi kwa kuhofia mkewe asianze kupatwa na wasiwasi na kupanic? Did you ever asked yourself that?
Mwanakijiji,
Kama ni hilo basi mimi sina haja ya kwenda kwa Mama Maria...nayajua mengi.
Wala sitathubutu kufanya hivyo huyu Bi Mkubwa na sawa na mama yangu.
Kuna vitu kwa ajili ya adabu huelezi watu wala huandiki watu wasome kwa kuwa
si mambo yatakayosaidia kuijua historia ya nchi yetu.
Baada ya uhuru palipitika upasi...tosheka na hilo ndugu yangu na turudi kwenye
yake yatakayotoa mwanga wa kuichambua historia yetu.
Mwanakijiji mimi ni mzao watu hawa...ndio walionileta duniani na kunilea hapa
hapa Dar es Salaam.
Kuna wakati mimi nikitembea Dar es Salaam Gerezani kule nina miaka kama sita
hivi akina mama wakiniita kwa jina la marehemu mama yangu "We mtoto wa Baya."
Nikenda wananishika kichwa na kunifariji kwani wakimkumbuka mama yangu, shoga
yao. Hapo kimoyomoyo wakiniombea dua Allah anikuze.
Hadi leo akina mama hawa wapo na kila n ikiwatembelea kwanza ni chozi kisha
mazungumzo.
Nenda kazungumze na Biti Hassan Machakomo. Bi wa Kizulu huyu jamaa zake akina
Sykes...
Huyu kaiona historia yote toka siku ya kwanza...
Mohamed