Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Mohamed,
Unaongopa hadi basi. Mwalimu kafanyakazi na WAISLAMU na UISLAMU tangu TAA. Ipo siku alifunga na WAISLAMU akiombea kitu fulani. Kichwa kikamuuma. Hiyo hadithi aliisimulia katika moja ya hotuba zake akimtaja Mzee wako mmoja wa Bagamoyo. Amefanya kazi na Waislamu wengi wa Zanzibar. Amehudhuria mabaraza ya IDD. Majibu ya Mwalimu kwa Mwilima mngeyavumilia? Mwalimu alikuwa mkweli sana. Asingemjibu Mwilima halafu akaeleweka misikitini.
 
Soma jibu Na. 4 kwenye ile post yako. Mwalimu alizikalia pesa za Gaddafi kweli? Mama Maria akaona mtetemeko na kaburi kuwaka moto! Porojo na kejeli zingine zinapotolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kama wewe Faiza haipendezi.

Hakuna porojo hapo soma:
 
WC,

Wanaomfahamu Nyerere wanasema alikuwa anakwepa sana ile ya uso kwa uso yaani nipe nikupe. Nadhani umenifahamu.

Ninazozifahamu mimi za nipe nikupe uso kwa uso ni nne na zote kapambana na Waislam:
  1. Schneider Plantan baada ya kuachiwa kutoka kizuizini alimfata Nyerere nyumbani kwale kukawa na mnakasha wa aina yake.
  2. Bilali Rehani Waikela, katika mkutano wa EAMWS Ukumbi wa Shule ya Wasichana Agakhan, Dar es Salaam1963, ilikuwa hotuba ya kuonyeshana vidole
  3. IGP Hamza Aziz baada ya kukataa kutii amri kumkamata Mufti Sheikh Hassan bin Amir, ndani ya katika Kamati Kuu
  4. Mwilima, ndani ya Kamati Kuu
Mohamed
 
Hongera sana Mwakajila kwa mchango wako wa kuelimisha jamaa zetu hapo juu, japo nadhani hawakuelewa kulingana na sisis watanzania tulivo wavivu wa kusoma takwimu, na vitabu mbalimbali
 

Mwalimu hakuwa mkweli alikuwa mnafiki, mchoyo na mbaguzi

Alifanya upendeleo kwa kanisa akifikiri kupata dhawabu kwa Mungu wake (udini)

Ila hakuwa mwizi tu
 
Nipe darsa jingine. Ilikuwaje huko Nchi za Kiarabu ambako ndiko chimbuko halisi la Uislamu wakakubali kutawaliwa namna ile ya Tunisia, Libya, Misri, SaudArabia, Syria,.....Halafu wanazinduka sasa na kuanza kuchinjana?
 
Nipe darsa jingine. Ilikuwaje huko Nchi za Kiarabu ambako ndiko chimbuko halisi la Uislamu wakakubali kutawaliwa namna ile ya Tunisia, Libya, Misri, SaudArabia, Syria,.....Halafu wanazinduka sasa na kuanza kuchinjana?

Hatupo katika mjadala huu kuizungumzia Tunisia, Libya, Misri, Saudi Arabia wala Syria. Soma Kichwa cha mjadala hapo juu kisha njoo na maswali na majibu yanayohusu.

Ukipenda kujadili hayo mengine yafungulie nyuzi na wenye interest nayo watakuja kujibu.
 
Soma jibu Na. 4 kwenye ile post yako. Mwalimu alizikalia pesa za Gaddafi kweli? Mama Maria akaona mtetemeko na kaburi kuwaka moto! Porojo na kejeli zingine zinapotolewa na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri kama wewe Faiza haipendezi.

Kama ile haijakutosha hii hapa nyingine, hakuna porojo hapa:

Field Marshall ES
...Matetemeko mawili mfululizo, yalitokea tena jana katika maeneo hayo ya mazishi huko Butiama...
 
Sio Mwalimu tunayemfahamu! Akataliwe hata na aloowateua akina IGP Hamza Aziz wa Mtoni kwa Aziz Ali? Mwalimu alikuwa mvumilivu na msikivu pia. Ukumbuke pia kwamba kuijenga nchi isiyo na DINI kutoka TANU ya WAISLAMU wa misimamo mikali kama masheikh unaowataja hapo haikuwa kazi ndogo.
 
Ngoja nikupe darsa kidogo; Maana ya dini kwa kiarabu (kumbuka dini ni neno lenye asili ya kiarabu) ni mfumo wa maisha, ni namna mtu unavyochaguwa kuishi.

Maana ya neno dini na maana ya dini inaweza kuwa ni vitu viwili tofauti ndugu yangu. Ukiuulizwa neno kiti lina maana gani na ukiulizwa kiti ni nini ni maswali mawili yanayohusu kitu kimoja kwa muktadha tofauti. Dini kwa maana ya matendo ya mtu na dini kwa maana ya jina ni vitu viwili tofauti. Mtu anaweza kuitwa muislamu lakini asiishi maisha ya kiislamu kwani uislamu una vitu vingi mno hata kiasi kwamba kimoja kikipungua huwezi kuutoa uislamu wa mtu.
kutukana ni kinyume cha uislamu lakini si kama anayetukana unauvua uislamu waka papo papo. Dini kama mfumo ni kitu cha kujadili. Na tafsiri ya neno huwa haina uhusiano na kitu chenyewe, Hebu angalia hii. Kiti, kichumbi, Ichumbi,Kigoda, chitengo au chair. haya maneno yanazungumzia dhana tofauti?


Mbona Mohamed Said kasema nyie waislamu huwa mnazaliwa mkiwa waislamu?


Neno siasa na siasa ni vitu viwili tofauti kwa sasa. Neno Demokrasia lilikotoka na jinsi demokrasia yenyewe inavyotafsiriwa sasa ni tofauti kabisa. Kwa asili neno Jambazi lilimaanisha jitu lenye miraba minne, haya majambazi yetu ya sasa hivi yana miraba minne?

Kwa hiyo kaa uelewe, hakuna siasa kama itadhalilisha dini "mfumo wa maisha" wa mmoja wapo ikawa hiyo siasa ni ya amani.

Siyo dini tu,siasa yoyote inayodhalilisha utu wa mtu ni siasa mbaya.


The word "alphabet" came into Middle English from the Late Latin word Alphabetum, which in turn originated in the Ancient Greek ἀλφάβητος (alphabētos), from alpha and beta, the first two letters of the Greek alphabet. Alpha and beta in turn came from the first two letters of the Phoenician alphabet, and meant ox and house respectively. There are dozens of alphabets in use today, the most common being Latin, deriving from the first true alphabet, Greek. Most of them are composed of lines (linear writing); notable exceptions are Braille, finger spelling, and Morse code.



Kama hujanielewa naomba uliza, si rahisi wengine kulielewa darsa, kwa wengine ni rahisi kulielewa darasa.
Darsa au darasa?
 
Mohamed,
Yote hayo nilishayasoma kwenye kitabu chako. Hakuna haja ya kuyarudiarudia hapa. Nimesema Nyerere hakuwa mdini, alikuwa nationalist. Na hilo huwezi kulisuta. Ulichotaka wewe ni kile kilichotokea Kenya ambako Kenyatta na ukoo wake na kabila lake walijiona wao ndio wana haki ya kuwa na lion's share ya national power. Lakini matokeo yake tuliyaona 2007. Wewe ulitaka Waislamu wa Gerezani ndio wawe akina Buhari, Tafawa Balewa (yaani Wahausa) wa Tanzania. Mwalimu alituepusha na hilo na leo kuna level playing field. Hilo huwezi kusuta. Haya mengine yote ni hadidu za rejea tu. Wenye udini ni ninyi mnaojiona kuwa mlinyang'anywa entitlements zenu.
 
Mwalimu hakuwa mkweli alikuwa mnafiki, mchoyo na mbaguzi

Alifanya upendeleo kwa kanisa akifikiri kupata dhawabu kwa Mungu wake (udini)

Ila hakuwa mwizi tu
Hauwezi kuwa mnafiki halafu ukaacha kuwa mwizi. Hizi ni sifa kama pacha wale wa yai moja.
 
Wenzako wanaiona hiyo ndio baadhi ya miujiza ya kumfanya Mwalimu awe MTAKATIFU wewe unadhani ni fedha za msikiti wa Gaddaffi?

Hao "wenzako" wanaoona huo ndio utakatifu sijui kigezo chao. Mimi siamini tetemeko la ardhi liwe ni "utakatifu".
 
Bi Faiza,
Acha uwongo. Nina hakika dini yako inakataza uwongo. Nilikuwepo Butiama wakati wa mazishi ya Mwalimu, na msikiti ule niliuona ukiwa umeshamalizika kujengwa. Leo unathubutu kuja hapa kuuambia kadamnasi kwamba msikiti ulijengwa na Mama Maria? Staflulaaah! Na hii ndiyo mindset yenu?
 

Nyerere hakutuepuesha chochote...

Yeye aliifaidisha kanisa na dini yake above national interest of course intention yake apate dhawabu kwa mungu wake (udini)
 

Kama ulikuwepo msikiti basi ni kabla ya kujengwa upya kwa fedha za Gaddafi alizozikalia Nyerere mpaka anakufa. Mama Maria mwenyewe alitangaza kuwa kuna fedha Nyerere alipewa na Gaddafi za kujengea msikiti na utajengwa huko. Kama ni huo umejengwa upya au kuna mwingine umejengwa kwa hizo fedha baada ya kufa Nyerere hilo pia linawezekana. Si sifa yangu kusema uongo na nnauhakika na niyasemayo.
 
Hao "wenzako" wanaoona huo ndio utakatifu sijui kigezo chao. Mimi siamini kuetetemeka kwa ardhi kuwe ni "utakatifu".
Sio "utakatifu" bali muujiza! Mwalimu hakuwa wa kawaida kama mimi na wewe tukibahatika kupewa nafasi alookuwa nayo. Mmekosa cha maana cha kumkosoa mmekimbilia UDINI.
 

Jasusi,

Tutakuwa tunarudia humo kwa humo.

Waislam baada ya kuzunguka nchi nzima wakiuelimisha umma kuhusu mfumokristo wametoa kijitabu kinachoonyesha viwango vya mambo mengi kati ya Waislam na Wakristo.

Bahati mbaya mimi sijakipata lakini katika ugawanajiwa madaraka Wakristo wamehodhi 83% na Waislam wamabakiziwa 17%.

Serikali imeombwa itoe maelezo hali hii imekujaje.

Tusubiri majibu.

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…