Zimmermann
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 3,506
- 2,606
bado unaendelea ..tukirudi kwenye posts zako zote utapona kweli we msomi?haibu = Aibu
kuhona = Kuona
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
bado unaendelea ..tukirudi kwenye posts zako zote utapona kweli we msomi?haibu = Aibu
kuhona = Kuona
Sheikh Mohamed,
Hiki kisa cha Karume ama kwa hakika chafurahisha na kusisimua sana. I wish na maraisi wengine wangekuwa na utaratibu kama huo!!
Nadhani itoshe kusema kwamba tunahitaji kufanya mambo mengine. Mnakasha huu umefika mahali ambapo hakuna jipya tena, ingawa ni ukweli kwamba tumejifunza mambo mengi sana yaliyodhahiri na mengine yaliyo nyuma ya pazia. Ni wajibu wetu kuyatafakari yote yaliyoandikwa hapa na kuyachambua kwa makini ili kila mmoja achukue hatua stahiki kwa mustakabali wa nchi yetu na mtu mmoja mmoja.
Bila shaka tutaendelea kukutana katika mijadala mingine, maana hapa JF ndio jungu kuu.
Msomi FF , itabidi nikuage kwa staili hii. "Usitupe mawe kama unaishi kwenye nyumba ya vioo".
hapo chini kwenye bold ulikuwa na maana ya 'live' au?.....Mbona tulikuelewa lakini hatukupiga kelele kama hizi zako hapo juu?
MM,
Nakushukuru sana kwa maneno yako mazuri.
Nina kitu sipati jibu labda unaweza kunisaidia.
Hebu nifahamishe nini khasa kinawakera baadhi ya wachangiaji humu kiasi cha kunitukana?
Ni hasad kuwa ni wazee wangu ndiyo waliojaliwa kuwa na historia hii (ambayo kwa hakika ni kitu cha kujivunia) au ni kitu gani?
Nakuuliza kwa dhati kabisa kwa kuwa mimi nishasikia mengi jinsi kanisa linavyosaidia nchi hii katika elimu, afya nk. nk. jambo ambalo ni kweli na serikali ikilisifia kanisa na kusema serikali itashirikiana na kanisa bega kwa bega kuleta maendeleo lakini haijanipelekea kuhamaki na kutoa matusi kuwatukana wanaoeleza ambo hayo.
Inakuwaje mimi kueleza juhudi na mchango wa wazee wangu katika kupambana na ukoloni ikawa kitu cha kukera?
Hii ni katika mambo ambayo akili yangu haijaweza kutambua.
Ikiwa una jibu tafadhali nisaidie.
Mohamed
Hili jina la "Mohamed Said" ni la kutilia mashaka. Iweje Mbantu tena Mtanganyika mwenye uchungu na nchi yake asitumie jina lake la ukoo la Kibantu akiwa kama Mwandishi? Obviously something fishy seems to be going on here. Vitabu na "papers" zote kwenye lugha ya Kiingereza vimeandikwa na watu au mtu mwingine, na "Mohamed Said" anapewa credit for authorship sababu "Mohamed Said" happens to be a very generic name among Muslims na inakuwa rahisi kwake kualikwa nje ya nchi etc kutumia jina la "Mohamed Said" ukilinganisha na tuseme kama angekuwa anajiita "Mohamed Said Mbukuzi".
Nasema kazi za uandishi anazodai kuandika "Mohamed Said" ni bogus unless atuwekee angalu video moja akichangia maada au chochote kwa lugha ya Kiingereza kwenye moja ya warsha, presentations, au mikutano lukuki ya Kisomi anazodai kuhudhuria nje ya nchi ( na kama anavyo-boast mwenyewe kwa jinsi passport yake ilivyojaa mihuri.)
Yes, nilikuwa na maana "live", na ahsante kwa kunirekebisha, ilmu haina mwisho.
Tatizo lenu mnaporekebishwa mnaona mmepigiwa kelele, Mohamed Said anarekebisha makosa yaliyokuwepo kwenye historia ya kujipatia madaraka Tanganyika, nayo mnaona anawapigia kelele.
Ahsante kwa kunirekebisha, huo ndio moyo tunaotakiwa tuwe nao wa kurekebishana kwenye makosa, na sisi wengine hufurahi sana tunaporekebishwa.
Nafikiri huku ni kukosa fadhila na kujawa na chuki na husda.
Ameshaweka hadharani machapisho yake na wapi amechapisha , sasa kwa mwenye busara na hikma ni wajibu wake kutafuta kupitia pale vilipochapishwa hata kupitia kwenye library zote kubwa kubwa (huko Tanzania pitia pale library ya UDSM) uvusome na kisha kutoa comment zako.
Kuweka video hiyo ni kutaka sasa kutafuniwa kabisaa wewe ubaki kumeza tu kitu ambacho sio sahihi kwa mwenye kutafuta elimu.
Kumbuka kuwa yeye hakusoma kwa nia ya kujionyesha bali amesoma kwa ajili yya Mola na hapa anatumikia kazi ya mola yaani kuuelimisha umma wote kwa kile alichojaaliwa kukipata na yeye anatupa na sisi.
nakupa pole sana
haibu = Aibu
kuhona = Kuona
mhandishi = muandishi.
enzi zile tukihadithiwa simulizi za simba na sungura na kina bibi/babu tuliamini kama wanyama hawa walikuwa katika mapori ya kina bibi na babu tu. lakini tulipokua(kama Mo) tukajua laa kumbe simba na sungura wapo kila mahala penye pori kama alivosema bibie FF. Tukaachana na mapokeo ya kina bibi. ni haibu kuhona kuwa mtu anayejinasibu kuwa mhandishi mzuri anaweza kutuletea hadithi za mapokeo alosimuliwa na babuze ati uhuru uliletwa na wapagazi wa gerezani kariakoo.
Hata utakatifu ni sifa na wala haihusiani na dini bali tabia ya mtu kwenye jamii. Kwa heri Bi Mkubwa tuonane kwenye thread nyingine!!
haya mafundisho ya kusadikishana ati uhuru wa Kariakoo Gerezani nani atayasikiza?
huyo Mohamed Said Mbona kaficha jina lake la ukoo.
mbona wewe ukoo wa mbweha na umeweka wazi wazi. Kwa nini atumiea majina ya kiarabu?
Jamani kama uhuru ulipiganiwa gerezani, basi Tanganyika bado haijapata uhuru.
bado unaendelea ..tukirudi kwenye posts zako zote utapona kweli we msomi?
Sheikh Mohamed,
Hiki kisa cha Karume ama kwa hakika chafurahisha na kusisimua sana. I wish na maraisi wengine wangekuwa na utaratibu kama huo!!
Nadhani itoshe kusema kwamba tunahitaji kufanya mambo mengine. Mnakasha huu umefika mahali ambapo hakuna jipya tena, ingawa ni ukweli kwamba tumejifunza mambo mengi sana yaliyodhahiri na mengine yaliyo nyuma ya pazia. Ni wajibu wetu kuyatafakari yote yaliyoandikwa hapa na kuyachambua kwa makini ili kila mmoja achukue hatua stahiki kwa mustakabali wa nchi yetu na mtu mmoja mmoja.
Bila shaka tutaendelea kukutana katika mijadala mingine, maana hapa JF ndio jungu kuu.
Nafikiri wewe jukwaa hili huliwezi..nenda kwenye yale mambo yenu mepesi
Ngoja nikuongezee kidogo: Sisi tunafundishwa unapo mpa mtu elimu inakuwa ni sadaka tena ni "Sadakat ul Jariah" sadaka ambayo hata ukifa kila inapotumika na wewe una ''jaza'a" ndani yake, ndio maana utaona hatuna choyo katika kufundisha. Na tunampenda afundishae.
Topical,
Hivyo ulivyomjibu humpati unampoteza kwa hiyo hatonufaika na mnakasha na elimu iliyokusudiwa imfikie.
Huyu anahitaji kunasiiwa kwa maneno mazuro kumweleza kuwa unaposema maneno ya jeri na kejeli mbele za watu si vyema nk. nk. lakini wewe unamfukuza kabisa jamvini ilhali ushamuona hali yake.
Huyu anahitaji kufunzwa adabu na akishaipata ikiwa si jeuri basi atakuwa mwerevu na atajua namna ya kuzungumza hadharani.
Ni sawasawa kumfunza mtoto adabu za kula. Anaelezwa kunawa, kula na mkono wa kulia, kumega kile chakula kilichopo karibu yake nk. nk.
Wakati mwingine sisi tunakosea kwa kudhani wote wamepita katika makuzi kama yetu.
Huyu bwana kuna mahali katoa tusi zito sana nimeogopa hata kulisemea kwa kuchelea wengine wasilione likakuzwa ikawa mie sasa ndiye nitukanae.
Insha Allah tumuombee dua akae sawa.
Mohamed
Nafikiri wewe jukwaa hili huliwezi..nenda kwenye yale mambo yenu mepesi
Kuna mtu aliyetokea kusikojulikana ambaye mpaka sasa ameacha sintofahamu ni wapi hasa aliipotokea na kuwaachia wana historia wabashiri ni wapi alitokea. Mtu huyo ambaye kwa maelezo yake walikuwa kwenye vita na wenzake watatu wakakimbizwa na maadui wao na hatimaye kutawanyika, mmoja akaenda Kaskazini, mwingine Kusini na Mmoja akafika eneo la Udzungwa mahali kunaitwa Ng'uruwe.
Mtu huyu ambaye jina lake halijulikani mpaka sasa alipewa majina mawili na wenyeji wa Udzungwa jina moja aliitwa Mfwimi = Mwindaji kwani alikuwa ni mwindaji hodari sana na jingine Muyinga yaani mtu aliyefika mahali kwa kutangatanga. Mtu anahisiwa kwamba inawezekana alikuwa ni mtu wa pwani kwani alipofika Ng'uruwe alikuwa na furushi la Chumvi, lakini dhana nyingine mtu huyu anaweza kuwa alikuwa ni Mkamba kutokana na umbo lake kubwa.
Mfwimi au Muyinga alizaa na Semduda mtoto wa mtawala wa eneo la Ng'uruwe mtoto aliyezaliwa akaitwa Muyinga. Muyinga akamzaa Maliga na Mkini, Maliga akamzaa Kilonge ambaye akawazaa watoto wawili, Ngaonalupembe na Munyigumba. Munyigumba alimuua Ngaonalupembe wakati mkewe akiwa mjamzito. Baada ya kufanya mauaji hayo Mnyigumba alisema mtoto atakayezaliwa atajwe kuwe ni wake
Mke wa Ngaonalupembe ambaye alikuwa ni Sekinyaga Semlimwandi alizaa mtoto wa Ngaonalupembe akiwa anaishi na Munyigumba, mtoto huyo aliitwa Kong'oke. watoto wa Mnyigumba ambao alizaa na mke wake Sengimba ni Mkwawa na Mpangile. Baadaye Mkwawa alikuja kumuua Kong'oke.
Baadhi ya watoto wa Mkwawa ni hawa
1. Sapi ambaye baadaye alisilimu na kuitwa Yusuph. Mama yake ni Semsilamgunda
2. Ligiliwe ambaye naye alisilimu akaitwa Mohamed. Mama yake ni Mganga Senyenza
3 Pancrass- Mkristo. Mama yake ni Semelele Msangu toka ukoo wa kina Melele.
4. Ananasi - Mkristo
5. Boniface - Mkristo
6. Mwanzali ambaye alisilimu akaitwa Athumani
7. Kilemaganga alikuwa ni mwanamke na aliolewa kwenye ukoo wa chifu wa Usangu Melele.
Ilikuwaje watoto wa Mkwawa wengine wakawa waislamu na wengine wakawa wakristo? Wakati yeye Mwenyewe hakuwa Muislamu wala Mkristo!!
hili jukwaa ndo limejaa mambo mepesi haswaa. hivi kuna umakini wowote mtu kutuletea makala za 'visa' na kutaka kutuaminisha kuwa hiyo ni historia?
kama anafanya promo ya machapisho yake hapa kwangu hapati kitu.
kwanza niambieni tofauti ya 'kisa' na 'historia'. kwa ufasaha bila kutafuna maneno.
historia ina heshima yake msituletee haraati zenu za kiislam hapa.
hili jukwaa ndo limejaa mambo mepesi haswaa. hivi kuna umakini wowote mtu kutuletea makala za 'visa' na kutaka kutuaminisha kuwa hiyo ni historia?
kama anafanya promo ya machapisho yake hapa kwangu hapati kitu.
kwanza niambieni tofauti ya 'kisa' na 'historia'. kwa ufasaha bila kutafuna maneno.
historia ina heshima yake msituletee haraati zenu za kiislam hapa.