Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


MM,

Nakushukuru sana kwa maneno yako mazuri.
Nina kitu sipati jibu labda unaweza kunisaidia.

Hebu nifahamishe nini khasa kinawakera baadhi ya wachangiaji humu kiasi cha kunitukana?
Ni hasad kuwa ni wazee wangu ndiyo waliojaliwa kuwa na historia hii (ambayo kwa hakika ni kitu cha kujivunia) au ni kitu gani?

Nakuuliza kwa dhati kabisa kwa kuwa mimi nishasikia mengi jinsi kanisa linavyosaidia nchi hii katika elimu, afya nk. nk. jambo ambalo ni kweli na serikali ikilisifia kanisa na kusema serikali itashirikiana na kanisa bega kwa bega kuleta maendeleo lakini haijanipelekea kuhamaki na kutoa matusi kuwatukana wanaoeleza ambo hayo.

Inakuwaje mimi kueleza juhudi na mchango wa wazee wangu katika kupambana na ukoloni ikawa kitu cha kukera?

Hii ni katika mambo ambayo akili yangu haijaweza kutambua.

Ikiwa una jibu tafadhali nisaidie.

Mohamed
 
Msomi FF , itabidi nikuage kwa staili hii. "Usitupe mawe kama unaishi kwenye nyumba ya vioo".
hapo chini kwenye bold ulikuwa na maana ya 'live' au?.....Mbona tulikuelewa lakini hatukupiga kelele kama hizi zako hapo juu?

Yes, nilikuwa na maana "live", na ahsante kwa kunirekebisha, ilmu haina mwisho.

Tatizo lenu mnaporekebishwa mnaona mmepigiwa kelele, Mohamed Said anarekebisha makosa yaliyokuwepo kwenye historia ya kujipatia madaraka Tanganyika, nayo mnaona anawapigia kelele.

Ahsante kwa kunirekebisha, huo ndio moyo tunaotakiwa tuwe nao wa kurekebishana kwenye makosa, na sisi wengine hufurahi sana tunaporekebishwa.
 

Mkuu shukrani sana kwa kutuwekea hii kitu hapa. Tumejifunza mengi.
Ningependa wakati unahitimisha huu mjadala(siku yeyote) utupe sisi wanajamvi latest facts and figures kuhusu haya hapa ya ‘Mfumo Kristo'.
Upendeleo wa ajira. Naomba utueleze hiyo 83% Christians–17% Muslims imetoka wapi?
Upendeleo kwenye Elimu.
Na jinsi Kanisa linavyoiendesha serikali.

Haya ni kati ya masuala ambayo umeshindwa kuyajibu na kuishia kutoa visingizio mbalimbali.
Sisi tunajiuliza kama kweli na usomi wako umefikia conclusion kwamba kuna mfumo kristo , facts ziko wapi?
Ukishindwa kuweka hapa facts baadhi yetu tutachukua hata hatua ya kuzishauri hizo taasisi za nje ya nchi ambazo unakwenda ku present papers zako zikushinikize kutoa facts and figures ambazo zinaendana na maisha yetu sasa hivi. THIS IS NOT A JOKE!
Tunataka facts siyo speculations.

Mkuu, hata sisi tulio kuja duniani miongo kadhaa baada yenu tunataka sisi ,watoto wetu, wajukuu zetu waikute Tanzania ileile ya amani na utulivu ila ikiwa na maendeleo na neema zaidi.
Nashukuru tena kwa dedication yako uliyoionyesha katika kujibu post nyingi za wanajamvi.
 

Nafikiri huku ni kukosa fadhila na kujawa na chuki na husda.

Ameshaweka hadharani machapisho yake na wapi amechapisha , sasa kwa mwenye busara na hikma ni wajibu wake kutafuta kupitia pale vilipochapishwa hata kupitia kwenye library zote kubwa kubwa (huko Tanzania pitia pale library ya UDSM) uvusome na kisha kutoa comment zako.

Kuweka video hiyo ni kutaka sasa kutafuniwa kabisaa wewe ubaki kumeza tu kitu ambacho sio sahihi kwa mwenye kutafuta elimu.

Kumbuka kuwa yeye hakusoma kwa nia ya kujionyesha bali amesoma kwa ajili yya Mola na hapa anatumikia kazi ya mola yaani kuuelimisha umma wote kwa kile alichojaaliwa kukipata na yeye anatupa na sisi.

nakupa pole sana
 


Ngoja nikuongezee kidogo: Sisi tunafundishwa unapo mpa mtu elimu inakuwa ni sadaka tena ni "Sadakat ul Jariah" sadaka ambayo hata ukifa kila inapotumika na wewe una ''jaza'a" ndani yake, ndio maana utaona hatuna choyo katika kufundisha. Na tunampenda afundishae.
 

Barubaru, ni vyema ukafahamu kuwa huyo anataka "video" ya Mohammed Said sio asome, bali anatafuta kila njia za kum"discredit", hazipati. Sasa ameona anhaaaa, "video" ndio maana kaikwamisha santuri hapo hapo kwenye "video", "video", "video". Hana zaidi.
 

Nafikiri wewe jukwaa hili huliwezi..nenda kwenye yale mambo yenu mepesi
 
Hata utakatifu ni sifa na wala haihusiani na dini bali tabia ya mtu kwenye jamii. Kwa heri Bi Mkubwa tuonane kwenye thread nyingine!!

Mbona umekatisha mazungumzo? ntapokukuta huko, kumbuka, ntakupa jibu ya hili.
 

Inaonesha huu mnakasha hujaupitia vizuri unakurupuka tu, Mohamed Said kataja ukoo wake wa pande zote mbili, kauelezea vilivyo, rejea posts utaukuta, hata wenzako wanakucheka ukisema hivyo. Unanshangaza.
 
bado unaendelea ..tukirudi kwenye posts zako zote utapona kweli we msomi?

Ngoja nikuongezee kidogo: Sisi tunafundishwa unapo mpa mtu elimu inakuwa ni sadaka tena ni "Sadakat ul Jariah" sadaka ambayo hata ukifa kila inapotumika na wewe una ''jaza'a" ndani yake, ndio maana utaona hatuna choyo katika kufundisha. Na tunampenda afundishae.
 

MM,
Hakika mnakasha ndio upo katikati na wengi wetu tunaofuatilia kwa makini tunaona kuna mengi sana Bw Moh'd Said alitaka kutudarsisha Lakin kumetokea kikundi cha watu chenye nia ya kutaka kutibua mnakasha kwa kuleta masuala ya kitoto na lugha za matusi na kebehi kwa nia ya kupindisha mada husika.

Hakika mimi naamini yoyote mwenye nia ya kujifunza basi anakaa kimya pale unapotolewa muhadhara na kuuliza kama ana suala pale panapowekwa nukta.

Sasa nazidi kusisitiza tuna mengi ya kujifunza kutoka katika bahri hii ya historia anazotupa Sheikh Mohamed Said. Hakika mimi nimejifunza mengi sana kutokana na maandiko yake hususan ya humu na kunipa hamu kubwa sana kupitia machapisho yake kwa nia ya kujua zaidi. Hii ni bahati kubwa sana tulionayo watu wa JF kwa kuwa na waandishi mahiri kama hawa. Tuwatumie vizuri ili kujifunza mengi.
 
Nafikiri wewe jukwaa hili huliwezi..nenda kwenye yale mambo yenu mepesi

Topical,

Hivyo ulivyomjibu humpati unampoteza kwa hiyo hatonufaika na mnakasha na elimu iliyokusudiwa imfikie.

Huyu anahitaji kunasiiwa kwa maneno mazuro kumweleza kuwa unaposema maneno ya jeri na kejeli mbele za watu si vyema nk. nk. lakini wewe unamfukuza kabisa jamvini ilhali ushamuona hali yake.

Huyu anahitaji kufunzwa adabu na akishaipata ikiwa si jeuri basi atakuwa mwerevu na atajua namna ya kuzungumza hadharani.

Ni sawasawa kumfunza mtoto adabu za kula. Anaelezwa kunawa, kula na mkono wa kulia, kumega kile chakula kilichopo karibu yake nk. nk.

Wakati mwingine sisi tunakosea kwa kudhani wote wamepita katika makuzi kama yetu.

Huyu bwana kuna mahali katoa tusi zito sana nimeogopa hata kulisemea kwa kuchelea wengine wasilione likakuzwa ikawa mie sasa ndiye nitukanae.

Insha Allah tumuombee dua akae sawa.


Mohamed
 

chaji imeisha na sekta ya Malima na Idrisa Rashid na Badra Masoud walishatukatia umeme siku nyingi.

nitarudi.

sitoacha kuchangia mnakasha huu mpaka Tanganyika itakapokuwa huru tena.
 

jombaa napenda kweli unapoandika kama unaimba ngonjera.

yote heri.

lakini kuna tusi kubwa katika makala zako kama la kumdhalilisha Nyerere kuwa alikuwa akinunuliwa mahitaji ya nyumbani kwake na wale wazee wa gerezani?

huyajui matusi wewe.

kajipange.

kumtukana Baba wa Taifa ni kukosa adabu kupindukia.

niwekee hilo tusi nione nitafakari kama nimetukana au unaendeleza makala zako za 'visa'.

we need history, not visa.
 
Nafikiri wewe jukwaa hili huliwezi..nenda kwenye yale mambo yenu mepesi

Topical,

Hivyo ulivyomjibu humpati unampoteza kwa hiyo hatonufaika na mnakasha na elimu iliyokusudiwa imfikie.

Huyu anahitaji kunasiiwa kwa maneno mazuro kumweleza kuwa unaposema maneno ya jeri na kejeli mbele za watu si vyema nk. nk. lakini wewe unamfukuza kabisa jamvini ilhali ushamuona hali yake.

Huyu anahitaji kufunzwa adabu na akishaipata ikiwa si jeuri basi atakuwa mwerevu na atajua namna ya kuzungumza hadharani.

Ni sawasawa kumfunza mtoto adabu za kula. Anaelezwa kunawa, kula na mkono wa kulia, kumega kile chakula kilichopo karibu yake nk. nk.

Wakati mwingine sisi tunakosea kwa kudhani wote wamepita katika makuzi kama yetu.

Huyu bwana kuna mahali katoa tusi zito sana nimeogopa hata kulisemea kwa kuchelea wengine wasilione likakuzwa ikawa mie sasa ndiye nitukanae.

Insha Allah tumuombee dua akae sawa.


Mohamed
 

Tunashukuru kwa uchambuzi wa familia ya Mkwawa,

Ila mambo mawili matatu naomba ufafanuzi. Kwanza ilikuwaje hadi Rumaliza alifanikiwa kupenya katika ngome ya wahehe na kupata influence kubwa? Pia BG Martin (1969) (Article nilishaitaja nyuma sina umuhimu wa kuirudia) alisema haya naomba unijibu:-

Mkwawa and Rumaliza became blood-brothers, and Rumaliza doubtless gave his ally advice on rebuilding in stone his earth fortress at Kalenga, near Iringa, against the day of German attack. On 30th October 1894 Rumaliza was in the fort with Mkwawa when it was asaulted by the Germans. Mkwawa commited suicide four years later, while Rumaliza escaped to Zanzibar by fishing boat to evade the Germans.


Huu ukaribu wa Rumaliza na Mkwawa ulikuwa wa nini mnaweza kufafanua hadi wa kufa na kufaana?

Labda nikuongezee nondo nyengine Edward Simpson et.al. (2008) katika kitabu chake kinachoitwa Stuggling with History: Islam and Cosmopolitan in Western Indian Ocean anasema:-

The sultan with help of Qadiriyya movement helped islamisation of uhehe and unyamwezi region during the first decade of the twentieth region and after 1880. (1880-1910).

Hapa nauliza je Mkwawa alikufa mwaka gani?

Na pengine hao wazee watuambie after the Germans defeated Wahehe. Moja ya masharti waliyokubaliana baina ya wahehe na wajerumani ni kuwa Wajerumani watatawala wahehe ila wahehe watabakiwa na mambo yao binafsi (Kama anavyoreport Marcia Wright.). Moja ya masuala hayo ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili na UISLAMU (references Marcia Wright, 1968, Local roots in German East Africa, Journal of African History, Cambridge University Press)

Jambo hili lilipingwa sana wamissionary wa kijerumani unaweza kutupatia maelezo ya kwanini walilipinga?
 

Ushausikia msemo wa kiswahili "usituletee visa vya kanisa"? ndio hivyo unatuletea wewe.

haraati = harakati.
 


tumejua kama upo piga kimya basi kuna watu tunafuatilia huu mjadala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…