Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Utajaza mwenyewe:


Mwislamu mmoja safi kabisa wa aina yako wewe na Mzee Mohamed aliniambia "hamkubaliani" na watu kama Mbowe kuvaa hivo. Nakumbuka pia Hijab ya Mama Fatma Kimario wa Igunga ilivoleta tafrani kule.
 
Hotuba za Mwalimu zimejibu mengi alooyaandika Mohamed. Mwalimu amefanyakazi na WAISLAMU wengi tu hadi alipostaafu na wengine walikuwa wapishi na madereva wake ambao waliushikilia uhai wake kwa karibu mno. Waislamu wa aina yako na Mohamed endeleeni kujiumbua kwa kuandika UONGO, CHUKI na FITNA nyingi tu kwa kisingizio cha UISLAMU. Bahati nzuri Mungu wetu sote hana DINI.
 

WC,

Laiti Allah angekujalieni uwezo wa kuandika "paper" au kitabu...
Labda mngekuja na kitu nanyi dunia ikakusomeni.

Ningekuwa nimeumbuka "publishers" wasingegusa kitabu changu wala vyuo visingesomesha kitabu changu wala nisingealikwa katika makongamano.

Nina heshima zangu ndio maana naalikwa kote huko.
Mimi ikitangazwa labda Radio Kheri au Radio Iman kuwa leo tutakuwa na mahojiano na Mohamed Said...

Maskio yote huwa hadhir kunisikiliza.
Alhamdulilah.


Mohamed
 
Mwislamu mmoja safi kabisa wa aina yako wewe na Mzee Mohamed aliniambia "hamkubaliani" na watu kama Mbowe kuvaa hivo. Nakumbuka pia Hijab ya Mama Fatma Kimario wa Igunga ilivoleta tafrani kule.

WC,

Huwa sipendi kumjibia mtu.

Mohamed
 
Hizo ndio Radio zako. Zinzoendana na kitabu chako na fikra zako. Wengi wa walengwa wako pia wanazisikiliza sana radio hizi. "Publishers" wako hawakukufahamu malengo yako kama sisi WATANZANIA tunaoishi na kukulia humu. Naamini mtandao huu wa JF unasomwa duniani. Ulifanya vizuri sana kuleta "thread" hii humu. Mwananchi nao naona waliacha kuchapisha zile makala zako. Mohamed, haukuwatendea haki WAISLAMU waliobaki TANU/CCM hadi leo. Wameendelea kuutumikia mfumoKristo kwa miaka 50 na bado wanao tu.
 

[ Learn wisdom from the pupil of the eye that looks upon all things and yet to its self is blind . ]
 

Barubaru,

Niliwapa Mwananchi makala ya maneno 12, 531 na walichapa makala takriban 20 kutoka humo.
Makala hizi ziliuza gazeti lao kama maandazi ya moto.

Wakati mwingine toleo moja nina makala nne. Niliwapa na picha alizopiga mpiga picha wa kwanza wa TANU Mzee Shebe Awadh. Picha hizi mimi nilikabidhiwa na mwanae. Kwa kweli ni hazina kubwa sana.

Ngoja nikupe kitu.
Studio ya Mzee Shebe ilikuwa Mtaa wa Livingstone mkabala na studio yake akiishi mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha biti Mohamed.

Mzee Shebe akiniita mie rafiki yake.

Nina picha kanipiga nina mwaka mmoja "black and white" ipo katika majlis yangu hadi leo.
Ndiyo maana nasema kinywa kipana mie ya Musoma wapi wapi siyajui lakini haya ya TANU Dar es Salaam.
Ah! Bwana...

Mzee Shebe kanipiga picha mie kwanza kabla hajampiga Nyerere Dogo hilo?
Turudi kwenye makala.

Kwengine naambiwa kuna watu wakisoma walikuwa wanatokwa na machozi...wanawakumbuka watu wao.

Juzi kuna mtu kajaribu kunijibu katika moja ya magazeti...karudia mle mle kwenye historia rasmi ya Nyerere na chama cha starehe, Nyerere na kuandika katiba, Nyerere na hiki na kile...

Watu wanauliza hivi Nyerere kaja Dar es Salaam na fedha za kiasi gani awe na ofisi na hela za kuendesha chama, mgeni mno awapate watu wa kumuunga mkono nk.

Hajui kuwa TANU pale kulikuwana Abdu na mdogo wake Ali, Dossa, Rupia, Mashado Plantan, Schneider Plantan, Iddi Faiz, Idd Tosiri, Masha Bilali, Rashid Ali Meli, Said Chamwenyewe watu wengi tu bila ya kuwataja hawa hiyo siyo historia ya TANU itakuwa kitu kingine.

Basi huyu bwana anachekesha tu watu wanamsoma wanajichekea.

Mohamed
 

WC,

Labda hujui.

Miezi michache iliyopita nilikuwa Washington DC na nilifanya mahojiano na VOA Swahili Service.

Huenda hujui.

Mwananchi walichapa makala zote.

Mohamed
 
Gazeti la Mwananchi lina soko lake zuri tu kwa sasa Tanzania hii. Sio makala zako zilizosababisha kununuliwa. Na wewe ulilipekea makala hizo ukilijua hilo. Ungepeleka Annur ungeula wa chuya. Nyerere utake usitake ndiye Rais wa Kwanza wa TANU ambacho ndicho chama kilichodai uhuru wa Tanganyika.
Mwalimu angeandika HISTORIA ya kudai UHURU wa Nchi hii wala asingewasahau wazee wako hawa kama ambavyo hakuwasahau kwenye hotuba zake nyingi tu. Historia RASMI ya NYERERE haipo. Unaongopa. Unamsingizia makusudi tu kuhalalisha UDINI wako. Endelea kuchochea tu kwa kuwa wewe umeshakula chumvi nyingi ya kutosha. Kuijenga NCHI isiyo na DINI haikuwa kazi ndogo hasa pale mwanzoni kama simulizi zako hizi zinavyojidhihirisha. Tumevuka kizingiti hicho, tunasonga mbele.
Kama dhulma ni akina Jakaya kuwa Marais nchi hii acha tuwe nayo dhulma hii.
 

WC,

Huenda na hili hujui.

Mwananchi walikuwa wakitafuta mtu mwenye kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika ndiyo wakaja kwangu.
Sikujipeleka.

Kuhusu Nyerere kuwa rais wa kwanza nani analipinga hilo?
Ugomvi wangu mie upo katika historia ya TANU pale siwezi kumpa sifa isiyomstahiki.

Nyerere alikuwa mwepesi wa kusahau.
Alimsahau Sharif Attas TANU office baada ya uhuru.

Nyerere alisahau Abdu Sykes alikuwa na cheo gani katika TAA hiyo mie namsikia mwenyewe mubashar "live" siku anaaga wazee wa TANU.

Wazee wakawa wanatazamana haya mambo vipi? Nyerere kasahau Abdu alikuwa na cheo gani wakati Abdu ndiye kamleta kwetu akiwa rais wa TAA 1952!

Kapanda basi kasahau kituo alichopandia.

Itafute ile hotuba uisikie.

Siku anatoa medali viwanja vya Ikulu Dossa kamsahau kaja kumpa peke yake baadae.
Au kisa hiki hukijui?

Mtemvu akanambia vipi utampa Dossa medali uwaache wenzake?

Mohamed
 
WC,

Labda hujui.

Miezi michache iliyopita nilikuwa Washington DC na nilifanya mahojiano na VOA Swahili Service.

Huenda hujui.

Mwananchi walichapa makala zote.

Mohamed

Haya mambo niliyoyafafanua mbona mko Kimyaaa!!

 

WC,

Inawezekana na hili hulijui.

Mwananchi walinitafuta niwaandikie makala zile.
Sikujipeleka.

Sina ugomvi kuwa Nyerere ni rais wa kwanza.
Ila siwezi kumpa sifa asiyostahili.

TANU si fikra yake.
TANU bila Abdulwahid Sykes ni historia nyingine hiyo si ya TANU.

Haya huyajui.
Nyerere alimsahau Shariff Attas.

Kama humjui Shariff Attas alikuwa nani niulize ntakwambia.

Nyerere alimsahau Dossa wakati anatoa medali Viwanja vya Ikulu ilibidi amwite Dossa peke yake na kumvisha medali.
Hili ulikuwa unalijua?

Nyerere Diamond Jubilee Hall siku anaaga alisahau Abdu Sykes alikuwa na cheo gani TAA (sikiliza hotuba yake kwa wazee wa Dar es Salaam).
Wazee wakawa wamepigwa na butwaa...mh! Nyerere kasahau cheo cha Abdu! Mtu aliyempokea Dar es Salaam na kumjulisha kwao!

Hili hulijui...
Mwenyekiti wa Kamati ya Medali alimuuliza Nyerere vipi fulani na fulani hawa si ndiyo walikuwa miamba na wafadhili wakuu vipi wa TANU na hasa huyu fulani si ndiye aliyekutembeza mji mzima kwa wazee wakuunge mkono?

Mohamed
 

Lakini pia nimekuwa nakueleza uongo wowote ukiachwa kwa muda mrefu basi unageuka kuwa kweli.
Barubaru,
Sasa nimeelewa kwa nini umekazana kueneza uwongo kwenye hii minakasha.
 
What do you mean anakufahamu by reputation. Nilishakwambia gazeti la Africa Events, kama kweli lilikusanywa na kuchomwa lilikusanywa wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi. Sasa hili unalihusishaje na Nyerere? Ulishaenda Butiama wewe? Nimeshapita pale kwenye museum yake mbona hicho kitabu sijakiona? Usijivimbishe kichwa isivyostahili.
 

Lakini pia nimekuwa nakueleza uongo wowote ukiachwa kwa muda mrefu basi unageuka kuwa kweli.
Barubaru,
Sasa nimeelewa kwa nini umekazana kueneza uwongo kwenye hii minakasha.

Jasusi,

Dawa ya hawa waongo ni kuja na ukweli ukauweka uwanjani.
Utakuwa ushawakomesha na uongo wao.

Lete ukweli tukate mzizi wa fitna.

Mohamed
 

Hili hulijui...
Mwenyekiti wa Kamati ya Medali alimuuliza Nyerere vipi fulani na fulani hawa si ndiyo walikuwa miamba na wafadhili wakuu vipi wa TANU na hasa huyu fulani si ndiye aliyekutembeza mji mzima kwa wazee wakuunge mkono?

Mohamed

Hizi ndio porojo zenyewe sasa huyo Mwenyekiti wa Kamati naye si marehemu?
 

Jasusi,

Mie wa kijivimbisha kichwa...
Kwa kisa gani?

Kitabu alikuwanacho na aliyempa namfahamu.

We nikikuambia nakala nilizo "autograph" (nakala ya Kiingereza) na kuwapa "watu" uso kwa macho hutothubutu kunambia "najivimbisha kichwa."

Mmoja katika "watu" alinitunuku kalamu ya dhahabu...pure gold...Waterman.

Mohamed
 
Sheikh Mohamed,

..hizi tuhuma zote ulizoweka ulizipeleka kwa wahusika wazijibu kabla hujachapisha kitabu chako?

..kama ulifanya hivyo wahusika walikupa majibu gani?

..kama hukuwasiliana na wahusika unaweza kueleza kwanini hukufanya hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…