Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Karani wa Wakala wa meli, "Mohamed Said" Kiingereza ni zero. Waandishi wa kweli wa vitabu na "papers' zake kwa lugha ya Kiingereza ni Maswahiba na Waswahilina wenzake wa gazeti la "Africa Events" waliopo London. Hata kile kitabu cha Historia cha darasa la 4 anachojidai kuandika, ukweli ni kwamba kimeandikwa na hao Wapemba na Waunguja who were behind the long defunct "Africa Events" magazine.

Dalili ya kushindwa kwa hoja.
 
Niliwahi kusema hapo nyuma uwongo ukipewa nafasi ya kurudiwa rudiwa lazima tu wapo watu watanasa na hasa wale wanaoongozwa kwa hisia na mbaya kuliko zote ni hisia za dini. Lakini tatizo lingine ni kuwa hata muongo mwenyewe anaanza kuuamini uwongo alioutunga na kuuona kama ukweli kwa sababu tu wako watu ambao watameza chochote kile mradi dini yao imeguswa. Anayoyahubiri Mohamed Said siyo mageni masikioni mwa wengi wetu kama anavyodhani, wengine tuliyasikia hata kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Ni kweli pia mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na Mohamed Said anayedai kuwa alipata malezi mema hatuna haja tena ya kujiuliza aina ya malezi aliyoyapata na anayoyaongelea. Lakini historia ina tabia moja ya kujirudia na ninaamini kwa jinsi ile ile Waislaam wema walivyowakataa wachochezi waliotaka kutuvuruga mwaka 1958, wengine wao wakiwa Wazee wa Mohamed Said ndivyo hivyo Waislaam wema wa leo watamkataa Mohamed Said na uchochezi wake kama tunavyoshuhudia humu kutoka kwa Mkandara na Nguruvi3.

Atawapata watu kama Barubaru, watu ambao kisirani chao wanashindwa hata kukificha kwani pamoja na kuukana uraia wa Tanzania bado wanafikiri utawala wa Kisultani utarejea. Nina imani kubwa na Waislaam wema ambao ninashiriki nao kila siku kwa shughuli mbali mbali na hawasiti kuwalaani hawa wachochezi ambao ni vigumu kuelezea hata wanavyoruhusiwa kupanda hizi mbegu za chuki. Mohamed Said kama anavyojisifu, atatembea sehemu nyingi ndani na nje ya nchi akieneza uwongo, lakini kwa watu makini ategemee kukwaa kisiki.

Mimi Mag3 sina haja ya kujibu hoja anazozitoa Mohamed Said kwani naamini kufanya hivyo ni kumpandisha daraja kama mwandishi wa historia na mtafiti, daraja ambalo kama wazee wake, atabaki akiiota tu kwani sifa hiyo kaipoteza kwa kusimulia uwongo. Toka miaka ya mwanzoni baada ya uhuru nimeishi jijini Dar es Salaam, najua nilivyoikuta na ilivyokuwa miaka kumi baadaye na mtu hanidanganyi hata kama alizaliwa Gerezani. Mohamed Said sasa yabidi ajitazame upya na kujiuliza, anataka kulipeleka taifa wapi na hizi porojo zake.

Angalia unavyojicontradict mwenyewe. Hivi nani ataamini maneno unayoyasema? Unasema huna haja ya kujibu hoja za MS; wakati huo huo umeanzisha hii thread just kujibu hoja zake. WOW!!
 
Bw. Said, itikadi ya chuki (an ideology of hate) itashindwa tu; haijawahi kufanikiwa mahali popote duniani. Iwe inatokana na ubaguzi wa rangi, udini, ukabila au hadhi. Watu wenye chuki hiyo Nyerere alisema hawana nafasi katika ulimwengu huu wa leo. Chuki unayojitahidi kuipandikiza ndani ya Watanzania itafunuliwa, itakataliwa na nguvu ya upendo na umoja itashinda. Kwani ni katika tofauti zetu ndio umoja hujengwa. Wamarekani wanasema "From Many, One - E pluribus unum" lakini mimi nasema "From differences, Unity - De differentiis unitatem" Sasa mzee nakuambia ukianzia kutoka tofauti na kuelekea umoja utaona jinsi ambavyo Watanzania wangeona uzuri wahoja zako. Bahati mbaya umechagua kutoka kwenye umoja kwenda kwenye utengano wa kidini. Hiki ndicho kinakataliwa na kitaendelea kukataliwa.

Inaonekana bado unashindwa/mnashindwa kuelewa points za mjadala huu. Let's focus on the topic.
 
JokaKuu;2801686]Sheikh Mohamed,
..hizi tuhuma zote ulizoweka ulizipeleka kwa wahusika wazijibu kabla hujachapisha kitabu chako?
..kama ulifanya hivyo wahusika walikupa majibu gani?
..kama hukuwasiliana na wahusika unaweza kueleza kwanini hukufanya hivyo?
Mohamed Said;2801766]JK,
Hilo swali lako halikukaa vizuri.Orodhesha hizo "tuhuma" na hao watuhumiwa kwanza.
Mengine yatafuatia.Mohamed
Mohamed majibu ya namna hii ayalingani na mtu anayetoa mhadhara ulaya na marekani. Kusema sijui au hapana hakumaanishi chochote zaidi ya kujenga ueledi.

Labda nikukumbushe tuhuma, nimeangalia kabrasha langu zipo 45 kubwa na 32 madogo. Kwa kumsaidia Joka kuu na sisi sote naorodhesha zifuatazo na utupe majibu.

1. Uliwahi kumhoji marhumu Kawawa jinsi Nyerere alivyotumia udini kuwaondoa waislam katika uongozi wa TANU na serikali.

2. Umewahi kumuuliza mzee Mwinyi kuhusu tuhuma za wizi wa funguo za madroo alizoongea na Malima wakati huo akiwa Ikulu.

3. Umeshawahi kumhoji mama Maria kuhusu kitoweo alichokuwa anapelekewa na mzee Kiyate, yeye ana kauli gani kwa jambo hili jema.

4. Umewahi kumhoji Salim Ahmed Salim au Butiku kuhusu kukataa kwao kupokea picha za wazee wako.

5. Umewahi kumhoji Tewa kwanini alikubali kuwa balozi nchini China huku akijua kuwa zilikuwa njama za kudhoofisha EAMWS

6.Umewahi kumhoji padre Sivlon kuhusu aliyoandika katika kitabu chake na anasemaje katika kuyathibitisha.

7. Uliwahi kumhoji Platan kuhusu ugomvi wa AMNUT na nini kilikuwa chanzo halisi(walikuwa wanatofautiana nini)

8. Umewahi kuuliza wizara ya elimu namba za mitihani zilianza kutumika lini

9. Umewahi kumhoji mkuu au makamu mkuu wa UDSM kwanini ma lecturer wakikristo hawataki kitabu chako kitumike

10. Umeahi kumhoji Rupia kuhusu tuhuma za Nyerere kuwa mdini na alikuwa na maoni gani

11. Uliwahi kumhoji marhum Bibi Titi Mohamed kwanini aliwekwa ndani, mwaka gani na aliwekwa pamoja na akina nani

12. Uliwahi kumhoji Munaka Bhoke juu ya kiasi gani alikusanya ili kujenga chuo kikuu cha Dar es Salaam

13. Uliwahi kumhoji sheikh Himid Jongo kwanini baada ya kadhia ya mwembechai alikabidhiwa msikiti na serikali ile ile unayoituhumu

14. Umeahi kumhoji Adam Nasibu kuhusu ushiriki wake katika kuanzisha BAKWATA

Ukishayajibu haya tunaweza kuendelea kidogo kidogo.

Ukumbi wako
 
Tate naneee.. watu mnakumbukumbu!!
 
Inaonekana bado unashindwa/mnashindwa kuelewa points za mjadala huu. Let's focus on the topic.

MM,

Chuki kwa kuwaadhimisha wazee wangu?
Najua historia hii yangu imekuchoma lakini huo ndiyo ukweli wa historia ya TANU.

Mohamed
 
MM,

Kajifunze mbinu na akida (principles) za utafiti ndipo urudi hapa tuhojiane.
Hili nishakueleza mara nyingi.

Ndiyo nasema wewe si wa kunihoji mie katika "academics."
Hujafika makamo hayo

Mohamed

kama ulichofanya unaweza kudai kimefuata kanuni za utafiti basi neno kanuni za utafiti limepoteza maana. Hukufuata kanuni hata moja.
 
MM,

Chuki kwa kuwaadhimisha wazee wangu?
Najua historia hii yangu imekuchoma lakini huo ndiyo ukweli wa historia ya TANU.

Mohamed

Wala haichomi kwani ingekuwa na ukweli labda ingechoma.

a. Ni historia yako - siyo historia ya Tanganyika, umekaa ukaitunga na kuipendezesha nakuiuza kwa wenye kuiamini.
b. Siyo historia ya 'ukweli' ya TANU. NI masimulizi tu ya wazee ambao walikuwa wamemchukia Nyerere kwa sababu ya Ukatoliki wake tangu miaka ya mwanzo ya 1950s na ambao hadi leo bado wamekwama kwenye miaka hiyo. Ni masimulizi mazuri na yanafurahisha lakini siyo ya kuaminika.
 
Mohamed majibu ya namna hii ayalingani na mtu anayetoa mhadhara ulaya na marekani. Kusema sijui au hapana hakumaanishi chochote zaidi ya kujenga ueledi.

Labda nikukumbushe tuhuma, nimeangalia kabrasha langu zipo 45 kubwa na 32 madogo. Kwa kumsaidia Joka kuu na sisi sote naorodhesha zifuatazo na utupe majibu.

1. Uliwahi kumhoji marhumu Kawawa jinsi Nyerere alivyotumia udini kuwaondoa waislam katika uongozi wa TANU na serikali.

2. Umewahi kumuuliza mzee Mwinyi kuhusu tuhuma za wizi wa funguo za madroo alizoongea na Malima wakati huo akiwa Ikulu.

3. Umeshawahi kumhoji mama Maria kuhusu kitoweo alichokuwa anapelekewa na mzee Kiyate, yeye ana kauli gani kwa jambo hili jema.

4. Umewahi kumhoji Salim Ahmed Salim au Butiku kuhusu kukataa kwao kupokea picha za wazee wako.

5. Umewahi kumhoji Tewa kwanini alikubali kuwa balozi nchini China huku akijua kuwa zilikuwa njama za kudhoofisha EAMWS

6.Umewahi kumhoji padre Sivlon kuhusu aliyoandika katika kitabu chake na anasemaje katika kuyathibitisha.

7. Uliwahi kumhoji Platan kuhusu ugomvi wa AMNUT na nini kilikuwa chanzo halisi(walikuwa wanatofautiana nini)

8. Umewahi kuuliza wizara ya elimu namba za mitihani zilianza kutumika lini

9. Umewahi kumhoji mkuu au makamu mkuu wa UDSM kwanini ma lecturer wakikristo hawataki kitabu chako kitumike

10. Umeahi kumhoji Rupia kuhusu tuhuma za Nyerere kuwa mdini na alikuwa na maoni gani

11. Uliwahi kumhoji marhum Bibi Titi Mohamed kwanini aliwekwa ndani, mwaka gani na aliwekwa pamoja na akina nani

12. Uliwahi kumhoji Munaka Bhoke juu ya kiasi gani alikusanya ili kujenga chuo kikuu cha Dar es Salaam

13. Uliwahi kumhoji sheikh Himid Jongo kwanini baada ya kadhia ya mwembechai alikabidhiwa msikiti na serikali ile ile unayoituhumu

14. Umeahi kumhoji Adam Nasibu kuhusu ushiriki wake katika kuanzisha BAKWATA

Ukishayajibu haya tunaweza kuendelea kidogo kidogo.

Ukumbi wako

Nguruvi3,

Ukumbi ni wenu nyie.
Mimi nishaingia kumbi hata hesabu zake sizijui.

Sasa hapo penye maswali hayo yenu ndipo pa kuanzia mkaandika kitabu.
Nikuelezeni hili mara ngapi ndugu zangu?

Mimi nina nina "papers" makala, kitabu nyinyi mna maneno.
Dunia ya kisomi haithamini maneno.

Ndiyo nakuelezeni bado hamjafikia makamo ya kusimama na mimi katika anga za kisomi.
Andikeni kwanza.

Mohamed
 
Wala haichomi kwani ingekuwa na ukweli labda ingechoma.

a. Ni historia yako - siyo historia ya Tanganyika, umekaa ukaitunga na kuipendezesha nakuiuza kwa wenye kuiamini.
b. Siyo historia ya 'ukweli' ya TANU. NI masimulizi tu ya wazee ambao walikuwa wamemchukia Nyerere kwa sababu ya Ukatoliki wake tangu miaka ya mwanzo ya 1950s na ambao hadi leo bado wamekwama kwenye miaka hiyo. Ni masimulizi mazuri na yanafurahisha lakini siyo ya kuaminika.

MM,

Mngekuwa haikuchomeni msigelikuwa mnatukana.
Historia ya kweli iko wapi?

Hii yangu ndiyo inayosomeshwa kote duniani.
Nenda chuo chochote Marekani na Ulaya utakikuta kitabu changu katika catalogue ya "Islam and Politics."

Hili hulijui.

Nilimesomesha vilevile..."from the horse's mouth" wanaita.

Mohamed
 
Angalia unavyojicontradict mwenyewe. Hivi nani ataamini maneno unayoyasema? Unasema huna haja ya kujibu hoja za MS; wakati huo huo umeanzisha hii thread just kujibu hoja zake. WOW!!

Mr Right.

Huyu kadanganyika na jina langu akadhani mie "easy meat" kama wengi walivyowahi kufanya mmoja ni yule ndugu yake alonita ofisini anitishe kwa lugha ya Kiingereza.

Si umeona humu baada ya kushindwa yote wanasema wanataka kunisikia nikisema Kiingereza. Kwani nikisema Kiswahili ndiyo kazi yangu itakuwa haina maana?

Huyu hana "intellect" ya kusimama na mimi.

Anachokijua kwa uhakika na mimi namsifia ni kutoa matusi.
Hana cha zaidi.

Mohamed
 
Ogah, Karani wa Wakala wa Meli, "Mohamed Said" anapenda afahamike kama "independent scholar", kwa hiyo usishangae viwango vya "tafiti" zake zipo somewhat off and way below acceptable and respectable mainstream scholarly or academic standards, and as far as I'm concerned appear to be more in line with those of a charlatan.

Ndjabu,

Angalau sasa hutukani.
Hata maadui zangu wasonipenda hawajasema kuwa naandikiwa.

Sie malezi yetu ubinadamu haupimwi kwa cheo.
Sasa hata ukiniita mie topasi kwangu halijawa tusi.

Hata ukiligeuza jina langu kuwa "Mwamedi" inanidhirishia wewe ni mtu wa malezi yapi hali kadhalika unapotukana.

Tena nakuambia kwa kauli yangu mwenyewe mimi sina cheo chochote ni mtu tu Mswahili niliyezaliwa Dar es Salaam na kukulia Dar es Salaam basi.

Sasa usipate tabu na hiyo "karani" hiyo ndiyo kazi yangu inayonipa riziki yangu halali.

Mohamed
 
the fact ni kwamba hiyo statement hapo juu haina UKWELI......period

Brother MS anaweza kuwa mtafiti sawa.......lakini kwa hizi hadithi za wazee wake huhitaji.......kuambiwa au kufanya utafiti kuona uongo na uchochezi wake........labda kama maana ya utafiti ya Brother MS au yako ni tofauti na tafiti ambazo zinaeleweka kitaaluma......

Ogah,

Mlivyokuwa na kibri cha kupindukia...
Kuna mtu hapa kanishauri nimpe kitabu changu Prof. mmoja na akanielekeza alipo ati akiweke sawa.

Akili yake inamzuga inamwambia Mohamed hawezi...

Mohamed
 
Nguruvi3,Ukumbi ni wenu nyie.
Mimi nishaingia kumbi hata hesabu zake sizijui.Sasa hapo penye maswali hayo yenu ndipo pa kuanzia mkaandika kitabu.
Nikuelezeni hili mara ngapi ndugu zangu?Mimi nina nina "papers" makala, kitabu nyinyi mna maneno.
Dunia ya kisomi haithamini maneno.Ndiyo nakuelezeni bado hamjafikia makamo ya kusimama na mimi katika anga za kisomi.
Andikeni kwanza.Mohamed
Mohamed, umemuuliza swali Joka kuu aorodheshe tuhuma, nasi sote kwa vile hili ni jamvi letu tumefanya hivyo.Tunategemea ujibu kama tunavyokujibu unapouliza, sasa haya mengine ya wewe una paper, umekwenda wapi na kwanini yanatoka wapi?

Unaposema tuandike vitabu sijui una maana kuwa hata hao unaowapa mihadhara huko ulaya na marekani wakikuhoji nao pia unawajibu hivyo!
Na kama ni hivyo kwanini unachagua maswali ya kujibu na usikae kimya kitu.

Hata hivyo, vitabu vikiandikwa kama cha Dr Maggoti unavipiga kejeli. Kejeli ile ile usioweza kufanya tofauti. Umeuliza kwanini Dr Maggoti hakuwahi kumhoji Kawawa hadi mauti yanamfika! Ndiyo maana swali langu la kwanza likawa hilo kwa vile wewe huenda ulimhoji.

Hoja ni hizo hapo, jibu na kama huna majibu sema huna majibu si dhambi au dhalili, kukimbia kimbia na kujibu hoja unazotaka ni dalili ya wazi kuwa huna utafiti, hujui umeandika nini na hujui unatetea nini. In short kama walivyosema wengine ni porojo na propaganda, kwa mazuzu ni elimu kwa wajanja ni hekaya, ngano na tamthilia.
Anayeamini kuwa umefanya utafiti aende akamuulize mwalimu wake wa darasa la kwanza ilikuwaje akawmwezesha kuandika jina lake.

Tutaendelea kukupiga shule hadi uelewe kama ulivyoanza kuelewa kuwa Rupia ni sehemu ya wazee wako(umetaja japo kwa soni).
Maswali kama hayo hapo juu huwezi kuulizwa cambridge kwasababu wananchi ndio wenye nchi. Hapa ni Cambridge huna sababu ya kusafiri kila siku, lete mada zako zinyumbulishwe neno hadi neno ili utakapoandika tena ujue unaandika nini na kwa akina nani.

Jibu hoja Mohamed
 
Huenda hujui,

Mimi kukupa wewe kujibu "papers" zangu tena za miaka na miaka ni mie kujidhalilisha.
Wewe ujibu kama nani?

Unafahamika katika dunia ya usomi?

Wewe hujafikia makamo ya kusimama na mimi.
Mimi siko hapa kujibishana na wewe kwa kitu usikchokijua.

Mimi hapa ni Maalim.
Andikeni kwanza kisha rudini hapa tujadili.

Mohamed
 
Nguruvi3,Huenda hujui,
Mimi kukupa wewe kujibu "papers" zangu tena za miaka na miaka ni mie kujidhalilisha.
Wewe ujibu kama nani?Unafahamika katika dunia ya usomi?Wewe hujafikia makamo ya kusimama na mimi.
Mimi siko hapa kujibishana na wewe kwa kitu usikchokijua.Mimi hapa ni Maalim.Andikeni kwanza kisha rudini hapa tujadili.
Mohamed
Jibu hoja Mohamed watu hawana interest na tambo wala majigambo, usomi wako unatakiwa ujidhihiri si kukimbia maswali na kujificha katika kichaka cha andika vitabu, hilo ni jibu lisilo na usomi hata kidogo na sasa tutalitumia JF kama kibwagizo.

Tumekupiga shule umekiri mambo 13 mazito. Nakutajia machache
Umekiri kuwa mgogoro wa Mwembechai hakuna mali ya mkristo iliyohujumiwa ikiwa ni pamoja na makanisa
Umekiri kuwa Rupia ni mmoja wa wazee wako hata kama si mwaislam kama unavyotaka iwe.
Umekiri kuwa hujafanya utafiti kuhusu TANU, vinginevyo usingeshindwa kujua nani walikuwepo kamati kuu
Umekiri kuwa Platan na Sykes walikuwa mamluki waliokuja kumsaidia mkoloni na kushambulia waislam na si wazalendo kama unavyodai
n.k

Endelea kuwajibu watu wa gogo vivu, JF is something different my brother. Sasa ulimwengu unajua jinsi gani tamthilia zako zilivyo na tenzi murua.
Mwananchi anachpaisha tena makala zako?

Jibu hoja na maswali, majibu mepesi ya majigambo yasiyo na kitu yanaondoa hata kale ka credibility kadogo kaliko baki.
 
Jibu hoja na maswali, majibu mepesi ya majigambo yasiyo na kitu yanaondoa hata kale ka credibility kadogo kaliko baki.

Mzee Said pamoja na ujuzi wote wa maneno na historia kuna kitu kimoja kiko wazi kuhusiana na hizi 'kazi' zake - amezikariri. Amekariri masimulizi ya utotoni na hata alivyozidi kupata ufahamu zaidi ndivyo hivyo hivyo alivyozidi kuzikariri. Hivyo anachotuelezea ni kile ambacho amekariri kwa kusimuliwa au kujisomea n.k Na hivyo anakirudia na ukiangalia kwa juu juu unaweza kweli kuwa impressed. Tatizo linakuja nipale unapozama chini na kuanza kufuatilia 'kujua'. Kuna tofauti kubwa kati ya kujua na kukariri.

Wapo wanafunzi ambao wanakaririshwa Table na hivyo ukimuambia akuambie table ya 12 anaweza akaiimba yote au 'tebo' ya sita akaiimba yote. Lakini mwanafunzi huyo anaweza asijue kuzidisha kwani ukianzia na table ya 13 au kwenda juu atapata shida au ukianza kuchanganya table na kujumlisha anaweza kushindwa. Lakini mwenye kujua kuzidisha anaweza kujua namna ya kuzidisha namba mbalimbali kwa urahisi kabisa na kwa haraka kuliko hata anayetumia kalamu. Kwa mfano, mtu anajua namba yoyote ukizidisha kwa namba yenye 10, 100, 1000 n.k basi unaongeza tu hiyo idadi ya sifuri na jibu linapatikana.

Kwenye historia au utafiti wa aina kama hii ni hivyo hivyo. Mtu anaweza kukariri matukio muhimu au watu muhimu walifanya nini na ni kile tu ambacho amekaririshwa ndicho pekee anaamini anakijua. Ukijaribu kumtoa tu kwenye kukariri anachanganyikiwa kabisa. Ni sawa na kumuweka swala mbele ya taa ya gari usiku akapigwa macho!

Maswali mengi anayoulizwa Bw. Said na watu wengi tangu kuanza kwa mjadala huu yanahitaji kujua siyo kukariri tu. Kwa mfano, Bw. Said anaweza kusema kuwa "tofauti kati ya Nyerere na Waislamu imeanza baada ya ile congress ya 1963". Sasa hicho ni cha kukariri. Ukitaka kumtoa jaribu kumuonesha kuwa walikuwepo Waislamu kabla ambao walikuwa wanamchukia Nyerere tangu siku ya kwanza ametambulishwa kwao na walimchukia si kwa sababu aliwadhulumu Wailslamu au aliwatendea jambo lolote baya - bali kwa sababu ya Ukatoliki wake. Ukimleta Said kwa hilo anapata shida kwa sababu ni kama kumlazimisha kujua.

Utaona maswali yote anayulizwa majibu yake ni ya kukariri.

SWALI: Kwanini kwa miaka karibu ishirini ambayo ulikuwa unafanyia hii historia 'yako' utafiti hukupata nafasi hata ya kuandika barua kwa Mwalimu Nyerere?

JIBU: Prof. Haroub Othman alishangazwa sana akamwendea Nyerere...

SWALI: Kwanini hadi leo hujawahi kumuuliza au hata kujaribu kwenda kuonana na Mama Maria Nyerere na kumhoji kuhusu Sykes na mtazamo wa Nyerere kuhusu Waislamu wakati akiwa madarakani?

JIBU: Maria Nyerere alikuwa anafahamiana sana na Binti Sudi, Binti Zubeda ambaye alikuwa akiishi mkabala na kwa Bw. Selemani ambaye nje ya nyumba yake tulikuwa tunacheza kombolela!

SWALI: Kwanini kama kweli ulikuwa unataka kuandika historia ya mashujaa 'waliosahauliwa' katika historia hukuwagusa wale ambao hawakuwa Waislamu au wale waliokuwa nje ya Dar?

JIBU: Kama na nyie mna wazee wenu nendeni mkaandike habari zao, miye nimeandika habari za wazee wangu na hiyo ndiyo historia yote ya TAnganyika!

SWALI: Je ni mahali gani ambapo wazee walioshiriki kupigania uhuru walipofanya hivyo kwa sababu ya Uislamu wao na kuwa waliongozwa na imani yao na siyo uzalendo wao kwa Tanganyika na kutaka uhuru uwanufaishe watu wote?

JIBU: Katika kampeni zote zilisomwa dua na Nyerere alikuwa anainamisha kichwa chini ili isomwe Al Fatha na wakati mwingine zilitolewa dua hadi wakatoka machozi!

Sasa mtu ambaye is untrained anaweza kuamini kabisa kuwa Bw. Said anajibu maswali lakini for any objective and trained mind anaweza kuona kuwa maswali hawezi kujibu kwa sababu yatamuondoa kwenye kukariri. Matokeo yake ni kuwa mtazungushana hapo hapo kwenye kukariri hadi mchoke kwa sababu alichokariri yeye ndio ukweli na chochote ambacho kitamfanya afikirie nje ya huko kukariri kutaaribu kabisa. Na ukifikiria sana utaona ni kweli. Wakati mwingine kujiuliza kuhusu kule unachoamini kunaweza kabisa kukusababisha ubadilishe mtazamo wako na kupindua kabisa maisha yako.

Bw. Said akitaka kujua anaweza lakini kujua kuna gharama - na gharama yake ni kuwa kwa kadiri mtu anavyopata ukweli ndivyo anavyoitwa kuufuata na wakati mwingine ukweli ni mgumu sana kuukubali. Ni mtu yule ambaye ana ujasiri wa dhamira yake ndiye pekee anaweza akutafuta ukweli, akauchunguzi na kuuhoji na akiona umethibitika atakuwa tayari kuhama kutoka kuliko alikokuweko.

Ndiyo Yesu alisema mojawapo ya misemo ya kifalsafa ya hali ya juu - 'MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU" Yoh. 8:32 Ukweli unafungua, unawapa watu sababu ya matumaini, unatuliza moyo na unamuinua mtu kutoka katika hali ya kutokujua. UKWELI wa historia yetu haupatikani katika kitabu cha Bw. Said nayeyote ambaye anasoma ataona kuwa hafunguki! Ila anajikuta anasukumizwa kwenye kifungo cha hatari sana kwenye gereza ambalo nje limeandikwa 'UDINI'. Na huyo anaweza kuanza kujikuta anatumikia hii itikadi ya chuki na atafunguliwa tu pale ambapo yeye mwenyewe atakuwa na ujasiri wa kuhoji anachoambiwa, kuuliza maswali sahihi na akiona majibu hayaji kuunda nadharia za kuelezea kwanini majibu hayaji.

Maswali ambayo yameulizwa ambayo karibu yanafikia 50 sasa hayawezi kujibiwa na Bw. Said kwa sababu yanahusiana na kutafuta ukweli. Kwa vile lengo lake siyo kutafuta ukweli bali kukaririsha watu kile alichosikia basi ni vigumu kabisa kumfanya akubali kuwa kuna vitu ambavyo kwa kweli angefanya jitihada kuvijua zaidi. Lakini itakuwaje kama angefanya jitihada hiyo na baadaye kujulishwa vitu ambavyo vingevunja vunja vile alivyokariri?
 
Back
Top Bottom