Huhitaji yangu lakini ya umma unaitaka sana ndiyo maana upo hapa ukieneza propaganda. Kwa jinsi masimulizi yako yanavyochambuliwa hapa hata mjinga aliyekuwa anapiga makofi sasa atajiuliza akupigie au la. Muhimu ni sisi kukupa ukweli na ukaukubali bila kupenda, hiyo ndiyo Cambridge si kule watu wasikojua maneromango ni wapi.
Fair enough, sasa tuangalie umezitumiaje hizo nyaraka kuandika historia yako Hapo juu umesema Tewa alikuachia hazina, sasa hili neno 'inasemekana' unalipata wapi wakati wewe una hazina? Tewa kafariki, kuna shida gani ukimnukuu hadi utumie neno inasemekana. Ikifika hapo wale mazuzu wanodhani umefanya utafiti wajiulize upi huo wa kusemekana.
Pili, tumeona Tewa alikwenda kuwa balozi bila polisi au jeshi, kwahiyari yake. Kama nia yake ilikuwa kuwaunganisha waislam na alignundua njama hizo,je kwenda china sio usaliti kwa uislam na waislam! yaani tumbo lake lilikuwa bora kuliko masilahi ya umma wa waislam. Huyu ni shujaa au msaliti. Think about that MohamedKwahiyo unatueleza kuwa elimu sasa ndiyo iliyokuwa inaingia uzaramo, lakini unataraji kuwa ingewezekana kupata katibu mkuu au waziri mzaramo.white elephant! Tunazidi kuona kurasa zilivyojaa neno inasemekana kutoka kwa mtafiti. Huko nyuma uliwahi kusema waislam wanachagua kiongozi, akaja mtu mmoja na kukushawishi kuwa waislam hawachagui viongozi na ukayumba yumba na kukubaliana naye. Hapa unatupa ushahidi kuwa unakubaliana na hoja ya kuchagua viongozi. Kuyumba kwako kunatokana na kujibu maswali ya habari uliyosimuliwa na kukariri, hivi bado kuna mtu anaamini kulikuwa na utafiti hapa!!!! Mohamed, huyu Tewa aliyewaacha waislam na kwenda kuwa balozi ana Taqwa? wapi alipata moral authority ya kuelezea nani awe kiongozi wakati yeye ni msaliti.Kwanza ni uongo unapomtaja Kawawa kama Mzanzibar, pili hukuwahi kutaja baraza la mawaziri mwaka 1962. Tatu umeficha ukweli kuwa kawawa hakuwa waziri tu alikuwa na cheo kikubwa uischotaka kukieleza kwasababu kitaua hoja yako.
Kibaya zaidi unatumia neno serikali nzima halafu unaweka sehemu ya serikali, hakuna kitu kama hicho Mohamed. Unaposema nzima ina maana yote. Kiswahili kinaleta taabu kwasababu ya kutaka kupindisha ukweli.
Mohamed ili kujenga hoja yake ya chuki sasa anawagawa waislam, kuwa wale waliokuwa baraza la mawaziri ni Wazanzibar kutoka kule kule alikopelekwa sheikh Amir. Hakuwahi kumhoji Jumbe au Maswanya nini kilitokea. Anataka tuamini 'inasemekana'.
Tuendelee kuiangalia simulizi hii katika darubini, hatuandiki kitabu hadi hiki kitakapochambulia herufi zote. umma unazidi kuelewa.
Mwananchi wanachapisha makala zako tena!