Historia kukumbukwa nijambo la tunu, historia kupotoshwa hutoke pia, historia kuandikwa ili watu na matendo yao yakishujaa au uoga yakumbukwe ni jambo zuri mno. Tafsiri na uchambuzi wa historia ni jambo muafaka japo kuwa hapo ndipo mizozo na mitafaruku hujikita. Historia ya uhuru wa Tanganyika ni ndefu na ina watu wengi sana waliochangia, walio hujumu, walioimarisha walio boresha na wanaoindeleza. Wapo ambao michango yao haijaandikwa popote pale kana kwamba hawakuwahi kuiishi na kulitumikia taifa hili, wapo ambao wanakumbukwa sana kanakwamba kama si wao taifa hili lisingekuwepo. Lakini wapo ambao michango yao leo ni kama sumu ya nyoka ikiingia mwilini inaondoa tunu ya uhai. Sijawahi kuamini dini au uwepo wa Mungu katika maisha yangu, lakini hakuna hata aliyejari au kunibagua kwa mtazamo wangu huo. Najua kuna watu humu wangepewa fursa ya kuongoza nchi wangekuwa wameutoa uhai wangu. Nyerere anayebezwa na waliovimbiwa amani, Nyerere anayetukanwa na wanaojiita watafiti wa historia mpya ya Tanganyika, Nyerere ambaye leo hayupo na kutokuwepo kwake wasomi wanaojiita ni wasemaji wa Mungu wanaanza kumhukumu kwa niaaba ya Mungu, ndie Nyerere aliyenijengea fursa ya elimu, afya na uhuru wakwenda popote na kuongea na yeyote sio kwa sababu ya "atheism" yangu la hasha, ila kwa sababu nilizaliwa Tanganyika na kukua humo. Maisha yangu yote sikuwahi kushuhudia ubaguzi wowote, Labda sasa ndio naanza kusikia kelele hizi kwa hao wasomi na watafiti wa historia mpya. Juzi nilikuwa Kilwa kisiwani nikaona magofu ya miskiti na majumba ya kifalme ya karne ya 13. Niliona majina ya wamiliki lakini sikuona majina ya mafundi na wajenzi wa majengo hayo. Historia imewasahau na kuwabeza mafundi, wabeba mawe wachoma chokaa na watia nakshi, historia inawakumbuka wa miliki tu. Je wamesahauliwa kwa sababu ya imani zao? Nyie watetezi wa imani amkeni basi muwatetee nahao. Kwanza karne ya 13 kisiwa kile kilikaliwa na waislam wenzenu tu.