UISLAMU au UKRISTO wa Mkwawa unatuhusu nini sisi? Hivi kweli Faiza ni UISLAMU uliokuleta humu JF? Akili yoote hiyo ulionayo ni kwa kuwa ni MUISLAMU? Ukibadili DINI kwa "kuolewa" na mimi kwa mfano basi utakuwa zezeta?
Kubaguliwa Waislaam katika historia ya Taifa, kubadilishwa majina ya Waislaam kwa makusudi kabisa, Kutotajwa michango ya Waislaam kama kina Mkwawa na Kimweri na wengine wengi waliofatia baada yao, kupotoshwa kwa historia kwa makusudi kabisa ili Uislaam na Waislaam wasionekane michango yao katika Taifa hili ndio mada yote iliposimamia.
Imeelezwa kwa ufasaha kabisa kuwa si tu kutokuandikwa kwa Waislaam kwenye historia ni kwa bahati mbaya au kwa kuwa hawana mchango wao katika Taifa hili, bali wao ndio waliokuwa mstari wa mbele na ndio walikuwa waasisi wa harakati zote za kudai madaraka, na ikaoneshwa kuwa haikuanzia kwa Waislaam walioanzisha AA, TAA, TANU bali ikabainishwa kuwa hata kina Songea walikuwa Waislaam na walipigania haki ya uzalendo wao na hata wao majina yao kwa makusudi yamefutwa yenye viashirio vya Uislaam, kwanini? Hilo ni swali jepesi sana kwa mtu mwenye fikra fupi, lakini kwa mtu anaeitakia mema hii nchi ni swali zito sana.
Tukatolewa huko tukapelekwa hadi Nyerere alipowageuka hawa wazee wa Kiislaam waliompokea na kufikia hadi kuwatia ndani na kuwafukuza nchi, swali linakuja, anaewatia watu ndani kwa sababu ya dini zao na sababu ya udini wao, huyo ni nani kama sio mdini? mlishasikia kuna askofu au padri amefukuzwa nchi kwa udini wake au kutiwa ndani kwa udini wake? hapana. Kwa hiyo wadini ni masheikh wa Kiislaam tu?
Tumeona mpaka Nyerere amenukuliwa akisema kuwa anaiendesha nchi kwa
"[SIZE=-0]In an interview with the Christian Century of March 1, 1972, Mwalimu Nyerere was quoted as saying that his efforts to build African socialism in Tanzania represented his determination to translate in practical terms the teachings contained in The Gospel of Jesus Christ.[/SIZE]"
Bado tu, na vielelezo vingine kibao, halafu unakuja kusema kuwa oooh "udini" udini ni nini? Udini wakati Muislaam anasema kaonewa na mfumo uliojengwa kwa makusudi kabisa? udini ni Muislaam anapouliza ilikuwaje 83% vs 17%? kwanini udini isiwe 83% iwe 17%? Kwanini Nyerere aseme atatekeleza ujamaa wake kwa mafundisho yaliomo kwenye injili ya Yesu kristo? na huo sio udini?
Kuweni wa kweli japo kidogo, Waislaam, tuna kila sababu ya kuandika historia ya nchi hii kama ilivyo na hilo ni kwa kila mtanzania mwenye uwezo wa kuandika. Ambae anaiona hitoria ya Mohamed Said ni ya udini, atuambie historia ya Nyerere na kupewa uwenye "heri"kuelekea "utakatifu" sio udini? au uwenye "heri" ni tuzo ya Serikali ya Tanzania na si ya kanisa?
Iweje kiongozi wa nchi awe mwenye "heri" wakati nchi kaiacha hohehahe? hapo sasa. Hiyo heri ni ipi? hakuna zaidi ya umaskini na ufukara aliouwacha Nyerere kwa wananchi wa Tanzania, walioachwa na utajiri wa Ardhi, mashule, mahospitali ni kanisa katoliki pekee na hilo halina ubishi. kwanini?
Leo Tanzania kanisa katoliki linahodhi ardhi zaidi ya tasisi nyingine yoyote baada ya Serikali, ni kwa bahati nzuri tuu? Leo kanisa katoliki lina shule na vyuo kuliko taasisi yoyote baada ya Serikali, ni kwa bahati nzuri tu? leo kanisa katoliki lina mahospitali kuliko taasisi yoyote baada ya Serikali, ni kwa bahati nzuri tu? leo kanisa katoliki linapokea ruzuku kubwa ya kifedha kutoka serikalini kuliko taasisi yoyote nyingine, ni kwa bahati nzuri tu? la hasha, hizo ndio sababu za Nyerere kupewa uwenye "heri" na si kingine, si kwa kulitumikia Taifa ni kwa kulitumikia kanisa, kwa mgongo wa nani? kwa fedha za nani? kwa rasilmali za nani? za walio wafuasi wa kanisa na wasio wafuasi wa kanisa, na wengi wao ni Waislaam.
Ni mengi, mengi sana madhila yaliofanywa na yanayoendelea kufanywa na ukiuliza unaitwa "mdini" haikuanzia leo na haitokuwa mwisho leo lakini "ngoma ikivuma sana...".
Waislaam wa leo na dunia ya leo si dunia ya kuburuzwa, leo ni dunia ya dot com. Kila kitu kiko wazi, hakuna kuzuia "media" kama wakati wa Nyerere, hakuna kuburuzwa kama wakati wa Nyerere, watu kuswagwa kama ng'ombe kupelekwa maporini kuanzisha vijiji vya ujamaa ambavyo havikuleta tija yoyote zaidi ya kututia kwenye lindi la umaskini. Ukitazama kwa undani utaona alikuwa hajashindwa bali ile ilikuwa ni kisingizio cha kuusambaza mfumo kristo.
Kuna siku tulikuwa tunapita njia za ndani kutokea Manyoni kuelekea Singida, siku hizo barabara kuu ya Manyoni haipitiki ikinyeesha mvua, malori yamekwama yamefunga njia, bahati mume wangu ni mzoefu wa mapori kwani ni "hobby" yake kuwinda, akatuambia tuingie hapa (kulia ukitokea manyoni kabla ya kufika Mkiwa) kuna njia za maporini "nazijuwa" zitatutoa karibu ya Singida, gari tuliokuwa nayo ilikuwa inaruhusu kukatiza porini, tukaingia, huko ndani mbugani niliona kitu cha ajabu sana, tulikuta kanisa, na majengo tofauti ndani ya uzio, na hapo ni mbali na kijiji chochote kile. Nikauliza kwanini wamejenga huku porini kabisa? nikaambiwa walijenga hapa wakati wa vijiji vya ujamaa, watu walihamishiwa huku kutoka vijiji vyao vya asili na Wakatoliki wakaja kujenga hilo kanisa shule na zahanati, elewa kuwa vijiji vya asili huko walipoondolewa watu kuletwa hapo porini vyote vilikuwa Waislaam 90% nani asiyejuwa Wanyaturu wa Mkiwa, Isuna na Puma kwa Uislaam wao? huo ndio ushindi wa Nyerere kwa vijiji vya ujamaa, ni nani ataewacha kupeleka mwanae hapo akasome wakati shule ya karibu na hili kanisa ni kilomita 20 na barabara hazipitiki na kama hiyo shule ya bure ilikuwa na waalim. Ni nani ataacha kupeleka mwanae akatibiwe hapo wakati zahanati ya Serikali ya karibu ni kilomita 20 kutoka hapo na kama ina dawa. Huo ni mfano mmoja tu, na nakumbuka jina la hao waliojenga hilo kanisa na hayo makazi mbugani, na juzi juzi niliona Pinda katolewa picha yake kapiga magoti akiwa huko (Tena alikuwa kanisa lao Mkiwa barababarani si hilo waliloliweka huko mbugani)
Huo ndio ushindi wa Nyerere wa kumpatia tuzo ya uwenye "heri" na "utakatifu", ni udini mtupu hakuna zaidi.