Hawa wazee kumbe walikuwa wakizungukana pia wao kwa wao? Ila unaposema baada ya uhuru hawa wasaliti waliachwa kufanya kazi na wale waliokuwa wanawahujumu inashangaza pia.
Proved,
Nilikuwa kila ninapozungumza na
Ally Sykes alikuwa heshi kumlaumu
Mwalimu Nyerere kwa kutowafukuza kazi.
Nadhani
Mwalimu aliwabakisha hawa kazini kwa ajili ya ujuzi ambao waliokuwanao katika kazi za kikachero.
Ally Sykes adui yake mkubwa alikuwa
Amiri Kweyamba, kijana wa Kihaya ambae alimwandama sana.
Soma mkasa huu:
Nitaeleza yale ninayoyajua na kutokana na kauli ya mwenyewe
Ally Sykes
kuhusu makachero wa wakoloni ambao waliwahangaisha sana wapigania
uhuru.
Jina Amiri Kweyamba lilikuwa sana katika ulimi wa
Ally Sykes na kuna kisa
alinihadithia akiwa pamoja na mkewe mama yetu
Bi. Zainab.
Miezi michache kabla ya kuundwa kwa TANU
Ally Sykes alikuwa akichapa
makaratasi ya uchochezi ambayo hayakuwa na nembo ya TAA yaliyokuwa
yameandikwa kwa kuanza na ujumbe huu: ''Kwa Waafrika Wote.''
Ally Sykes alikuwa na ''cyclostyle machine,'' ambayo alikuwa ameificha
nyumbani kwake Mtaa wa Kipata.
Ally Sykes alikuwa akishayachapa alikuwa anawapa wafanyakazi maalum
wa treni na hawa walikuwa wakiyagawa kwa watu maalum katika stesheni
za treni katika Reli ya Kati na ka njia hii makaratasi yake yaliweza kufika hadi
Kigoma na Mwanza.
Makaratasi haya yalifika mikononi mwa Special Branch na yakawa wanayatafuta
na hapo ndipo siku moja wakaingiliwa nyumbani na
Amir Kweyamba kuja
kufanyiwa upekuzi.
Mlango ulipogongwa
Ally Sykes alikuwa mitamboni anachapa na
Bi. Zainab
alipomfahamsiha kuwa Kweyamba yuko mlangoni ikawa heka heka na
Ally Sykes
anasema aliweza kwa haraka sana kuyachukua makaratasi na kuyatumbukiza
chooni na mashine ikarushwa ua kwa ua na
Kweyamba na askari wake walipoingia
ndani hapakuwa na kitu.
Nyumba za Dar es Salaam zamani zilikuwa na ua na mtu alikuwa anaweza kupita ua
kwa ua hata nyumba kumi bila kutoka barabarani.
Huyu
Kweyamba aliwahangaisha sana wanasiasa lakini kwa ninayoyajua mimi ni
kuwa ingawa
Kitwana Kondo alikuwa katika Special Branch lakini yeye hakushiriki
katika operesheni kama hizi za kuvamia majumba ya wapigania uhuru.