Historia ya uhuru kama ilivyoandikwa na Ramadhani Makero


NIMEELEWA KWA NINI UMELALAMIKA KILA UKIANZISHA UZI WAKO MOD WANAUUNGANISHA COZ INAONEKANA YOUR PATHETIC
 
shukrani kwa historia hii nzuri
 
naomba anipe habari kidogo kuhusu Aziz Ally,hasa utajiri wake
 
kwenye Siku hizi huoni! kama FaizaFoxy husema shuleni mmesomea nini vile!?
 
Faiza naomba maelezo kidogo kuhusu yule sheikh binamiri,sijajua jina lake spelling zake
 
Kwahiyo unapata pesa kwa upotoshaji?
 
nice
 
Kwahiyo unapata pesa kwa upotoshaji?
Duduwasha,
Hapana ingekuwa nimeandika kitabu chenye makosa nisingeweza kutiwa katika miradi hiyo ya Oxford na Harvard na kitabu kingekufa zamani sana.

Ikiwa wewe unaona kuna upotoshaji nifahamishe kile nilichopotosha.
 
Hawa wazee kumbe walikuwa wakizungukana pia wao kwa wao? Ila unaposema baada ya uhuru hawa wasaliti waliachwa kufanya kazi na wale waliokuwa wanawahujumu inashangaza pia.
Proved,
Nilikuwa kila ninapozungumza na Ally Sykes alikuwa heshi kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa kutowafukuza kazi.

Nadhani Mwalimu aliwabakisha hawa kazini kwa ajili ya ujuzi ambao waliokuwanao katika kazi za kikachero.

Ally Sykes adui yake mkubwa alikuwa Amiri Kweyamba, kijana wa Kihaya ambae alimwandama sana.

Soma mkasa huu:

Nitaeleza yale ninayoyajua na kutokana na kauli ya mwenyewe Ally Sykes
kuhusu makachero wa wakoloni ambao waliwahangaisha sana wapigania
uhuru.

Jina Amiri Kweyamba lilikuwa sana katika ulimi wa Ally Sykes na kuna kisa
alinihadithia akiwa pamoja na mkewe mama yetu Bi. Zainab.

Miezi michache kabla ya kuundwa kwa TANU Ally Sykes alikuwa akichapa
makaratasi ya uchochezi ambayo hayakuwa na nembo ya TAA yaliyokuwa
yameandikwa kwa kuanza na ujumbe huu: ''Kwa Waafrika Wote.''

Ally Sykes alikuwa na ''cyclostyle machine,'' ambayo alikuwa ameificha
nyumbani kwake Mtaa wa Kipata.

Ally Sykes alikuwa akishayachapa alikuwa anawapa wafanyakazi maalum
wa treni na hawa walikuwa wakiyagawa kwa watu maalum katika stesheni
za treni katika Reli ya Kati na ka njia hii makaratasi yake yaliweza kufika hadi
Kigoma na Mwanza.

Makaratasi haya yalifika mikononi mwa Special Branch na yakawa wanayatafuta
na hapo ndipo siku moja wakaingiliwa nyumbani na Amir Kweyamba kuja
kufanyiwa upekuzi.

Mlango ulipogongwa Ally Sykes alikuwa mitamboni anachapa na Bi. Zainab
alipomfahamsiha kuwa Kweyamba yuko mlangoni ikawa heka heka na Ally Sykes
anasema aliweza kwa haraka sana kuyachukua makaratasi na kuyatumbukiza
chooni na mashine ikarushwa ua kwa ua na Kweyamba na askari wake walipoingia
ndani hapakuwa na kitu.

Nyumba za Dar es Salaam zamani zilikuwa na ua na mtu alikuwa anaweza kupita ua
kwa ua hata nyumba kumi bila kutoka barabarani.

Huyu Kweyamba aliwahangaisha sana wanasiasa lakini kwa ninayoyajua mimi ni
kuwa ingawa Kitwana Kondo alikuwa katika Special Branch lakini yeye hakushiriki
katika operesheni kama hizi za kuvamia majumba ya wapigania uhuru.
 
Wanalazimisha tuwatambue wehu wengine waliokuwa wanashinda kwenye bao wakati mwalimu yupo busy kuweka mikakati ya kuikomboa Nchi

Hawa wazee ni kuwaacha tu wanamatatizo mengi
Tatitzo kubwa ni udini umeathiri fahamu zao


Kauli hii ni ya kishetani kabisa,

Mwalimu nyerere katika moja ya hutuba zake za kung'atuka alipata kusema juu ya mchango wa Waislamu juu harakati za kupigania uhuru, na specifically--- alitaja siku alipoitwa na wazee kwenda usiku kwa mzee Jumbe Tambaza kwa ajili ya kumfanyia "Kafara", akielezea , Nyerere alisema kwamba alipofika akakuta Beberu la mbuzi na Shimo limechimbwa, yule beberu alichinjwa huku damu yake kumiminiwa mle shimoni kisha Nyerere akaambiwa atambuke lile shimo, alipotambuka wale wazee wakasema Twinning amekwisha, sasa nenda zako hakuwezi tena.

Kabla ya nyerere kufanyiwa kafara alifanyiwa dua na baadaye ikaja hiyo kafara.

Baadaye akaelezea jinsi alivyokwenda Bagamoyo kwa Shk Ramia, ambapo walikuwa wakishinda makaburini wakifanya matambiko kwa ajili ya kudai uhuru, na akaeleza kisa kimoja juu ya vita vya maumau, kwamba Shk Ramia akasema inawapasa wafunge saumu kwa ajili ya kuwaombea mashujaa wa Maumau waliofungwa, Nyerere anasema ilipofika muda mchana wa saumu alisikia kichwa kinauma sana na akamuomba shk Aspro (dawa ya zamani ya maumivu), Shk Ramia akamjibu; asubiri, ilipofika muda wa kufuturu, wakafuturu baada ya muda kidogo, shk Ramia akamuuliza Nyerere ; je kichwa bado kinauma??---- Nyerere akajibu hapana, na, anasimulia; kumbe kile kichwa kilikuwa ni sababu ya njaa (saumu).

Nyerere akasema; yeye na wale wazee wake wa kiislamu walitoka mbali sana na walielewana vizuri sana, yeye MKRISTO peke yake na wao waislamu na safari fulani John Rupia aliambatana na nyerere.

πŸ–•πŸ»Maneno hayo yamo katika moja ya hotuba za Nyerere muda mfupi baada ya kung'atuka alipokuwa akiwaaga wazee wa Dar.

Sasa Nyerere anathamii mchango wa Waislamu katika harakati za uhuru, anatokea mtu na chuki za kidini na wala asiyejua historia na anaanza kukashifu.πŸ€”πŸ€”
 
Faiza naomba maelezo kidogo kuhusu yule sheikh binamiri,sijajua jina lake spelling zake

Hilo la Sheikh Hassan Bin Amir nnamwachia kaka yangu Allama Mohamed Said maana anamfahamu vizuri sana.

Allama nnaomba nisaidie kujibu hilo swali.

Mimi nnakuwekea clip utampata humo akielezewa...

 
Faiza naomba maelezo kidogo kuhusu yule sheikh binamiri,sijajua jina lake spelling zake
Pablo,
Sheikh Hassan bin Ameir.


Ukitaka kumjua zaidi Maalim Faiza kaweka video clip.
Nami nakuongezea hapo chini:


Mwisho kulia ni Tewa Said Tewa

 


Ni historia nzuri ya kisiasa na kidini "iliyofichwa" kuhusu Marhum Shk, Hassan bi Ameir.
Mungu amlaze peponi.

Nimefurahi sana kuona Lugha safi sana ya kiingereza imetumika kuelezea historia hiyo, dunia itajua japo sisi tumefunga macho na masikio. 🀝🏻
 
Mokaze,
Amin.
 
History nzuri tu.kwa watu wa Dar hasa,mitaa ya kariakoo haya majina ni yalikuwa yanasikika sana mpaka miaka ya themanin,wengi walikuwa bado wanaishi nakumbuka kumuona mzee mtemvu kariakoo mtaa wa Narung'ombe,nilipoambiwa huyu ndio alikuwa mwanasiasa TAA nilishangaa alikuwa kachoka kidogo na mkononi kabeba kikapu cha ukindu.Wengi tunakuelewa mkuu.
 
Hili haliepukukiki, maana wapiginai na Uhuru wengi walikuwa waislam ,mfano akina mkwawa,kinjekitile, millambo nk
 
mkuu wewe umesimuliwa na kusoma historia.

huyu mzee kaishi katika hiyo historia.

bila shaka ungerega sikio uzuri mzee akufunze maisha yao waati huo vipi yalikuwa.

tuliza akili hapo akupe habari uzidi kuujaz ubongo zaidi ya hapo.
 
aisee pascal mayalla hata nikimuangalia namuona kabisa ni mtupu katika mambo ya historia zetu kwani anaonekana ni mtu msomi wa historia kuliko uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…