Historia ya Vita ya Kagera 1978-1979

Umenifundisha vitu vingi sana mkuu, umenikumbusha Mkurya mwenzangu Mwita Chacha, pale nyumbani Mogabiri na sehemu jirani anajulikana kama Mwita Wabachira [emoji1787][emoji3]

Nasubiri muendelezo kwa hamu kubwa sana
 
Umenifundisha vitu vingi sana mkuu, umenikumbusha Mkurya mwenzangu Mwita Chacha, pale nyumbani Mogabiri na sehemu jirani anajulikana kama Mwita Wabachira [emoji1787][emoji3]

Nasubiri muendelezo kwa hamu kubwa sana
Poapoa mkuu nauleta Sasa hivi

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Nachukiaga kusoma story halafu Jitu kumbe limecopy na kupaste kutoka source bila ku-acknowledge

Mwizi wa hatimiliki , naona anaendelea tu kama hajui tumeshtukia........... 🤣
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA.

Awamu ya pili ya vita yaanza, JWTZ yaingia Uganda.

#Sehemu #ya - 11.

Sehemu ya kumi ya mfululizo wa makala zangu hizi,tuliona Mwalimu Nyerere alipokabiliwa na Nchi Huru za Afrika (OAU) pamoja na mataifa kadhaa wakimtaka asitishe vita dhidi ya Uganda na kutoa masharti matatu.

Moja, OAU imkemee Idi Amin kwa kitendo chake cha uvamizi.

Pili, Idi Amin aahidi na
akane kwamba hataki sehemu yoyote ya Tanzania.

Na tatu, Amin aahidi kulipa fidia kwa uharibifu alioufanya.

OAU haikumkemea Amin, Nyerere akaamuru JWTZ iingie Uganda kumng’oa.

Hapo ndipo awamu ya pili ya Vita vya Kagera ilipoanzia.

Sasa endelea......

Kuingia ndani ya Uganda ilikuwa ni awamu ya pili ya Vita vya Kagera.
Kabla awamu hiyo haijaanza,kulifanyika mabadiliko ya uongozi kwenye uwanja wa vita.

Baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu akiwapanga wapiganaji wa JWTZ na kuirejesha ardhi ya Tanzania iliyotekwa na Idi Amin,Brigedia Jenerali Tumainieli Kiwelu alirejeshwa Dar es Salaam.

Kazi ya kuingia Uganda ikaenda mikononi mwa kamanda mwingine,Meja Jenerali David Msuguri.

Ilipangwa miji ambayo ingeanza kutekwa ambayo ni Masaka na Mbarara.

Hii ikabatizwa jina la Mapigano ya Masaka ambayo ilidumu kwa siku mbili tu.

Na hatimaye siku ya Ijumaa na Jumamosi ya Februari 23 na 24, 1979 na ikamalizika.

Lakini kabla Masaka haijafikiwa kulikuwa na miji midogo midogo ya kutekwa, mmojawapo ni mji wa Lukoma ambako kuna uwanja mdogo wa ndege uliojengwa mahsusi kwa shughuli za kivita na ni umbali wa kilomita 20 kutoka mpaka wa Tanzania na Uganda.

Ndege za kijeshi zilizoishambulia Tanzania zilipaa kutoka katika uwanja huo uliozungukwa na vilima vya Nsambya,Kikandwa na Simba.
Vilima vyote hivi askari wa Idi Amin walikuwa wametanda wakiwa na silaha kali za kivita vikiwamo vifaru na mizinga mikubwa.

Brigedi tatu zilizokamilika za jeshi la wananchi wa Tanzania ambazo ni 201, 207 na 208 zilitumwa kuingia Masaka.

Mpango wa awali ulikuwa ni kuzitumia brigedi za 201 na 208 kushambilia vilima vya Simba kutokea Kusini-Magharibi na Brigedi ya 207 ishambulie kutokea Mashariki.

Lakini baadaye taarifa za kiintelijensia zilisema kulikuwa na zaidi ya askari 5000 wa Idi Amin wakiwa na vifaru na mizinga mikubwa eneo la Katera kwenye rasi ya Sango Bay,eneo la Kakuuto upande wa pili wa Ziwa Victoria.

Kuwaacha hawa ingefanya eneo la upande huo wa Tanzania kuwa hatarini zaidi kushambuliwa.

Kwa hiyo iliamuliwa Brigedi ya 207 ianze kushambulia Katera,na kulikuwa na njia mbili za kufika Katera kutokea Minziro.

Njia ya kwanza na rahisi zaidi ilikuwa ni barabara kuu,lakini kwa kutumia njia hiyo jeshi la Tanzania lingekutana na mashambulizi ya uso kwa uso kutoka jeshi la Idi Amin.

Njia ya pili na ngumu zaidi ni kupita kwenye uchochoro wenye mabwawa yaliyojaa maji kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha.Huu ni upande wa pili wa Ziwa Victoria.

Askari wachache waliozaliwa katika vijiji vilivyozunguka ziwa karibu na Bukoba na ambao walijua lugha na tamaduni za eneo hilo walichaguliwa wasonge mbele,wakivalia nguo za kiraia na kubeba matairi ya baiskeli na bidhaa nyingine kama vile wanakwenda sokoni,askari waliobaki nyuma wakawafuatilia kwa kufuata nyayo zao.

Siku iliyofuata walirudi wakiwa wamechoka kupita kiasi na wengine wakiwa wagonjwa,na waliripoti kuwa mvua kubwa iliyonyesha iliharibu sana barabara kiasi cha kutopitika.

Pamoja na ripoti ya wanajeshi hao,Kamanda wa brigedi hiyo, Brigedia John Butler Walden,aliamua ni lazima wasonge mbele hata kama hali ya hewa ni mbaya kiasi gani.Huyu ni brigedia aliyeitwa ‘Black Mamba’.

Kwa kuwa alijua wanajeshi wake wasingepata moyo wa kusonga mbele bila yeye kwenda nao bega kwa bega, aliamua kutembea nao kwa mwendo wa zaidi ya kilomita nane za kwanza kutoka Minziro hadi kilima cha Bulembe.

Brigedia Walden alidhani mwendo kwa hizo kilomita nane ungewachukua saa chache kupita kwenye msitu mnene,lakini iliwachukua karibu saa 11 wakipambana na matope, madimbwi makubwa ya maji,mbu na mbung’o na maeneo mengine walilazimika kutembea kwenye madimbwi ya maji yaliyowafika mabegani karibu kabisa na kuzama.

Hatimaye walipofika eneo ambalo lilikuwa kavu kwa kiasi fulani,Brigedi ya 207 ilipumzika kidogo kisha ikaanza tena matembezi marefu kuelekea Kaskazini umbali wa kilomita 28 kuingia ndani ya Uganda katika mji wa Katera.

Walipodhani masaibu yamekwisha,ndipo yalipoongezeka maana kuna wakati fulani wadudu kama mbu na mbung’o waliwasumbua.

Brigedi ya 207 ikajikuta katika vita ya aina mbili kupambana na jeshi la Idi Amin na wadudu wanaokera katika msitu mnene,huku mvua ikinyesha na barabara yenye madimbwi kujaa maji.

Silaha walizokuwa nazo zikalowa maji.

Kutokana na barabara kutopitika kwa gari hata zile gari za jeshi askari wa brigedi hii walilazimika kubeba vichwani mwao silaha zao na zana zingine za kivita.

Hatari kubwa zaidi kuliko mbu na mbung’o ilikuwa ni wanyama kama mamba na viboko waliokuwa maeneo hayo,hususan kuelekea Sango Bay.
Kwa hiyo kulikuwa na hofu nyingine ya wanajeshi hao kushambuliwa na hata kuliwa na wanyama hao wakali.

Kwa umbali wa kilomita 28,na kutokana na ubovu mkubwa wa njia waliyopita ikiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji,ikijumlishwa na mashambulizi ya wadudu,Brigedi hiyo ilitumia muda wa saa zaidi ya 50 bila kupumzika wala kula.

Redio za mawasiliano walizokuwa nazo zililowa maji hata zikashindwa kufanya kazi.Kwa hiyo walipoteza mawasiliano kabisa na makao makuu ya kikosi chao.

JWTZ ilianza kuwatafuta wanajeshi hao bila mafanikio.Kukawa na hofu kubwa kuwa Brigedi ya 207 imeshambuliwa na kufyekwa yote.

Hakukuwapo na namna yoyote ambayo yeyote katika brigedi hiyo angeweza kufikiwa.

Hatimaye ilipofika saa 11 jioni ya siku ya tatu, brigedi hiyo ikaibuka kutoka kwenye mabwawa ya maji na matope.

Angalau sasa redio zikaanza kufanya kazi na wakaweza kuwasiliana na kituo chao cha kazi.
Ingawa hakuna mwanajeshi hata mmoja aliyepoteza maisha,zaidi ya 200 miongoni mwao walikuwa wagonjwa na wachovu mno kiasi kwamba walishindwa kusonga mbele.

Wengine walifikia hatua ya kushindwa hata kutembea kiasi kwamba ilitumwa helikopta ya jeshi kuwabeba.

Kwa kuwa wanajeshi wa JWTZ walikuwa wamechoka sana, iliamuliwa kuwa wasubiri hadi kupambazuke ndipo mashambulizi yaanze.

Je, walianza kushambulia? Na walishambuliaje?
 
Tupo pamoja.
 
Aisee!Safi sana!
 
Humu ndani kuna matakata wengi including wewe kazi yenu ni kuponda kazi za wenzenu mbwa wewe

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Sina muda huo muda wa mipasho
Wewe ni mwizi wa hakimiliki, eti unaita hii ni kazi yako, This is plagiarism

"Plagiarism"
the practice of taking someone else's work or ideas and passing them off as one's own.
Maana:
(Uhalifu wa kuchukua kazi au maoni ya msanii mwingine na kuipitisha kama ya kwako na kukiuka sheria ya hakimiliki).

Katika sheria ya hakimiliki, msanii ametafsiriwa kama mwigizaji, mwandishi, mwimbaji, mwanamuziki, mchezaji (dancer) au mtu anayeigiza, kuchonga au kufanya maonesho jukwaani.
kifungu cha 3(i) cha sheria hii, kazi zinazolindwa na sheria hii ni zile ambazo zimetengenezwa na mtunzi wa Kitanzania au zile ambazo mtunzi wake si Mtanzania lakini ana makazi yake ya kudumu hapa nchini au kazi hiyo iliyotengenezwa kwa mara ya kwanza hapa Tanzania, au kazi ambazo ni za kusikika na kuona (audio-visual) ambazo mtayarishaji wake ni Mtanzania au makao makuu yake yakutengeneza kazi hizo zipo nchini.

Umevunja sheria..................End Off
 
Wivu tu
 
#HISTORIA #NA #KUMBUKUMBU #YA #VITA #YA #KAGERA:



Majeshi ya Tanzania yauteka mji wa Masaka Uganda.

#Sehemu #ya - 13.

Toleo lililopita tuliona jinsi wapiganaji wa Tanzania walivyoteka maeneo ya Uganda na silaha za jeshi lao.Maeneo yaliyotekwa ni vilima vya Kikanda, Nsambya na Simba.
Baada ya mafanikio hayo ndipo ikaanza safari ya kwenda kuteka miji ya Masaka na Mbarara.

Je, Masaka na Mbarara zilitekwaje?

BAADA ya kuviteka vilima vya Kikanda, Nsambya na Simba, sasa kazi iliyofuata ni kuteka miji ya Masaka na Mbarara.

Vikosi vilivyoelekea Masaka havikupata tabu kama vile vilivyoelekea Mbarara. Brigedia Silas Mayunga aliyekuwa akiongoza Brigedi ya 206 ndiye aliyekutana na hali ngumu zaidi.

Kiasi cha kilomita 45 kutoka mpaka wa Tanzania,karibu na mji wa Gayaza vifaru viwili vya Tanzania vya kikosi cha Luteni Nshimani vilipigwa kombora na majeshi ya Idi Amin.

Kwa jinsi Nshimani alivyokasirika,alianza kuwakimbilia maadui waliorusha makombora hayo."Kitabu cha War in Uganda" kinasema alipokuwa akiwafukuza kwenye barabara ya kuelekea ufukweni mwa Ziwa Nakivale, Luteni Nshimani aligutuka kuwa alikuwa akielekea kwenye hatari kubwa.

Karibu na kona mmoja ya barabara hiyo alikutana na mzee mmoja mwanamume aliyekuwa akipita eneo hilo.

Alimsimamisha na kumuuliza kama ameyaona majeshi ya Amin maeneo hayo.
Mzee alimjibu kwamba wote wameshakimbia.
Wakati Nshimani alipogeuka na kuelekea kwenye kona ya barabara hiyo,mtikisiko mkubwa wa milio ya risasi za bunduki za SMG ulitikisa dunia katika eneo hilo.

Risasi hizo zilikuwa zikipigwa kutoka pande tatu.
Watanzania walikuwa wameingia kwenye mtego mbaya kuliko wowote katika vita yote ya Tanzania dhidi ya Uganda.

Milio ya risasi ilidumu kwa muda fulani,na ilipotulia hatimaye, tayari Watanzania 25 walikuwa wameshapoteza maisha.

Haya yalikuwa ni mauaji makubwa zaidi kwa wanajeshi wa Tanzania kuliko wakati mwingine wowote wa kipindi chote cha vita ile.

Shambulio hili lililofanywa na askari wa Idi Amin lilikuwa ni mojawapo ya yale machache waliyofanya kwa umakini mkubwa kipindi chote cha vita.

Shambulio la Ziwa Nakivale likawatia hasira majeshi ya Tanzania,lakini hawakuvunjika moyo.

Wakasonga taratibu kuelekea Masaka upande wa mashariki na Mbarara upande wa magharibi.

Katika njia nzima kulikuwa na mapigano karibu katika kila kitongoji mengine madogo na mengine makubwa.

Maeneo ambayo kulikuwa na mapigano makubwa ni pamoja na miji ya Kyotera, Kalisizo, Bukeri, Sanga, Miakitele na baadhi ya maeneo mengine.

Wakati wote huu kusonga mbele kulifanyika kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa kabla ya shambulio la Nakivale.

Wanajeshi wa Jeshi la Amin wakawa wanakimbia ovyo na kufyatua risasi ovyo, Wakihofia mizinga ya Tanzania,askari wa Amin walianza kujificha kwenye miji kwa imani kuwa Tanzania ingesita kupiga mabomu maeneo ya raia na hata kama wangepiga mabomu hayo basi raia wa Uganda wangekasirishwa sana na wanajeshi wa Tanzania na hivyo kushirikiana na askari wa Amin.

Lakini hali ilikuwa kinyume. Raia walikuwa tayari wameshaikimbia miji hiyo hata kabla askari wa Amin hawajafika wala wale wa Tanzania.Kutokana na sababu hiyo,wanajeshi wa Tanzania hawakuwa na hofu ya kutumia mizinga yake kushambulia miji hiyo kwa sababu hawakuwa na hofu ya kuwapo kwa raia katika maeneo hayo.

Vikosi vilivyoelekea Masaka havikupata tabu kama vile vilivyoelekea Mbarara. Brigedia Silasi Mayunga aliyekuwa akiongoza Brigedi ya 206 ndiye aliyekutana na hali hiyo.

Kwa mujibu wa kitabu cha "War in Uganda: The Legacy of Idi Amin (uk. 82), wapiganaji wa Tanzania walipofika umbali wa kilometa kama 30 kusini mwa mji wa Masaka walikutana na kijana wa Kitanzana ambaye aliwaambia alitekwa na majeshi ya Idi Amin na kupelekwa Uganda sasa alifanikiwa kutoroka na alikuwa njiani kurudi nyumbani.

Walipomhoji zaidi aliwaambia wanajeshi hao kuwa ameacha zaidi ya raia 2,000 wa Tanzania katika kambi ya mateso ya Kalisizo.

Lakini walipofika Kalisizo hawakukuta hata raia mmoja wa Tanzania aliyekuwa ameshikiliwa na, badala yake,waliwakuta askari wapatao 600 wa Amin wakisubiri kushambulia.

Huenda tayari walikuwa wameachiwa baada ya kupata habari kuwa majeshi ya Tanzania yanakaribia.
Askari wa Amin waliokuwa wakiwasubiri askari wa Tanzania ili wawashambulie,walianza kufanya hivyo,lakini walipopigwa mzinga wakajikuta wameyeyuka kama samli kwenye kikaango.

JWTZ haikuishia hapo wakaendelea kushambulia zaidi kutokea pande tatu.

Askari wa Amin wakachanganyikiwa zaidi walipoona hali kwao inazidi kuwa ngumu,waliobahatika kukimbia walianza kukimbia ovyo kuelekea Masaka.

Zaidi ya askari 200 wa Amin waliuawa siku hiyo katika shambulio hilo moja la Kalisizo.
Walionusurika kuuawa na wakabahatika kukimbia, walikuwa wakipiga mayowe njia nzima kuelekea Masaka.

Askari wa Amin ambao hawakuwa eneo la tukio, lakini wakawaona wenzao wakikimbia kwa hofu huku wakipiga mayowe,nao wakajiunga nao na kuanza kukimbia ovyo.

Askari wengine waliopata habari za yaliyotukia walivunjika mioyo na wakapoteza hamu ya kuendelea na vita.

Baada ya ushindi wa Kalisizo,Jeshi la Tanzania walikuwa na nafasi nzuri zaidi za kusonga mbele kuelekea Masaka,lakini badala yake walitulia wakaanza kujipanga.

Usiku wa kuamkia Jumamosi ya Febriari 24, 1979, mji wa Masaka ukawa umezingirwa na JWTZ kwa pande tatu na, baada ya muda mfupi, brigedi za 201 na 208 zikaanza mashambulizi.

Sehemu ya kwanza kushambuliwa ilikuwa ni kambi ya jeshi ya Kikosi cha Suicide kilichoachwa peke yake kulinda mji wa Masaka.

Vikosi vingine vilikuwa vimetoweka kuelekea Lukaya walipoelemewa, kikosi cha Suicide nacho kikatoweka,kikakimbilia Villa Maria.

JWTZ walikuwa na amri ya kuiteketeza Masaka.
Mji uliteketezwa.Ilipofika jioni ya Jumamosi ya Februari 24, mji wa Masaka ukawa tayari umeharibiwa vibaya,na sasa majeshi ya Tanzania yakaridhika kwamba Idi Amin ameanza kulipa gharama za kuteka ardhi ya Tanzania.

Awamu ya pili ya vita ikawa imemalizika.Sasa ikaingia awamu ya tatu.

Endelea kufuatilia udambwi udambwi huu uzidi kuhabarishwa juu ya vita hii iliyopiganwa na majirani hawa wawili wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Nini kilifuata baada ya Masaka kutekwa?

Fuatilia sehemu ya 14 na 15 [emoji1666]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…