NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Yani hii Tanzania ukienda mikoa nje ya Mbeya, ukiuliza jiji la Mbeya linakaliwa na kabila gani, fasta mtu anakujibu wanyakyusa lakini ukweli ni kwamba wasafwa ndio wenyeji wa kihistoria na hata hili jina la Mbeya lina asili ya neno la Kisafwa "Ibheya" ambayo maana yake ni chumvi, kilotokea nini hadi wasafwa wakapoteza utambulisho wao wa kufahamika kuwa wenyeji wa jiji hili ?
ni kwamba nchi ilipopata uhuru, Mbeya jiji ikapewa hadhi ya kuwa makao makuu ya mkoa wa Mbeya, wanyakyusa waliokuwa wilaya za karibu kama Rungwe na Kyela walianza kuja kwenye makao makuu ya kupata huduma za kijamii bora, kusoma, kufanya biashara, n.k.
Muda huo wakazi wa mbeya mjini wengi walikuwa ni wazawa ambao ni wasafwa, shida ikaja kwamba wasafwa wakiona wageni walikuwa hawataki kuchangamana na jamii zingine, ilikuwa ni kwa sababu za kulinda na kuzithamini zaidi tamaduni zao zisiingiliwe na makundi mengine, hivyo walikuwa wakiona kuna wageni wenye tamaduni tofauti, wao wanahamisha makazi kwenda sehem ambayo wapo peke yao. mji ulizidi kupanuka, wanyakyusa na wageni wengi zaidi walifikia Mbeya mjin, hii ilileta usumbufu kwa wasafwa kuhama hama mji unavyozidi kupanuka, ikafikia kipindi wengine wakaanza kukimbilia maeneo ya mbali zaidi milimani. Kwa wakati huu wote wanyakyusa na wageni wengine walifikia muafaka kwamba wasafwa wanahama kwasababu ni waoga, ila kwa uhalisia wasafwa walikuwa wana sababu zao za kitamaduni.
matokeo yake hapa mjini makabila ya ziada yaliyofika kama wanyiha, wandali, wakinga, wahehe, wangoni, wabena, n.k. wao wakawa wanajua huu mji ni wa wanyakyusa maana wakifika mjini wanakutana na wanyakyusa wengi, Pia wnyakyusa wengi waliwahi kutoka nje ya Mbeya kwenda mikoa mingine kikazi, kielimu, siasa, n.k. hivyo watu wa mikoa waliyofikia walijua Mbeya ni ya wanyakyusa. wakati huo wasafwa waliokuwa wenyeji original ilikuwa ngumu kuwajua sababu walikuwa wanaishi mbali ya mji na maeneo yasiyofikika kirahisi ikawa vigumu kwa watu wa mikoa mingine kuwajua.
Laiti wasafwa wangebaki kwenye huu mji huenda wangekuwa na maendeleo sana an kufahamika zaidi kuzidi wanyakyusa, mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini hii bahati wakaichezea na. wasafwa waliletewa hivi vitu vizuri hapa mjini ila wakavikimbia.
-serikali ilijenga shule nyingi ila wasafwa walizikimbia, wakawaachia wanyakyusa na wageni wengine.
-Serikali na makampuni yalitoa nafasi za ajira lakini wasafwa walikuwa mbali, wanyakyusa na wageni walizifaidi
-mji ulianza kujaa na kukawa na fursa za biashara ambazo wasafwa wangeweza kupata pesa lakini kujitenga kwao kukaliacha soko wazi kwa wanyakyusa na wageni wengine.
-madaraka, vyeo na teuzi serikalini za kuongoza mji huu wakawaachia wanyakyusa na wageni wengine, nafasi hizi zilitumika na wanyakyusa kuwekana maofisini na kupeana vyeo.
-viwanja vingi waliviacha ama kuviuza na kukimbilia milimani kusiko hata na huduma za jamii, n.k. leo hii nyumba nyingi maeneo ya mjini ni za wanyakyusa japo kwa sikuhizi wageni wengine nao wanajenga sana,
Ni historia yenye kusikitisha ila ina funzo kubwa sana, mkataa kwao hugeuka mtumwa.
Mwisho kwa kuhitimisha naweza kutoa ushauri kwa wasafwa kwamba historia haiwezi kubadilika itabaki kwajili ya kujifunza lakini mnachoweza kubadilisha ni future kwa kuanza kutia bidii muda wa sasa (present)
- wasafwa mzingatieni sana elimu pambanieni na ikibidi mjinyime watoto wasome shule hasa za private na jumuia ya wazazi zilizojaa tele Mbeya jiji, mhakikishe watoto wafike vyuoni nanyi mjae jae maofisini na vyeo.
- mjipanue na kutafuta fursa mpya za kibiashara na kujiajiri, Mbeya ni jiji lina watu wengi wenye mahitaji mengi muangalie ni sehemu zipi mnaweza kuchota pesa.
- muwe na bidii ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na uongozi kwenye huu mji wenu, mpambanie nafasi za kupaza sauti ya kero zetu wageni wa mbeya na zenu wazawa halisi wa mbeya.
-msaidiane na kubebana ili walio chini nao wawe na maendeleo, roho za umimi na ubinafsi haziwezi leta maendeleo