Kweli nami nimesikia mkuuKuna redio fulan za Malawi.....nikiwa tukuyu zinaongea kinnyakyusa fluent....
Kile cha ndan ndani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli nami nimesikia mkuuKuna redio fulan za Malawi.....nikiwa tukuyu zinaongea kinnyakyusa fluent....
Kile cha ndan ndani
Ah kabisaKuna redio fulan za Malawi.....nikiwa tukuyu zinaongea kinnyakyusa fluent....
Kile cha ndan ndani
Yah mbeya napita tu mkuuNaona ni wazi kabisa Mbeya hujaenda miaka, Mbeya imebadilika sana mkuu, hio erland hotel ilishakufa walijenga tawi la karibu la chuo kinaitwa teku. kwa sasa hapa Mbeya kuna hoteli kama Tughimbe, Desderia (ya sugu), Mdope, usungilo, n. k hizi zote nilizotaja wamiliki ni wakinga.
hotel hio ya silver stone sijajua maana ipo mkoa mpya wa Songwe, mambo yalivyobadilika kwa sasa siwezi shangaa nayo ikawa ni tbt zilizopendwa
Silver stone Hotel ipo tundumaNaona ni wazi kabisa Mbeya hujaenda miaka, Mbeya imebadilika sana mkuu, hio erland hotel ilishakufa walijenga tawi la karibu la chuo kinaitwa teku. kwa sasa hapa Mbeya kuna hoteli kama Tughimbe, Desderia (ya sugu), Mdope, usungilo, n. k hizi zote nilizotaja wamiliki ni wakinga.
hotel hio ya silver stone sijajua maana ipo mkoa mpya wa Songwe, mambo yalivyobadilika kwa sasa siwezi shangaa nayo ikawa ni tbt zilizopendwa
Enzi hizo mzee wangu alikuwa ananunua maeneo kule ituha ilikuwa wasafwa tupu lakini sasa hivi kumekuwa mji na wasafwa hawapo tena.Nakumbuka ukiwa blot T Kutokea hapo fanya unakwenda shule ya sec ivumweee juu huko mlimani
Wasafwa walikuwa wengi huko milimani.....
Kitu kikubwa wasafwa walichonqcho ni uoga na upole
Hivi kwa sasa kuna Don mbeya msafwa
Ova
Kuuza Nyanya au maparachichi si ndiyo kujiajili kwenyewe?wazawa watabaki kuwa wazawa mkuu, kule mteremko wa mbalizi na mlima wa nyoka, magari yanapopata sana ajali wanaofanya mila ni wasafwa, wasafwa walichokosea ni kukimbia maeneo wakiona wageni (hadi leo wanataniwa kwa jambo hili)
ila kwa idadi ya wakazi naweza kusema ni wanyakyusa japo nao wana kubarua kizito cha kujikwamua kiuchumi hasa kwenye utafutaji, wanyakyusa wengu ukifatilia wamejazana maeneo yenye maendeleo ya chini ama kawaida kama nzovwe, mamajoni, n.k. zile sehemu zenye maendeleo kama forest, block t, isyesye, n.k wamejazana wakinga pamoja na wageni wengine.
uzuri ni kwamba angalau wanyakyusa shule inawabeba wanapata ajira lakini sikuhizi kuna tatizi kubwa la ajira linalowalazimu vijana wageukie kujitafutia, ubaya ni kwamba kwenye utafutaji wa biashara na kujiajiri wanyakyus hapa wapo nyuma, ukifika sehemu kama mwanjelwa na kabwe maduka mengi yanamilikiwa na wakinga au wageni wa makabila ya kigeni,,, wanyakyusa wengi utawakuta nyuma ya soko wanauza maparachichi na baadhi mitumba.
Dah umezunguka mzee Hadi chimala. Kumi Bora unapakumbuka ?Yah mbeya napita tu mkuu
Ila nmeishi sana mbeya kuanzia chimala,mbeya mjini nmeishi jacaranda,Ghana,bkock t
Nlisoma form 1 sangu
Mbeya nlizunguka sana wakati huo na mtu akiniambia moja ya mkoa ninayoikubali ntakutajia mbeya
Dah erland iliondoka,aise
Ila ile sehemu ya Monrovian bado ipo
Hapo block t
Ova
Nyie ni wavamiziMbeya ni yetu sisi wanyakyusa....
Jiangalieni lieni wanyakyusa,lazima wengine asili yenu iko Malawi [emoji1]
Ova
Ha ha ha!
Kuna wanyakyusa Malawi-wanaitwa wa Ngonde, Zambia na hata Zimbabwe.
Kuna redio fulan za Malawi.....nikiwa tukuyu zinaongea kinnyakyusa fluent....
Kile cha ndan ndani
Kweli nami nimesikia mkuu
ni kawaida kukuta kabila la mpakani wapo pia nchi ya jirani, tuna mipaka iliyochorwa na wakoloni kutenganisha nchi lakini sio makabila.Ah kabisa
Kuna muingiliano huko
Ova
Ni sawasawa na mji wa mbalizi na kabila la Wamalila.
Ila Wamalila nao hawajulikani kisa ni uchache wao
wamalila ni wasafwa hao hao tu, ni sawa na wachaga kuna wa kibosho, rombo, machame, n.k.Mbeya n mkoa wenye makabila mengi kuna wamalila pia wamesaulika kabisa
Wanajisemaga eti walitokana na waruguru kwao ni morogoro wakati walitokea malawi na kilugha kinaingiliana.Jiangalieni lieni wanyakyusa,lazima wengine asili yenu iko Malawi [emoji1]
Ova
Mkuu NGONDE ni uwanda wa sehemu za Kyela mpaka kuingia Malawi.Maana ya neno MBEYA unaipata kwenye lugha gani?
Namfahamu jamaa akiitwa Ngonde kwa jina la UKOO na ni msafwa, ana ndugu Malawi, anazungumzia NGONDE Empire mara nyingi nikikutana naye, anasema ilikuwa kubwa na hata sasa ipo kubwa isipokuwa kutokana na mambo ya lugha sijui Lahaja, Rejesta, jin linatoholewa, mara Gonde, Gondwe, Ngonde n.k
Historia inasemaje kuhusu wamisionari na mkoa wa Mbeya? Isije kuwa kama Wachaga, Wahaya na Umisionari, wameingilia huko, wakawapa madini wakwanza, basi wakajiona viiiiichwa, kumbe ni hali ya kutangulia tu.
Sina ninalojua zaidi ya kumfahamu huyo bwana Ngonde mmoja alitejipambanua kwa maelezo yake!Mkuu NGONDE ni uwanda wa sehemu za Kyela mpaka kuingia Malawi.
Muda wote nasoma hadidhi yako namkumbuka mzungu mmoja nilimletaga mbeya kutoka Netherlands akasema mbeya kumefanana na Afghanistan kwa kila kitu mam yule aliweza kuishi Afghanistan hyvo alisema japo Ni jiji pana ila kwa Kweli Kuna ushamaba na umasikini mno nyumba za mbeyani mbovu mbovu hatar sas HV ndio nao wanaazna kujenga kwa tofali za blokuWASAFWA NDIO WAZAWA HALISI WA WILAYA ZA JIJI LA MBEYA, KILITOKEA NINI MPAKA WANYAKYUSA WA WILAYA ZA NJE YA JIJI KUFAHAMIKA NDIO WENYEJI?
Yani hii Tanzania nzima ukiuliza jiji la Mbeya linakaliwa na kabila gani, fasta mtu anakujibu wanyakyusa lakini ukweli ni kwamba wasafwa ndio wenyeji na hata hili jina la Mbeya lina asili ya kisafwa. si ajabu mtu anaweza asijue kwamba waoambnaji wakuu na matajiri wengi wa mbeya wenye maduka mengi, mahoteli, viwanda na makampuni ni wakinga lakini ukimuuliza swali mwenyeji wa hapa mbeya ni nani, atakujibu fasta tu mnyakyusa, kilotokea nini hadi ikawa hivi?
ni kwamba nchi ilipopata uhuru kulikuwa kuna wanyakyusa wengi wazawa wa wilaya za rungwe na kyela walianza kuja na kuhamia wilaya ya Mbeya mjini (kwa sasa jiji) ambako ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya, wageni wengine nao pia walikuja kuhamia mjini kupata huduma za kijamii, kusoma, kufanya biashara, n.k.
Muda huo wakazi wa mbeya mjini wengi walikuwa ni wazawa ambao ni wasafwa kundi la wamalila, shida ikaja kwamba wasafwa wakiona wageni walikuwa hawataki kuchangamana nao walikuwa wanahamisha makazi kwenda sehem ambayo wapo peke yao, mji ulizidi kuchanganya na kufanya wanyakyusa na wageni wazidi kuja mjini na ikawa usumbufu kwa wasafwa kuhama hama mji unavyozidi kupanuka, ikafikia kipindi wengine wakaanza kukimbilia maeneo ya mbali zaidi hata milimani.
matokeo yake hapa mjini makabila ya ziada yaliyokuja kama wanyiha, wandali, wakinga, wahehe, wangoni, wabena, n.k. wao wakawa wanajua huu mji ni wa wanyakyusa maana wasafwa wengi walikimbilia milimani ikawa vigumu kuwajua wao ndio wenye mji.
Laiti wasafwa wangebaki kwenye huu mji huenda wangekuwa na maendeleo sana kuzidi hata wanyakyusa, mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini hii bahati wakaichezea na ni ngumu kurudi tena. wasafwa waliletewa hivi vitu vizuri hapa mjini ila wakavikimbia.
-hapa mjini serikali ilijenga shule nyingi ila wasafwa walizikimbia
-ajira nzuri enzi hizo zinahitaji elimu hata za shule ya msingi au form 4 zilikuwepo mjini wao zikawa zinawapita
-mji ulianza kujaa na kukawa na fursa za biashara ambazo wasafwa wangeweza kupata pesa lakini kujitenga kwao kukaliacha soko wazi kwa wageni.
-madaraka, vyeo na teuzi serikalini za kuongoza mji huu wakawaachia wageni ambao nao walitumia bahati hii kuwekana maofisini na kupeana vyeo.
-viwanja vingi waliviacha ama kuviuza na kukimbilia milimani kusiko hata na huduma za jamii, n.k.
-baadhi ya wasafwa waliorudi hapa mjini ama waliobaki maeneo ya karibu wakaanza kujitambulisha ni wanyakyusa kwa kuogopa aibu na wengine kufikia hatua ya kufuta majina ya ukoo ili kuepukana na aibu, hii tabia hadi sasa inaendelea.
Ni historia yenye kusikitisha ila ina funzo kubwa sana, mkataa kwao hugeuka mtumwa.
Mwisho kwa kuhitimisha naweza kutoa ushauri kwa wasafwa kwamba historia haiwezi kubadilika itabaki kwajili ya kujifunza lakini mnachoweza kubadilisha ni muda wa mbele (future) kwa maamuzi mnayoweza kuanza kuyatekeleza sasa ili angalau mrudishe hadhi, mapendekezo yangu kwenu:
- wasafwa mzingatieni sana elimu pambanieni na ikibidi mjinyime watoto wasome.
- mjipanue na kutafuta fursa mpya za kibiashara na kujiajiri, Mbeya ni jiji lina watu wengi wenye mahitaji mengi muangalie ni sehemu zipi mnaweza kuchota pesa.
- muwe na bidii ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na uongozi kwenye huu mji wenu, mpambanie nafasi za kupaza sauti ya kero zetu wageni wa mbeya na zenu wazawa halisi wa mbeya.
-msaidiane na kubebana ili walio chini nao wawe na maendeleo, roho za umimi na ubinafsi haziwezi leta maendeleo.
-mjivunie asili yenu ya usafwa, kuna baadhi ya wasafwa hufuta majina yao ya ukoo na wengine kukana kabila lao, huu ni ujinga, jivunie kabila lako, nyumbani ni nyumbani kwa jirani sio kwako.
bila kufanya haya hakuna kitachobadilika..
Sahihi kabisa .....makao makuu ya morovian yapo karibu shule ya rungwe Boyz .....na chuo Cha ufundiMkuu NGONDE ni uwanda wa sehemu za Kyela mpaka kuingia Malawi.
Na wanyakyusa wa sehemu hizi wanaongea dialect tofauti kidogo tu na ndugu zao wa milimani kule Rungwe.
Wazung walipofik waliwaita wanyakyusa wa sehemu hizo watu wa ngonde na ndipo baadaye wakaja kuwaona ndugu zao wa milimani.
Wamissionari wa kwanza kufika Mbeya walitokea Afrika ya Kusini kwa kuitia Malawi.
Na ndio maana unaona makao makuu ya madhehebu ya Moravian, na Lutheran yalikuwa Rungwe Mission na Manow, Busokelo.
Sababu kubwa ya kuweka makao makuu hayo ni ile hali yahewa kulingana na kwao wazungu walikotoka.
Kanisa la Moravian likaenea baadaye hadi Mbeya(na Songwe) na Tabora na liliishia mikoa hiyo.
Kanisa la Lutheran nalo lilisambaa baadaye sehemu nyngine za mkoa wa Mbeya.
Ngonde ni sehemu ya uwanda tambarare huko zkyela/Malawi na Gondwe ni uko mkubwa huko Malawi.Sina ninalojua zaidi ya kumfahamu huyo bwana Ngonde mmoja alitejipambanua kwa maelezo yake!