Habari za wakati Great Thinkers wa JF...
Mheshimiwa Maxence Melo,
Waheshimiwa Moderators wote, JF Senior members, JF Expert members, Members kama mimi, Wataalamu woooote wa masuala ya historia,,, Itifaki imezingatiwa...
Mimi nimezaliwa katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera lakini sijakulia huko hivyo sikubahatika kujua asili yangu hadi nilipokua na kuanza research mbalimbali zisizo rasmi na kupata machache sana kupitia wahenga na mitandao ya kijamii hususani JF.
Lakini maelezo ambayo nimekuwa nikiyapata yanatofautiana kiasi kwamba sielewi niamini lipi niache lipi. Baadhi husema sisi ni jamii ndogo ya wahaya, wengine husema sivyo.
Ni kabila linaloonekana kuwa dhaifu sana ukilinganisha na jamii nyingine za mkoa wa Kagera. Tupo chini kielimu, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, hata "kupenda misifa" ambayo ni asili ya Kagera tupo chini. Sijui hata tujivunie nini kwenye ka-wilaya ketu ambako hata serikali ilishakatenga kwenye maendeleo (japo mkoa mzima wa Kagera umetengwa).
Kwa yeyote mwenye kuelewa historia ya kabila la wasubi, wilaya ya biharamulo pamoja watu maarufu wa kabila hili anaowafahamu atoe mchango wake hapa.
"Jasiri haachi asili"
Sote ni watanzania lakini kuijua asili si dhambi.
Karibuni...
Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app