SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mechi ya marudiano ya Simba vs Raja AC iliyochezwa jana mjini Casablanca ilitegemewa kuwa ni mechi yenye ushindani mkubwa pamoja na kwamba ilikuwa ni mechi ya kirafiki ya kukamilisha ratiba.
Pamoja na kwamba timu zote mbili zilicheza kwa tahadhari na kujaribu kutafuta ushindi lakini ile hali ya kupata ushindi kwa njia zote halali au haramu haikuwepo wala kutegemewa jana.
Ngoja nikwambie mambo kadhaa niliyoyaona inayofanya mechi hii kukidhi vigezo vya kuitwa ya kirafiki:
1. Simba toka wamefika Morocco wamekuwa wanatumia mabasi ya timu ya Raja.
2. Simba toka wamefika Morocco wametumia uwanja wa mazoezi na facilities za timu ya Raja.
3. Simba walivaa home kit na Raja walivaa away kit.
4. Kwenye mechi yenyewe timu zote mbili zilionekana kuepuka kutenda makosa yanayoweza kuleta majeraha kwa wachezaji wa timu pinzani na pale ilipotokea, wachezaji walikuwa na haraka kuomba radhi.
5. Mengine ya nyuma ya pazia.
Ushauri wangu ambao nakumbuka niliutoa pia baada ya game ya kwanza, Simba waendeleze mahusiano ya karibu na Raja AC. Nadhani kiroho safi wanaweza kuisaidia Simba mbinu za kujenga club bora na ya kisasa zaidi hasa yenye msingi wa football academy.
Simba sasa wamepata picha kamili ya level wanayotaka kufika na Raja AC ndiyo kioo chao.