Anita Kajembe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2021
- 215
- 487
Kuna kundi kubwa la watu wazima wanaotafuta kazi za ndani. Wengine ni kutokana na changamoto za maisha, kuachwa na mume, kufiwa, kupoteza ulivyonavyo na kubidi kuanza upya, haya yote si sababu ya kuanzisha uzi huu.
Watu wazima wengi wanajielewa, kazi umamwelekezi mara moja tu na huwa hawapendi kujivunjia heshima. Wengi hupenda uhuru wao, apate off mara moja kwa wiki hata kwenda kumsalimia binamu yake tu.
Jambo muhimu sana ni usalama wa ndoa. Unakuta mama huyu anawazidi wewe na mume wako umri. Baba hawezi kumgongea mlango usiku.
Changamoto nyingine ni sehemu ya kujistir. Wengi wetu mijini tunaishi kwa kubanana sana. Kupata chumba na kitanda kwa mama au baba huyu ni vigumu.
Watu wazima ni wazuri kwa usalama wa nyumba pia unaposafiri. Wengi hawakaribishi vijana wa mtaani wanaoweza kuwa vibaka.
Unapokutana na mtu mzima mwenye uhitaji wa ajira, fikiria kumpa nafasi.