Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
1.Mbowe ana uwezo wa kutumia mbinu tofautitofauti katika kupigania mabadiliko,Kwa kifupi hakuna kipya ambacho atafanya Lissu Mbowe hajakifanya,kama ni kugomea Uchaguzi Mbowe alifanya 2019,kama ni kuandamana Mbowe alishafanya,kama ni kuongea Mezani Mbowe alishafanya kwahiyo Mbinu nyingi zitakuwa ni marudio.Kwa kifupi Mbowe ni Kiongozi anayejua atumie Mbinu gani wakati gani.Ikumbukwe bila Mbowe kufanya Vikao vya kuongea na CCM huenda hata Uchaguzi wa CHADEMA usingefanyika wala Lissu asingerudi tusisahau hali iliyokuwepo hata Vikao vya ndani vilikuwa vinavamiwa na Polisi.
2.Mbowe anawajali Wanachama na Viongozi wake kuliko Lissu ndiyo maana alisema haandai Chama cha kigaidi cha kupeleka watu kwenye kifo,Hii hoja kuwa Mbowe hajali wanaouwawa niweke kumbukumbu sawa Maandamano ya Mwisho yalikuwa juu ya kuuwawa Mzee Kibao walijificha wote akabaki Mbowe mwenyewe Magomeni pale na Familia yake, leo wanasema hakufanya Ushawishi wao walikuwa Sehemu ya Uongozi kwanini wanajitenga walizuiwa kushawishi?
Mbowe alishafanya Press na Familia zilizopotelewa na watu wao na amekuwa akipigia kelele mambo hayo kwenye hotuba zake nyingi.
3.Mbowe anafanya Mikutano mingi ya kujenga Chama kuliko Lissu na ana mbinu nyingi kama kutumia Helikopta, kuvaa Magwanda ya Kikamanda yanayovutia nk,ndiyo maana Viongozi nchi nzima wanamfahamu kwa kazi aliyoifanya chini.
4.Mbowe ana uwezo wa kuibua Vipaji kuliko Lissu ndiyo maana katengeneza watu wengi sana kuwa wanasiasa wakubwa akiwemo Lissu,ila muulize Lissu ana wanasiasa wangapi ambao anaweza kujivunia na kuwaonyesha kwa Umma kuwa aliwatengeneza na kuwainua.
5.Mbowe ana uwezo Mkubwa wa kuongea na Umma akaeleweka kuliko Lissu kwasababu ana utulivu, busara hekima nyingi na anajua aongee nini,lini,wapi na kwa nani tofauti na Lissu.
6.Mbowe anaheshimiwa na Wadau na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kisiasa,Viongozi wa Dini,Wafanyabiashara wakubwa wenzake nk kuliko Lissu ndiyo maana anaweza kuongea kitu kikapokelewa na kueleweka na wenye akili kubwa na anaweza kukusanya Rasilimali Fedha za kuendesha Chama kuliko Lissu.
7.Mbowe siyo njaa kali sana kama Lissu ambaye ukimuangalia kukitokea Mkwamo mkubwa wa kirasilimali utakuwa Mtihani kwa Chama.
8.Lissu ni Jasiri na Mwanaharakati kuliko Mbowe ndiyo maana kwa mbaali naona Mgomo na Maandamano na naona CCM na Dola vikikabiliana je nini kitatokea?
Namnukuu Mbowe Time will Tell.
9.Mbowe ni Mwanasiasa na Kiongozi mwenye uwezo wa kujenga Taasisi kwa maono kuliko Lissu.
Kwa hoja hizo nahitimisha kusema Mbowe ni Zaidi ya Lissu hata kama Demokrasia imeamua,ila hii itaeleweka kwa wenye akili kubwa tu na wenye upeo mkubwa na uwezo wa kuona mambo kwa upana.
Naruhusu kuweka hoja nyingine na naruhusu kutoka povu.